Yohana 2 – NEN & HHH

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Yohana 2:1-25

Arusi Huko Kana

12:1 Yn 4:46; 21:2; Mt 12:46Siku ya tatu kulikuwa na arusi katika mji wa Kana ya Galilaya, naye mama yake Yesu alikuwepo pale. 2Yesu pamoja na wanafunzi wake walikuwa wamealikwa arusini pia. 3Divai ilipokwisha, mama yake Yesu akamwambia, “Wameishiwa na divai.”

42:4 Yn 19:26; Mt 8:26; 26:18; Yn 7:6Yesu akamwambia, “Mwanamke, nina nini nawe? Saa yangu haijawadia.”

52:5 Mwa 41:55Mama yake akawaambia wale watumishi, “Lolote atakalowaambia, fanyeni.”

62:6 Mk 7:3-4; Yn 3:25Basi ilikuwepo mitungi sita ya kuhifadhia maji iliyotengenezwa kwa mawe kwa ajili ya kujitakasa kwa desturi ya Kiyahudi; kila mtungi ungeweza kuchukua vipipa viwili au vitatu.2:6 Kipipa kimoja chenye ujazo wa lita 40; hivyo kila mtungi ulikuwa na ujazo wa lita 80 au 120.

7Yesu akawaambia wale watumishi, “Ijazeni hiyo mitungi maji.” Nao wakaijaza ile mitungi mpaka juu.

8Kisha akawaambia, “Sasa choteni hayo maji kidogo, mpelekeeni mkuu wa meza.”

Hivyo wakachota, wakampelekea. 92:9 Yn 4:46Yule mkuu wa meza akayaonja yale maji ambayo yalikuwa yamebadilika kuwa divai. Hakujua divai hiyo ilikotoka ingawa wale watumishi waliochota yale maji wao walifahamu. Basi akamwita bwana arusi kando 10akamwambia, “Watu wote hutoa kwanza divai nzuri, kisha huleta ile divai hafifu wageni wakisha kunywa vya kutosha, lakini wewe umeiweka ile nzuri kupita zote mpaka sasa.”

112:11 Mt 12:38; Yn 1:14; Kut 14:31Huu, ndio uliokuwa muujiza wa kwanza Yesu aliofanya Kana ya Galilaya. Hivyo Yesu alidhihirisha utukufu wake, nao wanafunzi wake wakamwamini.

Yesu Atakasa Hekalu

(Mathayo 21:12-13; Marko 11:15-17; Luka 19:45-46)

12Baada ya hayo, Yesu pamoja na mama yake, ndugu zake na wanafunzi wake, walishuka mpaka Kapernaumu, wakakaa huko siku chache.

132:13 Yn 11:55; Kum 16:1-6; Lk 2:41Ilipokaribia wakati wa Pasaka ya Wayahudi, Yesu alipanda kwenda Yerusalemu. 142:14 Mt 21:12; Mk 11:15; Lk 19:452:14 Mt 21:12, 13; Mk 11:15-17; Lk 19:45, 46Huko Hekaluni aliwakuta watu wakiuza ngʼombe, kondoo na njiwa, nao wengine walikuwa wameketi mezani wakibadili fedha. 15Akatengeneza mjeledi kutokana na kamba, akawafukuza wote kutoka kwenye eneo la Hekalu, pamoja na kondoo na ngʼombe. Akazipindua meza za wale wabadili fedha na kuzimwaga fedha zao. 162:16 Lk 2:49Akawaambia wale waliokuwa wakiuza njiwa, “Waondoeni hapa! Mnathubutuje kuifanya nyumba ya Baba yangu kuwa mahali pa biashara?”

172:17 Za 69; 9Wanafunzi wake wakakumbuka kuwa imeandikwa: “Wivu wa nyumba yako utanila.”

182:18 Mt 12:38Ndipo Wayahudi wakamuuliza, “Unaweza kutuonyesha ishara gani ili kuthibitisha mamlaka uliyo nayo ya kufanya mambo haya?”

192:19 Mt 26:61; Mdo 6:14Yesu akawajibu, “Libomoeni hili Hekalu, nami nitalijenga tena kwa siku tatu!”

20Wale Wayahudi wakamjibu, “Hekalu hili lilijengwa kwa muda wa miaka arobaini na sita, nawe wasema utalijenga kwa siku tatu?” 212:21 1Kor 6:19Lakini yeye Hekalu alilozungumzia ni mwili wake. 222:22 Lk 24:5-8; Yn 14:26Baada ya kufufuliwa kutoka kwa wafu, wanafunzi wake wakakumbuka yale aliyokuwa amesema. Ndipo wakayaamini Maandiko na yale maneno Yesu aliyokuwa amesema.

232:23 Yn 3:15Ikawa Yesu alipokuwa Yerusalemu kwenye Sikukuu ya Pasaka, watu wengi waliona ishara na miujiza aliyokuwa akifanya, wakaamini katika jina lake. 24Lakini Yesu hakujiaminisha kwao kwa sababu aliwajua wanadamu wote. 252:25 Kum 31:21; Mt 9:4Hakuhitaji ushuhuda wa mtu yeyote kuhusu mtu, kwa kuwa alijua yote yaliyokuwa moyoni mwa mtu.

Habrit Hakhadasha/Haderekh

הבשורה על-פי יוחנן 2:1‏-25

1‏-2כעבור יומיים נערכה חתונה בכפר־קנה שבגליל, ובין האורחים היו ישוע, אמו ותלמידיו. 3כשראתה אמו של ישוע כי אזל היין, פנתה אל בנה ואמרה: ”אזל היין.“

4אולם ישוע השיב: ”למה את אומרת לי את זה? עדיין לא הגיע זמני.“

5למרות תשובה זאת אמרה אמו של ישוע למשרתים: ”עשו כל מה שיגיד לכם לעשות.“

6ששה כדים גדולים מאבן עמדו שם; בכל כד אפשר להכיל מאה עד מאה־חמישים ליטר (אלה היו סוג הכדים שהיהודים השתמשו בהם למנהג הטהרה).

7”מלאו את הכדים במים“, ביקש ישוע, והמשרתים מלאו את הכדים עד הסוף. 8”הגישו מן המשקה לראש המסיבה“, המשיך ישוע, והם עשו כדבריו. 9ראש המסיבה לא ידע מאיפה היין, אבל המשרתים ידעו. כשטעם את המים שהפכו ליין, קרא לחתן ואמר: 10”זהו יין משובח מאוד! בדרך־כלל מגיש המארח תחילה את היין המשובח, ולאחר ששתו כולם לרוויה וכבר לא מסוגלים להבחין כל כך בטעם, הוא מגיש את היין הזול. אבל אתה שמרת את היין המשובח לסוף!“

11הנס הזה בכפר־קנה היה הראשון שישוע חולל. הוא הביא את תלמידיו לידי אמונה בו.

12לאחר החתונה הלכו ישוע, אמו, אחיו ותלמידיו לכפר־נחום למספר ימים. 13חג הפסח התקרב, וישוע עלה לירושלים. 14הוא הלך לבית־המקדש ומצא שם סוחרי צאן, בקר ויונים (לצורך הקרבת הקרבנות) ומחליפי כספים. 15הוא לקח מספר חבלים, שזר אותם לשוט עבה וגירש משם את כל האנשים ואת הצאן והבקר; הוא פיזר לכל עבר את מטבעותיהם של החלפנים, והפך את שולחנותיהם.

16ישוע פנה אל סוחרי היונים וקרא: ”הוציאו מכאן את כל היונים, ואל תהפכו את בית אבי לשוק!“

17תלמידיו נזכרו בנבואה מתהלים:2‏.17 ב 17 תהלים סט 10 ”כי קנאת ביתך אכלתני.“ 18”באיזו רשות אתה עושה את כל הדברים האלה? תן לנו אות או הוכחה כדי שנאמין לך.“

19”הרסו את המקדש הזה,“ ענה ישוע, ”ואני אקים אותו מחדש תוך שלושה ימים!“

20”מה?“ קראו בתמיהה. ”המקדש הזה ניבנה במשך ארבעים־ושש שנים, ואתה טוען שתוכל להקימו מחדש תוך שלושה ימים?“ 21ואולם באומרו ”מקדש“ הוא התכוון לגופו. 22לאחר שקם לתחייה נזכרו תלמידיו בדבריו והאמינו בכתוב ובדברי ישוע, כי ראו שהכול התקיים.

23כאשר היה ישוע בירושלים בחג הפסח, אנשים רבים האמינו שהוא המשיח, כי הם ראו את הנסים והנפלאות שחולל. 24‏-25אך ישוע לא השתכנע שהם באמת מאמינים, משום שידע מה הפכפך אופיו של האדם.