Yohana 15 – Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) NEN

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Yohana 15:1-27

Yesu Mzabibu Wa Kweli

115:1 Za 80:8-11“Mimi ndimi mzabibu wa kweli na Baba yangu ndiye mkulima. 215:2 Mt 3:10; Za 92:14; Mt 3:8; 7:20; Gal 5:22; Efe 5:9; Flp 1:11; Yn 16:6Kila tawi ndani yangu lisilozaa matunda, Baba yangu hulikata, nalo kila tawi lizaalo, hulisafisha ili lipate kuzaa matunda zaidi. 315:3 Yn 17:17; Efe 5:26Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya lile neno nililonena nanyi. 415:4 Yn 6:56; 2:6Kaeni ndani yangu, nami nikae ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa matunda lisipokaa ndani ya mzabibu, vivyo hivyo ninyi msipokaa ndani yangu hamwezi kuzaa matunda.

515:5 1Kor 12:12, 27; 2Kor 3:5“Mimi ni mzabibu, ninyi ni matawi. Akaaye ndani yangu, nami ndani yake, huyo huzaa sana, maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya jambo lolote. 615:6 Mt 3:10; 13:40; Eze 15:4; Yn 15:2Mtu yeyote asipokaa ndani yangu, hutupwa nje kama tawi na kunyauka. Matawi kama hayo hukusanywa na kutupwa motoni, yakateketea. 715:7 Mk 11:24; Yn 6:56; Mt 7:7Ninyi mkikaa ndani yangu na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni lolote mtakalo, nanyi mtatendewa. 815:8 Mt 5:16; Yn 8:31Kwa hiyo Baba yangu hutukuzwa, kwa vile mzaavyo matunda mengi, nanyi mtakuwa wanafunzi wangu.

915:9 Yn 17:23, 24, 26“Kama vile Baba alivyonipenda mimi, hivyo ndivyo mimi nilivyowapenda ninyi. Basi kaeni katika pendo langu. 1015:10 Yn 14:15Mkizishika amri zangu mtakaa katika pendo langu, kama mimi nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake. 1115:11 Yn 3:29Nimewaambia mambo haya ili furaha yangu iwe ndani yenu na furaha yenu iwe kamili. 1215:12 Yn 13:34; 1Yn 3:11; Mk 12:30Amri yangu ndiyo hii: Mpendane kama mimi nilivyowapenda ninyi. 1315:13 Mwa 44:33; Rum 5:7, 8Hakuna mtu mwenye upendo mkuu kuliko huu, mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake. 1415:14 Mit 18:24; Mt 12:50Ninyi ni rafiki zangu mkifanya ninayowaamuru. 1515:15 Yn 8:26Siwaiti ninyi watumishi tena, kwa sababu watumishi hawajui bwana wao analofanya, bali nimewaita ninyi rafiki, kwa maana nimewajulisha mambo yote niliyoyasikia kutoka kwa Baba yangu. 1615:16 Yn 6:70; 13:18Si ninyi mlionichagua, bali mimi ndiye niliyewachagua ninyi na kuwaweka mwende mkazae matunda, na matunda yenu yapate kudumu. Ili nalo lolote mtakalomwomba Baba katika Jina langu, awape ninyi. 1715:17 Yn 15:12Amri yangu ndiyo hii: Mpendane.

Ulimwengu Wawachukia Wanafunzi

1815:18 Isa 66:5“Kama ulimwengu ukiwachukia ninyi, kumbukeni kwamba ulinichukia mimi kabla yenu. 1915:19 Yn 15:16; 17:14Kama mngekuwa wa ulimwengu, ulimwengu ungeliwapenda kama vile unavyowapenda walio wake. Kwa sababu ninyi si wa ulimwengu, lakini mimi nimewachagua kutoka ulimwengu, hii ndiyo sababu ulimwengu unawachukia. 2015:20 Yn 13:16; 2Tim 3:12Kumbukeni lile neno nililowaambia, ‘Hakuna mtumishi aliye mkuu kuliko bwana wake.’ Kama wamenitesa mimi, nanyi pia watawatesa. Kama wamelishika neno langu, watalishika na neno lenu pia. 2115:21 Isa 66:5; Yn 16:3Watawatendea ninyi haya yote kwa ajili ya Jina langu, kwa sababu hawamjui yeye aliyenituma. 2215:22 Rum 1:20; 2:1Kama sikuja na kusema nao wasingalikuwa na hatia ya dhambi. Lakini sasa hawana udhuru kwa ajili ya dhambi zao. 2315:23 1Yn 2:23Yeyote anayenichukia mimi, anamchukia pia na Baba yangu. 2415:24 Yn 5:36Kama sikuwa nimefanya miujiza ambayo haijapata kufanywa na mtu mwingine yeyote, wasingalikuwa na hatia ya dhambi. Lakini sasa wameiona miujiza hii na bado wakatuchukia mimi na Baba yangu. 2515:25 Za 69:4; 109:3Lakini hii ni kutimiza lile neno lililoandikwa kwenye Sheria kwamba, ‘Walinichukia pasipo sababu.’

2615:26 Yn 14:15; 16:7; 14:17; 1Yn 4:4“Lakini atakapokuja huyo Msaidizi nitakayemtuma kwenu kutoka kwa Baba, yaani, huyo Roho wa kweli atokaye kwa Baba, yeye atanishuhudia mimi. 2715:27 Lk 24:48; 1:21; 1Yn 4:14Ninyi nanyi itawapasa kushuhudia kwa sababu mmekuwa pamoja nami tangu mwanzo.