Yohana 14 – NEN & HHH

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Yohana 14:1-31

Yesu Awatia Moyo Wanafunzi Wake

114:1 Yn 14:27; 3:19; Za 4:5; Mk 11:22Yesu akawaambia, “Msifadhaike mioyoni mwenu, mnamwamini Mungu, niaminini na mimi pia. 214:2 Yn 13:33, 36; 16:5Nyumbani kwa Baba yangu kuna makao mengi. Kama sivyo, ningeliwaambia. Naenda kuwaandalia makao. 314:3 Yn 12:26Nami nikienda na kuwaandalia makao, nitarudi tena na kuwachukua mkae pamoja nami, ili mahali nilipo, nanyi mpate kuwepo. 4Ninyi mnajua njia ya kufika ninakokwenda.”

Yesu Ndiye Njia Ya Kwenda Kwa Baba

514:5 Yn 11:16Tomaso akamwambia, “Bwana, sisi hatujui unakokwenda, tutaijuaje njia?”

614:6 Efe 2:18; Ebr 10:20; Yn 1:25; Mdo 4:12Yesu akawaambia, “Mimi ndimi njia na kweli na uzima. Mtu hawezi kuja kwa Baba isipokuwa kwa kupitia kwangu. 714:7 Yn 8:19; 1Yn 2:23Kama mngenijua mimi, mngemjua na Baba pia. Tangu sasa, mnamjua Baba yangu, tena mmemwona.”

814:8 Yn 1:43Filipo akamwambia, “Bwana, tuonyeshe Baba yako yatosha.”

914:9 Isa 9:6; Kol 1:15Yesu akamjibu, “Filipo, nimekaa nanyi muda huu wote hata usinijue? Mtu yeyote aliyeniona mimi, amemwona Baba. Sasa wawezaje kusema, ‘Tuonyeshe Baba’? 1014:10 Yn 14:20; 10:38; 17:21, 23; 5:19; 7:16Je, huamini ya kuwa mimi niko ndani ya Baba, naye Baba yuko ndani yangu? Maneno ninayowaambia siyasemi kwa ajili yangu mwenyewe, bali Baba akaaye ndani yangu ndiye atendaye hizi kazi. 1114:11 Yn 5:36; 10:38Nisadiki mimi kwamba niko ndani ya Baba na Baba yuko ndani yangu, la sivyo, niaminini kwa sababu ya zile kazi nizitendazo. 1214:12 Mt 21:21; Lk 10:17Amin, amin nawaambia, yeyote aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo yeye atazifanya, naam na kubwa kuliko hizi atazifanya, kwa sababu mimi ninakwenda kwa Baba. 1314:13 Mt 7:7Nanyi mkiomba lolote kwa Jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba apate kutukuzwa katika Mwana. 14Kama mkiniomba lolote kwa Jina langu nitalifanya.

Yesu Aahidi Roho Mtakatifu

1514:15 Za 103:18“Kama mnanipenda, mtazishika amri zangu. 1614:16 Yn 15:26; 16:7Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine akae nanyi milele. 1714:17 1Yn 4:6; 5:6; 1Kor 2:14Huyo ndiye Roho wa kweli ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa sababu haumwoni wala haumjui. Ninyi mnamjua kwa kuwa yuko pamoja nanyi naye anakaa ndani yenu. 1814:18 Mt 16:27Sitawaacha ninyi yatima, naja kwenu. 1914:19 Yn 7:33, 34; 16:16; 6:57Bado kitambo kidogo ulimwengu hautaniona tena, ila ninyi mtaniona, kwa kuwa mimi ni hai, ninyi nanyi mtakuwa hai. 2014:20 Yn 17:21Wakati huo mtajua ya kuwa mimi niko ndani ya Baba na ninyi mko ndani yangu na mimi niko ndani yenu. 2114:21 Yn 14:15; Kum 7:13; Yn 16:27Yeyote mwenye amri zangu na kuzishika ndiye anipendaye, naye anipendaye atapendwa na Baba yangu, nami nitampenda na kujidhihirisha kwake.”

2214:22 Lk 6:16; Mdo 1:13; 10:41Ndipo Yuda, siyo Iskariote, akamwambia, “Bwana, itakuwaje kwamba utajidhihirisha kwetu na si kwa ulimwengu?”

2314:23 Rum 8:10; Yn 14:15Yesu akamjibu, “Mtu yeyote akinipenda atalishika neno langu na Baba yangu atampenda, nasi tutakuja kwake na kufanya makao yetu kwake. 2414:24 Yn 5:19Mtu yeyote asiyenipenda hayashiki maneno yangu na maneno niliyowapa si yangu bali ni ya Baba aliyenituma.

25“Nimewaambia mambo haya yote wakati bado niko pamoja nanyi. 2614:26 Yn 15:26; 16:7; Mdo 2:33; Yn 16:13; 2:22; 1Yn 2:20, 27Lakini huyo Msaidizi, yaani, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atamtuma kwenu kwa Jina langu, atawafundisha mambo yote na kuwakumbusha yote niliyowaambia. 2714:27 Hes 6:26; Lk 2:14Amani nawaachia, amani yangu nawapa, amani hii niwapayo si kama ile ulimwengu utoayo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiogope.

2814:28 Mt 16:27; Yn 5:18; 10:29; Flp 2:6“Mlinisikia nikisema, ‘Ninakwenda zangu, lakini nitarudi tena.’ Kama kweli mngelinipenda mngelifurahi kwa kuwa naenda kwa Baba, kwani Baba ni mkuu kuniliko mimi. 2914:29 Yn 13:19; 16:4Nimewaambia mambo haya kabla hayajatukia, ili yatakapotukia mpate kuamini. 3014:30 Yn 12:31Sitasema nanyi zaidi, kwa sababu yule mkuu wa ulimwengu huu anakuja, naye hana kitu kwangu, 3114:31 Yn 10:18; 12:49lakini ulimwengu upate kujua kuwa ninampenda Baba, nami hufanya vile Baba alivyoniamuru.

“Haya inukeni; twendeni zetu.

Habrit Hakhadasha/Haderekh

הבשורה על-פי יוחנן 14:1-31

1”אל תתנו מקום לדאגה בלבבכם; האמינו באלוהים והאמינו בי. 2בבית אבי מעונות רבים, ואני הולך להכין לכם מקום. לולא היה הדבר נכון, לא הייתי מספר לכם זאת. 3לאחר שהכול יהיה מוכן אחזור ואקח אתכם אלי, כדי שתהיו תמיד במקום שבו אני נמצא. 4אתם יודעים לאן אני הולך וכיצד להגיע לשם.“

5”לא, איננו יודעים לאן אתה הולך“, קרא תומא. ”כיצד אתה מצפה שנדע את הדרך?“

6אולם ישוע ענה: ”אני עצמי הדרך, האמת והחיים. איש אינו יכול לבוא אל האב אלא באמצעותי. 7אילו ידעתם מי אני, הייתם יודעים גם מיהו אבי. מעתה ואילך אתם מכירים אותו וגם ראיתם אותו.“

8”אדוני, הראה לנו את האב ונסתפק בכך“, ביקש פיליפוס. 9אולם ישוע השיב: ”פיליפוס, לאחר שהייתי אתכם במשך כל הזמן הזה, עדיין אינך יודע מי אני? מי שראה אותי ראה את אבי, אם כן מדוע מבקש אתה לראותו? 10האם אינך מאמין שאני חי באבי, ושאבי חי בי? אין אלה המילים שלי, כי אם של אבי השוכן בקרבי והפועל דרכי.

11”האמינו לי שאני חי באבי ואבי חי בי; האמינו לי לפחות בזכות הנסים והנפלאות שחוללתי. 12אני אומר לכם בכנות וברצינות: כל מי שמאמין בי יוכל לעשות את כל מה שאני עושה, ואף הרבה יותר מזה, כי אני הולך אל אבי. 13אעשה למענכם כל מה שתבקשו בשמי, כדי שהאב יכובד בבנו. 14אכן, אעשה את כל מה שתבקשו בשמי.

15”אם אתם אוהבים אותי, שמעו בקולי; 16ואני אבקש מאבי שיתן לכם יועץ אחר שלא יעזוב אתכם לעולם – 17את רוח הקודש והאמת. רוב האנשים בעולם אינם יכולים לקבל את רוח הקודש, מפני שאינם מכירים אותו ואינם מעונינים בו כלל. אולם אתם מכירים אותו, כי עתה הוא נמצא אתכם ובקרוב אף ישכון בקרבכם. 18לא אעזוב אתכם כיתומים; אני אחזור אליכם. 19בעוד זמן קצר העולם כבר לא יראה אותי, אך אתם תראו אותי, כי אני חי וגם אתם תחיו. 20ביום ההוא תדעו שאני שוכן באבי, אתם שוכנים בי ואני בכם. 21כל השומע בקולי אוהב אותי; על כן אבי ואני נאהב אותו, ואני אתוודע אליו.“

22יהודה תלמידו (לא איש־קריות) פנה אליו: ”אדוני, מדוע רוצה אתה להתוודע אלינו בלבד, אל תלמידיך, ולא אל העולם כולו?“

23”מפני שאגלה את עצמי רק למי שאוהב אותי ושומע בקולי“, השיב ישוע. ”גם אבי יאהב את מי שאוהב אותי, ואנחנו נשכון בתוכו. 24מי שאינו שומע בקולי אינו אוהב אותי. זכרו, אין אלה דברי, כי אם דברי אבי אשר שלחני. 25אני אומר לכם דברים אלה כל עוד אני נמצא אתכם. 26כאשר אבי ישלח בשמי את המנחם, את רוח הקודש, הוא ילמד אתכם דברים רבים ויזכיר לכם כל מה שאמרתי.

27”אני משאיר לכם שלווה ושלום. לא לפי מושגי העולם, אלא שלומי שלי. לכן אל תפחדו ואל תדאגו. 28זכרו את מה שאמרתי לכם: אני הולך עכשיו, אולם אשוב אליכם. אם אתם באמת אוהבים אותי, תשמחו לשמוע שאני חוזר אל אבי, כי הוא גדול ממני. 29אני מספר לכם את כל הדברים האלה לפני התרחשותם, כדי שתאמינו בי כאשר הם יתרחשו.

30‏-31”לא נותר לי זמן רב לדבר אליכם, כי שר הרשע של העולם הזה מתקרב. הוא אינו יכול לגבור עלי, אך על העולם לדעת שאני אוהב את אבי; משום כך אני עושה כל מה שאבי מצווה עלי. הבה נלך מכאן.“