Warumi 7 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Warumi 7:1-25

Hatufungwi Tena Na Sheria

17:1 Gal 3:15; 5:18Ndugu zangu (sasa ninasema na wale wanaoijua sheria), je, hamjui ya kwamba sheria ina mamlaka tu juu ya mtu wakati akiwa hai? 27:2 1Kor 7:39Kwa mfano, mwanamke aliyeolewa amefungwa kwa mumewe wakati akiwa hai, lakini yule mume akifa, yule mwanamke amefunguliwa kutoka sheria ya ndoa. 37:3 Lk 16:18; Mt 5:32Hivyo basi, kama huyo mwanamke ataolewa na mwanaume mwingine wakati mumewe akiwa bado yuko hai, ataitwa mzinzi. Lakini kama mumewe akifa, mwanamke huyo hafungwi tena na sheria ya ndoa, naye akiolewa na mtu mwingine haitwi mzinzi.

47:4 Gal 2:19; 4:31; Kol 1:22Vivyo hivyo, ndugu zangu, ninyi mmeifia sheria kwa njia ya mwili wa Kristo, ili mweze kuwa mali ya mwingine, yeye ambaye alifufuliwa kutoka kwa wafu, ili tupate kuzaa matunda kwa Mungu. 57:5 Rum 7:7-11; 6:13Kwa maana tulipokuwa tunatawaliwa na asili ya dhambi, tamaa za dhambi zilizochochewa na sheria zilikuwa zikitenda kazi katika miili yetu, hivyo tulizaa matunda ya mauti. 67:6 Rum 2:29Lakini sasa, kwa kufia kile kilichokuwa kimetufunga kwanza, tumewekwa huru kutokana na sheria ili tutumike katika njia mpya ya Roho, wala si katika njia ya zamani ya sheria iliyoandikwa.

Sheria Na Dhambi

77:7 Rum 3:20; 4:15; Kut 20:17; Kum 5:21Tuseme nini basi? Kwamba sheria ni dhambi? La, hasha! Lakini, isingekuwa kwa sababu ya sheria, nisingalijua dhambi. Nisingalijua kutamani ni nini kama sheria haikusema, “Usitamani.” 87:8 Rum 4:15; 1Kor 15:56Lakini dhambi kwa kupata nafasi katika amri, hii ikazaa ndani yangu kila aina ya tamaa. Kwa maana pasipo sheria, dhambi imekufa. 9Wakati fulani nilikuwa hai pasipo sheria, lakini amri ilipokuja, dhambi ikawa hai, nami nikafa. 107:10 Law 18:5; Lk 10:26-28Nikaona kwamba ile amri iliyokusudiwa kuleta uzima, ilileta mauti. 117:11 Mwa 3:13Kwa maana dhambi kwa kupata nafasi katika amri, ilinidanganya, na kupitia katika hiyo amri, ikaniua. 127:12 Gal 3:21; 1Tim 1:8Hivyo basi, sheria yenyewe ni takatifu, na amri ni takatifu na ya haki, tena ni njema.

137:13 Rum 6:23; 7:12; 5:20Je, kile kilicho chema basi kilikuwa mauti kwangu? La, hasha! Lakini ili dhambi itambuliwe kuwa ni dhambi, ilileta mauti ndani yangu kupitia kile kilichokuwa chema, ili kwa njia ya amri dhambi izidi kuwa mbaya kupita kiasi.

Mgongano Wa Ndani

147:14 1Kor 3:1; 1Fal 21:20-25; 2Fal 17:17Kwa maana tunajua kwamba sheria ni ya kiroho, lakini mimi ni wa kimwili nikiwa nimeuzwa kwenye utumwa wa dhambi. 157:15 Gal 5:17Sielewi nitendalo, kwa maana lile ninalotaka kulitenda, silitendi, lakini ninatenda lile ninalolichukia. 167:16 Rum 7:12Basi kama ninatenda lile nisilotaka kutenda, ni kwamba ninakubali kuwa sheria ni njema. 177:17 Rum 7:20Lakini, kwa kweli si mimi tena nitendaye lile nisilotaka bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu. 187:18 Gal 5:24Kwa maana ninafahamu kwamba hakuna jema lolote likaalo ndani yangu, yaani, katika asili yangu ya dhambi. Kwa kuwa nina shauku ya kutenda lililo jema, lakini siwezi kulitenda. 197:19 Rum 7:15Sitendi lile jema nitakalo kutenda, bali lile baya nisilolitaka, ndilo nitendalo. 207:20 Rum 7:17Basi kama ninatenda lile nisilotaka kutenda, si mimi tena nifanyaye hivyo, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu.

217:21 Rum 7:23, 25Hivyo naiona sheria ikitenda kazi. Ninapotaka kutenda jema, jambo baya liko papo hapo. 227:22 Efe 3:16; Za 1:2; 40:8Kwa maana katika utu wangu wa ndani naifurahia sheria ya Mungu. 237:23 Yak 4:1; 1Pet 2:11Lakini ninaona kuna sheria nyingine inayotenda kazi katika viungo vya mwili wangu inayopigana vita dhidi ya ile sheria ya akili yangu. Sheria hii inanifanya mateka wa ile sheria ya dhambi inayofanya kazi katika viungo vya mwili wangu.

247:24 Rum 6:6; 8:2Ole wangu mimi maskini! Ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti?

25Ashukuriwe Mungu kwa njia ya Yesu Kristo Bwana wetu! Hivyo basi, mimi mwenyewe kwa akili zangu ni mtumwa wa sheria ya Mungu, lakini katika asili ya dhambi ni mtumwa wa sheria ya dhambi.

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

罗马书 7:1-25

婚姻关系的例子

1弟兄姊妹,我现在对那些熟悉律法的人说:你们难道不知道律法只在人活着的时候管辖人吗? 2比方说,一个妇人结了婚,只要丈夫还在世,她就受律法的约束要与丈夫在一起。如果丈夫死了,她就脱离了与丈夫的婚姻关系。 3丈夫还活着的时候,她若与别的男人发生性关系,便算淫妇。丈夫若死了,她就脱离了与丈夫的婚姻关系,即使改嫁,也不是淫妇。

4我的弟兄姊妹,同样,你们借着基督的身体向着律法也死了,使你们可以归于那位从死里复活的基督,好为上帝结果子。 5从前我们受自己罪恶本性7:5 罪恶本性”希腊文是“肉体”,以下皆用相同译法。的控制,因律法而激发的罪恶欲望在我们身上发作,以致结出死亡的果子。 6但现在,我们既然向着一度捆绑我们的律法死了,就脱离了律法的控制,能够以圣灵所赐的新样式,而不是以拘守教条的旧样式事奉上帝。

律法使人知罪

7那么,我们可以说律法本身是罪吗?当然不是!没有律法,我们就不知道什么是罪。律法若不说“不可贪心”,我就不知道什么是贪心。 8然而,罪却趁机利用诫命在我里面生出各种贪念,因为没有律法,罪是死的。 9我没认识律法之前是活的,但律法来了之后,罪就活了,而我却死了。 10我发现那本来要使人活的诫命反而叫我死, 11因为罪利用诫命趁机引诱我,而且借着诫命杀了我。

12其实律法是圣洁的,诫命也是圣洁、公义、良善的。 13既然如此,难道是良善的诫命叫我死吗?当然不是!是罪借着良善的诫命叫我死。这样,罪借着诫命叫我死就显出它实在是邪恶至极!

善恶相争

14我们知道律法是属灵的,我却属乎肉体,已经卖给罪做奴隶了。 15我不明白自己的所作所为,因为我想做的,我做不到;而我憎恨的恶事,我偏偏去做! 16既然我不想做的,我反倒去做,我就得承认律法是好的。 17其实那并不是我做的,而是住在我里面的罪做的。 18我也知道,在我的罪恶本性里面毫无良善,我有行善的心愿,却没有行善的力量。 19我想行善,却不能行;我不想作恶,反倒去作。 20如果我不想做的,我反倒去做,这就不是我自己做的,而是住在我里面的罪做的。

21因此,我发现一个律:我想行善的时候,恶就不放过我。 22按着我里面的意思7:22 里面的意思”希腊文是“里面的人”。,我喜爱上帝的律。 23然而,我发觉在我身体内另有一个律和我心中的律作战,将我俘虏,使我服从身体内犯罪的律。 24我真是苦啊!谁能救我脱离这个被死亡控制的身体呢? 25感谢上帝,祂借着我们的主耶稣基督救了我!这样看来,我的内心服从上帝的律法,但我罪恶的本性却服从犯罪的律。