Zaburi 12
Kuomba Msaada
Kwa mwimbishaji. Mtindo wa sheminithi. Zaburi ya Daudi.
112:1 Isa 57:1; Mik 7:12Bwana tusaidie, kwa kuwa wacha Mungu wametoweka;
waaminifu wametoweka miongoni mwa wanadamu.
212:2 Za 5:6; 34:13; 141:3; 5:9; Mt 6:19; 12:17; 13:3; Isa 32:7; Rum 16:18Kila mmoja humwambia jirani yake uongo;
midomo yao ya hila huzungumza kwa udanganyifu.
312:3 Mit 26:28; 28:23; Za 73:9; Ufu 13:5; Dan 7:8; Yak 3:5Bwana na akatilie mbali midomo yote ya hila
na kila ulimi uliojaa majivuno,
412:4 Mt 18:21; Yak 3:6ule unaosema, “Kwa ndimi zetu tutashinda;
midomo ni mali yetu, bwana wetu ni nani?”
512:5 Kut 3:7, 8; Mhu 4:1, 5, 8; Isa 3:15; 5:7; 30:12; 59:13; Mdo 7:34; Za 44:24; 62:10; 72:14; 73:8; 6:6; 3:7; 34:6; 35:10“Kwa sababu ya uonevu wa wanyonge
na kulia kwa uchungu kwa wahitaji,
nitainuka sasa,” asema Bwana.
“Nitawalinda kutokana na wale
wenye nia mbaya juu yao.”
612:6 2Sam 22:31; Isa 48:10; Za 18:30; 119:140; Ay 23:10; 28:1; Zek 13:9Maneno ya Bwana ni safi,
kama fedha iliyosafishwa katika tanuru,
iliyosafishwa mara saba.
712:7 Za 16:1; 27:5; 37:28; Yn 17:12Ee Bwana, utatuweka salama
na kutulinda na kizazi hiki milele.
812:8 Za 55:10-11Watu waovu huenda wakiringa kila mahali
wakati ambapo yule aliye mbaya sana
ndiye anayeheshimiwa miongoni mwa watu.