Warumi 1 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Warumi 1:1-32

11:1 1Kor 1:1; Mdo 9:15; 1The 2:8, 9; 1Pet 4:17Paulo, mtumishi wa Kristo Yesu, aliyeitwa kuwa mtume na kutengwa kwa ajili ya Injili ya Mungu, 21:2 Gal 3:8; Tit 1:2; Rum 16:25, 26; Mdo 26:6; 3:21; Mt 4:3Injili ambayo Mungu alitangulia kuiahidi kwa vinywa vya manabii wake katika Maandiko Matakatifu, 31:3 Yn 1:14; Rum 9:5yaani, Injili inayomhusu Mwanawe, yeye ambaye kwa uzao wa mwili alikuwa mzao wa Daudi, 41:4 Mt 4:3; Mdo 2:24; 1Kor 1:2; Mdo 13:33na ambaye kwa uwezo wa Roho wa utakatifu alidhihirishwa kuwa Mwana wa Mungu kwa ufufuo wake kutoka kwa wafu, yaani, Yesu Kristo, Bwana wetu. 51:5 Mdo 9:15; 6:7; Rum 16:27Kwa kupitia kwake na kwa ajili ya Jina lake, tumepokea neema na utume ili kuwaita watu miongoni mwa watu wa mataifa yote, waje kwenye utii utokanao na imani. 61:6 Yud 1; Ufu 17:14Ninyi nyote pia mko miongoni mwa watu walioitwa ili mpate kuwa mali ya Yesu Kristo.

71:7 Rum 8:39; 1The 1:4; Efe 1:2; Tit 1:4Kwa wote walioko Rumi wapendwao na Mungu na kuitwa kuwa watakatifu:

Neema na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana wetu Yesu Kristo iwe nanyi.

Maombi Na Shukrani

81:8 Efe 1:16; 1The 2:13; Rum 10:18; 16:19Kwanza kabisa, namshukuru Mungu wangu kwa njia ya Yesu Kristo kwa ajili yenu nyote, kwa sababu imani yenu inatangazwa duniani kote. 91:9 2Tim 1:1; Yer 42:5; Gal 1:20Kwa maana Mungu ninayemtumikia kwa moyo wangu wote katika kuhubiri Injili ya Mwanawe, ni shahidi wangu jinsi ninavyowakumbuka 101:10 Rum 15:32; Mdo 19:21; Rum 15:23, 32; 1Sam 12:23; Lk 18:1; Efe 1:16; Flp 1:4; Kol 1:9; 2The 1:11; 2Tim 1:3; Mdo 18:21; Rum 15:32katika maombi yangu siku zote, nami ninaomba kwamba hatimaye sasa kwa mapenzi ya Mungu, njia ipate kufunguliwa kwa ajili yangu ili nije kwenu.

111:11 Rum 15:23; 1:7; Mdo 28:31Ninatamani sana kuwaona ili nipate kuweka juu yenu karama za rohoni ili mwe imara, 121:12 2Pet 1:1; Tit 1:4au zaidi, ninyi pamoja nami tuweze kutiana moyo katika imani sisi kwa sisi. 131:13 Rum 15:22, 23; Yn 15:16; 1The 2:18; Flp 4:17; Mdo 13:23; 16:7Ndugu zangu, napenda mfahamu kwamba mara nyingi nimekusudia kuja kwenu (ingawa mpaka sasa nimezuiliwa), ili nipate kuvuna mavuno miongoni mwenu kama nilivyovuna miongoni mwa wengine ambao ni watu wa Mataifa wasiomjua Mungu.

141:14 1Kor 9:16Mimi ni mdeni kwa Wayunani na kwa wasio Wayunani, kwa wenye hekima na kwa wasio na hekima. 151:15 Rum 15:20Ndiyo sababu ninatamani sana kuihubiri Injili kwenu pia ninyi mlioko Rumi.

161:16 2Tim 1:8; 1Kor 1:18; Mdo 3:26; 13:26; Rum 2:9, 10Mimi siionei haya Injili ya Kristo kwa maana ni uweza wa Mungu uletao wokovu kwa kila aaminiye, kwanza kwa Myahudi na kwa Myunani pia. 171:17 Rum 3:21; Flp 3:9; Hab 2:4Kwa maana katika Injili haki itokayo kwa Mungu imedhihirishwa, haki ile iliyo kwa njia ya imani hadi imani. Kama ilivyoandikwa: “Mwenye haki ataishi kwa imani.”

Ghadhabu Ya Mungu Kwa Wanadamu

18Ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni dhidi ya uasi wote na uovu wa wanadamu ambao huipinga kweli kwa uovu wao, 191:19 Mdo 14:17; 17:24-28; Yn 1:9kwa maana yote yanayoweza kujulikana kumhusu Mungu ni dhahiri kwao, kwa sababu Mungu mwenyewe ameyadhihirisha kwao. 201:20 Za 19:1-6; Ebr 11:3; Ay 12:7-9; Rum 2:1Kwa maana tangu kuumbwa kwa ulimwengu, asili ya Mungu asiyeonekana kwa macho, yaani, uweza wake wa milele na asili yake ya Uungu, imeonekana waziwazi, ikitambuliwa kutokana na yale aliyoyafanya ili wanadamu wasiwe na udhuru.

211:21 Mwa 8:21; Efe 4:18; Ufu 14:7Kwa maana ingawa walimjua Mungu, hawakumtukuza yeye kama ndiye Mungu wala hawakumshukuru, bali fikira zao zimekuwa batili na mioyo yao ya ujinga ikatiwa giza. 221:22 Kol 1:20, 27; 3:18, 19Ingawa walijidai kuwa wenye hekima, wakawa wajinga 231:23 Yer 2:11; Mdo 17:29na kubadili utukufu wa Mungu aishiye milele kwa sanamu zilizofanywa zifanane na mwanadamu ambaye hufa, na mfano wa ndege, wanyama na viumbe vitambaavyo.

241:24 Za 81:12; Efe 4:19; 1Pet 4:3Kwa hiyo, Mungu akawaacha wazifuate tamaa mbaya za mioyo yao katika uasherati, hata wakavunjiana heshima miili yao wao kwa wao. 251:25 Isa 44:20; Yer 13:25; 16:19, 20; Rum 9:5; 2Kor 11:31Kwa sababu waliibadili kweli ya Mungu kuwa uongo, wakaabudu na kutumikia kiumbe badala ya Muumba, ahimidiwaye milele! Amen.

261:26 Efe 4:19; 1The 4:5; Law 18:22, 23Kwa sababu hii, Mungu aliwaacha wavunjiane heshima kwa kufuata tamaa zao za aibu. Hata wanawake wao wakabadili matumizi ya asili ya miili yao wakaitumia isivyokusudiwa. 271:27 Law 20:13; 1Kor 6:18Vivyo hivyo wanaume pia wakiacha matumizi ya asili ya wanawake wakawakiana tamaa wao kwa wao. Wanaume wakafanyiana matendo ya aibu na wanaume wengine nao wakapata katika maisha yao adhabu iliyowastahili kwa ajili ya upotovu wao.

281:28 Rum 1:24-26; Efe 5:4Nao kwa kuwa hawakuona umuhimu wa kudumisha ufahamu wa Mungu, yeye akawaachilia wafuate akili za upotovu, watende mambo yale yasiyostahili kutendwa. 291:29 3Yn 10Wakiwa wamejawa na udhalimu wa kila namna, uasherati, uovu, tamaa mbaya na hila. Wamejawa na husuda, uuaji, ugomvi, udanganyifu, hadaa na nia mbaya. Wao pia ni wasengenyaji, 301:30 2Tim 3:2wasingiziaji, wanaomchukia Mungu, wajeuri, wenye kiburi na majivuno, wenye hila, wasiotii wazazi wao, 311:31 2Tim 3:3wajinga, wasioamini, wasio na huruma na wakatili. 321:32 Rum 6:23; Za 50:18; Lk 11:48Ingawa wanafahamu sheria ya haki ya Mungu kwamba watu wanaofanya mambo kama hayo wanastahili mauti, si kwamba wanaendelea kutenda hayo tu, bali pia wanakubaliana na wale wanaoyatenda.

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

羅馬書 1:1-32

問候

1我是基督耶穌的奴僕保羅,蒙召作使徒,奉命傳上帝的福音。 2這福音是上帝從前藉著眾先知在聖經中應許的, 3講的是上帝的兒子——我們的主耶穌基督的事。從肉身來說,祂是大衛的後裔; 4從聖潔的靈來看,祂從死裡復活,用大能顯明自己是上帝的兒子。 5我們從祂領受了恩典並成為使徒,要帶領萬民信從祂,使祂的名得榮耀。 6你們也是其中蒙召信從耶穌基督的人。 7我問候所有住在羅馬、上帝所愛、蒙召做聖徒的人。願我們的父上帝和主耶穌基督賜給你們恩典和平安!

保羅渴望去羅馬

8首先,我藉著耶穌基督為各位感謝我的上帝,因為你們的信心正在傳遍天下。 9-10我在祂兒子的福音事工上全心事奉的上帝可以為我做見證:我如何在禱告中常常想到你們,並求上帝讓我照祂的旨意最終能去你們那裡。 11因為我實在想見你們,好將一些屬靈的恩賜分給你們,使你們堅固, 12也可以說是藉著我們彼此的信心互相激勵。

13弟兄姊妹,我希望你們知道,我曾多次計劃去你們那裡,要在你們中間收穫一些福音的果子,像在其他外族人中一樣,只是至今仍有攔阻。 14不論是希臘人、非希臘1·14 非希臘人」希臘文是「未開化的人」,指在希臘、羅馬文化影響之外的人。、智者、愚人,我對他們都有義務。 15所以,我也切望能將福音傳給你們在羅馬的人。

16我不以福音為恥,因為這福音是上帝的大能,要拯救一切相信的人,先是猶太人,然後是希臘人。 17這福音顯明了上帝的義,這義始於信,終於信,正如聖經上說:「義人必靠信心而活。」

人類的罪惡

18上帝的烈怒從天上降下,要懲罰一切心中無神、行為不義、壓制真理的人。 19有關上帝的事情,可以讓人類知道的都已經顯而易見,因為上帝已經向人類顯明了。 20自從創造天地以來,上帝永恆的大能和神性是明明可知的,雖然肉眼看不見,但透過受造之物就可以領悟,因而人類毫無藉口推說不知。 21他們雖然明知有上帝,卻不把祂當作上帝,既不將榮耀歸給祂,也不感謝祂。他們的思想因此變得荒謬無用,無知的心也變得昏暗不明。 22他們自以為聰明,其實愚不可及, 23以必朽的人、飛禽、走獸和爬蟲的形像來取代永恆上帝的榮耀。

24因此,上帝任憑他們隨從內心的情慾行污穢的事,玷污彼此的身體。 25他們把上帝的真理當作謊言,祭拜、供奉受造之物,卻不敬拜、事奉造物主。主是永遠值得稱頌的。阿們!

26因此,上帝任憑他們放縱可恥的情慾。女人放棄正常的兩性關係,做出變態反常的事。 27男人也背棄了和女人正常的兩性關係,慾火焚燒,同性之間彼此貪戀。男人和男人做出羞恥不堪的事,他們必在自己的身體上遭受應得的報應。

28既然他們故意不認識上帝,上帝就任憑他們心思敗壞,做不當做的事。 29他們心裡塞滿了各種不義、邪惡、貪婪、陰險、嫉妒、兇殺、紛爭、詭詐、惡毒;說長道短、 30背後批評、怨恨上帝、欺侮別人、心驕氣傲、自高自大、自我吹捧、無惡不作、違背父母、 31愚鈍無知、不守信用、無情無義、毫無憐憫。 32他們明知,按上帝公義的法則,做這些事的人該死,不但執迷不悟,還喜歡別人跟他們同流合污。