Zaburi 101 – NEN & KJV

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Zaburi 101:1-8

Zaburi 101

Ahadi Ya Kuishi Kwa Uadilifu Na Kwa Haki

Zaburi ya Daudi.

1101:1 Za 33:1; 51:14; 89:1; 145:7Nitaimba juu ya upendo wako na haki yako;

kwako wewe, Ee Bwana, nitaimba sifa.

2101:2 Mwa 17:1; 18:10; 1Sam 18:14; Kum 6:7; Flp 1:10; 1Fal 9:4; 3:14Nitazingatia kuishi maisha yasiyo na lawama:

utakuja kwangu lini?

Nitatembea nyumbani mwangu

kwa moyo usio na lawama.

3101:3 Yos 23:6; 1Sam 12:20; Yer 16:18; Eze 11:21; Hos 9:10; Za 5:5Sitaweka mbele ya macho yangu

kitu kiovu.

Ninayachukia matendo ya watu wasio na imani;

hawatashikamana nami.

4101:4 Mit 3:32; 6:16-19; 11:20; Mt 7:23; 1Kor 5:11; 2Tim 2:19Moyo wa ukaidi utakuwa mbali nami;

nitajitenga na kila ubaya.

5101:5 Kut 20:16; Law 19:16; Za 10:5; Mit 6:17; Lk 18:14Kila amsingiziaye jirani yake kwa siri,

huyo nitamnyamazisha;

mwenye macho ya dharau na moyo wa kiburi

huyo sitamvumilia.

6101:6 Za 101:2; 119:1Macho yangu yatawaelekea waaminifu katika nchi,

ili waweze kuishi pamoja nami;

yeye ambaye moyo wake hauna lawama

atanitumikia.

7Mdanganyifu hatakaa

nyumbani mwangu,

yeye asemaye kwa uongo

hatasimama mbele yangu.

8101:8 Za 5:3; 75:10; 118:10-12; 46:4; Yos 21:12; 2Sam 3:39; Hos 9:2Kila asubuhi nitawanyamazisha

waovu wote katika nchi;

nitamkatilia mbali kila mtenda mabaya

kutoka mji wa Bwana.

King James Version

Psalms 101:1-8

A Psalm of David.

1I will sing of mercy and judgment: unto thee, O LORD, will I sing.

2I will behave myself wisely in a perfect way. O when wilt thou come unto me? I will walk within my house with a perfect heart.

3I will set no wicked thing before mine eyes: I hate the work of them that turn aside; it shall not cleave to me.101.3 wicked…: Heb. thing of Belial

4A froward heart shall depart from me: I will not know a wicked person.

5Whoso privily slandereth his neighbour, him will I cut off: him that hath an high look and a proud heart will not I suffer.

6Mine eyes shall be upon the faithful of the land, that they may dwell with me: he that walketh in a perfect way, he shall serve me.101.6 in a…: or, perfect in the way

7He that worketh deceit shall not dwell within my house: he that telleth lies shall not tarry in my sight.101.7 shall not tarry: Heb. shall not be established

8I will early destroy all the wicked of the land; that I may cut off all wicked doers from the city of the LORD.