Yeremia 33 – Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) NEN

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Yeremia 33:1-26

Ahadi Ya Kurudishwa

133:1 Yer 32:2; 37:21; 38:28; Za 88:8; Yer 13:3Wakati Yeremia alipokuwa angali amefungwa kwenye ua wa walinzi, neno la Bwana lilimjia mara ya pili kusema: 233:2 Yer 10:16; Za 136:6; Kut 3:15; 15:3“Hili ndilo Bwana asemalo, yeye aliyeumba dunia, Bwana aliyeifanya na kuithibitisha, Bwana ndilo jina lake: 333:3 Mwa 18:17; Yer 29:12; Isa 55:6; Ay 28:11‘Niite nami nitakuitika na kukuambia mambo makuu na yasiyochunguzika, usiyoyajua.’ 433:4 2Fal 25:1; Eze 4:2; 26:8; Hab 1:10; Yer 32:24Kwa maana hili ndilo Bwana, Mungu wa Israeli, asemalo kuhusu nyumba katika mji huu na majumba ya kifalme ya Yuda yaliyobomolewa ili yatumiwe dhidi ya kule kuzungukwa na jeshi na upanga 533:5 Yer 21:4-7; Kum 31:17; Isa 8:17katika kupigana na Wakaldayo: ‘Zitajazwa na maiti za watu nitakaowachinja katika hasira na ghadhabu yangu. Nitauficha uso wangu kwa sababu ya maovu yake yote.

633:6 Kum 32:39; Isa 30:26; 9:6“ ‘Hata hivyo, nitauletea afya na uponyaji, nitawaponya watu wangu na kuwafanya wafurahie amani tele na salama. 733:7 Yer 32:44; Eze 39:25; Amo 9:14; Isa 1:26; Yer 24:6; 30:3Nitawarudisha Yuda na Israeli kutoka nchi ya kutekwa kwao, na kuwajenga tena kama walivyokuwa hapo awali. 833:8 Law 16:30; Ebr 9:13-14; 2Sam 24:14; Mik 7:18; Yer 31:34Nitawatakasa dhambi zote walizofanya dhidi yangu, na nitawasamehe dhambi zote za uasi dhidi yangu. 933:9 Isa 60:18; Yer 13:11; Isa 64:2; Yer 3:17; 1Yn 1:7-9; Isa 55:13Kisha mji huu utaniletea utukufu, furaha, sifa na heshima mbele ya mataifa yote ya dunia yatakayosikia mambo yote mazuri ninayoufanyia. Nao watashangaa na kutetemeka kwa ajili ya wingi wa mafanikio na amani nitakayoupatia.’

1033:10 Yer 32:43; 9:11“Hili ndilo asemalo Bwana: ‘Mnasema kuhusu mahali hapa kwamba, “Ni mahali palipoachwa ukiwa, pasipo na wanadamu wala wanyama.” Lakini katika miji ya Yuda na barabara za Yerusalemu ambazo zimeachwa, ambazo hazikaliwi na wanadamu wala wanyama, huko kutasikika kwa mara nyingine 1133:11 Za 51:8; 24:8; Law 7:12; 2Nya 5:13; Za 25:8; 100:4-5; 14:7sauti za shangwe na furaha, sauti za bibi na bwana arusi, na sauti za wale waletao sadaka za shukrani katika nyumba ya Bwana, wakisema,

“ ‘ “Mshukuruni Bwana Mwenye Nguvu Zote,

kwa maana Bwana ni mwema;

upendo wake wadumu milele.”

Kwa kuwa nitairudishia nchi baraka kama zilivyokuwa hapo awali,’ asema Bwana.

1233:12 Yer 32:43; Isa 65:10; Eze 34:11-15“Hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote: ‘Mahali hapa, ambapo ni ukiwa, pasipo na wanadamu wala wanyama: katika miji yake, patakuwepo tena malisho kwa ajili ya wachungaji kupumzisha makundi yao ya kondoo. 1333:13 Yer 32:43; Isa 65:10; Eze 34:11-15Katika miji ya nchi ya vilima, ya vilima vya magharibi na ya Negebu, katika nchi ya Benyamini, katika vijiji vinavyoizunguka Yerusalemu na katika miji ya Yuda, makundi ya kondoo yatapita tena chini ya mkono wa yeye ayahesabuye,’ asema Bwana.

1433:14 Kum 28:1-14; Yos 23:15; Yer 29:10“ ‘Siku zinakuja,’ asema Bwana, ‘wakati nitakapotimiza ahadi yangu ya rehema niliyoifanya kwa nyumba ya Israeli na kwa nyumba ya Yuda.

1533:15 Isa 4:2; Za 72:2; Isa 11:1; 2Sam 7:12“ ‘Katika siku hizo na wakati huo

nitalifanya Tawi la haki lichipuke kutoka ukoo wa Daudi,

naye atafanya lile lililo haki na sawa

katika nchi.

1633:16 Isa 45:17; 1Kor 1:30; Zek 8:3, 16; Sef 3:13; Eze 48:35; Yer 3:17; Isa 59:14; Yer 32:37Katika siku hizo, Yuda ataokolewa

na Yerusalemu ataishi salama.

Hili ndilo jina atakaloitwa:

Bwana Haki Yetu.’

1733:17 2Sam 7:13; 2Nya 7:18; Za 89:29-37Kwa maana hili ndilo asemalo Bwana: ‘Daudi kamwe hatakosa mtu wa kukalia kiti cha enzi cha nyumba ya Israeli, 1833:18 Kum 18:1; Ebr 13:15; Hes 25:11-13; Ebr 7:17-22wala hata makuhani, ambao ni Walawi, kamwe hawatakosa mtu wa kusimama mbele zangu daima ili kutoa sadaka za kuteketezwa, ili kuteketeza sadaka ya nafaka na kutoa dhabihu.’ ”

19Neno la Bwana likamjia Yeremia kusema: 2033:20 Za 89:36; Mwa 8:22; Isa 54:9; Mwa 1:14“Hili ndilo asemalo Bwana: ‘Ikiwa mtaweza kuvunja agano langu kuhusu usiku na mchana, ili usiku na mchana visiwepo kwa nyakati zake, 2133:21 Za 89:34; 2Sam 7:13-18; 2Nya 7:18basi agano langu na Daudi mtumishi wangu, na agano langu na Walawi ambao ni makuhani wanaohudumu mbele zangu, linaweza kuvunjwa, na Daudi hatakuwa tena na mzao wa kutawala katika kiti chake cha enzi. 2233:22 Mwa 15:5; Hos 1:10; Mwa 13:16; Yer 30:19; Mwa 12:2Nitawafanya wazao wa Daudi mtumishi wangu na Walawi wanaohudumu mbele zangu wengi, wasioweza kuhesabika kama nyota za angani, tena wasiopimika kama mchanga wa ufuoni mwa bahari.’ ”

23Neno la Bwana likamjia Yeremia kusema: 2433:24 Eze 37:22; Neh 4:4; Yer 30:17; Eze 36:20“Je, hujasikia kwamba watu hawa wanasema, ‘Bwana amezikataa zile falme mbili alizozichagua?’ Kwa hiyo wamewadharau watu wangu, na hawawaoni tena kama taifa. 2533:25 Mwa 1:18; Yer 31:35-36; Za 74:16-17; 148:6Hili ndilo asemalo Bwana: ‘Kama sijathibitisha agano langu na usiku na mchana, na kuziweka wakfu sheria za mbingu na nchi, 2633:26 Law 26:44; Yer 31:37; Isa 14:1; Zek 10:6; Za 14:7; Yer 30:18basi nitawakataa wazao wa Yakobo na Daudi mtumishi wangu, na sitachagua mmoja wa wanawe kutawala juu ya wazao wa Abrahamu, Isaki na Yakobo. Kwa maana nitawarudisha kutoka nchi ya kutekwa kwao na kuwaonea huruma.’ ”