Yoshua 21 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Yoshua 21:1-45

Miji Kwa Walawi

121:1 Yos 14:1; Hes 34:17; Yos 17:4; 24:33Basi viongozi wa jamaa ya Walawi, wakamwendea kuhani Eleazari, Yoshua mwana wa Nuni, na viongozi wa jamaa nyingine za makabila ya Israeli 221:2 Yos 18:1; Hes 35:2-3; Law 25:2; Yos 14:4huko Shilo katika Kanaani na kuwaambia, “Bwana aliamuru kupitia Mose kuwa mtupe miji ya kuishi yenye sehemu za malisho kwa mifugo yetu.” 3Hivyo kama vile Bwana alivyoamuru, Waisraeli wakawapa Walawi miji ifuatayo pamoja na sehemu zake za malisho kutoka urithi wao wenyewe.

4Kura ya kwanza ikaangukia Wakohathi, ukoo kwa ukoo. Walawi waliokuwa wazao wa kuhani Aroni walipewa miji kumi na mitatu kutoka makabila ya Yuda, Simeoni na Benyamini. 5Wazao wengine waliobaki wa Wakohathi walipewa miji kumi kutoka koo za makabila ya Efraimu, Dani na nusu ya Manase.

621:6 Hes 3:17; Mwa 30:18; Yos 17:7Wazao wa Gershoni walipewa miji kumi na mitatu kutoka koo za makabila ya Isakari, Asheri, Naftali na nusu ya Manase huko Bashani.

721:7 Kut 6:16; Yos 19:10Wazao wa Merari, ukoo kwa ukoo, walipewa miji kumi na miwili kutoka makabila ya Reubeni, Gadi na Zabuloni.

821:8 Mwa 49:7; Hes 35:2-3; Yos 18:6; Mit 16:33Kwa hiyo Waisraeli wakawapa Walawi miji hii pamoja na sehemu zake za malisho, kama vile Bwana alivyokuwa ameamuru kupitia kwa Mose.

9Kutoka makabila ya Yuda na Simeoni waligawa miji ifuatayo kwa majina 10(miji hii walipewa wazao wa Aroni ambao walitokana na koo za Wakohathi wa Walawi, kwa sababu kura ya kwanza iliwaangukia):

1121:11 Yos 15:48-50Waliwapa Kiriath-Arba (yaani Hebroni), pamoja na sehemu zake za malisho zilizoizunguka, katika nchi ya vilima ya Yuda. (Arba alikuwa baba wa Anaki.) 1221:12 Yos 15:13Lakini mashamba na vijiji vilivyozunguka mji mkubwa walikuwa wamempa Kalebu mwana wa Yefune kuwa milki yake.

1321:13 Hes 35:6; 33:20; 1Nya 6:57Kwa hiyo wazao wa kuhani Aroni wakapewa Hebroni (mji mkuu wa makimbilio kwa ajili ya yeyote aliyeshtakiwa kwa mauaji), Libna, 1421:14 Yos 15:48-50; Kum 4:43; 1Fal 22:3Yatiri, Eshtemoa, 15Holoni, Debiri, 1621:16 Hes 34:11; Yos 15:55; 15:10Aini, Yuta na Beth-Shemeshi, pamoja na sehemu zake za malisho, ilikuwa miji tisa kutoka kwa makabila haya mawili.

1721:17 Yos 9:3; Neh 11:31; 1Nya 6:55; Mwa 23:2; Yos 14:15; 2Sam 2:1-3; Lk 1:39Kutoka kabila la Benyamini wakawapa Gibeoni, Geba, 1821:18 2Sam 23:27; 1Fal 2:26; Ezr 2:23; Neh 7:27; 11:32; Isa 10:30; Yer 1:1; 11:21; 32:7; Yos 14:14Anathothi na Almoni, pamoja na sehemu zake za malisho, ilikuwa miji minne.

1921:19 2Nya 31:15; Yos 20:7-9; 15:54; Isa 37:8Miji yote waliyopewa makuhani, wazao wa Aroni, ilikuwa kumi na mitatu, pamoja na sehemu zake za malisho.

20Koo nyingine za Wakohathi, ambao pia ni Walawi, walipewa miji kutoka kabila la Efraimu:

2121:21 Yos 17:7; 10:33; 20:7; Mwa 33:19; Amu 9:1; 1Fal 12:1Katika nchi ya vilima ya Efraimu walipewa Shekemu (mji mkubwa wa makimbilio kwa yeyote anayeshtakiwa kwa mauaji) na Gezeri, 2221:22 Yos 10:10; 1Sam 1:1Kibsaimu na Beth-Horoni, pamoja na sehemu zake za malisho, ilikuwa miji minne.

2321:23 Yos 19:44Pia kutoka kabila la Dani wakapokea Elteke, Gibethoni, 2421:24 Yos 10:12; 19:45Aiyaloni na Gath-Rimoni pamoja na sehemu zake za malisho, ilikuwa miji minne

2521:25 Yos 12:21Kutoka nusu ya kabila la Manase, wakapokea Taanaki na Gath-Rimoni pamoja na sehemu zake za malisho, ilikuwa miji miwili.

26Miji yote hii kumi pamoja na sehemu zake za malisho ilipewa koo za Wakohathi zilizobaki.

2721:27 Yos 12:5; Hes 35:6; Kum 4:43; 1Nya 6:71-76Koo za Walawi za Wagershoni walipewa:

kutoka nusu ya kabila la Manase,

Golani katika Bashani (mji mkuu wa makimbilio kwa yeyote aliyeshtakiwa kwa mauaji) na Beeshtera, pamoja na sehemu zake za malisho, ilikuwa miji miwili;

2821:28 Mwa 30:18; Yos 19:20; 19:12kutoka kabila la Isakari walipewa,

Kishioni, Daberathi, 2921:29 Yos 10:3; 15:34Yarmuthi na En-Ganimu, pamoja na sehemu zake za malisho, ilikuwa miji minne

3021:30 Yos 17:7; 19:26-28kutoka kabila la Asheri walipewa,

Mishali, Abdoni, 3121:31 Yos 19:28Helkathi na Rehobu, pamoja na sehemu zake za malisho, ilikuwa miji minne.

3221:32 Yos 12:22; Hes 35:6; Yos 12:22Kutoka kabila la Naftali walipewa,

Kedeshi katika Galilaya (mji wa makimbilio kwa ajili ya yeyote anayeshtakiwa kwa mauaji), Hamoth-Dori na Kartani, pamoja na sehemu zake za malisho, ilikuwa miji mitano.

33Miji yote ya koo za Wagershoni ilikuwa kumi na mitatu, pamoja na sehemu zake za malisho.

3421:34 Yos 19:10; 12:22Koo za Wamerari (Walawi waliobaki) walipewa:

kutoka kabila la Zabuloni,

Yokneamu, Karta, 3521:35 Yos 19:15Dimna na Nahalali, pamoja na sehemu zake za malisho, ilikuwa miji minne;

3621:36 Yos 20:8; Hes 21:23; Kum 2:32; Amu 11:20kutoka kabila la Reubeni walipewa

Bezeri, Yahasa, 3721:37 Yos 13:18Kedemothi na Mefaathi, pamoja na sehemu zake za malisho, ilikuwa miji minne;

3821:38 Kum 4:43; Yos 12:2; Mwa 32:2kutoka kabila la Gadi walipewa,

Ramothi katika Gileadi (mji wa makimbilio kwa ajili ya yeyote anayeshtakiwa kwa ajili ya mauaji), Mahanaimu, 3921:39 Yos 13:25Heshboni na Yazeri, pamoja na sehemu zake za malisho, ilikuwa miji minne.

40Miji yote waliyopewa koo za Wamerari, waliokuwa mabaki ya Walawi, ilikuwa ni kumi na miwili.

4121:41 Hes 35:7; Mwa 49:7; Kum 33:10Miji yote ya Walawi katika eneo lililoshikwa na Waisraeli lilikuwa arobaini na minane, pamoja na sehemu zake za malisho. 42Kila mmoja wa miji hii ulikuwa na sehemu ya malisho kuuzunguka; ndivyo ilivyokuwa kwa miji hii yote.

4321:43 Kum 34:4; 11:31; 17:14Kwa hiyo Bwana akawapa Israeli nchi yote aliyokuwa ameapa kuwapa baba zao, nao wakaimiliki na kukaa humo. 4421:44 Kut 33:14; Kum 6:19; Kut 23:31; Kum 21:10; 7:24Bwana akawapa pumziko kila upande, kama vile alivyokuwa amewaapia baba zao, hakuna hata mmoja wa adui zao aliyeweza kusimama mbele yao, Bwana akawatia adui zao wote mikononi mwao. 4521:45 Yos 23:14; Neh 9:8; Isa 49:7-8; Mt 24:35; Lk 21:33Hakuna hata mojawapo ya ahadi nzuri ya Bwana kwa nyumba ya Israeli ambayo haikutimia; kila moja ilitimia.

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

约书亚记 21:1-45

分给利未人的城邑

1-2利未人的众族长到迦南示罗见祭司以利亚撒的儿子约书亚以色列各支派的首领,说:“耶和华借着摩西曾吩咐你们把一些城邑分给我们住,让我们可以在城郊牧养牲畜。” 3以色列人便按照耶和华的吩咐,从他们的产业中把以下的城邑及城郊分给了利未人。

4利未哥辖宗族中大祭司亚伦的子孙从犹大西缅便雅悯支派的产业中抽签得了十三座城。 5哥辖宗族中其他的人也从以法莲玛拿西半个支派的产业中抽签得了十座城。 6革顺的子孙从以萨迦亚设拿弗他利和在巴珊玛拿西半个支派的产业中抽签得了十三座城。 7米拉利的子孙按宗族从吕便迦得西布伦支派的产业中抽签得了十二座城。

8以色列人照耶和华对摩西的吩咐,把这些城邑及其草场用抽签的方式分给利未人。

9-10利未支派哥辖宗族中亚伦的子孙得到第一签,以下是从犹大西缅两支派的产业中抽出来分给他们的土地: 11犹大山区的基列·亚巴及其草场,亚巴原是亚衲人的祖先,基列·亚巴就是希伯仑12而城周围的田地和乡村已经分给耶孚尼的儿子迦勒作产业。

13以色列人把避难城希伯仑分给祭司亚伦的子孙,并把立拿14雅提珥以实提莫15何仑底璧16亚因淤他伯·示麦共九座城及其草场分给了他们。这都是从犹大西缅两支派分出来的。 17便雅悯支派的产业中分给他们的城有:基遍迦巴18亚拿突亚勒们四座城及其草场。 19亚伦的子孙中做祭司的共分到十三座城邑及其草场。

20利未哥辖宗族其他的子孙从以法莲支派的产业中分到的城邑有: 21以法莲山区的避难城示剑基色22基伯先伯·和仑共四座城及其草场。 23支派的产业中分给他们的城邑有:伊利提基基比顿24亚雅仑迦特·临门四座城及其草场。 25他们从玛拿西半个支派的产业中分到他纳迦特·临门两座城及其草场。 26以上是哥辖其他的子孙所分到的十座城及其草场。

27以色列人分给利未支派中革顺子孙的城邑有:玛拿西半个支派中巴珊哥兰避难城和比·施提拉及其草场,共两座城; 28以萨迦支派的基善大比拉29耶末隐·干宁四座城及其草场; 30亚设支派的米沙勒押顿31黑甲利合四座城及其草场; 32拿弗他利支派的哈末·多珥加珥坦加利利的避难城基低斯三座城及其草场。 33革顺人按宗族共分到十三座城邑及其草场。 34其余的利未人,就是米拉利的子孙所分到的城邑有:西布伦支派的约念加珥他35丁拿拿哈拉四座城及其草场; 36吕便支派的比悉雅杂37基底莫米法押四座城及其草场; 38迦得支派的玛哈念基列的避难城拉末39希实本雅谢四座城及其草场。 40利未人中米拉利的子孙按宗族所分到的城邑共有十二座。

41利未人从以色列各支派共分到四十八座城及其草场, 42这些城周围都有草场,城城如此。

43这样,耶和华把从前起誓赐给以色列人祖先的整个地区都赐给了以色列人,以色列人都分到土地,住了下来。 44耶和华照着给他们祖先的应许,使他们四境安宁,没有仇敌能抵挡他们。耶和华将所有仇敌都交在了他们手中。 45耶和华给以色列人的美好应许没有一句落空,全部实现了。