11:1 Mdo 15:13; Rum 1:1; Tit 1:1; Mdo 26:7; Kum 32:26; Yn 7:35Yakobo, mtumwa wa Mungu na wa Bwana Yesu Kristo:
Kwa makabila kumi na mawili yaliyotawanyika ulimwenguni:
Salamu.
Imani Na Hekima
21:2 Mt 5:12; Ebr 12:11; 10:34; Mdo 5:41; 1Pet 4:12, 16; 1:6Ndugu zangu, hesabuni kuwa ni furaha tupu mnapopatwa na majaribu mbalimbali, 31:3 1Pet 1:7; Ebr 10:36; Rum 5:3kwa sababu mnajua ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi. 41:4 1Kor 2:6Saburi na iwe na kazi timilifu, ili mpate kuwa wakamilifu, mmekamilishwa, bila kupungukiwa na kitu chochote. 51:5 1Fal 3:9, 10; Mit 2:3-6; Dan 1:17; Mt 7:7; 1Fal 3:9, 10; Mit 2:3-6; Za 51:6; Dan 2:21; Mt 7:7Kama mtu yeyote miongoni mwenu amepungukiwa na hekima na amwombe Mungu, yeye awapaye watu wote kwa ukarimu wala hana kinyongo, naye atapewa. 61:6 Mt 21:21; Mk 11:24; 1Tim 2:8Lakini anapoomba, lazima aamini wala asiwe na shaka, kwa sababu mtu aliye na shaka ni kama wimbi la bahari, lililochukuliwa na upepo na kutupwa huku na huku. 7Mtu kama huyo asidhani ya kuwa atapata kitu chochote kutoka kwa Bwana. 81:8 Za 119:113; Yak 4:8; 2Pet 2:14; 3:16Yeye ni mtu mwenye nia mbili, mwenye kusitasita katika njia zake zote.
Umaskini Na Utajiri
91:9 Mt 23:12Ndugu asiye na cheo kikubwa yampasa ajivunie hali hiyo maana ametukuzwa. 101:10 Ay 14:2; 1Kor 7:31Lakini yeye aliye tajiri afurahi kwa kuwa ameshushwa, kwa sababu atatoweka kama ua la shambani. 111:11 Za 102:4, 11; Isa 40:6-8Kwa maana jua kali lenye kuchoma huchomoza na kuliunguza, likayakausha majani, na ua lake likapukutika, nao uzuri wake huharibika. Vivyo hivyo tajiri naye atanyauka akiwa anaendelea na shughuli zake.
Kujaribiwa
121:12 1Kor 9:25; Kut 20:6; 1Kor 8:3Heri mtu anayevumilia wakati wa majaribu, kwa sababu akiisha kushinda hilo jaribio atapewa taji la uzima Mungu alilowaahidia wale wampendao.
13Mtu anapojaribiwa asiseme, “Ninajaribiwa na Mungu.” Kwa maana Mungu hawezi kujaribiwa na maovu wala yeye hamjaribu mtu yeyote. 141:14 Mit 19:3; Rum 7:7-10Lakini kila mtu hujaribiwa wakati anapovutwa na kudanganywa na tamaa zake mwenyewe zilizo mbaya. 151:15 Mwa 3:6; Isa 59:4; Rum 6:23Basi ile tamaa mbaya ikishachukua mimba, huzaa dhambi, nayo ile dhambi ikikomaa, huzaa mauti.
161:16 1Kor 6:9; Yak 2:5Ndugu zangu wapendwa, msidanganyike. 171:17 Za 85:12; 102:27; Mt 3:6Kila kitolewacho kilicho chema na kilicho kamili, hutoka juu, na hushuka kutoka kwa Baba wa mianga, ambaye kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeukageuka. 181:18 Yn 1:13; Yer 2:3; Efe 1:12Kwa mapenzi yake mwenyewe alituzaa kwa neno la kweli, kusudi tuwe kama mazao ya kwanza katika viumbe vyake vyote.
Kusikia Na Kutenda
191:19 Mit 10:19; Yak 1:16; 2:5; 3:3-12; Mhu 5:1, 2; Mit 14:17Ndugu zangu wapendwa, fahamuni jambo hili: Kila mtu awe mwepesi wa kusikiliza, lakini asiwe mwepesi wa kusema wala wa kukasirika. 201:20 Mt 5:22Kwa maana hasira ya mwanadamu haitendi haki ya Mungu. 211:21 Efe 4:22; 1:13; Kol 3:8; 1Pet 2:1; Mdo 13; 26; Rum 1:16; 1Kor 15:2Kwa hiyo, ondoleeni mbali uchafu wote na uovu ambao umezidi kuwa mwingi, mkalipokee kwa unyenyekevu lile Neno lililopandwa ndani yenu ambalo laweza kuokoa nafsi zenu.
221:22 Mt 7:21; Yak 2:14-20Basi kuweni watendaji wa Neno wala msiwe wasikiaji tu, huku mkijidanganya nafsi zenu. 231:23 Lk 6:47; Mdo 2:14Kwa maana kama mtu ni msikiaji tu wa Neno wala hatendi kile linachosema, yeye ni kama mtu ajitazamaye uso wake kwenye kioo 24na baada ya kujiona alivyo, huenda zake na mara husahau jinsi alivyo. 25Lakini yeye anayeangalia kwa bidii katika sheria kamilifu, ile iletayo uhuru, naye akaendelea kufanya hivyo bila kusahau alichosikia, bali akalitenda, atabarikiwa katika kile anachofanya.
261:26 Za 39:1; 1Pet 3:10Kama mtu akidhani ya kuwa anayo dini lakini hauzuii ulimi wake kwa hatamu, hujidanganya moyoni mwake, wala dini yake mtu huyo haifai kitu. 271:27 Mt 25:36; Za 146:9; Isa 1:17, 23; Rum 12:2; 2Pet 2:20Dini iliyo safi, isiyo na uchafu, inayokubalika mbele za Mungu Baba yetu, ndiyo hii: Kuwasaidia yatima na wajane katika dhiki zao na kujilinda usitiwe madoa na dunia.
1我是作上帝和主耶穌基督奴僕的雅各,問候散居各地的十二支派的人。
信心和忍耐
2我的弟兄姊妹,當你們遭遇各種磨煉的時候,都要認為是喜樂的事。 3要知道你們的信心經過考驗會產生堅忍。 4你們要堅忍到底,使你們纯全、完備、毫無缺欠。
5如果你們誰缺少智慧,就當求慷慨施恩、不責備人的上帝,上帝必賜給他智慧。 6-8但他要憑信心毫不疑惑地祈求,因為疑惑的人三心二意,行事為人沒有定見,就像海上隨風翻騰的波濤,這種人從主那裡什麼也得不到。
9卑微的弟兄高升,應當快樂。 10富有的弟兄降卑,也要快樂,因為他會像花草一樣衰殘。 11驕陽升起,草就乾枯,花也凋謝,美麗就消失了。富有的人在忙忙碌碌中也會如此衰殘。
12在試煉中能夠忍耐到底的人有福了,因為他若經得起考驗,就會得到主應許賜給愛祂之人的生命冠冕。 13當人受到誘惑時,不可說:「是上帝在誘惑我。」因為上帝不受邪惡的誘惑,也不誘惑人。 14其實每個受到誘惑的人都是受自己的私慾慫恿和誘惑。 15私慾懷了胎,便生出罪,罪一旦長成,便帶來死亡。
16我親愛的弟兄姊妹,不要上當受騙。 17一切良善的施予和完美的恩賜都是從天上,從眾光之父那裡來的。祂不像轉動的影子變幻無常。 18祂按照自己的旨意,藉著真道重生了我們,使我們在祂所造的萬物之中好像初熟的果實。
聽道與行道
19我親愛的弟兄姊妹,請記住:每個人都要快快地聽,慢慢地說,慢慢地動怒。 20因為人的憤怒不能成就上帝的公義。 21所以你們要除去所有的污穢和一切的惡習,謙卑地領受那已經栽種在你們心裡、能救你們靈魂的真道。
22你們要行道,不要只是聽道,自己欺騙自己。 23因為人聽道而不行道,就像照鏡子一樣, 24看過後就走了,隨即忘記了自己的容貌。 25但詳細查考那使人得自由的全備律法並且持之以恆的人,不是聽了就忘,而是身體力行,這樣的人必在他所行的事上蒙福。
26如果有人自以為虔誠,卻不勒住自己的舌頭,就等於是自己欺騙自己,他的所謂虔誠也毫無價值。 27在父上帝看來,純潔無暇的虔誠是指照顧患難中的孤兒寡婦,並且不讓自己被世俗玷污。