Yeremia 31 – Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) NEN

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Yeremia 31:1-40

Mahamisho Kurudi Kwa Shangwe

131:1 Law 26:12; Yer 30:22“Wakati huo, nitakuwa Mungu wa koo zote za Israeli nao watakuwa watu wangu,” asema Bwana.

231:2 Hes 14:20; Kut 33:14; Kum 12:9Hili ndilo asemalo Bwana:

“Watu watakaopona upanga

watapata upendeleo jangwani;

nitakuja niwape Israeli pumziko.”

331:3 Rum 11:28; Kum 4:37; Hos 11:4; Yn 6:44Bwana alitutokea wakati uliopita, akisema:

“Nimekupenda kwa upendo wa milele,

nimekuvuta kwa wema.

431:4 Yer 30:18-19; 2Fal 19:21; Mwa 31:27; Kut 15:20; Yer 30:19Nitakujenga tena nawe utajengeka upya,

ewe Bikira Israeli.

Utachukua tena matari yako

na kwenda kucheza na wenye furaha.

531:5 Yer 33:13; Oba 1:19; Isa 65:12; Amo 9:14; Kum 20:6; Yer 50:19; Isa 37:30Utapanda tena shamba la mizabibu

juu ya vilima vya Samaria,

wakulima watapanda

na kufurahia matunda yake.

631:6 Kum 33:19; Mik 4:2; Isa 52:8; 56:10; Yer 50:4-5Itakuja siku wakati walinzi watakapowapigia kelele

juu ya vilima vya Efraimu wakisema,

‘Njooni, twendeni juu Sayuni,

kwake Bwana Mungu wetu.’ ”

731:7 Kum 28:13; Isa 61:9; Za 14:7; 28:9; Isa 37:31; 12:6Hili ndilo asemalo Bwana:

“Mwimbieni Yakobo kwa furaha,

mpigieni kelele aliye mkuu wa mataifa.

Zifanyeni sifa zenu zisikike, nanyi mseme,

‘Ee Bwana, okoa watu wako,

mabaki ya Israeli.’

831:8 Yer 3:18; Mwa 33:13; Za 106:47; Isa 42:16; Eze 34:16; 34:12-14Tazama, nitawaleta kutoka nchi ya kaskazini

na kuwakusanya kutoka miisho ya dunia.

Miongoni mwao watakuwepo vipofu na viwete,

mama wajawazito na wenye utungu wa kuzaa.

Umati mkubwa wa watu utarudi.

931:9 Ezr 3:12; Za 126:5; Isa 63:13; Za 126:5; Isa 63:13; 40:4; 49:11; Kut 4:22; Hes 20:8Watakuja wakilia;

wataomba wakati ninawarudisha.

Nitawaongoza kando ya vijito vya maji

katika mapito yaliyo tambarare ambapo hawatajikwaa,

kwa sababu mimi ndimi baba wa Israeli,

naye Efraimu ni mzaliwa wangu wa kwanza.

1031:10 Isa 66:19; Kum 30:4; Isa 11:12; 40:11; Eze 34:12; Yer 25:22; Law 26:33“Sikieni neno la Bwana, enyi mataifa,

litangazeni katika nchi za pwani ya mbali:

‘Yeye aliyewatawanya Israeli atawakusanya

na atalichunga kundi lake la kondoo kama mchungaji.’

1131:11 Kut 6:6; Isa 44:23; Za 142:6; 9:16Kwa kuwa Bwana atamlipia fidia Yakobo

na kuwakomboa mkononi mwa walio na nguvu kuliko wao.

1231:12 Eze 40:2; Mik 4:1; Yoe 3:18; Hes 18:12; Hos 2:21-22; Wim 4:15; Yn 16:22; Isa 58:11; Wim 4:15; Isa 30:19Watakuja na kupiga kelele kwa furaha katika miinuko ya Sayuni;

watashangilia ukarimu wa Bwana:

nafaka, divai mpya na mafuta,

wana-kondoo wachanga

na ndama wa makundi ya ngʼombe nitakaowapa.

Watakuwa kama bustani iliyonyeshewa vizuri,

wala hawatahuzunika tena.

1331:13 Isa 61:3; Za 30:11; Isa 51:11Kisha wanawali watacheza na kufurahi,

vijana waume na wazee pia.

Nitageuza maombolezo yao kuwa furaha,

nitawapa faraja na furaha badala ya huzuni.

1431:14 Law 7:35-36; Za 36:8; Isa 30:23Nitawashibisha makuhani kwa wingi,

nao watu wangu watajazwa kwa ukarimu wangu,”

asema Bwana.

1531:15 Yos 18:25; Mwa 37:35; Yer 10:20; Mt 2:17-18; Ay 7:21Hili ndilo asemalo Bwana:

“Sauti imesikika huko Rama,

maombolezo na kilio kikubwa,

Raheli akiwalilia watoto wake

na anakataa kufarijiwa,

kwa sababu watoto wake hawako tena.”

1631:16 Za 30:5; Isa 25:8; Rut 2:12; Eze 11:17-18; 2Nya 15:7; Yer 30:3; Isa 30:19Hili ndilo asemalo Bwana:

“Izuie sauti yako kulia,

na macho yako yasitoe machozi,

kwa kuwa kazi yako itapata thawabu,”

asema Bwana.

“Watarudi kutoka nchi ya adui.

17Kwa hiyo kuna tumaini kwa siku zijazo,”

asema Bwana.

“Watoto wako watarudi nchi yao yenyewe.

1831:18 Ay 5:17; Hos 4:16; 10:11; Za 80:3-4; Mao 5:21; Yer 50:11“Hakika nimeyasikia maombolezo ya Efraimu:

‘Ulinirudi kama ndama mkaidi,

nami nimekubali kutii.

Unirudishe, nami nitarudi,

kwa sababu wewe ndiwe Bwana, Mungu wangu.

1931:19 Za 95:10; Eze 36:31; 21:12; Lk 18:13; Yer 8:4; Ezr 9:6; Za 25:7Baada ya kupotea, nilitubu;

baada ya kuelewa, nilijipiga kifua.

Niliaibika na kuona haya

kwa sababu niliibeba aibu ya ujana wangu.’

2031:20 Isa 44:21; Hos 4:4; Mik 7:18; 1Fal 3:26; Mao 3:33; Isa 55:7Je, Efraimu si mwanangu mpendwa,

mtoto ninayependezwa naye?

Ingawa mara kwa mara ninanena dhidi yake,

bado ninamkumbuka.

Kwa hiyo moyo wangu unamwonea shauku,

nina huruma kubwa kwa ajili yake,”

asema Bwana.

2131:21 Isa 35:8; Yer 50:5; Isa 52:11; Yer 3:12; Eze 21:19“Weka alama za barabara,

weka vibao vya kuelekeza.

Zingatia vyema njia kuu,

barabara ile unayoipita.

Rudi, ee Bikira Israeli,

rudi kwenye miji yako.

2231:22 Yer 2:23; Hos 4:16; Isa 43:19; Kum 32:10Utatangatanga hata lini,

ee binti usiye mwaminifu?

Bwana ameumba kitu kipya duniani:

mwanamke atamlinda mwanaume.”

2331:23 Yer 30:18; Isa 1:26; Zek 8:3; Mwa 28:3; Hes 6:24; Isa 2:2; Za 48:1Hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo, “Nitakapowarudisha toka nchi ya kutekwa kwenu, watu walio katika nchi ya Yuda na miji yake kwa mara nyingine tena watatumia maneno haya: ‘Bwana akubariki, ee makao ya haki, ee mlima mtakatifu.’ 2431:24 Yer 33:12, 18; Zek 8:4-8; Yer 30:18Watu wataishi pamoja katika Yuda na miji yake yote, wakulima na wote wanaohamahama na mifugo yao. 2531:25 Yn 4:14; Isa 40:29Nitawaburudisha waliochoka na kuwatuliza walio na huzuni.”

26Kwa jambo hili niliamka na kuangalia pande zote. Usingizi wangu ulikuwa mtamu kwangu.

2731:27 Eze 36:9-11; Hos 2:23; Yer 16:14Bwana asema, “Siku zinakuja, nitakapoongeza idadi ya watu, na kuzidisha hesabu ya mifugo katika nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda. 2831:28 Yer 18:8; 44:27; Kum 30; 9; Amo 9:14; Ay 29:2; Eze 36:10-11; Yer 1:10Kama vile nilivyowaangalia ili kungʼoa na kubomoa, kuharibu, kuangamiza na kuleta maafa juu yao, vivyo hivyo nitawaangalia ili kujenga na kupanda,” asema Bwana. 2931:29 Mwa 9:25; Kum 24:16; Eze 18:2; Mao 5:7“Katika siku hizo, watu hawatasema tena,

“ ‘Baba wamekula zabibu chachu,

nayo meno ya watoto yakatiwa ganzi.’

3031:30 2Fal 14:6; Gal 6:7; Isa 3:11Badala yake, kila mmoja atakufa kwa ajili ya dhambi zake mwenyewe; yeyote alaye zabibu chachu, meno yake mwenyewe yatatiwa ganzi.

3131:31 Kum 29:14; Ebr 8:8-12; Yer 33:14; Lk 22:20; Isa 42:6; 54:10; Ebr 10:16-17“Siku zinakuja,” asema Bwana,

“nitakapofanya agano jipya

na nyumba ya Israeli

na nyumba ya Yuda.

3231:32 Kut 24:8; Kum 5:3; 1:31; Yer 11:4; Isa 54:5Halitafanana na agano

nililofanya na baba zao

wakati nilipowashika mkono

kuwaongoza watoke Misri,

kwa sababu walivunja agano langu,

ijapokuwa nilikuwa mume kwao,”

asema Bwana.

3331:33 Kum 6:6; 2Kor 3:3; Yer 24:7; Ebr 10:16; Za 40:8; Kut 4:15“Hili ndilo agano nitakalofanya na nyumba ya Israeli

baada ya siku zile,” asema Bwana.

“Nitaweka sheria yangu katika nia zao,

na kuiandika mioyoni mwao.

Nitakuwa Mungu wao,

nao watakuwa watu wangu.

3431:34 1Yn 2:27; Yn 6:45; Isa 54:13; Za 85:2; Mik 7:19; Rum 11:27; Isa 11:9Mtu hatamfundisha tena jirani yake,

wala mtu kumfundisha ndugu yake akisema, ‘Mjue Bwana Mungu,’

kwa sababu wote watanijua mimi,

tangu aliye mdogo kabisa kwao, hadi aliye mkuu sana,”

asema Bwana.

“Kwa sababu nitasamehe uovu wao,

wala sitazikumbuka dhambi zao tena.”

3531:35 Za 136:7-9; Mwa 1; 16; Yer 10:16; Kut 14:21; Za 93:3Hili ndilo asemalo Bwana,

yeye aliyeweka jua

liwake mchana,

yeye anayeamuru mwezi na nyota

kungʼaa usiku,

yeye aichafuaye bahari

ili mawimbi yake yangurume;

Bwana Mwenye Nguvu Zote ndilo jina lake:

3631:36 Ay 38:33; Isa 54:9-10; Za 89:36-37; Yer 33:20-26“Ikiwa amri hizi zitaondoka machoni pangu,”

asema Bwana,

“ndipo wazao wa Israeli watakoma

kuwa taifa mbele yangu daima.”

3731:37 Ay 38:5; Yer 33:22, 24, 26; Rum 11:1-5Hili ndilo asemalo Bwana:

“Ikiwa mbingu zilizo juu zitaweza kupimika

na misingi ya dunia chini

ikaweza kuchunguzwa,

ndipo nitakapowakataa wazao wote wa Israeli

kwa sababu ya yote waliyoyatenda,”

asema Bwana.

3831:38 Yer 30:18; Neh 3:1; 2Nya 25:23; Zek 14:10; Yer 24:6; 2Fal 14:13“Siku zinakuja,” asema Bwana, “wakati mji huu utajengwa upya kwa ajili yangu, kuanzia mnara wa Hananeli hadi Lango la Pembeni. 3931:39 1Fal 7:23Kamba ya kupimia itaanzia hapo kuendelea hadi kwenye kilima cha Garebu, na kisha kugeuka kuelekea Goa. 4031:40 Yer 2:23; 7:31-32; 1Sam 15:23; Yn 18:1; 2Fal 11:16; Yoe 3:17; Zek 14:21Bonde lote watupwapo maiti na majivu pia na matuta yote kutoka Bonde la Kidroni upande wa mashariki hadi pembe ya Lango la Farasi, itakuwa takatifu kwa Bwana. Kamwe mji huu hautangʼolewa tena wala kubomolewa.”