Yeremia 36 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Yeremia 36:1-32

Yehoyakimu Achoma Kitabu Cha Yeremia

136:1 2Nya 36:5Katika mwaka wa nne wa Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda, neno hili lilimjia nabii Yeremia kutoka kwa Bwana, kusema: 236:2 Yer 25:3; Za 40:7; Hab 2:2; Kut 17:14; Eze 2:7; 25:3“Chukua kitabu uandike ndani yake maneno yote niliyonena nawe kuhusu Israeli, Yuda na mataifa mengine yote, tangu nilipoanza kunena nawe wakati wa utawala wa Yosia hadi sasa. 336:3 Eze 12:3; Amo 5:15; Isa 6:9; Yer 18:8; Mdo 3:19; Yn 3:8; Mk 14:8; Mdo 26:20; Mk 4:12; 2Fal 17:13Labda watu wa Yuda watakaposikia juu ya kila maafa ninayokusudia kuwapiga nayo, kila mmoja wao atageuka kutoka njia zake mbaya, kisha nitasamehe uovu wao na dhambi yao.”

436:4 Yer 32:12; Zek 5:1; Yer 45; 1; Eze 2:9; Yer 51:59Hivyo Yeremia akamwita Baruku mwana wa Neria, naye Yeremia alipokuwa akiyakariri maneno yote aliyoyasema Bwana, Baruku akayaandika katika kitabu. 5Kisha Yeremia akamwambia Baruku, “Nimezuiliwa, mimi siwezi kuingia katika Hekalu la Bwana. 636:6 Kut 4:16; 2Nya 20:4Basi wewe nenda katika nyumba ya Bwana siku ya kufunga, uwasomee watu maneno ya Bwana kutoka kitabu hiki yale uliyoyaandika kutoka kinywani mwangu. Wasomee watu wote wa Yuda waliofika kutoka miji yao. 736:7 Yer 26:3; Kum 31:17; 29:18; Yer 37:20Labda wataomba na kusihi mbele za Bwana na kila mmoja akageuka kutoka njia zake mbaya, kwa sababu hasira na ghadhabu zilizotamkwa dhidi ya watu hawa na Bwana ni kubwa.”

8Baruku mwana wa Neria akafanya kila kitu nabii Yeremia alichomwambia kufanya. Alisoma maneno ya Bwana katika Hekalu la Bwana kutoka kile kitabu. 936:9 2Nya 20:3; Amu 20:26Katika mwezi wa tisa, mnamo mwaka wa tano wa Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda, wakati wa kufunga mbele za Bwana, ilitangazwa kwa watu wote walioko Yerusalemu, na wale wote waliokuwa wamekuja kutoka miji ya Yuda. 1036:10 Yer 52:25; Mwa 23:10; Yer 26:10; 29:3; 26:24Kutoka chumba cha Gemaria mwana wa Shafani mwandishi, kilichokuwa katika ua wa juu kwenye ingilio la Lango Jipya la Hekalu, Baruku akawasomea watu wote waliokuwa katika Hekalu la Bwana maneno ya Yeremia kutoka kwenye kile kitabu.

11Basi Mikaya mwana wa Gemaria, mwana wa Shafani, aliposikia maneno yote ya Bwana kutoka kwenye kile kitabu, 1236:12 Yer 26:22; 2Sam 8:17; Yer 38:4alishuka hadi kwenye chumba cha mwandishi kwenye jumba la kifalme, mahali walipokuwa wameketi maafisa wote: yaani Elishama mwandishi, Delaya mwana wa Shemaya, Elnathani mwana wa Akbori, Gemaria mwana wa Shafani, Sedekia mwana wa Hanania, na maafisa wengine wote. 13Baada ya Mikaya kuwaambia kila kitu ambacho alikuwa amesikia Baruku akiwasomea watu kutoka kwenye kile kitabu, 14maafisa wote wakamtuma Yehudi mwana wa Nethania, mwana wa Shelemia, mwana wa Kushi, kumwambia Baruku, “Leta hicho kitabu ambacho umewasomea watu, nawe mwenyewe uje.” Ndipo Baruku mwana wa Neria akawaendea akiwa na hicho kitabu mkononi mwake. 15Wakamwambia, “Tafadhali, keti na utusomee hicho kitabu.”

Ndipo Baruku akawasomea kile kitabu. 16Walipoyasikia maneno hayo yote, wakatazamana wao kwa wao kwa woga na kumwambia Baruku, “Lazima tutoe taarifa ya maneno haya yote kwa mfalme.” 17Kisha wakamuuliza Baruku, “Tuambie, uliandikaje haya yote? Je, yalitoka kinywani mwa Yeremia?”

1836:18 Isa 8:12; Mt 10:16-32; 1Pet 3:14-15Baruku akajibu, “Ndiyo, maneno haya yote yalitoka kinywani mwa Yeremia, nami nikayaandika kwa wino katika hiki kitabu.”

1936:19 1Fal 17:3; Yer 26:16Ndipo wale maafisa wakamwambia Baruku, “Wewe na Yeremia nendeni mkajifiche. Mtu yeyote asijue mahali mlipo.”

20Baada ya kuhifadhi kile kitabu ndani ya chumba cha Elishama mwandishi, wakamwendea mfalme katika ua wa nje na kumwarifu kila kitu. 2136:21 2Fal 22:10Mfalme akamtuma Yehudi akachukue kile kitabu. Yehudi akakileta hicho kitabu kutoka kwenye chumba cha Elishama mwandishi, na akakisoma mbele ya mfalme na maafisa wakiwa wamesimama kando ya mfalme. 2236:22 Amo 3:15; Amu 3:20Ulikuwa mwezi wa tisa, na mfalme alikuwa ameketi chumba cha wakati wa baridi akiota moto. 2336:23 1Fal 22:8; 2Tim 4:3Hata ikawa kila wakati Yehudi alipomaliza kusoma kurasa tatu au nne za hicho kitabu, mfalme alizikata kwa kisu cha mwandishi na kuzitupia motoni, hadi kitabu chote kikateketea. 2436:24 Hes 14:6; 2Fal 22:11; Isa 36:22; Mwa 37:29Mfalme na watumishi wake wote waliosikia yote yaliyosomwa hawakuonyesha hofu yoyote, wala hawakuyararua mavazi yao. 2536:25 Mwa 37:26; Rum 8:34Hata ingawa Elnathani, Delaya na Gemaria walimsihi mfalme asikichome kile kitabu, yeye hakuwasikiliza. 2636:26 Mt 23:34; 1Fal 17:3; Za 11:1Badala yake, mfalme akamwamuru Yerameeli, mwana wa mfalme, Seraya mwana wa Azrieli, na Shelemia mwana wa Abdeeli kuwakamata mwandishi Baruku na nabii Yeremia. Lakini Bwana alikuwa amewaficha.

27Baada ya mfalme kuchoma kile kitabu kilichokuwa na yale maneno Baruku aliyokuwa ameyaandika kutoka kinywani mwa Yeremia, neno la Bwana lilimjia Yeremia likisema: 28“Chukua kitabu kingine na uandike juu yake maneno yote yaliyokuwa katika kile kitabu cha kwanza, ambacho Yehoyakimu mfalme wa Yuda amekiteketeza kwa moto. 2936:29 Isa 30:10; Amo 5:10; Yer 33:12Mwambie pia Yehoyakimu mfalme wa Yuda, ‘Hili ndilo asemalo Bwana: Ulikiteketeza kile kitabu ukasema, “Kwa nini uliandika kwenye kitabu kwamba kwa hakika mfalme wa Babeli angekuja na kuangamiza nchi hii, na kuwakatilia mbali watu na wanyama kutoka humo?” 3036:30 Isa 14:19; Yer 22:19; 52:2; 8:2; 2Fal 24:6Kwa hiyo, hili ndilo asemalo Bwana kuhusu Yehoyakimu mfalme wa Yuda: Hatakuwa na mtu yeyote atakayekalia kiti cha enzi cha Daudi; maiti yake itatupwa nje kwenye joto wakati wa mchana na kupigwa na baridi wakati wa usiku. 3136:31 Kut 20:5; Mit 29:1; 1:24Nitamwadhibu yeye, watoto wake na watumishi wake kwa ajili ya uovu wao. Nitaleta juu yao na wote waishio Yerusalemu na watu wa Yuda kila maafa niliyoyasema dhidi yao, kwa sababu hawajasikiliza.’ ”

3236:32 Kut 34:1; Yer 30:2; Kut 4:15; Rum 16:22Kisha Yeremia akachukua kitabu kingine na kumpa mwandishi Baruku mwana wa Neria, naye kama Yeremia alivyosema, Baruku akaandika juu yake maneno yote ya kile kitabu ambacho Yehoyakimu mfalme wa Yuda alikuwa amekichoma moto, na maneno mengine mengi yaliyofanana na hayo yaliyoongezewa humo.

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

耶利米書 36:1-32

耶利米的書卷被焚毀

1猶大約西亞的兒子約雅敬執政第四年,耶和華對耶利米說: 2「你拿一個卷軸來,把從約西亞登基直到現在我告訴你有關以色列猶大和各國的事都寫在上面。 3或許猶大人聽了我打算要降給他們的災禍,便改邪歸正,我就赦免他們的過犯和罪惡。」 4耶利米就叫來尼利亞的兒子巴錄巴錄耶利米的口述把耶和華的話寫在卷軸上, 5耶利米對他說:「我被囚禁,不能進入耶和華的殿, 6所以你要在禁食的日子,在耶和華的殿中向猶大各城來的人宣讀卷軸上耶和華的話。 7或許他們會改邪歸正,懇求耶和華赦罪,因為耶和華說要向他們發烈怒。」 8尼利亞的兒子巴錄耶利米先知的吩咐,在耶和華的殿中宣讀卷軸上耶和華的話。

9猶大約西亞的兒子約雅敬執政第五年九月,耶路撒冷猶大各城的人都在耶和華面前宣告禁食。 10巴錄來到耶和華殿新門入口處的上院,在沙番的兒子書記基瑪利雅的房間,向眾人宣讀耶利米寫在卷軸上的話。 11沙番的孫子、基瑪利雅的兒子米該亞聽了卷軸上耶和華的話, 12就下到王宮,進入書記的房間。房間內坐著所有官長,即書記以利沙瑪示瑪雅的兒子第萊雅亞革波的兒子以利拿單沙番的兒子基瑪利雅哈拿尼雅的兒子西底迦等人。 13米該亞巴錄向眾人宣讀的話都告訴了他們。 14眾官長就派古示的曾孫、示利米雅的孫子、尼探雅的兒子猶底去請巴錄把當眾宣讀的卷軸拿來。巴錄拿著卷軸到他們那裡, 15他們請他坐下,把卷軸讀給他們聽。巴錄就讀給他們聽。 16他們聽後嚇得面面相覷,對巴錄說:「我們必須把這些話稟告王! 17請告訴我們,你是怎麼寫下這些話的?是耶利米口授的嗎?」 18巴錄說:「是耶利米口授、我記錄在卷軸上的。」 19他們說:「你和耶利米都要藏起來,不可讓人知道你們在哪裡。」

20他們把卷軸存放在書記以利沙瑪的房間,然後進宮把這件事稟告王。 21王就派猶底去把卷軸取來,猶底便從書記以利沙瑪的房間取來卷軸,讀給王和侍立在王周圍的官長聽。 22那時正是九月,王坐在冬宮,面前擺著一盆炭火。 23-24王和臣僕聽了這些話,既不懼怕,也沒有撕裂衣服。猶底每讀三四段,王就用書記的小刀把那幾段割下來扔進火盆裡,直到全卷被燒毀。 25雖然以利拿單第萊雅基瑪利雅懇求王不要把卷軸燒掉,王卻不聽, 26還命令自己的兒子耶拉篾亞斯列的兒子西萊雅亞伯德的兒子示利米雅去拘捕書記巴錄耶利米先知。但耶和華把他們藏了起來。

27王把耶利米口述、巴錄記錄的卷軸燒掉後,耶和華對耶利米說: 28「你再拿一卷軸,把猶大約雅敬先前燒毀的卷軸上的話寫下來。 29論到猶大約雅敬,你要這樣寫,『耶和華說,你把卷軸燒掉,還說為什麼上面寫著巴比倫王必來毀滅這地方和其中的人畜。 30所以耶和華說,猶大約雅敬啊,你的子孫沒有一人能登大衛的寶座,你的屍體必被棄之荒野,遭受烈日的暴曬和夜霜的侵襲。 31我要因你、你後裔和你臣僕的罪惡而懲罰你們。因為你們不聽我的警告,我要給你們以及耶路撒冷猶大的居民降下我說過的災禍。』」

32於是,耶利米又拿了一個卷軸,交給尼利亞的兒子書記巴錄,他按耶利米的口述,把猶大約雅敬燒毀的那卷軸上的話都記下來,還增添了許多類似的話。