Yeremia 9 – NEN & HTB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Yeremia 9:1-26

19:1 Mao 3:48; Isa 22:4; Za 119:136; Yer 13:17; 14:17; Mao 2:11Laiti kichwa changu kingekuwa chemchemi ya maji

na macho yangu yangekuwa kisima cha machozi!

Ningelia usiku na mchana

kwa kuuawa kwa watu wangu.

29:2 Hes 25:1; Hos 4:2; Za 55:7; Yer 23:10; Hos 7:4; 1Fal 19:10; Isa 24:16Laiti ningekuwa na nyumba

ya kukaa wasafiri jangwani,

ningewaacha watu wangu

na kwenda mbali nao,

kwa kuwa wote ni wazinzi,

kundi la watu wadanganyifu.

39:3 Kut 20:16; Mik 6:12; Amu 2:10; 1Sam 2:12; Za 64:3; Isa 44; 20; Yer 18:18“Huweka tayari ndimi zao kama upinde,

ili kurusha uongo;

wamekuwa na nguvu katika nchi

lakini si katika ukweli.

Wanatoka dhambi moja hadi nyingine,

hawanitambui mimi,”

asema Bwana.

49:4 Mik 7:5-6; Mwa 27:35; 2Sam 15:12; Kut 20:16; Law 19:16“Jihadhari na rafiki zako;

usiwaamini ndugu zako.

Kwa kuwa kila ndugu ni mdanganyifu,

na kila rafiki ni msingiziaji.

59:5 Za 15:2; Law 6:2; Isa 59:15Rafiki humdanganya rafiki,

hakuna yeyote asemaye kweli.

Wamefundisha ndimi zao kudanganya,

wanajichosha wenyewe katika kutenda dhambi.

69:6 Yer 5:27; Mit 1:24Unakaa katikati ya udanganyifu;

katika udanganyifu wao wanakataa kunitambua mimi,”

asema Bwana.

79:7 Ay 28:1; Isa 1:28; Hos 11:8; Yer 6:27Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote:

“Tazama, nitawasafisha na kuwajaribu,

kwani ni nini kingine niwezacho kufanya

kwa sababu ya dhambi ya watu wangu?

89:8 Za 35:20; Yer 5:26; Isa 3:5Ndimi zao ni mshale wenye sumu,

hunena kwa udanganyifu.

Kwa kinywa chake kila mmoja huzungumza maneno mazuri na jirani yake,

lakini moyoni mwake humtegea mtego.

99:9 Kum 32:43; Isa 10:3Je, nisiwaadhibu kwa ajili ya jambo hili?”

asema Bwana.

“Je, nisijilipizie kisasi

kwa taifa kama hili?”

109:10 Hos 4:3; Yoe 1:18; Yer 31:35; 32:18; 23:10; 4:25; 12:4Nitalia na kuomboleza kwa ajili ya milima

na kuomboleza kuhusu malisho ya jangwani.

Yamekuwa ukiwa, wala hakuna apitaye humo,

milio ya ngʼombe haisikiki.

Ndege wa angani wametoroka

na wanyama wamekimbia.

119:11 Ay 30:29; Isa 34:13; Law 26:31; Mao 1:4; Yer 26:18; Isa 25:2“Nitaifanya Yerusalemu lundo la magofu,

makao ya mbweha;

nami nitaifanya miji ya Yuda kuwa ukiwa

ili asiwepo atakayeishi humo.”

129:12 Za 107:43; Hos 14:9Ni mtu yupi aliye na hekima ya kutosha ayaelewe haya? Ni nani aliyefundishwa na Bwana awezaye kuyaeleza haya? Kwa nini nchi imeharibiwa na kufanywa ukiwa kama jangwa ambapo hakuna awezaye kupita?

139:13 2Nya 7:19; Za 89:30-32Bwana akasema, “Ni kwa sababu wameiacha sheria yangu, niliyoiweka mbele yao: hawajaniheshimu mimi wala kufuata sheria yangu. 149:14 Amo 2:4; Yer 3:17; 7:24; 2:8Badala yake wamefuata ukaidi wa mioyo yao, wamefuata Mabaali, kama vile baba zao walivyowafundisha.” 159:15 Mao 3:15; Yer 8:14; Za 80:5Kwa hiyo, hivi ndivyo asemavyo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli: “Tazama, nitawafanya watu hawa wale chakula kichungu na kunywa maji yenye sumu. 169:16 Law 26:33; Kum 28:64; 4:32; Eze 5:12; Yer 44:27; 8:19Nitawatawanya katika mataifa ambayo wao wala baba zao hawakuwajua, nikiwafuata kwa upanga mpaka niwe nimewaangamiza kabisa.”

179:17 2Nya 35:25; Amo 5:15-16; Mhu 12:5Hivi ndivyo asemavyo Bwana Mwenye Nguvu Zote:

“Fikiri sasa! Waite wanawake waombolezao waje,

waite wale walio na ustadi kuliko wote.

189:18 Za 119:136; Mao 3:48; Yer 14:17Nao waje upesi

na kutuombolezea,

mpaka macho yetu yafurike machozi

na vijito vya maji vitoke kwenye kope zetu.

199:19 Law 18:29; Yer 4:13Sauti ya kuomboleza imesikika kutoka Sayuni:

‘Tazama jinsi tulivyoangamizwa!

Tazama jinsi aibu yetu ilivyo kubwa!

Ni lazima tuihame nchi yetu

kwa sababu nyumba zetu zimekuwa magofu.’ ”

209:20 Isa 32:9-13; Yer 23:16Basi, enyi wanawake, sikieni neno la Bwana;

fungueni masikio yenu msikie maneno ya kinywa chake.

Wafundisheni binti zenu kuomboleza;

fundishaneni kila mmoja na mwenzake maombolezo.

219:21 2Nya 36:17; Isa 40:30; Yoe 2:9; Yer 16:6Mauti imeingia ndani kupitia madirishani,

imeingia kwenye majumba yetu ya fahari;

imewakatilia mbali watoto katika barabara

na vijana waume kutoka viwanja vya miji.

229:22 2Fal 9:37; Yer 8:2Sema, “Hili ndilo asemalo Bwana:

“ ‘Maiti za wanaume zitalala

kama mavi katika mashamba,

kama malundo ya nafaka nyuma ya mvunaji,

wala hakuna anayekusanya.’ ”

239:23 Ay 4:12; Isa 5:21; Mhu 9:11; Za 62:10; 1Fal 20:11; Mit 11:28; Eze 28:4-5; Yer 48:7Hili ndilo asemalo Bwana:

“Mwenye hekima asijisifu katika hekima yake,

au mwenye nguvu ajisifu katika nguvu zake,

wala tajiri ajisifu katika utajiri wake,

249:24 Gal 6:14; 2Kor 10:17; Za 34:2; Mik 6:8; Za 36:6; 1Kor 1:31lakini yeye ajisifuye, na ajisifu kwa sababu hili:

kwamba ananifahamu na kunijua mimi,

kwamba mimi ndimi Bwana, nitendaye wema,

hukumu na haki duniani,

kwa kuwa napendezwa na haya,”

asema Bwana.

259:25 Law 26:41; Rum 2:8-9; Amo 3:2“Siku zinakuja, nitakapowaadhibu wale wote ambao wametahiriwa kimwili tu, asema Bwana, 269:26 Yer 25:23; 49:32; Mdo 7:51; Rum 2:28; Eze 31:18; 1Sam 14:6yaani Misri, Yuda, Edomu, Amoni, Moabu na wote wanaoishi jangwani sehemu za mbali. Kwa maana mataifa haya yote hayakutahiriwa mioyo yao, nayo nyumba yote ya Israeli haikutahiriwa.”

Het Boek

Jeremia 9:1-26

Verdriet om het volk

1Ik wilde wel dat mijn ogen fonteinen van tranen waren, dan zou ik dag en nacht huilen om de gesneuvelden van mijn volk!

2Och, kon ik maar weggaan, hen vergeten en in een hut in de woestijn gaan wonen, want het zijn allemaal echtbrekers en verraders. 3‘Zij buigen hun tongen als bogen om hun leugens als pijlen weg te schieten. Zij besturen het land onrechtvaardig en gaan van kwaad tot erger, zij geven niets om Mij,’ zegt de Here. 4‘Pas op voor uw buurman! Kijk uit voor uw broer! Zij geven niets om een ander en verspreiden gemene leugens. 5De ene vriend bedriegt de andere. Met geoefende tong leiden zij elkaar met leugens om de tuin en zij vermoeien zichzelf met al hun zonden. 6Zij bouwen hun huis op bedrog en weigeren Mij te erkennen,’ zegt de Here. 7Daarom zegt de Here van de hemelse legers: ‘Kijk, Ik zal hen smelten en hen zuiveren en testen als metaal. Wat kan Ik anders met hen doen? 8Want hun tongen zijn net dodelijke speren. Zij praten vriendelijk met hun naasten, terwijl zij van plan zijn hen te doden. 9Moet Ik hen voor zulke dingen niet straffen?’ vraagt de Here. ‘Moet Ik Mij niet wreken op een volk als dit? 10Treurend en huilend kijk Ik naar de bergen en weilanden, want die liggen er verlaten bij. Er is geen levende ziel meer te bekennen. Weg is het geloei van het vee, weg zijn de vogels en de wilde dieren. Ze zijn allemaal gevlucht. 11Ik zal van Jeruzalem één grote steenhoop maken, een schuilplaats voor de jakhalzen. De steden van Juda zullen er verlaten en levenloos bijliggen.’

12Wie is wijs genoeg om dit alles te begrijpen? Waar is Gods vertrouweling die dit allemaal kan uitleggen? Waarom is het land één wildernis waar niemand doorheen durft te reizen? 13‘Omdat,’ antwoordt de Here, ‘mijn volk mijn geboden heeft verlaten en mijn wetten niet heeft nageleefd. 14Ze deden hun eigen zin en vereerden verschillende afgoden, zoals de vaders hun kinderen leerden.’ 15Daarom zegt de Here, de God van Israël: ‘Kijk, Ik zal hun bitter voedsel te eten en vergif te drinken geven. 16Ik zal hen over de hele wereld verspreiden zodat zij vreemdelingen zijn in verre landen, en Ik zal hen met het zwaard achtervolgen tot Ik hen volledig heb vernietigd.’ 17-18 De Here van de hemelse legers zegt: ‘Snel, haal klaagvrouwen hier! Begin snel met uw rouwklachten, zodat onze tranen stromen. 19Hoor hoe Jeruzalem vertwijfeld huilt.’ Dit is het einde! Wat een schande! Wij moeten onze huizen en ons land verlaten, alles is totaal vernield! 20Luister naar de woorden van God, treurende vrouwen. Leer uw dochters te rouwen en leer het ook elkaar. 21Want door de ramen is de dood onze huizen binnengeslopen. Hij heeft de jeugd laten sterven, de kinderen op straat en de jonge mannen op de pleinen. 22‘Vertel hun dit,’ zegt de Here: ‘Lijken liggen als mest over de akkers verspreid, als schoven achter de maaier en niemand zal ze verzamelen.’

23De Here zegt: ‘Laat de wijze man niet pochen op zijn wijsheid, de sterke niet op zijn kracht en de rijke niet op zijn rijkdom. 24Laten zij zich er alleen op beroemen dat zij Mij werkelijk kennen. Dat zij weten dat Ik de Here ben, een God van liefde die de aarde rechtvaardig regeert, want in deze dingen heb Ik genoegen.’

25-26 ‘Er komt een tijd,’ zegt de Here, ‘dat Ik allen zal straffen die wel lichamelijk, maar niet geestelijk zijn besneden, de Egyptenaren, Edomieten, Ammonieten, Moabieten, Arabieren en ja, zelfs u, het volk van Juda. Want alle heidense volken zijn onbesneden. Maar, Israël, als u uw harten niet besnijdt door van Mij te houden, dan bent u in wezen aan hen gelijk.’