Warumi 3 – NEN & KJV

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Warumi 3:1-31

Uaminifu Wa Mungu

1Basi kuna faida gani kuwa Myahudi? Au kuna thamani gani katika tohara? 23:2 Za 147:19; Mdo 7:38Kuna faida kubwa kwa kila namna! Kwanza kabisa, Wayahudi wamekabidhiwa lile Neno halisi la Mungu. 33:3 Rum 10:16; Ebr 4:2; 2Tim 2:13Ingekuwaje kama wengine hawakuwa na imani? Je, kutokuamini kwao kungebatilisha uaminifu wa Mungu? 43:4 Yn 3:33; Za 116:11La hasha! Mungu na aonekane mwenye haki, na kila mwanadamu kuwa mwongo, kama ilivyoandikwa:

“Ili uthibitike kuwa wa kweli unaponena,

na ukashinde utoapo hukumu.”

53:5 Rum 6:19; Gal 3:15Ikiwa uovu wetu unathibitisha haki ya Mungu waziwazi, tuseme nini basi? Je, Mungu kuileta ghadhabu yake juu yetu ni kwamba yeye si mwenye haki? (Nanena kibinadamu.) 63:6 Mwa 18:25; Rum 2:16La hasha! Kama hivyo ndivyo ilivyo, Mungu angehukumuje ulimwengu? 73:7 Rum 3:4; 9:19Mtu aweza kuuliza, “Kama uongo wangu unasaidia kuonyesha kweli ya Mungu na kuzidisha utukufu wake, kwa nini basi mimi nahukumiwa kuwa mwenye dhambi?” 83:8 Rum 6:1; Mdo 5:20; 6:1; 15Nasi kwa nini tusiseme, kama wengine wanavyotusingizia kuwa tunasema, “Tutende maovu ili mema yapate kuja?” Wao wanastahili hukumu yao.

Wote Wametenda Dhambi

93:9 1Fal 8:46; Gal 3:22Tusemeje basi? Je, sisi ni bora kuwaliko wao? La hasha! Kwa maana tumekwisha kuhakikisha kwa vyovyote kwamba Wayahudi na watu wa Mataifa wote wako chini ya nguvu ya dhambi. 103:10 Za 14:1, 3; 53:1Kama ilivyoandikwa:

“Hakuna mwenye haki, hakuna hata mmoja.

11Hakuna hata mmoja mwenye ufahamu,

hakuna hata mmoja amtafutaye Mungu.

123:12 Za 53:1-3; Mhu 7:20Wote wamepotoka,

wote wameoza pamoja;

hakuna atendaye mema,

naam, hakuna hata mmoja.”

133:13 Za 5:9; 140:3“Makoo yao ni makaburi wazi;

kwa ndimi zao wao hufanya udanganyifu.”

“Sumu ya nyoka iko midomoni mwao.”

143:14 Za 10:7“Vinywa vyao vimejaa laana na uchungu.”

153:15 Isa 59:7, 8; Mit 1:16“Miguu yao ina haraka kumwaga damu;

16maangamizi na taabu viko katika njia zao,

173:17 Isa 59:7, 9wala njia ya amani hawaijui.”

183:18 Za 36:1“Hakuna hofu ya Mungu machoni pao.”

193:19 Yn 10:34; Rum 2:12Basi tunajua ya kwamba chochote sheria inachosema, inawaambia wale walio chini ya sheria ili kila kinywa kinyamazishwe na ulimwengu wote uwajibike kwa Mungu. 203:20 Mdo 13:39; Gal 2:16; Rum 4:15; 7:7Kwa hiyo hakuna binadamu hata mmoja atakayehesabiwa haki mbele za Mungu kwa matendo ya sheria, kwa maana sheria hutufanya tuitambue dhambi.

Haki Kwa Njia Ya Imani

213:21 Isa 46:13; Rum 9:30; Mdo 10:43; Rum 1:2Lakini sasa, haki itokayo kwa Mungu imedhihirishwa pasipo sheria, ambayo Sheria na Manabii wanaishuhudia. 223:22 Rum 9:30; Gal 3:28; Kol 3:11Haki hii itokayo kwa Mungu hupatikana kwa Yesu Kristo kwa wote wamwaminio. Kwa maana hapo hakuna tofauti, 233:23 Rum 9:19; 5:2; 3:9; Gal 3:22kwa kuwa wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu, 243:24 2Kor 12:9; Tit 2:11; Za 130:7; Gal 4:5wanahesabiwa haki bure kwa neema yake kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu. 253:25 Za 65:3; Ebr 9:28; 1Pet 1:19; Ufu 1:5; Mdo 14:16; 17:30Yeye ambaye Mungu alimtoa awe dhabihu ya upatanisho kwa njia ya imani katika damu yake. Alifanya hivi ili kuonyesha haki yake, kwa sababu kwa ustahimili wake aliziachilia zile dhambi zilizotangulia kufanywa. 26Alifanya hivyo ili kuonyesha haki yake wakati huu, ili yeye awe mwenye haki na mwenye kumhesabia haki yule anayemwamini Yesu.

Umuhimu Wa Kuwa Na Imani

273:27 1Kor 1:29-31; Efe 2:9Basi, kujivuna kuko wapi? Kumewekwa mbali. Kwa sheria gani? Je, ni kwa ile ya matendo? La hasha, bali kwa ile sheria ya imani. 283:28 Gal 3:11; Yn 2:19Kwa maana twaona kwamba mwanadamu huhesabiwa haki kwa njia ya imani wala si kwa matendo ya sheria. 293:29 Mdo 10:34, 35Je, Mungu ni Mungu wa Wayahudi peke yao? Je, yeye si Mungu wa watu wa Mataifa pia? Naam, yeye ni Mungu wa watu wa Mataifa pia. 303:30 Rum 4:11, 12; Gal 3:8Basi kwa kuwa tuna Mungu mmoja tu, atawahesabia haki wale waliotahiriwa kwa imani na wale wasiotahiriwa kwa imani iyo hiyo. 31Je, basi ni kwamba tunaibatilisha sheria kwa imani hii? La, hasha! Badala yake tunaithibitisha sheria.

King James Version

Romans 3:1-31

1What advantage then hath the Jew? or what profit is there of circumcision? 2Much every way: chiefly, because that unto them were committed the oracles of God. 3For what if some did not believe? shall their unbelief make the faith of God without effect? 4God forbid: yea, let God be true, but every man a liar; as it is written, That thou mightest be justified in thy sayings, and mightest overcome when thou art judged. 5But if our unrighteousness commend the righteousness of God, what shall we say? Is God unrighteous who taketh vengeance? (I speak as a man) 6God forbid: for then how shall God judge the world? 7For if the truth of God hath more abounded through my lie unto his glory; why yet am I also judged as a sinner? 8And not rather, (as we be slanderously reported, and as some affirm that we say,) Let us do evil, that good may come? whose damnation is just.

9What then? are we better than they? No, in no wise: for we have before proved both Jews and Gentiles, that they are all under sin; 10As it is written, There is none righteous, no, not one: 11There is none that understandeth, there is none that seeketh after God. 12They are all gone out of the way, they are together become unprofitable; there is none that doeth good, no, not one. 13Their throat is an open sepulchre; with their tongues they have used deceit; the poison of asps is under their lips: 14Whose mouth is full of cursing and bitterness: 15Their feet are swift to shed blood: 16Destruction and misery are in their ways: 17And the way of peace have they not known: 18There is no fear of God before their eyes.

19Now we know that what things soever the law saith, it saith to them who are under the law: that every mouth may be stopped, and all the world may become guilty before God. 20Therefore by the deeds of the law there shall no flesh be justified in his sight: for by the law is the knowledge of sin.

21But now the righteousness of God without the law is manifested, being witnessed by the law and the prophets; 22Even the righteousness of God which is by faith of Jesus Christ unto all and upon all them that believe: for there is no difference: 23For all have sinned, and come short of the glory of God; 24Being justified freely by his grace through the redemption that is in Christ Jesus: 25Whom God hath set forth to be a propitiation through faith in his blood, to declare his righteousness for the remission of sins that are past, through the forbearance of God; 26To declare, I say, at this time his righteousness: that he might be just, and the justifier of him which believeth in Jesus. 27Where is boasting then? It is excluded. By what law? of works? Nay: but by the law of faith. 28Therefore we conclude that a man is justified by faith without the deeds of the law. 29Is he the God of the Jews only? is he not also of the Gentiles? Yes, of the Gentiles also: 30Seeing it is one God, which shall justify the circumcision by faith, and uncircumcision through faith. 31Do we then make void the law through faith? God forbid: yea, we establish the law.