Yoshua 3 – NEN & NUB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Yoshua 3:1-17

Kuvuka Yordani

13:1 Yos 2:1; Mwa 13:10; Ay 40:23; Hes 25:1; 33:49Yoshua na Waisraeli wote wakaondoka asubuhi na mapema kutoka Shitimu, wakaenda mpaka Mto Yordani, ambako walipiga kambi kabla ya kuvuka. 23:2 Mwa 40:13; Yos 2:16; Kum 1:16; Yos 1:11Baada ya siku tatu maafisa wakapita katika kambi yote, 33:3 Hes 10:33; 4:15; Kum 31:9; 1Fal 8:3; 1Sam 6:15wakitoa maagizo kwa watu, wakiwaambia: “Mtakapoona Sanduku la Agano la Bwana Mungu wenu, likichukuliwa na Walawi ambao ndio makuhani, mtaondoka hapo mlipo na kulifuata. 43:4 Hes 35:5; Kut 19:12; Kum 28:58; 1Nya 16:30; Za 2:11; 96:9; Ebr 12:28Ndipo mtakapotambua njia mtakayoiendea, kwa kuwa hamjawahi kuipita kabla. Lakini msisogee karibu, bali kuwe na umbali wa dhiraa 2,0003:4 Dhiraa 2,000 ni sawa na mita 900. kati yenu na Sanduku.”

53:5 Kut 20:1; Law 11:44; Amu 6:13; 1Nya 16:9, 24; Za 26:7; 75:1; Kut 10:10; Hes 11:18; Yos 7:13; 1Sam 16:5; Yos 2:16Ndipo Yoshua akawaambia hao watu, “Jitakaseni, kwa kuwa kesho Bwana atatenda mambo ya kushangaza katikati yenu.”

63:6 Hes 4:15Yoshua akawaambia makuhani, “Liinueni Sanduku la Agano mkatangulie mbele ya watu.” Hivyo wakaliinua na kutangulia mbele yao.

73:7 Yos 4:14; 1Nya 29:25; Yos 1:5Ndipo Bwana akamwambia Yoshua, “Leo nitaanza kukutukuza machoni pa Israeli yote, ili wapate kujua kuwa niko pamoja nawe kama nilivyokuwa pamoja na Mose. 8Uwaambie makuhani wanaochukua Sanduku la Agano, ‘Mnapofika kwenye ukingo wa maji ya Yordani, nendeni mkasimame ndani ya mto.’ ”

9Yoshua akawaambia Waisraeli, “Njooni hapa msikilize maneno ya Bwana Mungu wenu. 103:10 Kum 5:26; 1Sam 17:26, 36; 2Fal 19:4, 16; Za 18:46; 42:2; Isa 37:4, 17; Yer 10:10; 23:36; Dan 6:26; Hos 1:10; Mt 16:16; Kum 7:21; Mwa 26:24; Yos 17:15; 24:11; Amu 1:4; 3:5; Kut 3:8; 23:23; Kum 7:1; 9:1; 11:3; Amu 19:11; 1Nya 11:4Hivi ndivyo mtakavyojua ya kuwa Mungu aliye hai yupo katikati yenu, na kwamba kwa hakika atawafukuza mbele yenu hao Wakanaani, Wahiti, Wahivi, Waperizi, Wagirgashi, Waamori na Wayebusi. 113:11 Kut 19:5; Kum 14:10; Ay 9:10; 28:24; 41:11; Za 50:12; 97:5; Zek 6:5; Kum 9:3Tazameni, Sanduku la Agano la Bwana wa dunia yote litaingia ndani ya Mto Yordani likiwa limewatangulia. 123:12 Yos 4:2-4Sasa basi, chagueni watu kumi na wawili kutoka makabila ya Israeli, mtu mmoja kutoka kila kabila. 133:13 Yos 4:7; Kut 14:22; Isa 11:15; Za 78:13Mara tu nyayo za makuhani walichukualo Sanduku la Bwana, Bwana wa dunia yote, zitakapokanyaga ndani ya Mto Yordani, maji hayo yatiririkayo kutoka juu yatatindika na kusimama kama chuguu.”

143:14 Za 132:8; Mdo 7:44-45; Kut 25:10; 26:30; Hes 10:3; 2Nya 6:41; Ebr 9:4Basi, watu walipovunja kambi ili kuvuka Yordani, makuhani wakiwa wamebeba Sanduku la Agano waliwatangulia. 153:15 2Fal 3:6; Yos 4:18; 1Nya 12:15; Isa 8:7; Mwa 8:22; Yer 12:5; 49:19Wakati huu ulikuwa wakati wa mavuno, nao Mto Yordani ulikuwa umefurika hadi kwenye kingo zake. Ilikuwa kawaida ya Yordani kufurika nyakati zote za mavuno. Mara tu makuhani wale waliokuwa wamebeba Sanduku la Agano walipofika mtoni na nyayo zao kuzama ndani ya yale maji, 163:16 Za 66:6; 74:15; 114:3; Ay 38:37; Za 33:7; 1Fal 4:12; 7:46; Mwa 14:3; 8:1; Kut 14:22; 2Fal 2:4maji hayo yaliyotiririka kutoka upande wa juu yaliacha kutiririka yakasimama kama chuguu mbali kabisa nao, kwenye mji ulioitwa Adamu kwenye eneo la Sarethani, wakati yale maji yaliyokuwa yanatiririka kuingia kwenye Bahari ya Araba (yaani Bahari ya Chumvi), yalitindika kabisa. Hivyo watu wakavuka kukabili Yeriko.

173:17 Yos 4:3-9; Kut 14:22; Yos 2:10Wale makuhani waliobeba Sanduku la Agano la Bwana, wakasimama imara mahali pakavu katikati ya Mto Yordani, wakati Waisraeli wote wakiwa wanapita hadi taifa lote likaisha kuvuka mahali pakavu.

Swedish Contemporary Bible

Josua 3:1-17

Israel går över Jordan

1Tidigt följande morgon lämnade Josua och hela Israels folk Shittim och gick till Jordans strand där de slog läger innan de skulle gå över floden.

2På tredje dagen gick förmännen genom lägret 3och gav följande order: ”När ni ser de levitiska prästerna bära iväg Herrens, er Guds, förbundsark,3:3 Förbundsarken var en guldöverdragen kista där man förvarade stentavlorna med förbundsavtalet, de tio budorden. Se 2 Mos 25:10-22. ska ni bryta upp och följa dem. 4Håll er en kilometer bakom arken och se till att ni inte kommer närmare! Ni har aldrig gått den här vägen tidigare, men om ni följer arken, så vet ni vart ni ska gå.”

5Sedan sa Josua till folket: ”Rena er3:5 Jfr 2 Mos 19:10,14-15., för imorgon ska Herren göra under bland er!”

6Sedan gav Josua prästerna ordern: ”Ta arken och gå före folket!” Då lyfte de upp arken och började gå framför dem.

7”Idag ska jag börja upphöja dig”, sa Herren till Josua. ”Hela Israel ska förstå att jag är med dig precis som jag var med Mose. 8Säg till prästerna som bär arken att de ska stanna i vattenbrynet när de kommer till Jordan.”

9Sedan talade Josua till israeliterna: ”Kom och hör vad Herren, er Gud, har sagt! 10Av detta ska ni förstå att den levande Guden är mitt ibland er och att han verkligen kommer att driva undan kanaanéerna, hettiterna, hivéerna, perisséerna, girgashéerna, amoréerna och jevuséerna för er. 11Herren, hela jordens härskare, ska låta sin förbundsark leda er över floden.

12Välj nu ut tolv män, en från varje stam. 13När prästerna som bär Herrens, hela jordens härskares, ark nuddar vid vattnet med sina fötter, ska vattnet i floden sluta att rinna. Det ska stanna upp och stå som en mur.”

14Folket bröt upp från sitt läger för att gå över Jordanfloden och följde prästerna som bar förbundsarken. 15Det var skördetid och floden svämmade över sina bräddar som alltid. Men just när prästerna som bar arken skulle stiga ner i Jordan, 16stannade vattnet upp och reste sig som en mur långt borta vid Adam, en stad som låg nära Saretan. Nedströms däremot mot Aravasjön, Döda havet, rann allt vattnet undan. Folket gick då över floden mitt emot Jeriko 17och prästerna som bar Herrens förbundsark stod på torr mark mitt i Jordan och väntade tills allt folket hade kommit över.