Yeremia 4 – Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) NEN

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Yeremia 4:1-31

14:1 Yoe 2:12; Ezr 8:5; 2Fal 7:13; 21:4; Kum 4:30; Hos 12:6; Yer 16:18; 35:15“Ikiwa utataka kurudi, ee Israeli,

nirudie mimi,”

asema Bwana.

“Ikiwa utaondoa sanamu zako za kuchukiza mbele ya macho yangu

na usiendelee kutangatanga,

24:2 Kum 10:20; Hes 14:21; Gal 3:8; Hos 4:15; Mwa 12:2; Isa 19:18; 65:16; Yer 12:16ikiwa kwa kweli, kwa haki na kwa unyofu utaapa,

‘Kwa hakika kama vile Bwana aishivyo,’

ndipo mataifa yatakapobarikiwa naye

na katika yeye watajitukuza.”

34:3 Hos 10:12; Mk 4:18Hili ndilo asemalo Bwana kwa watu wa Yuda na kwa Yerusalemu:

“Vunjeni mabonge kwenye mashamba yenu,

wala msipande katikati ya miiba.

44:4 Law 26:41; Rum 2:28-29; Sef 2:2; Amo 5:6; Ay 41:21; Kut 32:22; Yer 8:14; Yos 10:20; Yer 5:20; Hes 10:2-7; Ay 39:24Jitahirini katika Bwana,

tahirini mioyo yenu,

enyi wanaume wa Yuda

na watu wa Yerusalemu,

la sivyo ghadhabu yangu itatoka kwa nguvu

na kuwaka kama moto

kwa sababu ya uovu mliotenda,

ikiwaka pasipo wa kuizima.

Maafa Kutoka Kaskazini

5“Tangaza katika Yuda na upige mbiu katika Yerusalemu na kusema:

‘Piga tarumbeta katika nchi yote!’

Piga kelele na kusema:

‘Kusanyikeni pamoja!

Tukimbilie katika miji yenye maboma!’

64:6 Yer 1:13-15; Isa 14:31; Za 74:4; Isa 31:9; Yer 50:2; 11:11; 18:11Onyesheni ishara ili kwenda Sayuni!

Kimbilieni usalama pasipo kuchelewa!

Kwa kuwa ninaleta maafa kutoka kaskazini,

maangamizi ya kutisha.”

74:7 Dan 7:4; Eze 12:20; Yer 2:15; Isa 6:11; Yer 25:38; Hos 5:14; Nah 2:12; Yer 6:26Simba ametoka nje ya pango lake,

mharabu wa mataifa amejipanga.

Ametoka mahali pake

ili aangamize nchi yenu.

Miji yenu itakuwa magofu

pasipo mtu wa kuishi humo.

84:8 1Fal 21:27; Yer 30:24; Isa 22:12; 3:24; Yer 6:26; Eze 7:18; Yer 7:29; 9:20Hivyo vaeni nguo za magunia,

ombolezeni na kulia kwa huzuni,

kwa kuwa hasira kali ya Bwana

haijaondolewa kwetu.

9“Katika siku ile,” asema Bwana

“mfalme na maafisa watakata tamaa,

makuhani watafadhaika,

na manabii watashangazwa mno.”

104:10 Eze 14:9; Kut 5:23; 2The 2:11; Isa 63:17; Yer 6:14; 8:11; Eze 13:10; Mik 3:5Ndipo niliposema, “Aa, Bwana Mwenyezi, umewadanganyaje kabisa watu hawa na Yerusalemu kwa kusema, ‘Mtakuwa na amani,’ wakati upanga uko kwenye koo zetu!”

114:11 Mwa 41:6; Hos 13:15; Eze 17:10; Law 26:33; Ay 1:19Wakati huo watu hawa na Yerusalemu wataambiwa, “Upepo wa moto kutoka miinuko iliyo kame katika jangwa unavuma kuelekea watu wangu, lakini sio kupepeta au kutakasa, 124:12 Isa 64:6; Yer 1:16upepo wenye nguvu sana kuliko wa kupepeta na kutakasa utakuja kwa amri yangu. Sasa natangaza hukumu zangu dhidi yao.”

134:13 Isa 5:28; 2Sam 22:10; Eze 26:10; Kum 28:49; Mao 4:19; Isa 66:15Tazama! Anakuja kama mawingu,

magari yake yanakuja kama upepo wa kisulisuli,

farasi wake wana mbio kuliko tai.

Ole wetu! Tunaangamia!

144:14 Rut 3; 3; Yak 4:8; Za 51:2; Isa 45:22; Za 6:3Ee Yerusalemu, usafishe uovu kutoka moyoni mwako na uokolewe.

Utaendelea kuficha mawazo mapotovu mpaka lini?

154:15 Yer 8:16; Mwa 30:6; Yer 31:6Sauti inatangaza kutoka Dani,

ikipiga mbiu ya maafa kutoka vilima vya Efraimu.

16“Waambie mataifa jambo hili,

piga mbiu hii dhidi ya Yerusalemu:

‘Jeshi la kuzingira linakuja kutoka nchi ya mbali,

likipiga kelele ya vita dhidi ya miji ya Yuda.

174:17 2Fal 25:1-4; 1Sam 12:15; Yer 5:23Wamemzunguka kama watu walindao shamba,

kwa sababu amefanya uasi dhidi yangu,’ ”

asema Bwana.

184:18 Za 107:17; Ay 20:6-11; Yer 2:17-19; Isa 1:28; Yer 5:25“Mwenendo wako na matendo yako mwenyewe

yameleta haya juu yako.

Hii ndiyo adhabu yako.

Tazama jinsi ilivyo chungu!

Tazama jinsi inavyochoma moyo!”

194:19 Isa 16:11; Mao 1:20; Hes 10:9; Yer 20:9; Sef 1:16; Isa 22:4; Yer 6:24Ee mtima wangu, mtima wangu!

Ninagaagaa kwa maumivu.

Ee maumivu makuu ya moyo wangu!

Moyo wangu umefadhaika ndani yangu,

siwezi kunyamaza.

Kwa sababu nimesikia sauti ya tarumbeta,

nimesikia kelele ya vita.

204:20 Kum 31:17; Za 42:7; Hes 24:5; Mao 2:4; Yer 10:20Maafa baada ya maafa,

nchi yote imekuwa magofu.

Kwa ghafula mahema yangu yameangamizwa,

makazi yangu kwa muda mfupi.

214:21 Hes 2:2; Isa 18:3; Yos 6:20; Hos 5:8Hata lini nitaendelea kuona bendera ya vita

na kusikia sauti za tarumbeta?

224:22 1Kor 14:20; Yer 5:21; 13:23; Za 36:3; Rum 16:19; Yer 5:21; 10:8; Za 14:4“Watu wangu ni wapumbavu,

hawanijui mimi.

Ni watoto wasio na akili,

hawana ufahamu.

Ni hodari kutenda mabaya,

hawajui kutenda yaliyo mema.”

234:23 Ay 9:7; 30:26; Isa 5:30; 59:9; Mao 3:2Niliitazama dunia,

nayo haikuwa na umbo tena ni tupu;

niliziangalia mbingu,

mianga ilikuwa imetoweka.

244:24 Eze 38:20; Ay 9:6; Isa 5:25; Kut 19:18Niliitazama milima, nayo ilikuwa ikitetemeka,

vilima vyote vilikuwa vikiyumbayumba.

254:25 Hos 4:3; Sef 1:3; Yer 7:20Nilitazama, wala watu hawakuwepo;

kila ndege wa angani alikuwa ameruka zake.

26Nilitazama, hata nchi iliyokuwa imestawi vizuri imekuwa jangwa,

miji yake yote ilikuwa magofu

mbele za Bwana,

mbele ya hasira yake kali.

274:27 Amo 9:8; Yer 5:10; 12:12; Eze 20:17; Yer 46:28Hivi ndivyo Bwana asemavyo:

“Nchi yote itaharibiwa,

ingawa sitaiangamiza kabisa.

284:28 Yer 14:2; Hos 4:3; Hes 23:19; Isa 5:30; Yer 30:24; 23:20; 12:4-11Kwa hiyo dunia itaomboleza

na mbingu zilizo juu zitakuwa giza,

kwa sababu nimesema nami sitarudi nyuma,

nimeamua na wala sitageuka.”

294:29 Yer 8:16; Isa 6:12; 2Fal 25:4; Yer 6:23; 1Sam 26:20; Kut 33:22Kwa sauti ya wapanda farasi na wapiga upinde

kila mji unakimbia.

Baadhi wanakimbilia vichakani,

baadhi wanapanda juu ya miamba.

Miji yote imeachwa,

hakuna aishiye ndani yake.

304:30 Isa 10:3-4; Eze 16:11; 23:40; 2Fal 9:30; Ay 19:14; Eze 23:9; Za 35:4Unafanya nini, ewe uliyeharibiwa?

Kwa nini unajivika vazi jekundu

na kuvaa vito vya dhahabu?

Kwa nini unapaka macho yako rangi?

Unajipamba bure.

Wapenzi wako wanakudharau,

wanautafuta uhai wako.

314:31 Mwa 3:16; Mik 4:10; Isa 42:14; Mao 1:17; Yer 6:24; 13:21; 22:23; Za 9:14; Isa 42:14; Kum 32:25; Mao 2:21Nasikia kilio kama cha mwanamke

katika utungu wa kuzaa,

kilio cha uchungu kama cha anayemzaa

mtoto wake wa kwanza:

kilio cha Binti Sayuni akitweta ili aweze kupumua,

akiinua mikono yake, akisema,

“Ole wangu! Ninazimia;

maisha yangu yamekabidhiwa kwa wauaji.”