Walawi 3 – Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) NEN

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Walawi 3:1-17

Sadaka Ya Amani

13:1 Kut 32:6; 12:5; Law 7:11-34; 17:5“ ‘Kama sadaka ya mtu ni sadaka ya amani, naye akatoa ngʼombe kutoka kundi, akiwa dume au jike, atamleta mnyama asiye na dosari mbele za Bwana. 23:2 Kut 29:15, 20; 40:2; 24:6; Hes 8:10; 18:17; Law 1:5; 17:6; Isa 53:4; Ebr 9:28; 1Pet 2:24; 3:18Ataweka mkono wake juu ya kichwa cha sadaka yake na kumchinja penye ingilio la Hema la Kukutania. Ndipo makuhani wana wa Aroni watanyunyiza damu yake pande zote za madhabahu. 33:3 Kut 29:13; 12:9; 3:4; 29:13; Law 4:9Kutoka kwenye hiyo sadaka ya amani ataleta sadaka iliyotolewa kwa Bwana kwa moto: mafuta yote ya mnyama yafunikayo sehemu za ndani, ama yanayoungana na hizo sehemu za ndani, 4figo zote pamoja na mafuta yote yanayozizunguka karibu na kiuno na yale yanayofunika ini, ambayo atayaondoa pamoja na figo. 53:5 Law 1:7-9; 7:29-34; Kut 29:13, 38-42; Hes 28:3-10; 1Sam 2:15-16Kisha wana wa Aroni wataiteketeza juu ya madhabahu, juu ya ile sadaka ya kuteketezwa iliyoko juu ya kuni zinazowaka, kama sadaka ya kuteketezwa kwa moto, harufu nzuri ya kumpendeza Bwana.

63:6 Law 22:21; Hes 15:3, 8; 2Kor 5:21; Tit 2:11-12; Ebr 7:26-27“ ‘Kama akitoa kondoo au mbuzi kutoka kundi kama sadaka ya amani kwa Bwana, atamtoa dume au jike asiye na dosari. 73:7 Law 17:3, 8-9; Hes 15:5; 28:5-8; 1Fal 8:62Kama akimtoa mwana-kondoo, atamleta mbele za Bwana. 83:8 Law 1:5Ataweka mkono wake juu ya kichwa cha sadaka yake, naye atamchinja mbele ya Hema la Kukutania. Kisha wana wa Aroni watanyunyiza damu yake kwenye madhabahu pande zote. 93:9 Isa 34:6; Yer 46:10; Eze 39:19; Sef 1:7Kutoka kwenye hiyo sadaka ya amani ataleta dhabihu iliyotolewa kwa Bwana kwa moto: mafuta yake, mafuta yote ya mkia uliokatwa karibu na uti wa mgongo, mafuta yote yanayofunika sehemu za ndani au yale yanayounganika nazo, 10figo mbili pamoja na mafuta yanayozizunguka yaliyo karibu na kiuno na yale yanayofunika ini, ambayo atayatoa pamoja na figo. 113:11 Law 21:6, 17; 9:18; Hes 28:2; Eze 44:7Kuhani ataviteketeza juu ya madhabahu kama chakula, sadaka iliyotolewa kwa Bwana kwa moto.

123:12 Law 1:10; 4:3“ ‘Kama sadaka yake ni mbuzi, ataileta mbele za Bwana. 133:13 Kut 24:6; Law 1:5Ataweka mkono wake juu ya kichwa chake na kumchinja mbele ya Hema la Kukutania. Kisha wana wa Aroni watanyunyiza damu yake kwenye madhabahu pande zote. 14Kutokana na ile sadaka anayotoa, atatoa sadaka hii kwa Bwana kwa moto: mafuta yote yanayofunika sehemu za ndani na yale yanayoungana nazo, 153:15 Law 7:4; 3:16; 7:31; 1:9; Mwa 4:4; 1Sam 2:16; Law 7:23; 2Nya 7:7figo zote mbili pamoja na mafuta yaliyo juu yake karibu na kiuno na yanayofunika ini, ambayo atayaondoa pamoja na figo. 16Kuhani ataviteketeza juu ya madhabahu kama chakula, sadaka iliyotolewa kwa moto, harufu nzuri. Mafuta yote ya mnyama ni ya Bwana.

173:17 Kut 12:14, 20; 27:21; Mwa 9:12; Law 7:25-26; 17:10-16; Kum 12:16; Mdo 15:20“ ‘Hii ni kanuni ya kudumu kwa vizazi vijavyo, popote muishipo: Msile mafuta yoyote ya mnyama wala damu.’ ”