Wimbo 6 – Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) NEN

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Wimbo 6:1-13

Marafiki

16:1 Wim 1:8; 5:6Mpenzi wako amekwenda wapi,

ewe mzuri kupita wanawake wote?

Mpenzi wako amegeukia njia ipi,

tupate kumtafuta pamoja nawe?

Mpendwa

26:2 Sef 3:17; Isa 40:11; Wim 4:12; 5:13; 5:6Mpenzi wangu amekwenda bustanini mwake,

kwenye vitalu vya vikolezo,

kujilisha bustanini

na kukusanya yungiyungi.

36:3 Wim 7:10; 2:16Mimi ni wake mpenzi wangu,

na mpenzi wangu ni wangu;

yeye hujilisha katikati ya yungiyungi.

Shairi La Tano

Mpenzi

46:4 2Kor 10:4; 1Fal 15:33; Yos 12; 24; Za 48:2; Hes 1:52; Za 50:2Wewe ni mzuri, mpenzi wangu, kama Tirsa,

upendezaye kama Yerusalemu,

umetukuka kama jeshi lenye bendera.

5Uyageuze macho yako mbali nami,

yananigharikisha.

Nywele zako ni kama kundi la mbuzi

wanaoteremka kutoka Gileadi.

6Meno yako ni kama kundi la kondoo

watokao kuogeshwa.

Kila mmoja ana pacha lake,

hakuna hata mmoja aliye peke yake.

76:7 Mwa 24:65; Wim 4:3Mashavu yako nyuma ya shela yako

ni kama vipande viwili vya komamanga.

86:8 Za 45:9; Mwa 22:24; Es 2:14Panaweza kuwepo malkia sitini,

masuria themanini

na mabikira wasiohesabika;

96:9 Wim 1:15; 5:2; 3:4lakini hua wangu, mkamilifu wangu,

ni wa namna ya pekee,

binti pekee kwa mama yake,

kipenzi cha yeye aliyemzaa.

Wanawali walimwona na kumwita aliyebarikiwa;

malkia na masuria walimsifu.

Marafiki

10Ni nani huyu atokeaye kama mapambazuko,

mzuri kama mwezi, mwangavu kama jua,

ametukuka kama nyota zifuatanazo?

Mpenzi

116:11 Wim 7:12Niliteremka kwenye bustani ya miti ya milozi

ili kutazama machipuko ya bondeni,

kuona kama mizabibu imechipua

au kama mikomamanga imechanua maua.

12Kabla sijangʼamua,

shauku yangu iliniweka

katikati ya magari ya kifalme ya kukokotwa na farasi ya watu wangu.

Marafiki

136:13 Kut 15:20Rudi, rudi, ee Mshulami;

rudi, rudi ili tupate kukutazama!

Mpenzi

Kwa nini kumtazama Mshulami,

kama kutazama ngoma ya Mahanaimu?6:13 Mahanaimu hapa ina maana ya majeshi mawili.