Yoshua 20 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Yoshua 20:1-9

Miji Ya Makimbilio

(Hesabu 35:9-34)

1Ndipo Bwana akamwambia Yoshua, 220:2 Kut 21:13; Hes 35:6-14; Kum 4:41-43; Ebr 6:18-19“Waambie Waisraeli, watenge miji mikubwa ya kukimbilia, kama nilivyokuagiza kupitia Mose, 320:3 Law 4:2; Hes 35:12ili mtu yeyote atakayemuua mtu kwa bahati mbaya na pasipo kukusudia aweze kukimbilia huko na kujiepusha na mlipiza kisasi wa damu.

420:4 Mwa 23:10; Rut 4:1; Yer 35:7; Yos 7:6“Anapokimbilia mojawapo ya hii miji mikubwa atasimama kwenye maingilio ya lango la mji mkuu na kueleza wazee wa mji kuhusu shauri lake. Kisha watampokea katika mji wao na kumpa mahali pa kuishi nao. 520:5 2Nya 10:1; Lk 1:39Kama mlipiza kisasi wa damu akimfuatilia, wasimkabidhi yule mshtakiwa, kwa sababu alimuua jirani yake bila kukusudia, na bila kuwa na nia ya kudhuru. 620:6 Hes 35:12Huyu aliyeua atakaa kwenye mji mkubwa huo mpaka awe amesimama kukabili mashtaka yake mbele ya kusanyiko na mpaka kuhani mkuu anayehudumu kwa wakati huo atakapokufa. Ndipo atakapoweza kurudi nyumbani kwake katika mji ambao aliukimbia.”

720:7 Yos 12:22; Mwa 12:6; 35:27; Yos 10:36; Lk 1:36; Yos 21:11, 32; 1Nya 6:76Basi wakatenga Kedeshi katika Galilaya kwenye nchi ya vilima ya Naftali, Shekemu katika nchi ya vilima ya Efraimu, na Kiriath-Arba (yaani Hebroni) kwenye nchi ya vilima ya Yuda. 820:8 Yos 21:36; 1Nya 6:78-80; Yos 12:2-5; 1Nya 6:71Katika upande wa mashariki mwa Yordani ya Yeriko wakatenga Bezeri katika jangwa katika uwanda wa juu katika kabila la Reubeni, Ramothi katika Gileadi katika kabila la Gadi, na Golani huko Bashani katika kabila la Manase. 920:9 Law 4:2; Kut 21:13; Hes 35:13Mwisraeli yeyote au mgeni yeyote aishiye miongoni mwao aliyemuua mtu kwa bahati mbaya, angeweza kukimbilia katika miji mikubwa hiyo iliyotengwa na asiuawe na mlipiza kisasi wa damu kabla hajasimama kukabili mashtaka mbele ya kusanyiko.

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

约书亚记 20:1-9

避难城

1耶和华对约书亚说: 2“你吩咐以色列人,照我以前借摩西所吩咐你们的,设立一些城邑作为避难城, 3好让那些误杀了人的可以逃到那里,免遭仇人追杀。 4逃进城的人要先站在城门口,向避难城的长老陈明事情的经过,长老就把他们收容到城里,给他们地方住。 5如果他们的仇人追到,长老们不可把他们交出来,因为他们是无意杀的,跟被杀者无冤无仇。 6这些人要住在城内,直到在会众面前受了审讯,并且还要等到在任的大祭司死后,才可离城回乡。”

7于是,民众便设立拿弗他利山区加利利境内的基低斯以法莲山区的示剑犹大山区的基列·亚巴,即希伯仑作为避难城。 8他们又在约旦河、耶利哥东面空旷的平原上设立吕便支派的比悉迦得支派基列境内的拉末玛拿西支派巴珊境内的哥兰作为避难城。 9这是为以色列人和那些从外地来寄居的人所设立的避难城,误杀了人的可以逃到那里,不致未在会众面前受审便死在报仇的人手里。