Warumi 10 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Warumi 10:1-21

110:1 Za 20:4; Mdo 22:23Ndugu zangu, shauku ya moyo wangu na maombi yangu kwa Mungu ni kwa ajili ya Waisraeli, kwamba waokolewe. 210:2 Mdo 21:20; 22:3; Gal 1:14; 4:17; Rum 9:32Kwa maana ninaweza nikashuhudia wazi kwamba wao wana juhudi kubwa kwa ajili ya Mungu, lakini juhudi yao haina maarifa. 310:3 Rum 1:17; 9:31; Flp 3:9Kwa kuwa hawakuijua haki itokayo kwa Mungu, wakatafuta kuweka haki yao wenyewe, hawakujitia chini ya haki ya Mungu. 4Kwa maana Kristo ni ukomo wa sheria ili kuwe na haki kwa kila mtu aaminiye.

Wokovu Ni Kwa Ajili Ya Wote

5Mose anaandika kuhusu haki ile itokanayo na sheria, kwamba, “Mtu atendaye matendo hayo ataishi kwa hayo.” 610:6 Rum 9:30; Kut 30:12Lakini ile haki itokanayo na imani husema hivi: “Usiseme moyoni mwako, ‘Ni nani atakayepanda mbinguni?’ ” (yaani ili kumleta Kristo chini) 710:7 Kum 30:13; Mdo 2:24“au ‘Ni nani atashuka kwenda kuzimu?’ ” (yaani ili kumleta Kristo kutoka kwa wafu.) 810:8 Kum 30:14Lakini andiko lasemaje? “Lile neno liko karibu nawe, liko kinywani mwako na moyoni mwako,” yaani, lile neno la imani tunalolihubiri. 910:9 Mt 10:32; Lk 12:8; Mdo 2:24Kwa sababu kama ukikiri kwa kinywa chako kwamba “Yesu ni Bwana,” na kuamini moyoni mwako kwamba Mungu alimfufua kutoka kwa wafu, utaokoka. 10Kwa maana kwa moyo mtu huamini na hivyo kuhesabiwa haki, tena kwa kinywa mtu hukiri na hivyo kupata wokovu. 1110:11 Isa 28:16; Mt 28:18; Mdo 10:36Kama yasemavyo Maandiko, “Yeyote amwaminiye hataaibika kamwe.” 12Kwa maana hakuna tofauti kati ya Myahudi na Myunani, yeye ni Bwana wa wote, mwenye utajiri kwa wote wamwitao. 1310:13 Mdo 2:21; Yoe 2:32Kwa maana, “Kila mtu atakayeliitia Jina la Bwana, ataokolewa.”

1410:14 Tit 1:3Lakini watamwitaje yeye ambaye hawajamwamini? Nao watawezaje kumwamini yeye ambaye hawajamsikia? Tena watamsikiaje bila mtu kuwahubiria? 1510:15 Isa 52:7Nao watahubirije wasipopelekwa? Kama ilivyoandikwa, “Tazama jinsi ilivyo mizuri miguu yao wale wanaohubiri habari njema!”

1610:16 Isa 53:1Lakini si wote waliotii Habari Njema. Kwa maana Isaya asema, “Bwana, ni nani aliyeamini ujumbe wetu?” 1710:17 Gal 3:2, 5; Kol 3:16Basi, imani chanzo chake ni kusikia, na kusikia huja kwa neno la Kristo. 1810:18 Za 19:4; Mt 24:14Lakini nauliza: Je, wao hawakusikia? Naam, wamesikia, kwa maana:

“Sauti yao imeenea duniani pote,

nayo maneno yao yameenea

hadi miisho ya ulimwengu.”

1910:19 Rum 11:11, 14; Kut 32:21Nami nauliza tena: Je, Waisraeli hawakuelewa? Kwanza, Mose asema,

“Nitawafanya mwe na wivu

kwa watu wale ambao si taifa.

Nitawakasirisha kwa taifa

lile lisilo na ufahamu.”

2010:20 Isa 65:1; Rum 9:20Naye Isaya kwa ujasiri mwingi anasema,

“Nimeonekana na watu wale ambao hawakunitafuta.

Nilijifunua kwa watu

wale ambao hawakunitafuta.”

2110:21 Isa 65:2; Yer 35:17Lakini kuhusu Israeli anasema,

“Mchana kutwa nimewanyooshea

watu wakaidi na wasiotii mikono yangu.”

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

罗马书 10:1-21

1弟兄姊妹,我心里切望并向上帝祈求的,就是以色列人能够得救。 2我可以证明,他们对上帝有热心,但不是基于真知。 3他们不知道上帝所赐的义,想努力建立自己的义,不肯服从上帝的义。 4其实基督是律法的终极目的,使所有信靠祂的人都可以得到义。

求告主名的都必得救

5关于律法的义,摩西写道:“人若遵行律法的诫命,就必活着。” 6但是论到以信心为基础的义,圣经上说:“不要心里说,‘谁要升到天上去呢?’意思是谁要把基督领下来, 7或说,‘谁要下到阴间去呢?’意思是谁要把基督从死人中领上来。” 8其实这里是说:“这道近在咫尺,就在你口里,在你心中。”这道就是我们所传的信主之道。 9你若口里承认耶稣是主,心里相信上帝使祂从死里复活,就必得救。 10因为人心里相信,就可以被称为义人,口里承认,就可以得救。 11正如圣经上说:“信靠祂的人必不致蒙羞。” 12犹太人和希腊人并没有分别,因为主是所有人的主,祂厚待所有求告祂的人, 13因为“凡求告主名的都必得救。”

14可是,人还没信祂,怎能求告祂呢?还没听说过祂,怎能信祂呢?没有人传道,怎能听说过祂呢? 15人没有受差遣,怎能传道呢?正如圣经上说:“那传福音之人的脚踪是何等佳美!” 16只是并非人人都信福音,就像以赛亚先知所说的:“主啊!谁相信我们所传的呢?”

17由此可见,听了道,才会信道;有了基督的话,才有道可听。 18但我要问,以色列人没有听过吗?当然听过。因为

“他们的声音传遍天下,

他们的话语传到地极。”

19我再问,难道以色列人不知道吗?首先,摩西说:

“我要借无名之民挑起你们的嫉妒,

用愚昧的国民激起你们的怒气。”

20后来,以赛亚先知又放胆地说:

“我让没有寻找我的人寻见,

我向没有求问我的人显现。”

21至于以色列人,他说:

“我整天伸出双手招呼那悖逆顽固的百姓。”