Zaburi 100 – NEN & KJV

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Zaburi 100:1-5

Zaburi 100

Dunia Yote Yaitwa Kumsifu Mungu

Zaburi ya shukrani.

1100:1 Za 98:6Mpigieni Bwana kelele za shangwe, dunia yote.

2100:2 Kum 10:12; Za 95:2Mwabuduni Bwana kwa furaha;

njooni mbele zake kwa nyimbo za shangwe.

3100:3 1Fal 18:21; Za 74:1; 46:10; 79:13; Isa 19:25; 63:8, 17-19; 64:9; Ay 10:3, 8, 9; Mhu 12:1; Efe 2:10; Eze 34:30Jueni kwamba Bwana ndiye Mungu.

Yeye ndiye alituumba, sisi tu mali yake;

sisi tu watu wake,

kondoo wa malisho yake.

4100:4 Za 42:4; 96:8; 116:17Ingieni malangoni mwake kwa shukrani

na katika nyua zake kwa kusifu,

mshukuruni yeye na kulisifu jina lake.

5100:5 1Nya 16:34; Ezr 3:11; Za 106:1; 108:4; 119:90Kwa maana Bwana ni mwema

na upendo wake wadumu milele;

uaminifu wake unadumu kwa vizazi vyote.

King James Version

Psalms 100:1-5

A Psalm of praise.

1Make a joyful noise unto the LORD, all ye lands.100.1 praise: or, thanksgiving100.1 all…: Heb. all the earth

2Serve the LORD with gladness: come before his presence with singing.

3Know ye that the LORD he is God: it is he that hath made us, and not we ourselves; we are his people, and the sheep of his pasture.100.3 and not…: or, and his we are

4Enter into his gates with thanksgiving, and into his courts with praise: be thankful unto him, and bless his name.

5For the LORD is good; his mercy is everlasting; and his truth endureth to all generations.100.5 to all…: Heb. to generation and generation