Walawi 7 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Walawi 7:1-38

Sadaka Ya Hatia

17:1 Law 5:15; Eze 40:39; Kut 29:27; Law 6:17; 21:22“ ‘Haya ndiyo masharti kwa ajili ya sadaka ya hatia, ambayo ni takatifu sana: 2Sadaka ya hatia itachinjiwa mahali pale ambapo sadaka ya kuteketezwa huchinjiwa, nayo damu yake itanyunyizwa pande zote za madhabahu. 37:3 Kut 29:13; Law 3:4-9Mafuta yake yote yatatolewa sadaka: mafuta ya mkia na mafuta yale yanayofunika sehemu za ndani, 47:4 Law 3:15figo zote mbili pamoja na mafuta yanayozizunguka yaliyo karibu na kiuno na yale yanayofunika ini, ambayo yataondolewa pamoja na hizo figo. 57:5 Kut 29:13; Tit 2:14; Ebr 9:28Kuhani atayateketeza juu ya madhabahu kuwa sadaka iliyotolewa kwa Bwana kwa moto. Hii ni sadaka ya hatia. 67:6 Law 6:18; Eze 42:13; Law 3:3; Za 93:5; Law 14:13Mwanaume yeyote katika jamaa ya kuhani aweza kuila, lakini lazima iliwe mahali patakatifu; ni takatifu sana.

77:7 Kut 30:10; Law 5:15; 2:3; 6:17; 14:13; 2Fal 12:16; 1Kor 9:13; 10:18; Hes 5:8“ ‘Sheria hii ya sadaka ya hatia ni sawasawa na ile ya sadaka ya dhambi: Nyama ya yule mnyama aliyetolewa sadaka ni ya yule kuhani anayesimamia ibada ya upatanisho. 8Kuhani anayetoa sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya mtu yeyote anaweza kuichukua ngozi ya mnyama yule aliyetolewa iwe yake. 97:9 Law 2:4-7; Hes 18:9; Eze 44:29Kila sadaka ya nafaka iliyookwa jikoni au kupikwa katika sufuria au katika kikaangio itakuwa ya kuhani anayeitoa. 10Nayo kila sadaka ya nafaka, iwe imechanganywa na mafuta au iko kavu, itakuwa ya wana wa Aroni, nayo itagawanywa sawa kati yao.

Sadaka Ya Amani

11“ ‘Haya ndiyo masharti kwa ajili ya sadaka ya amani ambayo mtu aweza kuileta kwa Bwana:

127:12 Law 2:1-4; 22:29; Za 50:14; 54:6; 107:22; 116:17; Yer 33:11; 44:19; Hes 6:19“ ‘Ikiwa mtu atatoa sadaka ya amani kwa ajili ya kuonyesha shukrani, pamoja na sadaka hii ya shukrani, atatoa maandazi yasiyotiwa chachu yaliyochanganywa na mafuta, mikate myembamba isiyotiwa chachu iliyopakwa mafuta, maandazi ya unga laini uliokandwa vizuri na kuchanganywa na mafuta. 137:13 Kut 34:22; Law 23:17; Amo 4:5Pamoja na sadaka hii ya amani ya shukrani ataleta sadaka ya maandazi yaliyotengenezwa kwa chachu. 147:14 Hes 18:8Ataleta moja ya kila aina ya andazi kama sadaka, matoleo kwa Bwana; hii ni ya kuhani anayenyunyiza damu ya sadaka ya amani. 157:15 Kut 12:10; Law 22:30; Ebr 3:13-15Nyama ya sadaka ya amani kwa ajili ya shukrani lazima iliwe siku iyo hiyo inapotolewa; hutabakiza kitu chochote mpaka asubuhi.

167:16 Mwa 28:20; Kum 12:6; 23:21-23; Kut 35:29; Law 19:5-9; 22:18-21; 23:38; Hes 15:3; 29:39; Za 54:6; Eze 46:12“ ‘Lakini kama sadaka yake ni kwa ajili ya nadhiri au ni sadaka ya hiari, sadaka hiyo italiwa siku hiyo inapotolewa, lakini chochote kinachobakia kinaweza kuliwa kesho yake. 177:17 Kut 12:10; Law 19:6Nyama yoyote ya sadaka inayobaki mpaka siku ya tatu lazima iteketezwe kwa moto. 187:18 2Nya 33:16; Law 5:1; 19:7; Hes 18:27; Mwa 4:4-5; Mit 15:8; 21:27; Yer 6:20; Amo 5:22Kama nyama yoyote ya sadaka ya amani italiwa siku ya tatu, Bwana hataikubali. Haitahesabiwa kwake huyo aliyeitoa, kwa kuwa ni najisi. Mtu atakayekula sehemu yake yoyote atahesabiwa hatia.

19“ ‘Nyama ile inayogusa chochote ambacho ni najisi kwa kawaida ya ibada kamwe haitaliwa, ni lazima iteketezwe kwa moto. Kuhusu nyama nyingine, mtu yeyote aliye safi kwa kawaida ya ibada anaweza kuila. 207:20 Law 5:3; 22:3-7; Mwa 17:14; Law 15:3Lakini kama mtu yeyote najisi akila nyama yoyote ya sadaka ya amani iliyotolewa kwa Bwana, huyo mtu lazima akatiliwe mbali na watu wake. 217:21 Law 5:2; 11:24-28; 11:10-13; Kum 14:3; Eze 4:14Kama mtu yeyote akigusa kitu kilicho najisi, iwe ni uchafu wa mwanadamu, au mnyama najisi, au kitu chochote kilicho najisi, kitu cha kuchukiza, kisha akala nyama yoyote ya sadaka ya amani iliyotolewa kwa Bwana, mtu huyo ni lazima akatiliwe mbali na watu wake.’ ”

Kula Mafuta Na Kunywa Damu Kwakatazwa

22Bwana akamwambia Mose, 237:23 Law 17:13; Kum 14:4; 1Sam 2:29“Waambie Waisraeli: ‘Msile mafuta yoyote ya ngʼombe, kondoo wala mbuzi. 247:24 Kut 22:31Mafuta ya mnyama aliyekutwa amekufa au ameraruliwa na mnyama pori yanaweza kutumika kwa kazi nyingine yoyote, lakini kamwe msiyale. 25Mtu yeyote alaye mafuta ya mnyama ambaye ametolewa sadaka kwa Bwana kwa moto ni lazima akatiliwe mbali na watu wake. 267:26 Mwa 9:4; Law 3:17; 17:10-14; Kum 12:16; 1Sam 14:33; Eze 44:15; Mdo 15:20Popote mtakapoishi, kamwe msinywe damu ya ndege yeyote wala ya mnyama. 277:27 Mwa 9:4; Mdo 15:20-29Ikiwa mtu yeyote atakunywa damu, mtu huyo lazima akatiliwe mbali na watu wake.’ ”

Fungu La Makuhani

28Bwana akamwambia Mose, 29“Waambie Waisraeli: ‘Mtu yeyote aletaye sadaka ya amani kwa Bwana ataleta sehemu ya sadaka hiyo kama dhabihu yake kwa Bwana. 307:30 Kut 29:24; Hes 6:20; Law 8:27; 9:21Ataleta sadaka kwa mikono yake mwenyewe iliyotolewa kwa Bwana kwa moto; ataleta mafuta ya huyo mnyama pamoja na kidari, naye atainua hicho kidari mbele za Bwana kuwa sadaka ya kuinuliwa. 317:31 Kut 29:27, 31Kuhani atayateketeza hayo mafuta juu ya madhabahu, lakini kidari kitakuwa cha Aroni na wanawe. 327:32 Kut 29:27; Law 10:14-15; Hes 5:9; 6:20; 18:18Paja la kulia la sadaka zako za amani utampa kuhani kama matoleo. 33Mwana wa Aroni atoaye damu na mafuta ya sadaka ya amani ndiye atakayepewa paja hilo la kulia kuwa fungu lake. 347:34 Kut 29:22, 27; Law 10:15; Hes 6:20; 18:18-19; 1Sam 9:24Kutoka kwenye sadaka za amani za Waisraeli, mimi Mungu nimepokea kidari kile kilichoinuliwa pamoja na lile paja lililotolewa, nami nimevitoa kwa kuhani Aroni na wanawe kuwa fungu lao la kawaida kutoka kwa Waisraeli.’ ”

35Hii ndiyo sehemu ya sadaka zilizotolewa kwa Bwana kwa moto, ambazo zilitengwa kwa ajili ya Aroni na wanawe siku ile walipowekwa wakfu ili kumtumikia Bwana katika kazi ya ukuhani. 367:36 Law 8:12, 30; Kut 40:13-15; Ebr 7:18-28; 8:1-13Siku ile walipotiwa mafuta, Bwana aliagiza kwamba Waisraeli wawape hili kama fungu lao la kawaida kwa vizazi vijavyo.

377:37 Law 6:9, 14; Kut 29:31; Law 6:20Basi haya ndiyo masharti kuhusu sadaka ya kuteketezwa, sadaka ya nafaka, sadaka ya dhambi, sadaka ya hatia, sadaka ya kuwekwa wakfu, na sadaka ya amani, 387:38 Law 26:46; Hes 36:13; Kum 4:5; 29:1-3; Kut 19:11ambayo Bwana alimpa Mose juu ya Mlima Sinai siku ile alipowaagiza Waisraeli walete sadaka zao kwa Bwana, katika Jangwa la Sinai.

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

利未記 7:1-38

祭司獻贖過祭的條例

1「以下是獻贖過祭的條例。

「贖過祭是至聖的。 2要在殺燔祭牲的地方宰贖過祭祭牲,祭牲的血要灑在祭壇周圍。 3要獻上祭牲的所有脂肪,包括肥尾巴、遮蓋內臟的脂肪、 4兩個腎臟和腎臟上靠近腰部的脂肪以及肝葉。 5祭司要在壇上焚燒這一切,作為獻給耶和華的火祭。這是贖過祭。 6祭司家的任何男子都可以吃剩下的祭肉,但要在聖潔之處吃,因為這是至聖之物。 7祭物要歸主持祭禮的祭司,這一條例也適用於贖罪祭。 8燔祭牲的皮要歸主持祭禮的祭司。 9至於素祭,不論是用爐烤的,還是用平底鍋或煎鍋做的,都要歸主持祭禮的祭司。 10但調油的或乾的素祭要歸亞倫的子孫,由他們均分。

獻平安祭的條例

11「以下是向耶和華獻平安祭的條例。

12「如果有人為感謝耶和華而獻平安祭,除了獻祭牲以外,要一同獻上調油的無酵餅、塗油的無酵薄餅及調油的細麵餅, 13也要一同獻上有酵餅。 14他要從每種餅中各取一個,作為舉祭獻給耶和華。舉祭歸灑平安祭祭牲血的祭司。 15至於祭牲的肉,要在獻祭的當天吃完,不可留到次日早晨。 16如果是自願獻的或為了還願而獻的祭物,要在當天吃祭肉,剩下的可以留到第二天吃。 17但到第三天,必須燒掉剩下的祭肉。 18如果第三天仍然吃,所獻的祭便不蒙悅納,毫無價值,是不潔淨的。吃的人要自擔罪責。

19「祭肉如果接觸到任何不潔之物,就不可以吃,要燒掉。潔淨的人都可以吃平安祭的祭肉。 20如果有人不潔淨,卻吃獻給耶和華的平安祭祭肉,要將他從民中剷除。 21如果有人接觸到人或獸的不潔之物,或任何不潔的可憎之物,又吃獻給耶和華的平安祭祭肉,要將他從民中剷除。」

22耶和華對摩西說: 23「你把以下條例告訴以色列人。

「你們不可吃牛、綿羊或山羊的脂肪。 24自然死亡或被野獸咬死的動物的脂肪也不可吃,但可以作其他用途。 25無論誰吃了獻給耶和華的火祭祭牲的脂肪,都要將他從民中剷除。 26你們無論住在哪裡,都不可吃鳥和獸的血。 27凡吃血的,要將他從民中剷除。」

28耶和華對摩西說: 29「你把以下條例告訴以色列人。

「凡向耶和華獻平安祭的,都要從平安祭中取出一份獻給耶和華作禮物。 30他要親手將這獻給耶和華的火祭帶來,將祭牲的脂肪和胸肉帶來,在耶和華面前將胸肉搖一搖,當作搖祭獻上。 31祭司要把脂肪放在壇上焚燒,胸肉歸亞倫及其子孫。 32你們要把祭牲的右腿獻為舉祭,歸給祭司。 33要把右腿歸給亞倫子孫中獻平安祭的血和脂肪的那位祭司。 34因為耶和華已經從以色列人獻的平安祭中,把作搖祭的胸肉和作舉祭的腿肉賜給祭司亞倫及其子孫。他們在以色列人中要永遠享有這一份。 35亞倫及其子孫受膏為祭司事奉耶和華開始,在獻給耶和華的火祭中,這是他們應得之份。 36祭司受膏之日,耶和華就命令以色列人把這部分祭肉分給他們,這是他們世世代代應得之份。」

37以上是獻燔祭、素祭、贖罪祭、贖過祭、平安祭和授聖職時所獻之祭的條例。 38這些條例是耶和華在西奈山上吩咐摩西的。同一天,摩西命令以色列人在西奈曠野向耶和華獻祭。