Yakobo 5 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Yakobo 5:1-20

Onyo Kwa Matajiri

15:1 1Tim 6:9; Mit 11:28; Lk 6:24Basi sikilizeni, ninyi matajiri, lieni na kuomboleza kwa ajili ya hali mbaya sana inayowajia. 25:2 Za 39:11; Ay 13:22; Mt 6:20; Yak 2:2Utajiri wenu umeoza na mavazi yenu yameliwa na nondo. 3Dhahabu yenu na fedha yenu vimeliwa na kutu. Kutu yake itashuhudia dhidi yenu nayo itaila miili yenu kama vile moto. Mmejiwekea hazina kwa ajili ya siku za mwisho. 45:4 Mt 3:5; Kum 24:15; Rum 9:29Angalieni! Ule ujira wa vibarua waliolima mashamba yenu mliouzuia kwa hila unapiga kelele dhidi yenu na vilio vya wavunaji vimefika masikioni mwa Bwana Mwenye Nguvu Zote. 55:5 Yer 12:3; 25:34Mmeishi duniani kwa anasa na kwa starehe, mmejinenepesha tayari kwa siku ya kuchinjwa. 65:6 Mit 3:34; Yak 2:6; Ebr 10:38; Yak 4:2Mmewahukumu na kuwaua watu wenye haki, waliokuwa hawapingani nanyi.

Uvumilivu Katika Mateso

75:7 Yer 5:24; Yoe 2:23Kwa hiyo, ndugu zangu, vumilieni hadi kuja kwake Bwana. Angalieni jinsi mkulima angojavyo ardhi itoe mavuno yake yaliyo ya thamani na jinsi anavyovumilia kwa ajili ya kupata mvua za kwanza na za mwisho. 85:8 Rum 13:11; 1Pet 4:7Ninyi nanyi vumilieni, tena simameni imara, kwa sababu kuja kwa Bwana kumekaribia. 95:9 Yak 4:11; Za 94:2; 1Kor 4:5; Mt 24:33Ndugu zangu, msinungʼunikiane msije mkahukumiwa. Hakimu amesimama mlangoni!

105:10 Mt 5:12; Ebr 11:25Ndugu zangu, waangalieni manabii walionena kwa Jina la Bwana, ili kuwa mfano wa uvumilivu katika kukabiliana na mateso. 115:11 Mt 5:10; Ay 2:10; Ebr 10:36; Ay 42:10; 12:17; Kut 34:6Kama mnavyojua, tunawahesabu kuwa wabarikiwa wale waliovumilia. Mmesikia habari za uvumilivu wake Ayubu na mmeona kile ambacho hatimaye Bwana alimtendea. Bwana ni mwingi wa huruma, na amejaa rehema.

125:12 Mt 5:31-34; Yak 1:25Zaidi ya yote, ndugu zangu, msiape, iwe kwa mbingu au kwa dunia, au kwa kitu kingine chochote. “Ndiyo” yenu na iwe ndiyo, na “Hapana” yenu iwe hapana, la sivyo mtahukumiwa.

Maombi Ya Imani

135:13 Za 50:15; Kol 3:16Je, mtu yeyote miongoni mwenu amepatwa na taabu? Basi inampasa aombe. Je, kuna yeyote mwenye furaha? Basi na aimbe nyimbo za kusifu. 145:14 Za 23:5; Mdo 11:30; Isa 1:6; Mk 6:13; 16:18; Lk 10:38Je, kuna yeyote miongoni mwenu aliye mgonjwa? Basi inampasa awaite wazee wa kanisa wamwombee na kumpaka mafuta kwa Jina la Bwana. 155:15 Yak 1:6; Isa 33:24; Mt 9:2Kule kuomba kwa imani kutamwokoa huyo mgonjwa, naye Bwana atamwinua na kama ametenda dhambi, atasamehewa. 165:16 Mdo 19:18; Ebr 12:13; Mt 7:7Kwa hiyo ungamianeni dhambi zenu ninyi kwa ninyi na kuombeana ili mpate kuponywa. Maombi ya mwenye haki yana nguvu tena yanafaa sana.

175:17 Mdo 14:15; 1Fal 17:1; Lk 4:25Eliya alikuwa mwanadamu kama sisi. Akaomba kwa bidii kwamba mvua isinyeshe, nayo haikunyesha juu ya nchi kwa muda wa miaka mitatu na miezi sita. 185:18 1Fal 18:41-45Kisha akaomba tena, nazo mbingu zikatoa mvua nayo ardhi ikatoa mazao yake.

195:19 Yak 3:14; Mt 18:15Ndugu zangu, yeyote miongoni mwenu akipotoka na kuicha kweli, naye akarejezwa na mtu mwingine, 205:20 Rum 11:14; 1Pet 4:8hamna budi kujua kwamba yeyote amrejezaye mwenye dhambi kutoka upotovu wake, ataiokoa roho ya huyo mwenye dhambi kutoka mauti na kusitiri wingi wa dhambi.

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

雅各书 5:1-20

警告为富不仁者

1你们这些富有的人啊!为那将要临到你们身上的灾难痛哭哀号吧! 2你们的财物朽坏了,衣服也被虫蛀了。 3你们的金银生了锈,那锈必要指控你们,像火一样吞噬你们的身体。在末世的日子里,你们只知道积攒财宝。 4工人替你们收割庄稼,你们却克扣他们的工钱。那工钱发出不平的呼喊,工人的冤声已经传到万军之主的耳中了。 5你们在世上奢侈享乐,在被宰杀的日子里,把自己养得肥肥胖胖。 6你们冤枉好人、残害无辜,他们也没有反抗。

要忍耐到底

7弟兄姊妹,你们要一直忍耐到主来。你们看农夫怎样耐心等候地里宝贵的出产,等候秋雨和春雨的降临。 8同样,你们也要忍耐,心志坚定,因为主快来了。 9弟兄姊妹,不要互相埋怨,免得受审判。你们看,审判的主已经站在门外了。 10弟兄姊妹,你们要效法从前奉主的名说话的先知,以他们的受苦和忍耐为榜样。 11我们认为那些忍耐到底的人是有福的。你们都知道约伯的忍耐,也知道主最终怎样待他,因为主充满怜悯和慈悲。

12我的弟兄姊妹,最重要的是不可起誓,不可指着天起誓,也不可指着地起誓,不可指着任何东西起誓。你们说话,是就说是,不是就说不是,免得你们受审判。

祷告的力量

13你们中间正在受苦的人应该祷告,喜乐的人应该唱歌赞美, 14生病的人应该请教会的长老来,奉主的名用油抹他的身体并为他祷告。 15出于信心的祷告必能使病人痊愈,主必使他康复。倘若他犯了罪,也必得到赦免。 16所以你们要彼此认罪,互相代祷,好得到医治。义人的祷告有极大的力量和功效。 17以利亚先知和我们一样同是血肉之躯,他恳切地祈求不要下雨,结果三年半没有下雨。 18后来他再祷告求雨,天就降雨,地也长出了庄稼。

19我的弟兄姊妹,如果有人领一个偏离真道的人归回正路, 20他该知道:使一个迷途中的罪人归回正路就是救一个灵魂脱离死亡,并且会遮盖许多罪。