Yohana 1 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Yohana 1:1-51

Neno Alifanyika Mwili

11:1 1Yn 1:2; Yn 17:5; Flp 2:6; Isa 55:11Hapo mwanzo alikuwako Neno, huyo Neno alikuwa pamoja na Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. 21:2 Ufu 1:8; Mwa 1:1Tangu mwanzo huyo Neno alikuwa pamoja na Mungu.

31:3 Kol 1:16; Ebr 1:2Vitu vyote viliumbwa kwa yeye, wala pasipo yeye hakuna chochote kilichoumbwa ambacho kimeumbwa. 41:4 1Yn 5:20; Ufu 1:8; Yn 12:46Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima na huo uzima ulikuwa nuru ya watu. 51:5 Yn 3:19Nuru hungʼaa gizani nalo giza halikuishinda.

61:6 Mt 3:1Alikuja mtu mmoja aliyetumwa kutoka kwa Mungu, jina lake Yohana. 71:7 Yn 3:26; 5:33; 3:15Alikuja kama shahidi apate kuishuhudia hiyo nuru, ili kwa kupitia kwake watu wote waweze kuamini. 81:8 Yn 1:20Yeye mwenyewe hakuwa ile nuru, bali alikuja kuishuhudia hiyo nuru. 91:9 1Yn 2:8; Isa 49:6Kwamba nuru halisi, imwangaziayo kila mtu ilikuwa inakuja ulimwenguni.

101:10 Yn 1:3; Ebr 1:2; 11; 3Huyo Neno alikuwako ulimwenguni na ingawa ulimwengu uliumbwa kupitia kwake, haukumtambua. 111:11 Lk 19:14; Mdo 3:26; 13:46Alikuja kwa walio wake, lakini wao hawakumpokea. 121:12 Isa 56:5; Rum 8:15; Gal 3:26; 2Pet 1:4; 1Yn 3:1Bali wote waliompokea, aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake. 131:13 Tit 3:5; Yak 1:18Hawa ndio wasiozaliwa kwa damu, wala kwa mapenzi ya mwili au kwa mapenzi ya mtu, bali kwa mapenzi ya Mungu.

141:14 1Yn 1:1-2; 4:2; Yn 14:6Neno alifanyika mwili, akakaa miongoni mwetu, nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba, amejaa neema na kweli.

151:15 Yn 1:32; 3:32; 5:33; Mt 3:11; Mk 1:7; Lk 3:16; Yn 1:27, 30; 3:31; 8:58; Kol 1:17Yohana alishuhudia habari zake, akapaza sauti, akisema, “Huyu ndiye yule niliyewaambia kwamba, ‘Yeye ajaye baada yangu ni mkuu kuniliko mimi, kwa kuwa alikuwepo kabla yangu.’ ” 161:16 Kol 1:19; 2:9Kutokana na ukamilifu wake, sisi sote tumepokea neema juu ya neema. 171:17 Kum 32:46Kwa kuwa sheria ilitolewa kwa mkono wa Mose, lakini neema na kweli imekuja kupitia Yesu Kristo. 18Hakuna mtu yeyote aliyemwona Mungu wakati wowote, ila ni Mungu Mwana pekee, aliye kifuani mwa Baba ndiye ambaye amemdhihirisha.

Ushuhuda Wa Yohana Mbatizaji

(Mathayo 3:1-12; Marko 1:1-8; Luka 3:1-18)

191:19 Yn 7:1; 10:24Huu ndio ushuhuda wa Yohana wakati Wayahudi walipowatuma makuhani na Walawi kutoka Yerusalemu kumuuliza, “Wewe ni nani?” 201:20 Yn 3:28; Lk 3:15-16Yohana alikiri waziwazi pasipo kuficha akasema, “Mimi si Kristo.”1:20 Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta.

211:21 Kum 18:15; Mt 11:4Wakamuuliza, “Wewe ni nani basi? Je, wewe ni Eliya?”

Yeye akajibu, “Hapana, mimi siye.”

“Je, wewe ni yule Nabii?”

Akajibu, “Hapana.”

22Ndipo wakasema, “Basi tuambie wewe ni nani ili tupate jibu la kuwapelekea wale waliotutuma. Wewe wasemaje juu yako mwenyewe?”

231:23 Mt 3:1; Isa 40:3Akawajibu kwa maneno ya nabii Isaya, akisema, “Mimi ni sauti ya mtu aliaye nyikani, ‘Yanyoosheni mapito ya Bwana.’ ”

24Basi walikuwa wametumwa watu kutoka kwa Mafarisayo 251:25 Mt 21:25wakamuuliza, “Kama wewe si Kristo, wala si Eliya na wala si yule Nabii, kwa nini basi unabatiza?”

261:26 Mt 3:11; Mk 1:7, 8Yohana akawajibu, “Mimi ninabatiza kwa maji,1:26 Hapa tafsiri zingine zinasema ndani ya maji. lakini katikati yenu yupo mtu msiyemjua. 271:27 Yn 3:26; Mdo 13:25Yeye ajaye baada yangu, sistahili hata kufungua kamba za viatu vyake.”

281:28 Yn 3:26; 10:40Mambo haya yote yalitukia huko Bethania, ngʼambo ya Mto Yordani, mahali Yohana alipokuwa akibatiza.

Yesu Mwana-Kondoo Wa Mungu

291:29 Mwa 22:8; Ufu 5:6Siku iliyofuata, Yohana alimwona Yesu akimjia akasema, “Tazama, Mwana-Kondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu! 301:30 Yn 15:27Huyu ndiye yule niliyewaambia kwamba, ‘Mtu anakuja baada yangu ambaye ni mkuu kuniliko mimi, kwa kuwa alikuwepo kabla yangu.’ 311:31 Mal 3:1; Mt 3:6; Lk 1:17, 76, 77; 3:3, 4Mimi mwenyewe sikumfahamu, lakini sababu ya kuja nikibatiza kwa maji ni ili yeye apate kufunuliwa kwa Israeli.”

321:32 Mt 3:16; Mk 1:10Kisha Yohana akatoa ushuhuda huu: “Nilimwona Roho akishuka kutoka mbinguni kama hua, akakaa juu yake. 331:33 Mk 1:4; Mt 3:11Mimi nisingemtambua, lakini yeye aliyenituma nibatize kwa maji alikuwa ameniambia, ‘Yule mtu utakayemwona Roho akimshukia na kukaa juu yake, huyo ndiye atakayebatiza kwa Roho Mtakatifu.’ 341:34 Mt 4:3Mimi mwenyewe nimeona jambo hili na ninashuhudia kuwa huyu ndiye Mwana wa Mungu.”

Wanafunzi Wa Kwanza Wa Yesu

351:35 Mt 3:1Siku iliyofuata, Yohana alikuwa huko tena pamoja na wanafunzi wake wawili. 361:36 Yn 1:29Alipomwona Yesu akipita, akasema, “Tazama, Mwana-Kondoo wa Mungu!”

37Wale wanafunzi wawili walipomsikia Yohana akisema haya, wakamfuata Yesu. 381:38 Mt 23:7Yesu akageuka, akawaona wakimfuata akawauliza, “Mnataka nini?”

Wakamwambia, “Rabi,” (maana yake Mwalimu), “Unaishi wapi?”

39Yesu akawajibu, “Njooni, nanyi mtapaona!”

Hivyo wakaenda na kupaona mahali alipokuwa anaishi, wakakaa naye siku ile, kwa kuwa ilikuwa yapata saa kumi.

401:40 Mt 4:18-22Andrea nduguye Simoni Petro, alikuwa mmoja wa wale wawili waliosikia yale Yohana aliyokuwa amesema, naye ndiye alimfuata Yesu. 411:41 Yn 4:25Kitu cha kwanza Andrea alichofanya ni kumtafuta Simoni nduguye na kumwambia, “Tumemwona Masiya” (yaani, Kristo). 421:42 Mwa 32:28; Mt 16:18Naye akamleta kwa Yesu.

Yesu akamwangalia na kusema, “Wewe ni Simoni mwana wa Yohana. Utaitwa Kefa” (ambalo limetafsiriwa Petro1:42 Petro kwa Kiyunani au Kefa kwa Kiaramu; maana yake ni Kipande cha mwamba.).

Yesu Awaita Filipo Na Nathanaeli

431:43 Mt 10:3; Yn 14:8-9; Mt 4:9Siku iliyofuata Yesu aliamua kwenda Galilaya. Akamkuta Filipo, akamwambia, “Nifuate.”

441:44 Yn 12:21Basi Filipo alikuwa mwenyeji wa Bethsaida, mji alikotoka Andrea na Petro. 451:45 Yn 21:2; Lk 24:27; Mt 2:23; Lk 3:23Filipo naye akamkuta Nathanaeli na kumwambia, “Tumemwona yeye ambaye Mose aliandika habari zake katika Sheria na ambaye pia manabii waliandika kumhusu, yaani, Yesu wa Nazareti, mwana wa Yosefu.”

461:46 Yn 7:41-42, 52Nathanaeli akauliza, “Nazareti! Je, kitu chochote chema chaweza kutoka Nazareti?” Filipo akamwambia, “Njoo uone.”

471:47 Za 32:2; Rum 9:4-6Yesu alipomwona Nathanaeli anakaribia, akanena habari zake akasema, “Tazama huyu ni Mwisraeli kweli kweli; hana hila ndani yake.”

48Nathanaeli akamuuliza, “Umenifahamuje?”

Yesu akamjibu, “Nilikuona ulipokuwa bado uko chini ya mtini, kabla hata Filipo hajakuita.”

491:49 Mt 23:7; 4:3; 2; 2; 27:42Nathanaeli akamwambia, “Rabi, wewe ni Mwana wa Mungu! Wewe ni Mfalme wa Israeli!”

50Yesu akamwambia, “Unaamini kwa kuwa nilikuambia nilikuona ulipokuwa bado uko chini ya mtini? Basi utaona mambo makuu zaidi kuliko hilo.” 511:51 Mt 3:16; 8:20; Mwa 28:12Ndipo akawaambia, “Amin, amin nawaambia, ninyi mtaona mbingu ikifunguka na malaika wa Mungu wakipanda na kushuka juu ya Mwana wa Adamu.”

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

约翰福音 1:1-51

生命之道

1太初,道已经存在,道与上帝同在,道就是上帝。 2太初,道就与上帝同在。 3万物都是借着祂造的1:3 造的”或译“存在”。,受造之物没有一样不是借着祂造的。 4祂里面有生命,这生命是人类的光。 5光照进黑暗里,黑暗不能胜过1:5 胜过”或译“接受”或“明白”。光。

6有一个人名叫约翰,是上帝差来的。 7他来是要为光做见证,叫世人可以借着他而相信。 8约翰不是那光,他来是为那光做见证。 9那照亮世人的真光来到了世上。 10祂来到自己所创造的世界,世界却不认识祂。 11祂来到自己的地方,自己的人却不接纳祂。 12但所有接纳祂的,就是那些信祂的人,祂就赐给他们权利成为上帝的儿女。 13这些人既不是从人的血缘关系生的,也不是从人的情欲或意愿生的,而是从上帝生的。

14道成为肉身,住在我们中间,充满了恩典和真理。我们见过祂的荣耀,正是父独一儿子的荣耀。

15约翰为祂做见证的时候,高声喊道:“这就是我以前所说的那位,‘祂在我以后来却比我位分高,因为祂在我之前已经存在了。’” 16从祂的丰盛里,我们一次又一次地领受了恩典。 17因为律法是借着摩西颁布的,恩典和真理是借着耶稣基督赐下来的。 18从来没有人见过上帝,只有父怀中的独一上帝1:18 独一上帝”有古卷作“独一儿子”。把祂显明出来。

施洗者约翰的见证

19以下是约翰的见证。犹太人从耶路撒冷派祭司和利未人来找约翰,查问他是谁。 20约翰毫不隐瞒地说:“我不是基督。”

21他们问:“那么,你是谁?是以利亚吗?”

他说:“不是。”

他们又问:“你是那位先知吗?”

他说:“也不是。”

22他们又追问:“你到底是谁?我们好回复差我们来的人。你自己说你是谁?”

23他说:“我就是在旷野大声呼喊‘修直主的路’的那个人,正如以赛亚先知所言。”

24派来的人当中有几个法利赛人1:24 派来的人当中有几个法利赛人”或译“法利赛人派来的那几个人”。,他们问他: 25“你既然不是基督,不是以利亚,也不是那位先知,那你为什么给人施洗呢?”

26约翰答道:“我是用水施洗,但在你们中间有一位你们不认识的, 27祂虽然是在我以后来的,我就是给祂解鞋带也不配。” 28这事发生在约旦河东岸的伯大尼,那里是约翰给人施洗的地方。

上帝的羔羊

29次日,约翰看见耶稣走过来,就说:“看啊!上帝的羔羊,除去世人罪恶的! 30这就是我以前所说的那位,‘有一个人在我以后来却比我位分高,因为祂在我之前已经存在了。’ 31我以前并不认识祂,现在我用水给人施洗,是要把祂显明给以色列人。”

32约翰又做见证说:“我看见圣灵好像鸽子一样从天降下,住在祂身上。 33我本来不认识祂,但那位差我来用水给人施洗的告诉我,‘你看见圣灵降下,住在谁身上,谁就是用圣灵给人施洗的。’ 34我看见了,便做见证,祂就是上帝的儿子。”

第一批门徒

35再次日,约翰和两个门徒站在那里, 36他看见耶稣经过,就说:“看啊!这是上帝的羔羊!” 37两个门徒听见他的话,便跟从了耶稣。 38耶稣转过身来,看见他们跟着,便问:“你们想要什么?”

他们说:“老师1:38 老师”希腊文是“拉比”,特指犹太教的老师,下同。,你住在哪里?”

39耶稣说:“你们来看吧。”他们便跟着去看耶稣住的地方。到了那里大约下午四点了,他们就住在耶稣那里。 40听见约翰的话后跟从耶稣的两个人中,有一个是西门·彼得的弟弟安得烈41他首先去找他哥哥西门,说:“我们找到弥赛亚了!”弥赛亚的意思是基督1:41 希伯来文的“弥赛亚”和希腊文的“基督”都是“受膏者”的意思。42他带着西门去见耶稣。

耶稣看着西门,对他说:“约翰的儿子西门,你要改名为矶法。”矶法的意思是彼得

43又过了一天,耶稣决定去加利利。祂遇见了腓力,就对他说:“跟从我!” 44腓力伯赛大人,与彼得安得烈是同乡。 45腓力去找拿但业,对他说:“我们遇见了摩西律法书和先知书记载的那位!祂是约瑟的儿子耶稣,从拿撒勒来的。”

46拿但业说:“拿撒勒还会出什么好东西?”

腓力说:“你来看看吧!”

47耶稣看见拿但业走过来,就指着他说:“看啊,这是个真正的以色列人!他心里毫无诡诈。”

48拿但业问耶稣:“你怎么会认识我?”

耶稣答道:“腓力还没有去找你之前,我就看见你在无花果树下了。”

49拿但业说:“老师,你是上帝的儿子!你是以色列的王!”

50耶稣说:“我说看见你在无花果树下,你就信我吗?将来你还要看见比这更大的事。 51我实实在在地告诉你们,你们会看见天门敞开,上帝的天使以人子1:51 人子”是耶稣的自称,耶稣在这里自比天梯,背景请参见创世记28:12为梯上上下下。”