Yohana 18 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Yohana 18:1-40

Yesu Akamatwa

(Mathayo 26:47-56; Marko 14:43-50; Luka 22:47-53)

118:1 2Sam 15:23; Mt 21:1; 26:36Yesu alipomaliza kuomba, akaondoka na wanafunzi wake wakavuka Bonde la Kidroni. Upande wa pili palikuwa na bustani, yeye na wanafunzi wake wakaingia humo.

218:2 Lk 21:37; 22:39Basi Yuda, yule aliyemsaliti alipafahamu mahali hapo kwani Yesu alikuwa akikutana humo na wanafunzi wake mara kwa mara. 318:3 Mt 26:47; Mk 14:43; Lk 22:47; Mdo 1:16Hivyo Yuda akaja bustanini. Aliongoza kikosi cha askari wa Kirumi, na baadhi ya maafisa kutoka kwa viongozi wa makuhani na Mafarisayo. Nao walikuwa wamechukua taa, mienge na silaha.

418:4 Yn 6:64; 13:1; 11; 19:28Yesu akijua yale yote yatakayompata, akajitokeza mbele yao akawauliza, “Mnamtafuta nani?”

518:5 Mk 1:4Wao wakamjibu, “Yesu wa Nazareti.”

Yesu akawajibu, “Mimi ndiye.” Yuda, yule aliyemsaliti alikuwa amesimama pamoja nao. 6Yesu alipowaambia, “Mimi ndiye,” walirudi nyuma na kuanguka chini!

718:7 Yn 18:4Akawauliza tena, “Mnamtafuta nani?”

Nao wakamjibu, “Yesu wa Nazareti.”

8Yesu akawaambia, “Nimekwisha kuwaambia kuwa, mimi ndiye; kwa hiyo kama mnanitafuta mimi, waacheni hawa watu waende zao.” 918:9 Yn 6:39; 17:12Hii ilikuwa ili litimie lile neno alilosema, “Sikumpoteza hata mmoja miongoni mwa wale ulionipa.”

1018:10 Mt 26:51; Mk 14:47; Lk 22:49, 50Simoni Petro, aliyekuwa na upanga, akaufuta na kumkata sikio la kuume mtumishi wa kuhani mkuu. Jina la mtumishi huyo aliitwa Malko.

1118:11 Mt 20:22Yesu akamwambia Petro, “Rudisha upanga wako kwenye ala yake. Je, hainipasi kukinywea kikombe alichonipa Baba?”

Yesu Mbele Ya Kuhani Mkuu

1218:12 Yn 18:3Hivyo wale askari, wakiwa pamoja na majemadari wao na maafisa wa Wayahudi, wakamkamata Yesu na kumfunga. 1318:13 Yn 18:24; Mt 26:3Kwanza wakampeleka kwa Anasi, mkwewe Kayafa, aliyekuwa kuhani mkuu mwaka ule. 1418:14 Yn 11:49-51Kayafa ndiye alikuwa amewashauri Wayahudi kwamba imempasa mtu mmoja kufa kwa ajili ya watu.

Petro Anamkana Yesu

(Mathayo 26:69-70; Marko 14:55-64; Luka 22:66-71)

1518:15 Mt 26:3; 26:58; Mk 14:54Simoni Petro pamoja na mwanafunzi mwingine walikuwa wakimfuata Yesu. Huyu mwanafunzi mwingine alikuwa anafahamika kwa kuhani mkuu, hivyo aliingia ndani ya ukumbi pamoja na Yesu. 1618:16 Mt 26:69; Mk 14:66; Lk 22:54Lakini Petro alisimama nje karibu na lango, ndipo yule mwanafunzi mwingine, aliyejulikana na kuhani mkuu, akazungumza na msichana aliyekuwa analinda lango, akamruhusu Petro aingie ndani.

1718:17 Yn 17:25Yule msichana akamuuliza Petro, “Je, wewe pia si mmoja wa wanafunzi wa mtu huyu?”

Petro akajibu, “Sio mimi.”

1818:18 Yn 21:9; Mk 14:54, 67Wale watumishi na askari walikuwa wamesimama wakiota moto wa makaa kwa sababu palikuwa na baridi, Petro naye alikuwa amesimama pamoja nao akiota moto.

Kuhani Mkuu Amhoji Yesu

19Wakati huo kuhani mkuu akawa anamuuliza Yesu kuhusu wanafunzi wake na mafundisho yake.

2018:20 Mt 4:23; 26:55; Yn 7:26Yesu akamjibu, “Nimekuwa nikizungumza waziwazi mbele ya watu wote. Siku zote nimefundisha katika masinagogi na Hekaluni, mahali ambapo Wayahudi wote hukusanyika. Sikusema jambo lolote kwa siri. 21Mbona unaniuliza mimi maswali? Waulize wale walionisikia yale niliyowaambia. Wao wanajua niliyosema.”

2218:22 Yer 20:2; Mdo 23:2; Mt 16:21Alipomaliza kusema hayo, mmoja wa askari aliyekuwa amesimama karibu naye, akampiga Yesu kofi usoni, kisha akasema, “Je, hivyo ndivyo unavyomjibu kuhani mkuu?”

2318:23 Mt 5:39; Mdo 26:3Yesu akamjibu akasema, “Kama nimesema jambo baya, shuhudia huo ubaya niliousema. Lakini kama nimesema yaliyo kweli, mbona umenipiga?” 2418:24 Yn 18:13; Mt 26:3Ndipo Anasi akampeleka Yesu kwa kuhani mkuu Kayafa, akiwa bado amefungwa.

Petro Amkana Yesu Tena

(Mathayo 26:71-75; Marko 14:69-72; Luka 22:58-62)

2518:25 Yn 18:18; 18:17; Mt 26:69, 71; Mk 14:69; Lk 22:58Wakati huo Simoni Petro alikuwa amesimama akiota moto. Baadhi ya wale waliokuwepo wakamuuliza, “Je, wewe si mmoja wa wanafunzi wake?”

Petro akakana, akasema, “Sio mimi.”

2618:26 Yn 18:1; 10Mmoja wa watumishi wa kuhani mkuu, ndugu yake yule mtu ambaye Petro alikuwa amemkata sikio, akamuuliza, “Je, mimi sikukuona kule bustanini ukiwa na Yesu?” 2718:27 Yn 13:38Kwa mara nyingine tena Petro akakana, naye jogoo akawika wakati huo huo.

Yesu Apelekwa Kwa Pilato

(Mathayo 27:1-2, 11-14; Marko 15:1-5; Luka 23:1-5)

2818:28 Mt 27:2; Yn 18:33; 19:9; 11:55Ndipo Wayahudi wakamchukua Yesu kutoka kwa Kayafa na kumpeleka kwenye jumba la kifalme la mtawala wa Kirumi.18:28 Jumba la mfalme la mtawala wa Kirumi lilikuwa linaitwa Praitorio. Wakati huo ilikuwa ni alfajiri, ili kuepuka kuwa najisi kwa taratibu za ibada, Wayahudi hawakuingia ndani kwa sababu ya sheria za Kiyahudi. Wangehesabiwa kuwa najisi kama wangeingia nyumbani mwa mtu asiye Myahudi na wasingeruhusiwa kushiriki katika Sikukuu ya Pasaka. 29Hivyo Pilato akatoka nje walikokuwa akawauliza, “Mmeleta mashtaka gani kumhusu mtu huyu?”

30Wao wakamjibu, “Kama huyu mtu hakuwa mhalifu tusingemleta kwako.”

31Pilato akawaambia, “Basi mchukueni ninyi mkamhukumu kwa kufuata sheria zenu.”

Wayahudi wakamjibu, “Sisi haturuhusiwi kutoa hukumu ya kifo kwa mtu yeyote.” 3218:32 Mt 20:19; 26:2Walisema hivyo ili yale maneno aliyosema Yesu kuhusu kifo atakachokufa yapate kutimia.

3318:33 Mt 27:11; Yn 19:9; Lk 23:3; Mt 2:2Kwa hiyo Pilato akaingia ndani ya jumba la kifalme, akamwita Yesu, akamuuliza, “Wewe ndiye mfalme wa Wayahudi?”

3418:34 Mt 16:13Yesu akamjibu, “Je, unauliza swali hili kutokana na mawazo yako mwenyewe, au uliambiwa na watu kunihusu mimi?”

3518:35 Yn 1:11; Mt 21:39Pilato akamjibu, “Mimi si Myahudi, ama sivyo? Taifa lako mwenyewe na viongozi wa makuhani wamekukabidhi kwangu. Umefanya kosa gani?”

3618:36 Mt 3:2; 26:53; Lk 17:21; Yn 6:51Yesu akajibu, “Ufalme wangu si wa ulimwengu huu. Ufalme wangu ungekuwa wa ulimwengu huu, wafuasi wangu wangenipigania ili nisitiwe mikononi mwa Wayahudi. Lakini kama ilivyo, ufalme wangu hautoki hapa ulimwenguni.”

3718:37 Yn 3:32; 8:47; 1Yn 4:6Pilato akamuuliza, “Kwa hiyo wewe ni mfalme?” Yesu akajibu, “Wewe wasema kwamba mimi ni mfalme. Kwa kusudi hili nilizaliwa, na kwa ajili ya hili nilikuja ulimwenguni, ili niishuhudie kweli. Mtu yeyote aliye wa kweli husikia sauti yangu.”

3818:38 Lk 23:4-6Pilato akamuuliza Yesu, “Kweli ni nini?” Baada ya kusema haya Pilato akaenda nje tena akawaambia wale viongozi wa Wayahudi waliomshtaki Yesu, “Sioni kosa lolote alilotenda mtu huyu. 3918:39 Mt 27:15; Mk 15:6; Lk 23:19Lakini ninyi mna desturi yenu kwamba wakati wa Pasaka nimwachie huru mfungwa mmoja mnayemtaka. Je, mnataka niwafungulie huyu ‘Mfalme wa Wayahudi’?”

4018:40 Mdo 3:14Wao wakapiga kelele wakisema, “Si huyu mtu, bali tufungulie Baraba!” Yule Baraba alikuwa mnyangʼanyi.

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

约翰福音 18:1-40

耶稣被捕

1耶稣祷告完毕,就带着门徒渡过汲沦溪,进了那里的一个园子。 2因为耶稣时常带着门徒到那里聚会,所以出卖耶稣的犹大也知道那地方。 3这时,犹大带着一队士兵以及祭司长和法利赛人的差役,拿着灯笼、火把和兵器来了。 4耶稣早就知道将要发生在自己身上的一切事,于是出来问他们:“你们找谁?”

5他们回答说:“拿撒勒人耶稣!”

耶稣说:“我就是。”那时出卖耶稣的犹大也站在他们当中。

6他们听到耶稣说“我就是”,便后退跌倒在地上。

7耶稣又问:“你们找谁?”

他们说:“拿撒勒人耶稣。”

8耶稣说:“我已经告诉你们我就是。你们既然找我,就让这些人走吧。” 9这是要应验祂以前说的:“你赐给我的人一个也没有失掉。”

10这时,西门·彼得带着一把刀,他拔刀向大祭司的奴仆马勒古砍去,削掉了他的右耳。

11耶稣对彼得说:“收刀入鞘吧!我父赐给我的杯,我怎能不喝呢?”

12千夫长带着士兵和犹太人的差役上前把耶稣捆绑起来,带了回去。 13他们押着耶稣去见亚那,就是那一年的大祭司该亚法的岳父。 14这个该亚法以前曾对犹太人建议说:“让祂一个人替众人死对你们更好。”

彼得不认主

15西门·彼得和另一个门徒跟在耶稣后面。由于那门徒和大祭司认识,他就跟着耶稣来到大祭司的院子。 16彼得留在门外。后来,大祭司所认识的那个门徒出来对看门的女仆说了一声,便把彼得也带了进去。

17看门的女仆问彼得:“你不也是这个人的门徒吗?”

他说:“我不是。”

18天气很冷,奴仆和差役生了一堆火,站着烤火取暖,彼得也跟他们站在一起烤火取暖。 19此时,大祭司正在盘问耶稣有关祂的门徒和祂的教导之事。

20耶稣说:“我是公开对世人讲的,我常在犹太人聚集的会堂和圣殿教导人,没有在背地里讲过什么。 21你何必问我呢?问那些听过我讲的人吧,他们知道我讲过什么。”

22耶稣话才说完,站在旁边的差役就打了祂一耳光,说:“你敢这样回答大祭司!”

23耶稣说:“如果我说错了,你可以指出我错在哪里。如果我说的对,你为什么打我呢?”

24亚那把被捆绑起来的耶稣押到大祭司该亚法那里。

25那时西门·彼得仍然站着烤火,有人问他:“你不也是那人的门徒吗?”

彼得否认说:“我不是!”

26一个大祭司的奴仆,就是被彼得削掉耳朵的那个人的亲戚说:“我不是看见你和祂一起在园子里吗?” 27彼得再次否认。就在那时,鸡叫了。

彼拉多审问耶稣

28黎明的时候,众人从该亚法那里把耶稣押往总督府,他们自己却没有进去,因为怕沾染污秽,不能吃逾越节的晚餐。 29彼拉多出来问他们:“你们控告这个人什么罪?”

30他们回答说:“如果祂没有为非作歹,我们也不会把祂送到你这里来。”

31彼拉多说:“你们把祂带走,按照你们的律法去审理吧。”

犹太人说:“可是我们无权把人处死。” 32这是要应验耶稣预言自己会怎样死的话。

33彼拉多回到总督府提审耶稣,问道:“你是犹太人的王吗?”

34耶稣回答说:“你这样问是你自己的意思还是听别人说的?”

35彼拉多说:“难道我是犹太人吗?是你们犹太人和祭司长把你送来的。你到底犯了什么罪?”

36耶稣答道:“我的国不属于这个世界,如果我的国属于这个世界,我的臣仆早就起来争战了,我也不会被交在犹太人的手里。但我的国不属于这个世界。”

37于是彼拉多对祂说:“那么,你是王吗?”

耶稣说:“你说我是王,我正是为此而生,也为此来到世上为真理做见证,属于真理的人都听从我的话。”

38彼拉多说:“真理是什么?”说完了,又到外面对犹太人说:“我查不出祂有什么罪。 39不过按照惯例,在逾越节的时候,我要给你们释放一个人。现在,你们要我释放这个犹太人的王吗?”

40众人又高喊:“不要这个人!我们要巴拉巴!”巴拉巴是个强盗。