Yoshua 15 – Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) NEN

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Yoshua 15:1-63

Mgawo Kwa Yuda

115:1 Hes 34:3; 13:21; Yos 18:5Mgawo kwa kabila la Yuda, ulienea ukoo kwa ukoo, ukishuka kufikia eneo la Edomu, hadi Jangwa la Sini mwisho kabisa upande wa kusini.

215:2 Mwa 14:3Mpaka wao wa kusini ulianzia kwenye ghuba iliyoko kwenye ncha ya kusini mwa Bahari ya Chumvi, 315:3 Hes 34:4; Kum 1:2ukakatiza kusini mwa Akrabimu, ukaendelea hadi Sini ukaenda hadi kusini mwa Kadesh-Barnea. Tena ukapitia Hesroni ukapanda hadi Adari na ukapinda hadi Karka. 415:4 Hes 34:5; Mwa 15:18; 1Fal 8:65Kisha ukaendelea mpaka Azmoni na kuunganika na Kijito cha Misri, na kuishia baharini. Huu ndio mpaka wao wa upande wa kusini.

515:5 Hes 34:10; Mwa 14:3Mpaka wa upande wa mashariki ni Bahari ya Chumvi ukienea mahali Mto Yordani unapoingilia.

Mpaka wa upande wa kaskazini ulianzia penye ghuba ya bahari mahali Mto Yordani unapoingilia, 615:6 Yos 18:17-21ukapanda hadi Beth-Hogla, na kuendelea kaskazini mwa Beth-Araba hadi kwenye Jiwe la Bohani mwana wa Reubeni. 715:7 Yos 10:3; 7:24, 26; Kum 11:30; Yos 18:16-17; 2Sam 17:17; 1Fal 1:9; Hos 2:15Kisha mpaka ulipanda hadi Debiri kutoka Bonde la Akori na kugeuka kaskazini hadi Gilgali inayotazamana na materemko ya Adumimu, kusini mwa bonde. Ukaendelea sambamba hadi maji ya En-Shemeshi na kutokeza huko En-Rogeli. 815:8 2Nya 28:3; Yer 19:6; Yos 18:16, 28; Amu 1:21; 19:10; 2Sam 5:6; 1Nya 11:4; Ezr 9:1; Yos 10:1; 2Fal 23:10; 2Sam 5:18, 22; 1Nya 14:9; Isa 17:5Kisha ukapanda kwa kufuata Bonde la Ben-Hinomu sambamba na mteremko wa kusini wa mji mkubwa wa Wayebusi (yaani Yerusalemu). Kutoka hapo ukapanda juu ya kilima magharibi ya Bonde la Hinomu mwisho wa ncha ya kaskazini mwa Bonde la Warefai. 915:9 Yos 18:15; 2Sam 6:2; 1Nya 13:9; Yos 9:17Kutoka juu ya kilima mpaka ule ukaendelea hadi kwenye chemchemi ya maji ya Neftoa, ukatokea kwenye miji ya Mlima Efroni na kuteremka kuelekea Baala (yaani Kiriath-Yearimu). 1015:10 Hes 24:18; Yos 19:22; 21:16; Amu 1:33; 1Sam 6:9; 1Fal 4:9; 2Fal 14:11; Mwa 38:12Kisha ukapinda upande wa magharibi kutoka Baala hadi Mlima Seiri, ukafuatia sambamba mteremko wa kaskazini mwa Mlima Yearimu (yaani Kesaloni), ukaendelea chini hadi Beth-Shemeshi na kukatiza hadi Timna. 1115:11 Yos 13:3; 19:43Ukaelekea hadi kwenye mteremko wa kaskazini mwa Ekroni, ukageuka kuelekea Shikeroni, ukapita hadi Mlima Baala na kufika Yabineeli. Mpaka ule ukaishia baharini.

1215:12 Kum 11:2415:12 Hes 34:6Mpaka wa magharibi ni pwani ya Bahari Kuu.

Hii ndiyo mipaka ya watu wa Yuda kwa koo zao.

Nchi Aliyopewa Kalebu

(Waamuzi 1:11-15)

1315:13 1Sam 25:3; 30:14; Mwa 23:2; Yos 10:36; 21:12; 1Nya 6:56; Hes 13:22Kwa kufuata maagizo ya Bwana kwake, Yoshua alimpa Kalebu mwana wa Yefune sehemu katika Yuda: Kiriath-Arba, yaani Hebroni (Arba alikuwa baba wa zamani wa Anaki). 1415:14 Hes 13:33; 13:12; Amu 1:10, 20Kutoka Hebroni Kalebu alifukuza hao wana watatu wa Anaki, nao ni Sheshai, Ahimani na Talmai, wazao wa Anaki. 1515:15 Yos 10:38Kutoka hapo akaondoka kupigana dhidi ya watu walioishi Debiri (jina la Debiri hapo kwanza uliitwa Kiriath-Seferi). 1615:16 1Nya 2:49; Amu 1:12Kalebu akasema, “Nitamwoza binti yangu Aksa kwa mtu atakayeweza kupigana na kuteka Kiriath-Seferi.” 1715:17 Amu 3:9; 1Nya 4:13; 27:15; Hes 32:12; Yos 14:6Basi Othnieli mwana wa Kenazi, ndugu yake Kalebu, akauteka; hivyo Kalebu akamtoa Aksa binti yake aolewe naye.

1815:18 Amu 1:14; Mwa 24:64; 1Sam 25:23Siku moja Aksa alipokuja kwa Othnieli, alimsihi Othnieli amwombe baba yake, Kalebu, shamba. Aksa aliposhuka kutoka juu ya punda wake, Kalebu akamuuliza, “Je, wataka nikufanyie nini?”

1915:19 Yos 10:40; Mwa 36:24Akamjibu, “Naomba unifanyie jambo moja la hisani. Kwa kuwa umenipa ardhi huko Negebu, nipe pia chemchemi za maji.” Basi Kalebu akampa chemchemi za juu na za chini.

Miji Ya Yuda

2015:20 Mwa 49:8-12; Kum 33:7Huu ndio urithi wa kabila la Yuda, ukoo kwa ukoo:

2115:21 Yos 10:40; 2Sam 23:20; 1Nya 11:22; Mwa 35:21Miji ya kusini kabisa ya kabila la Yuda katika Negebu kuelekea mpaka wa Edomu ilikuwa:

Kabseeli, Ederi, Yaguri, 22Kina, Dimona, Adada, 2315:23 Yos 12:22; 11:1Kedeshi, Hazori, Ithnani, 2415:24 1Sam 23:14; 2Nya 11:8Zifu, Telemu, Bealothi, 25Hazor-Hadata, Kerioth-Hezroni (yaani Hazori), 2615:26 Yos 19:2; 1Nya 4:28; Neh 11:26Amamu, Shema, Molada, 27Hasar-Gada, Heshmoni, Beth-Peleti, 2815:28 Yos 19:3; 1Nya 4:28; Mwa 21:14Hasar-Shuali, Beer-Sheba, Biziothia, 2915:29 Yos 19:3; 1Nya 4:29Baala, Iyimu, Esemu, 3015:30 Yos 19:4; Hes 14:45Eltoladi, Kesili, Horma, 3115:31 Yos 19:5; 1Nya 4:30; 12:1; Neh 11:28; 1Nya 2:49Siklagi, Madmana, Sansana, 3215:32 Hes 34:11; Yos 19:7; Amu 20:45; 21:13; Zek 14:10Lebaothi, Shilhimu, Aini na Rimoni; hiyo yote ni miji ishirini na tisa, pamoja na vijiji vyake.

3315:33 Yos 19:41; Amu 13:25; 16:31; 18:2; 13:2; 18:11; 2Nya 11:10; Neh 11:29Kwenye shefela ya magharibi:

Eshtaoli, Sora, Ashna, 3415:34 Yos 15:34; 1Nya 4:18; Neh 3:13; 11:30; Yos 19:21; 21:29; 12:17Zanoa, En-Ganimu, Tapua, Enamu, 3515:35 Yos 10:3; Mwa 38:1; 1Fal 4:10; Yos 10:10Yarmuthi, Adulamu, Soko, Azeka, 3615:36 1Sam 17:52; 1Nya 4:31; 12:4Shaaraimu, Adithaimu na Gedera (au Gederothaimu); yote ni miji kumi na minne, pamoja na vijiji vyake.

37Senani, Hadasha, Migdal-Gadi, 3815:38 Yos 11:3; 2Fal 14:7Dileani, Mispa, Yoktheeli, 3915:39 Yos 10:3; 2Fal 22:1; 14:19Lakishi, Boskathi, Egloni, 40Kaboni, Lamasi, Kitlishi, 4115:41 2Nya 28:18; Yos 19:27; 10:10Gederothi, Beth-Dagoni, Naama na Makeda; yote ni miji kumi na sita pamoja na vijiji vyake.

4215:42 Hes 33; 20; Yos 19:7; 1Sam 30:30; 1Nya 4:32; 6:59Libna, Etheri, Ashani, 43Yifta, Ashna, Nesibu, 4415:44 1Sam 23:1-2; 1Nya 4:19; Neh 3:17-18; Yos 19:29; Amu 1:31; Mik 1:14-15Keila, Akzibu na Maresha; yote ni miji tisa pamoja na vijiji vyake.

4515:45 Yos 13:3Ekroni, pamoja na viunga vyake na vijiji vyake; 4615:46 Yos 11:22magharibi ya Ekroni, maeneo yote yaliyokuwa karibu na Ashdodi, pamoja na vijiji vyake; 4715:47 Yos 11:22; Mwa 15:18; Hes 34:6Ashdodi, miji yake na vijiji vyake na Gaza viunga vyake na vijiji vyake, hadi kufikia Kijito cha Misri na Pwani ya Bahari Kuu.

4815:48 Amu 10:1; Yos 21:14; 1Sam 30:27; 1Nya 6:57Katika nchi ya vilima:

Shamiri, Yatiri, Soko, 4915:49 Yos 10:3Dana, Kiriath-Sana (yaani Debiri), 5015:50 Yos 11:21; 21:14; 1Sam 30:28Anabu, Eshtemoa, Animu, 5115:51 Yos 10:41; 21:15; Yer 48:21; 2Sam 15:12Gosheni, Holoni na Gilo; miji kumi na mmoja pamoja na vijiji vyake.

5215:52 Mwa 25:14Arabu, Duma, Ashani, 53Yanimu, Beth-Tapua, Afeka, 5415:54 Mwa 35:27; Yos 14:15; Amu 1:10Humta, Kiriath-Arba (yaani Hebroni), na Siori; miji tisa pamoja na vijiji vyake.

5515:55 Amu 10:12; 1Sam 23:24-25; 25:1-2; 1Nya 2:45; Yos 12:22; 21:16Maoni, Karmeli, Zifu, Yuta, 5615:56 Yos 17:16; 19:18; Amu 6:33; 1Sam 25:43; 1Fal 18:45; 1Nya 3:1; Hos 1:5Yezreeli, Yokdeamu, Zanoa, 5715:57 Yos 18:28; 24:33; Amu 19:12; 20:4; 2Sam 23:29; 1Nya 11:31; Mwa 38:12Kaini, Gibea na Timna; miji kumi pamoja na vijiji vyake.

5815:58 1Nya 2:45; 2Nya 11:7; Neh 3:16; 1Nya 4:36; 12:7Halhuli, Beth-Suri, Gedori, 59Maarathi, Beth-Anothi na Eltekoni; miji sita pamoja na vijiji vyake.

6015:60 Yos 9:17; Kum 3:11; Yos 18:14; 1Sam 7:1, 2; 1Nya 13:6Kiriath-Baali (yaani Kiriath-Yearimu) na Raba; miji miwili pamoja na vijiji vyake.

6115:61 Yos 8:15Huko jangwani:

Beth-Araba, Midini, Sekaka, 6215:62 1Sam 23:29; 24:1; Eze 47:10Nibshani, Mji wa Chumvi, na En-Gedi; miji sita pamoja na vijiji vyake.

6315:63 Yos 16:10; 17:12; Amu 1:21; Yos 10:1; Eze 48:7; Amu 19:10-12; Hes 13:29; 2Sam 14:16, 18; 2Nya 3:1; Zek 9:7Yuda hakuweza kuwafukuza Wayebusi, waliokuwa wakiishi Yerusalemu; hadi leo Wayebusi huishi huko pamoja na watu wa Yuda.