Walawi 27 – Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) NEN

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Walawi 27:1-34

Kukomboa Kile Kilicho Cha Bwana

1Bwana akamwambia Mose, 227:2 Mwa 28:20; Hes 6:2; Kum 23:21-23; Amu 11:30-39; Ay 22:27; Yn 1:16; Mdo 21:23“Sema na Waisraeli uwaambie: ‘Kama mtu yeyote ataweka nadhiri maalum ili kuweka watu wakfu kwa Bwana, kwa kutoa kiasi cha thamani inayolingana, 327:3 Kut 30:13; Hes 3:47; 18:16; Eze 45:12thamani ya kukomboa mwanaume mwenye kati ya umri wa miaka ishirini na miaka sitini itakuwa shekeli hamsini27:3 Shekeli 50 za fedha ni sawa na gramu 600. za fedha, kulingana na shekeli ya mahali patakatifu; 4ikiwa ni mwanamke, weka thamani yake kwa shekeli thelathini.27:4 Shekeli 30 za fedha ni sawa na gramu 360. 527:5 Mwa 37:28Kama ni mtu mwenye umri wa miaka kati ya mitano na ishirini, weka thamani ya mwanaume kuwa shekeli ishirini,27:5 Shekeli 20 za fedha ni sawa na gramu 240. na mwanamke shekeli kumi.27:5 Shekeli 10 za fedha ni sawa na gramu 120. 627:6 Hes 3:47; 18:16Kama ni mtu mwenye umri kati ya mwezi mmoja na miaka mitano, weka thamani ya mwanaume kuwa shekeli tano za fedha, na ile ya mwanamke kuwa shekeli tatu27:6 Shekeli tatu za fedha ni sawa na gramu 36. za fedha. 7Kama ni mtu mwenye miaka sitini na zaidi, weka thamani ya mwanaume kuwa shekeli kumi na tano,27:7 Shekeli 15 za fedha ni sawa na gramu 180. na mwanamke shekeli kumi. 827:8 Law 5:11; 12:8; 14:21-22; Lk 21:1; 2Kor 8:12Kama mtu yeyote anayeweka nadhiri ni maskini mno kuweza kulipa kiasi kilichowekwa, atampeleka huyo mtu kwa kuhani, ambaye ataweka thamani yake kulingana na kile mweka nadhiri anachoweza kulipa.

927:9 Mwa 28:20; Kut 40:9; Hes 6:20; 18:17; Kum 15:19“ ‘Kama kile mtu alichokiwekea nadhiri ni mnyama anayekubalika kama sadaka kwa Bwana, mnyama wa namna hiyo aliyetolewa kwa Bwana anakuwa mtakatifu. 10Mtu haruhusiwi kumbadilisha au kutoa mnyama mzuri kwa mbaya, au mnyama mbaya kwa mzuri. Kama atatoa mnyama badala ya mwingine, wanyama wote wawili, yaani yule aliyetolewa na yule aliyebadiliwa, ni watakatifu. 1127:11 Kut 13:13; Hes 18:15Kama alichokiwekea nadhiri ni mnyama aliye najisi kiibada, yaani yule asiye kubalika kuwa sadaka kwa Bwana, huyo mnyama lazima aletwe kwa kuhani, 12ambaye ataamua ubora wa mnyama huyo, kama ni mzuri au mbaya. Thamani yoyote atakayoweka kuhani, hivyo ndivyo itakavyokuwa. 1327:13 Law 25:25; 5:16Kama mwenye mnyama atapenda kumkomboa mnyama huyo, lazima aongeze sehemu ya tano ya thamani yake.

1427:14 Law 25:29-31; Hes 18:14; 2Kor 9:10“ ‘Kama mtu ataweka nyumba yake wakfu kama kitu kitakatifu kwa Bwana, kuhani ataamua ubora wa nyumba hiyo, kama ni nzuri au mbaya. Thamani yoyote kuhani atakayoweka, basi hivyo ndivyo itakavyokuwa. 15Kama mtu aliyeweka nyumba yake wakfu ataikomboa, lazima aongeze sehemu ya tano ya thamani yake, nayo nyumba itakuwa yake tena.

16“ ‘Kama mtu anaweka sehemu ya ardhi ya jamaa yake wakfu kwa Bwana, thamani yake itawekwa kulingana na kiasi cha mbegu inayohitajiwa kupandwa katika ardhi hiyo, yaani homeri27:16 Homeri moja ni sawa na efa 10, ambazo ni sawa na kilo 100. moja ya mbegu za shayiri kwa shekeli hamsini za fedha. 17Kama akiweka shamba lake wakfu katika Mwaka wa Yubile, ile thamani iliyokwisha wekwa itakuwa iyo hiyo. 1827:18 Law 25:10-15; 25:15-16Lakini kama akiweka shamba lake wakfu baada ya Yubile, kuhani ataweka thamani kulingana na idadi ya miaka iliyobaki kufikia Mwaka wa Yubile unaofuata, na thamani yake iliyoamuliwa itapunguzwa. 1927:19 Law 25:25Kama mtu anayeweka wakfu shamba anataka kulikomboa, lazima aongeze sehemu ya tano ya thamani yake, nalo shamba litakuwa lake tena. 20Kama pengine halikomboi shamba hilo, au kama ameliuza kwa mtu mwingine, kamwe haliwezi kukombolewa. 2127:21 Law 25:10; Hes 18:14; Eze 44:29Shamba hilo litakapoachiwa mwaka wa Yubile, litakuwa takatifu, kama shamba lililotolewa kwa Bwana, nalo litakuwa mali ya makuhani.

22“ ‘Kama mtu ameweka wakfu kwa Bwana shamba alilonunua, ambalo si sehemu ya ardhi ya jamaa yake, 2327:23 Law 25:15kuhani ataamua thamani yake hadi Mwaka wa Yubile, naye huyo mtu atalazimika kulipa thamani yake siku hiyo kama kitu kitakatifu kwa Bwana. 2427:24 Law 25:28Katika Mwaka wa Yubile, shamba litarudishwa kwa mtu yule ambaye lilinunuliwa kutoka kwake, yule ambaye ardhi ilikuwa mali yake. 2527:25 Kut 30:13; Hes 3:47; Eze 45:12; Hes 18:16Kila thamani lazima iwekwe kulingana na shekeli ya mahali patakatifu,27:25 Shekeli moja ya mahali patakatifu ni sawa na gramu 11. gera ishirini kwa shekeli.

2627:26 Kut 13:12; 22:30; Hes 18:17; Kut 15:19“ ‘Lakini hakuna mtu atakayeweka wakfu mzaliwa wa kwanza wa mnyama, kwa kuwa mzaliwa wa kwanza tayari ni mali ya Bwana; awe ngʼombe au kondoo, ni wa Bwana. 27Kama ni mmoja wa wanyama walio najisi, aweza kumnunua kwa bei iliyowekwa, akiongeza sehemu ya tano ya thamani yake. Kama hatamkomboa, mnyama huyo atauzwa kwa bei iliyowekwa.

2827:28 Hes 18:14; Yos 6:17-19; Amu 11:30-31“ ‘Lakini chochote kile mtu alicho nacho na akakiweka wakfu27:28 Akakiweka wakfu ina maana ya kumpa Mungu kabisa, daima, bila kurudiwa. kwa Bwana, iwe ni binadamu, au mnyama, au ardhi ya jamaa, hakiwezi kuuzwa au kukombolewa. Chochote kilichowekwa wakfu ni kitakatifu sana kwa Bwana.

2927:29 Kum 7:26“ ‘Mtu yeyote aliyewekwa wakfu ili kuangamizwa, hawezi kukombolewa. Mtu kama huyo lazima auawe.

3027:30 Hes 18:26; Kum 7:6; 12:6, 17; 14:22-28; 2Nya 31:6; Neh 10:37; 12:44; 13:5; Mal 3:8; Ezr 9:2; Isa 6:13“ ‘Zaka ya kila kitu kutoka shambani, iwe ni nafaka kutoka kwa ardhi, au tunda kutoka kwa miti, ni mali ya Bwana; ni takatifu kwa Bwana. 3127:31 Law 25:25; 5:16Kama mtu akikomboa chochote cha zaka yake, lazima aongeze sehemu ya tano ya thamani yake. 3227:32 Za 89:32; Yer 33:13; Eze 20:37; Mik 7:14Zaka yote ya kundi la ngʼombe au la kondoo na mbuzi, kila mnyama wa kumi apitaye chini ya fimbo ya yule awachungaye, atakuwa mtakatifu kwa Bwana. 3327:33 Hes 18:21Yule mnyama wa kumi hatachaguliwa kwa kigezo cha uzuri au ubaya, naye haruhusiwi kubadiliwa. Ikiwa atabadiliwa, basi mnyama yule wa kwanza na huyo aliyebadiliwa wote watahesabiwa kuwa watakatifu, na haiwezekani kuwakomboa.’ ”

3427:34 Kut 19:11; Law 7:38; Kum 4:5; Mdo 7:38Haya ndiyo maagizo Bwana aliyompa Mose juu ya Mlima Sinai kwa ajili ya Waisraeli.