Yohana 6 – NEN & TNCV

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Yohana 6:1-71

Yesu Alisha Wanaume 5,000

(Mathayo 14:13-21; Marko 6:30-44; Luka 9:10-17)

16:1 Mt 14:15; Mk 6:35; Lk 9:10, 12Baada ya haya, Yesu alikwenda ngʼambo ya Bahari ya Galilaya, ambayo pia huitwa Bahari ya Tiberia. 26:2 Yn 2:11-13Umati mkubwa wa watu uliendelea kumfuata, kwa sababu waliona ishara nyingi za miujiza alizofanya kwa wagonjwa. 36:3 Yn 6:15Kisha Yesu akapanda mlimani akaketi huko pamoja na wanafunzi wake. 46:4 Yn 11:55Pasaka ya Wayahudi ilikuwa imekaribia.

56:5 Yn 1:43Yesu alipotazama na kuuona ule umati mkubwa wa watu ukimjia, akamwambia Filipo, “Tutanunua wapi mikate ili watu hawa wale?” 6Aliuliza swali hili kumpima, kwa maana alishajua la kufanya.

76:7 Hes 11:21, 22Filipo akamjibu, “Hata fedha kiasi cha dinari mia mbili,6:7 Dinari 200 ni sawa na mshahara wa kibarua wa siku 200; mshahara wa kibarua ulikuwa dinari moja kwa siku. hazitoshi kununua mikate ya kuwapa watu hawa ili kila mtu apate kidogo.”

86:8 Yn 1:40Mmoja wa wanafunzi wake aitwaye Andrea, ndugu yake Simoni Petro, akamwambia, 96:9 2Fal 4:43“Hapa kuna mvulana mmoja mwenye mikate mitano ya shayiri na samaki wawili wadogo. Lakini hivi vitatosha nini kwa umati huu wote?”

10Yesu akasema, “Waketisheni watu chini.” Palikuwa na majani mengi katika eneo lile, nao watu wakaketi. Palikuwa na wanaume wapatao 5,000. 116:11 Mt 14:19Ndipo Yesu akachukua ile mikate, akamshukuru Mungu na kuwagawia wale watu waliokuwa wameketi. Akafanya vivyo hivyo na wale samaki. Kila mtu akapata kadiri alivyotaka.

12Watu wote walipokwisha kula na kushiba, akawaambia wanafunzi wake, “Kusanyeni vipande vilivyobaki vya ile mikate, kisipotee chochote.” 13Hivyo wakavikusanya, wakajaza vikapu kumi na viwili kwa vipande vya ile mikate mitano ya shayiri na samaki wale wawili wadogo vilivyobakishwa na waliokula.

146:14 Yn 2:11; Kum 18:15-18; Mt 21:11Baada ya watu kuona muujiza ule Yesu aliofanya, walianza kusema, “Hakika huyu ndiye Nabii ajaye ulimwenguni!” 156:15 Yn 18:36; Mt 14:23; Mk 6:46Yesu akijua kwamba walitaka kuja kumfanya awe mfalme wao, kwa nguvu, akajitenga nao akaenda milimani peke yake.

Yesu Atembea Juu Ya Maji

(Mathayo 14:22-33; Marko 6:45-52)

166:16 Mt 14:22-33; Mk 6:45-52Ilipofika jioni, wanafunzi wake waliteremka kwenda baharini. 17Wakaingia kwenye mashua, wakaanza kuvuka bahari kwenda Kapernaumu. Wakati huu kulikuwa tayari giza na Yesu alikuwa hajajumuika nao. 18Bahari ikachafuka kwa sababu upepo mkali ulikuwa unavuma. 196:19 Ay 9:8Wanafunzi walipokuwa wamekwenda mwendo wa karibu maili tatu au nne,6:19 Maili tatu au nne ni kama kilomita 5 au 6. walimwona Yesu akitembea juu ya maji akikaribia mashua, nao wakaogopa sana. 206:20 Mt 14:27Lakini Yesu akawaambia, “Ni mimi. Msiogope.” 21Ndipo wakamkaribisha kwa furaha ndani ya mashua, na mara wakafika ufuoni walikokuwa wakienda.

Watu Wanamtafuta Yesu

226:22 Yn 6:2; 15:21Siku iliyofuata, wale watu waliokuwa wamebaki ngʼambo waliona kwamba palikuwepo na mashua moja tu na kwamba Yesu hakuwa ameondoka pamoja na wanafunzi wake, ila walikuwa wameondoka peke yao. 236:23 Yn 6:1, 11Lakini zikaja mashua nyingine kutoka Tiberia zikafika karibu na mahali pale walipokula mikate baada ya Bwana kumshukuru Mungu. 24Mara wale watu wakatambua kwamba Yesu hakuwepo hapo, wala wanafunzi wake. Wakaingia kwenye mashua hizo, wakaenda Kapernaumu ili kumtafuta Yesu.

Yesu Ni Mkate Wa Uzima

256:25 Mt 23:7Walipomkuta Yesu ngʼambo ya bahari wakamuuliza, “Rabi, umefika lini huku?”

266:26 Yn 2:11Yesu akawajibu, “Amin, amin nawaambia, ninyi hamnitafuti kwa kuwa mliona ishara na miujiza, bali kwa sababu mlikula ile mikate mkashiba. 276:27 Mt 25:46; Yn 4:14; Mt 8:20; 2Tim 2:19; Ufu 7:3Msishughulikie chakula kiharibikacho, bali chakula kidumucho hata uzima wa milele, ambacho Mwana wa Adamu atawapa. Yeye ndiye ambaye Mungu Baba amemtia muhuri.”

28Ndipo wakamuuliza, “Tufanye nini ili tupate kuitenda kazi ya Mungu?”

296:29 1Yn 3:23; 3:17Yesu akawajibu, “Kazi ya Mungu ndiyo hii: Mwaminini yeye aliyetumwa naye.”

306:30 Yn 2:11; Mt 12:38Hivyo wakamuuliza, “Utafanya ishara gani ya muujiza, ili tuione tukuamini? Utafanya jambo gani? 316:31 Hes 11:7-9; Neh 9:15; Za 105:40Baba zetu walikula mana jangwani, kama ilivyoandikwa, ‘Aliwapa mikate kutoka mbinguni ili wale.’ ”

326:32 Yn 6:49Yesu akawaambia, “Amin, amin nawaambia, si Mose aliyewapa mikate kutoka mbinguni, bali Baba yangu ndiye anawapa mkate wa kweli kutoka mbinguni. 336:33 Yn 3:13, 31Kwa maana mkate wa Mungu ni yule ashukaye kutoka mbinguni na kuupa ulimwengu uzima.”

346:34 Yn 4:15Wakamwambia, “Bwana, kuanzia sasa tupatie huo mkate siku zote.”

356:35 Yn 4:14; 6:48; 7:37Yesu akawaambia, “Mimi ndimi mkate wa uzima. Yeye ajaye kwangu, hataona njaa kamwe na yeye aniaminiye, hataona kiu kamwe. 366:36 Yn 6:26, 29Lakini kama nilivyowaambia, mmeniona lakini bado hamwamini. 376:37 Yn 17:2-6, 9, 24Wale wote anipao Baba watakuja kwangu na yeyote ajaye kwangu, sitamfukuzia nje kamwe. 386:38 Yn 3:17; 4:34Kwa kuwa nimeshuka kutoka mbinguni si ili kufanya mapenzi yangu, bali mapenzi yake yeye aliyenituma. 396:39 Isa 27:3; Yn 18:9Haya ndiyo mapenzi yake yeye aliyenituma, kwamba, nisimpoteze hata mmoja wa wale alionipa, bali niwafufue siku ya mwisho. 406:40 Mt 25:26Kwa maana mapenzi ya Baba yangu ni kwamba kila mmoja amtazamaye, Mwana na kumwamini awe na uzima wa milele, nami nitawafufua siku ya mwisho.”

41Wayahudi wakaanza kunungʼunika kwa kuwa alisema, “Mimi ndimi mkate ulioshuka kutoka mbinguni.” 426:42 Lk 4:22; Yn 7:27, 28Wakasema, “Huyu si Yesu, mwana wa Yosefu, ambaye baba yake na mama yake tunawajua? Anawezaje basi sasa kusema, ‘Nimeshuka kutoka mbinguni’?”

43Hivyo Yesu akawaambia, “Acheni kunungʼunikiana ninyi kwa ninyi. 44Hakuna mtu awezaye kuja kwangu kama asipovutwa na Baba aliyenituma, nami nitamfufua siku ya mwisho. 456:45 Isa 54:13; 1Kor 2:13Imeandikwa katika Manabii, ‘Wote watafundishwa na Mungu.’ Yeyote amsikilizaye Baba na kujifunza kutoka kwake, huyo huja kwangu. 466:46 Yn 1:18; 7:29Hakuna mtu yeyote aliyemwona Baba isipokuwa yeye atokaye kwa Mungu, yeye ndiye peke yake aliyemwona Baba. 476:47 Mt 25:46Amin, amin nawaambia, yeye anayeamini anao uzima wa milele. 486:48 Yn 6:35, 51Mimi ni mkate wa uzima. 496:49 Yn 6:3, 58Baba zenu walikula mana jangwani, lakini wakafa. 506:50 Yn 6:33Lakini hapa kuna mkate utokao mbinguni, ambao mtu yeyote akiula, hatakufa. 516:51 Ebr 10:10Mimi ni mkate wa uzima ule uliotoka mbinguni. Mtu yeyote akiula mkate huu, ataishi milele. Mkate huu ni mwili wangu, ambao nitautoa kwa ajili ya uzima wa ulimwengu.”

526:52 Yn 9:16; 10:19Ndipo Wayahudi wakaanza kuhojiana vikali wao kwa wao wakisema, “Mtu huyu awezaje kutupatia mwili wake tuule?”

536:53 Mt 26:26; 8:20; 26:28Hivyo Yesu akawaambia, “Amin, amin nawaambia, msipoula mwili wa Mwana wa Adamu na kuinywa damu yake, hamna uzima ndani yenu. 546:54 Yn 6:39Mtu yeyote aulaye mwili wangu na kunywa damu yangu, anao uzima wa milele. Nami nitamfufua siku ya mwisho. 55Kwa maana mwili wangu ni chakula cha kweli na damu yangu ni kinywaji cha kweli. 566:56 1Yn 2:24; 3:24Yeyote alaye mwili wangu na kunywa damu yangu, atakaa ndani yangu nami nitakaa ndani yake. 576:57 Yn 3:17Kama vile Baba aliye hai alivyonituma mimi, na kama nami ninavyoishi kwa sababu ya Baba, hivyo anilaye mimi ataishi kwa sababu yangu. 586:58 Yn 3:36; 5:24Huu ndio mkate ushukao kutoka mbinguni, si kama ule mkate baba zenu waliokula nao wakafa. Lakini yeye aulaye mkate huu ataishi milele.” 59Yesu alisema maneno haya alipokuwa akifundisha katika sinagogi huko Kapernaumu.

Wafuasi Wengi Wamwacha Yesu

606:60 Yn 6:66; 6:52Wengi wa wafuasi wake waliposikia jambo hili wakasema, “Mafundisho haya ni magumu. Ni nani awezaye kuyapokea?”

616:61 Mt 13:57Yesu alipojua kwamba wafuasi wake wananungʼunika kuhusu mafundisho yake, akawaambia, “Je, jambo hili limewaudhi? 626:62 Mk 16:19; Yn 17:5Ingekuwaje basi kama mngemwona Mwana wa Adamu akipaa kwenda zake huko alipokuwa kwanza? 636:63 2Kor 3:6Roho ndiye atiaye uzima, mwili haufai kitu. Maneno haya niliyowaambia ni Roho tena ni uzima. 646:64 Yn 2:24-25Lakini baadhi yenu hamwamini.” Kwa maana Yesu alifahamu tangu mwanzo wale ambao hawangemwamini miongoni mwao na yule ambaye angemsaliti. 656:65 Mt 13:11Akaendelea kusema, “Hii ndiyo sababu niliwaambia kwamba hakuna mtu awezaye kuja kwangu isipokuwa amejaliwa na Baba yangu.”

666:66 Yn 6:60Tangu wakati huo wafuasi wake wengi wakarejea nyuma wakaacha kumfuata.

676:67 Mt 10:2Hivyo Yesu akawauliza wale wanafunzi wake kumi na wawili, “Je, ninyi pia mnataka kuondoka?”

686:68 Mt 16:16Simoni Petro akamjibu, “Bwana, tuondoke twende kwa nani? Wewe unayo maneno ya uzima wa milele. 696:69 Mk 1:24; Lk 9:20Tunaamini na kujua kuwa wewe ndiwe Aliye Mtakatifu wa Mungu.”

706:70 Yn 15:16-19; 13:27; 17:12Ndipo Yesu akajibu, “Je, sikuwachagua ninyi kumi na wawili? Lakini mmoja wenu ni ibilisi.” 716:71 Mt 26:14; 10:4(Hapa alikuwa anasema juu ya Yuda, mwana wa Simoni Iskariote. Ingawa alikuwa mmoja wa wale kumi na wawili, ndiye ambaye baadaye angemsaliti Yesu.)

Thai New Contemporary Bible

ยอห์น 6:1-71

พระเยซูทรงเลี้ยงคนห้าพันคน

(มธ.14:13-21; มก.6:32-44; ลก.9:10-17)

1ต่อมาพระเยซูทรงข้ามทะเลกาลิลี (คือทะเลทิเบเรียส) ไปยังอีกฟากหนึ่ง 2ประชาชนกลุ่มใหญ่ติดตามพระองค์ไปเพราะพวกเขาเห็นหมายสำคัญที่ได้ทรงกระทำแก่คนป่วย 3แล้วพระเยซูทรงขึ้นไปบนเนินเขาและประทับนั่งกับเหล่าสาวกของพระองค์ 4ขณะนั้นใกล้ถึงเทศกาลปัสกาของชาวยิวแล้ว

5เมื่อพระเยซูทรงมองไปเห็นคนหมู่ใหญ่มาหาพระองค์ก็ตรัสกับฟีลิปว่า “เราจะไปซื้อหาอาหารที่ไหนมาให้คนเหล่านี้รับประทาน?” 6พระองค์ตรัสถามเช่นนี้เพียงเพื่อทดสอบฟีลิป เพราะพระองค์ทรงดำริไว้แล้วว่าจะทำอะไร

7ฟีลิปทูลตอบพระองค์ว่า “เงินค่าแรงแปดเดือน6:7 ภาษากรีกว่าสองร้อยเดนาริอันยังซื้อขนมปังได้ไม่พอให้คนเหล่านี้กินกันคนละคำ!”

8สาวกอีกคนหนึ่งคืออันดรูว์น้องชายของซีโมนเปโตรทูลขึ้นว่า 9“เด็กคนหนึ่งที่นี่มีขนมปังข้าวบาร์เลย์ห้าก้อนกับปลาเล็กๆ สองตัว แต่จะพออะไรกับคนมากมายขนาดนี้?”

10พระเยซูตรัสว่า “ให้ประชาชนนั่งลง” ที่นั่นมีหญ้ามาก พวกผู้ชายจึงนั่งลง พวกเขามีราวห้าพันคน 11แล้วพระเยซูทรงรับขนมปังมา ขอบพระคุณพระเจ้า และแจกจ่ายให้ผู้ที่นั่งอยู่ได้กินกันมากเท่าที่เขาต้องการ พระองค์ทรงหยิบปลามาทำเช่นเดียวกัน

12เมื่อทุกคนอิ่มแล้ว พระองค์ตรัสสั่งเหล่าสาวกว่า “จงเก็บรวบรวมเศษที่เหลือ อย่าให้เสียของ” 13พวกเขาจึงเก็บเศษที่เหลือจากขนมปังข้าวบาร์เลย์ห้าก้อนได้เต็มสิบสองตะกร้า

14หลังจากประชาชนเห็นหมายสำคัญที่พระเยซูได้ทรงกระทำ ก็เริ่มพูดกันว่า “นี่คือผู้เผยพระวจนะนั้นที่จะเข้ามาในโลกอย่างแน่นอน” 15พระเยซูทรงทราบว่าพวกเขาตั้งใจจะมาใช้กำลังบังคับให้พระองค์ขึ้นเป็นกษัตริย์ จึงเสด็จเลี่ยงขึ้นไปบนภูเขาแต่ลำพังอีก

พระเยซูทรงดำเนินบนน้ำ

(มธ.14:22-33; มก.6:47-51)

16พอพลบค่ำเหล่าสาวกของพระองค์มาที่ทะเลสาบ 17แล้วลงเรือข้ามฟากไปยังเมืองคาเปอรนาอุม ขณะนั้นมืดแล้วและพระเยซูยังไม่ได้เสด็จไปสมทบกับพวกเขา 18ทะเลปั่นป่วนเพราะลมพัดจัด 19พวกเขาตีกรรเชียงไปได้ประมาณ 5 หรือ 6 กิโลเมตร6:19 ภาษากรีกว่า25 หรือ 30 ซทาดิออน ก็เห็นพระเยซูทรงดำเนินบนน้ำเข้ามาหาเรือ พวกเขาจึงตกใจกลัว 20แต่พระองค์ตรัสกับพวกเขาว่า “นี่เราเอง อย่ากลัวเลย” 21แล้วพวกเขาจึงเต็มใจรับพระองค์ขึ้นเรือ และทันใดนั้นเรือก็ถึงฝั่งที่กำลังมุ่งหน้าไป

22วันรุ่งขึ้นประชาชนที่อยู่อีกฟากเห็นว่าก่อนหน้านั้นที่นั่นมีเรืออยู่ลำเดียว และพระเยซูก็ไม่ได้ลงเรือลำนั้นไปกับเหล่าสาวก พวกสาวกไปกันเองตามลำพัง 23มีเรือลำอื่นๆ จากทิเบเรียสมาจอดใกล้ๆ ที่ซึ่งประชาชนได้กินขนมปังหลังจากพระเยซูได้ทรงขอบพระคุณพระเจ้าแล้ว 24เมื่อพวกเขาเห็นว่าพระเยซูกับเหล่าสาวกไม่ได้อยู่ที่นั่น จึงลงเรือมายังเมืองคาเปอรนาอุมเพื่อตามหาพระเยซู

พระเยซูคืออาหารแห่งชีวิต

25เมื่อประชาชนพบพระองค์ที่อีกฟากของทะเลสาบก็ทูลถามพระองค์ว่า “รับบี ท่านมาถึงที่นี่เมื่อใด?”

26พระเยซูตรัสตอบว่า “เราบอกความจริงแก่ท่านว่า พวกท่านตามหาเราไม่ใช่เพราะเห็นหมายสำคัญ แต่เพราะได้กินขนมปังจนอิ่ม 27อย่าขวนขวายหาอาหารที่เน่าเสียได้ แต่จงหาอาหารที่คงอยู่ถึงชีวิตนิรันดร์ซึ่งบุตรมนุษย์จะให้แก่ท่าน พระเจ้าพระบิดาทรงประทับตรารับรองบุตรมนุษย์แล้ว”

28แล้วพวกเขาทูลถามพระองค์ว่า “พวกเราต้องทำประการใด เพื่อจะทำงานที่พระเจ้าทรงประสงค์?”

29พระเยซูตรัสตอบว่า “งานของพระเจ้าคือ จงเชื่อในผู้ที่พระองค์ทรงส่งมา”

30ดังนั้นพวกเขาจึงทูลถามพระองค์ว่า “ท่านจะให้หมายสำคัญอะไรเพื่อเราจะได้เห็นและเชื่อท่าน? ท่านจะทำอะไรบ้าง? 31บรรพบุรุษของเราได้กินมานาในถิ่นกันดารตามที่มีเขียนไว้ว่า ‘พระองค์ประทานอาหารจากสวรรค์ให้พวกเขารับประทาน’6:31 ดูอพย.16:4,15นหม.9:15สดด.78:24; 105:40

32พระเยซูตรัสกับพวกเขาว่า “เราบอกความจริงแก่ท่านว่า ไม่ใช่โมเสสที่ให้อาหารจากสวรรค์นั้นแก่ท่าน แต่เป็นพระบิดาของเราที่ประทานอาหารแท้จากสวรรค์แก่ท่าน 33เพราะอาหารจากพระเจ้า คือผู้ที่ลงมาจากสวรรค์และให้ชีวิตแก่โลก”

34พวกเขาทูลว่า “ท่านเจ้าข้า จากนี้ไปโปรดให้อาหารนี้แก่เราเถิด”

35แล้วพระเยซูประกาศว่า “เราเป็นอาหารแห่งชีวิต ผู้ที่มาหาเราจะไม่มีวันหิวโหยและผู้ที่เชื่อในเราจะไม่มีวันกระหายอีกเลย 36แต่ตามที่เราได้บอกท่านไว้แล้ว ท่านได้เห็นเราแต่ก็ยังไม่เชื่อ 37คนทั้งปวงที่พระบิดาประทานแก่เราจะมาหาเรา และผู้ที่มาหาเรา เราก็จะไม่มีวันขับไล่เขาไป 38เพราะเราได้ลงมาจากสวรรค์มิใช่เพื่อทำตามใจของเราเองแต่เพื่อทำตามพระประสงค์ของพระองค์ผู้ทรงส่งเรามา 39และพระประสงค์ของพระองค์ผู้ทรงส่งเรามาคือ ไม่ให้เราสูญเสียคนทั้งปวงที่พระองค์ประทานแก่เราไปแม้สักคนเดียว แต่จะให้คนเหล่านี้เป็นขึ้นมาในวันสุดท้าย 40เพราะพระบิดาของเราทรงประสงค์ให้ทุกคนที่เห็นและเชื่อในพระบุตรมีชีวิตนิรันดร์ และเราจะให้เขาเป็นขึ้นมาในวันสุดท้าย”

41แล้วพวกยิวจึงเริ่มพากันบ่นเกี่ยวกับพระองค์ เพราะพระองค์ตรัสว่า “เราเป็นอาหารที่ลงมาจากสวรรค์” 42พวกเขาพูดว่า “นี่คือเยซูลูกชายของโยเซฟไม่ใช่หรือ? เราก็รู้จักพ่อแม่ของเขา เขาพูดได้อย่างไรว่า ‘เราลงมาจากสวรรค์’?”

43พระเยซูตรัสตอบว่า “หยุดบ่นกันได้แล้ว 44ไม่มีใครมาหาเราได้ นอกจากพระบิดาผู้ทรงส่งเรามานั้นทรงชักนำเขามาหาเรา และเราจะให้เขาเป็นขึ้นในวันสุดท้าย 45มีเขียนไว้ในหนังสือผู้เผยพระวจนะว่า ‘เขาทั้งหลายจะรับการสอนจากพระเจ้า’6:45 อสย.54:13 ทุกคนที่ฟังพระบิดาและเรียนรู้จากพระองค์ก็มาหาเรา 46ไม่มีใครได้เห็นพระบิดา เว้นแต่ผู้ซึ่งมาจากพระเจ้าเท่านั้นที่ได้เห็นพระบิดา 47เราบอกความจริงแก่ท่านว่าผู้ที่เชื่อก็มีชีวิตนิรันดร์ 48เราเป็นอาหารแห่งชีวิต 49บรรพบุรุษของท่านได้กินมานาในถิ่นกันดาร ถึงกระนั้นพวกเขาก็ตาย 50แต่นี่คืออาหารที่ลงมาจากสวรรค์ซึ่งคนใดได้กินแล้วจะไม่ตาย 51เราเป็นอาหารซึ่งให้ชีวิตที่ลงมาจากสวรรค์ ถ้าผู้ใดได้กินอาหารนี้ ผู้นั้นจะมีชีวิตอยู่ตลอดไป อาหารนี้คือเนื้อ6:51 ในภาษากรีกคำที่แปลว่าเนื้ออาจแปลว่าร่างกายก็ได้ของเราซึ่งเราจะให้เพื่อโลกนี้จะได้มีชีวิต”

52แล้วชาวยิวจึงเริ่มทุ่มเถียงกันอย่างรุนแรงว่า “ผู้นี้จะเอาเนื้อของเขาให้เรากินได้อย่างไร?”

53พระเยซูตรัสกับพวกเขาว่า “เราบอกความจริงแก่ท่านว่าหากท่านไม่กินเนื้อของบุตรมนุษย์และดื่มโลหิตของพระองค์ ท่านก็ไม่มีชีวิตอยู่ภายในตัวท่าน 54ผู้ใดกินเนื้อและดื่มโลหิตของเรา ผู้นั้นก็มีชีวิตนิรันดร์และเราจะให้เขาเป็นขึ้นมาในวันสุดท้าย 55เพราะเนื้อของเราเป็นอาหารแท้และโลหิตของเราเป็นเครื่องดื่มแท้ 56ผู้ใดกินเนื้อและดื่มโลหิตของเรา ผู้นั้นก็อยู่ในเราและเราอยู่ในเขา 57พระบิดาผู้ทรงพระชนม์อยู่ทรงส่งเรามา และเรามีชีวิตอยู่เพราะพระบิดาฉันใด ผู้ที่กินเราก็จะมีชีวิตอยู่เพราะเราฉันนั้น 58นี่คืออาหารที่ลงมาจากสวรรค์ บรรพบุรุษของท่านกินมานาและตายไป แต่ผู้ที่กินอาหารนี้จะมีชีวิตอยู่ตลอดไป” 59พระองค์ตรัสสิ่งเหล่านี้ขณะทรงสั่งสอนอยู่ในธรรมศาลาในเมืองคาเปอรนาอุม

สาวกหลายคนเลิกติดตามพระเยซู

60สาวกของพระองค์หลายคนได้ฟังเช่นนั้นก็พูด ว่า “คำสอนนี้ยากจริง ใครจะรับได้?”

61พระเยซูทรงทราบว่าเหล่าสาวกของพระองค์กำลังบ่นกันเรื่องนี้ ก็ตรัสกับพวกเขาว่า “เรื่องนี้ทำให้พวกท่านขุ่นเคืองใจหรือ? 62จะว่าอย่างไรถ้าท่านเห็นบุตรมนุษย์ขึ้นสู่สถานที่ซึ่งพระองค์เคยอยู่มาก่อน! 63พระวิญญาณประทานชีวิต เนื้อหนังไม่สำคัญอะไรเลย ถ้อยคำที่เรากล่าวกับท่านเป็นวิญญาณ6:63 หรือพระวิญญาณและเป็นชีวิต 64ถึงกระนั้นก็มีบางคนในพวกท่านที่ไม่เชื่อ” เนื่องจากพระเยซูทรงทราบตั้งแต่แรกว่าคนใดในพวกเขาที่ไม่เชื่อและใครจะทรยศพระองค์ 65พระองค์ตรัสต่อไปว่า “เพราะเหตุนี้เราจึงได้บอกท่านว่า ไม่มีใครมาหาเราได้ นอกจากพระบิดาจะทรงโปรดให้เขามา”

66ตั้งแต่นั้นมาสาวกของพระองค์หลายคนก็หันกลับและเลิกติดตามพระองค์

67พระเยซูตรัสถามสาวกทั้งสิบสองคนว่า “แล้วพวกท่านจะจากไปด้วยหรือ?”

68ซีโมนเปโตรทูลตอบว่า “พระองค์เจ้าข้า เราจะไปหาใคร? พระองค์ทรงมีถ้อยคำแห่งชีวิตนิรันดร์ 69ข้าพระองค์ทั้งหลายเชื่อและรู้ว่าพระองค์ทรงเป็นองค์บริสุทธิ์ของพระเจ้า”

70แล้วพระเยซูจึงตรัสตอบว่า “เราได้เลือกพวกท่านทั้งสิบสองคนไม่ใช่หรือ? ถึงกระนั้นคนหนึ่งในพวกท่านคือมารร้าย!” 71(พระองค์ทรงหมายถึงยูดาสผู้เป็นบุตรของซีโมนอิสคาริโอท ถึงแม้ยูดาสเป็นหนึ่งในสาวกสิบสองคน แต่ภายหลังเขาก็ทรยศพระองค์)