Walawi 26 – Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) NEN

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Walawi 26:1-46

Thawabu Ya Utii

(Kumbukumbu 7:12-24; 28:1-14)

126:1 Kut 20:4; 23:24; Za 97:2; Isa 48:5; Yer 44:9; Hab 2:18; Hes 33:52; Kum 4:16-19; Isa 44:9-20; Za 97:7“ ‘Msijitengenezee sanamu au kusimamisha kinyago cha kuchonga, au mnara, wala jiwe la kuabudia, na pia msijiwekee jiwe lililochongwa katika nchi yenu na kusujudu mbele yake. Mimi ndimi Bwana Mungu wenu.

226:2 Kut 20:8; Law 19:30“ ‘Zishikeni Sabato zangu na kuheshimu mahali patakatifu pangu. Mimi ndimi Bwana.

326:3 Mwa 26:5; Kut 24:8; Kum 6:17; 7:12; 11:13, 22; 28:1, 9“ ‘Ikiwa mtafuata amri zangu na kuwa waangalifu kutii maagizo yangu, 426:4 Kum 11:14; 28:12; Za 65:9; 67:6; 68:9; 104:13; 147:8; Yer 5:24; Hos 6:3; Yoe 2:23; Zek 10:1; Ay 5:10; 14:9; Kut 23:24; Law 25:19nitawanyeshea mvua katika majira yake, nayo ardhi itatoa mazao yake, na miti ya mashambani itazaa matunda yake. 526:5 Kum 6:11; 11:15; Eze 36:29-30; Yoe 2:19, 26; Law 25:18Kupura nafaka kwenu kutaendelea mpaka wakati wa kuvuna zabibu. Pia kuvuna zabibu kutaendelea mpaka wakati wa kupanda mbegu, nanyi mtakula na kushiba, na mtaishi salama katika nchi yenu.

626:6 Za 3:5; 4:8; 29:11; 37:11; 85:8; 147:14; Isa 17:2; 26:3; 54:13; 60:18; Hag 2:9; Mit 3:24; Ay 11:18-19; Yer 30:10; Mik 4:4; Sef 3:13; Mwa 37:20“ ‘Nitawapa amani katika nchi, mpate kulala pasipo kutiwa hofu na yeyote. Nitawaondoa wanyama wakali watoke kwenye nchi, nao upanga hautapita katika nchi yenu. 726:7 Za 18:37; 44:5Mtawafukuza adui zenu, nanyi mtawaua kwa upanga mbele yenu. 826:8 Isa 30:17; Kum 28:7; 32:30; Yos 23:10; Amu 15:15; 1Nya 12:14Watu wenu watano watafukuza adui mia, watu wenu mia watafukuza adui elfu kumi, nao adui zenu wataanguka kwa upanga mbele yenu.

926:9 Mwa 1:22; 17:6, 7; Neh 9:23; Kut 2:25; 2Fal 13:23“ ‘Nitawaangalia kwa upendeleo na kuwafanya mzae na kuzidisha idadi yenu, nami nitalishika Agano langu na ninyi. 1026:10 Law 25:22Wakati wa kuvuna mtakuwa bado mnakula mavuno ya mwaka uliopita, na itawalazimu kuyaondoa ghalani ili mpate nafasi ya mavuno mapya. 1126:11 Kut 25:8; Za 74:7; 76:2; Eze 37:27; Kum 31:6; 1Sam 12:22; 1Fal 6:13; 2Fal 17:15Nitafanya makao yangu miongoni mwenu, nami sitawachukia. 1226:12 Mwa 3:8; 17:7; Kut 6:7; Yer 7:23; 11:4; 24:7; 30:22; 31:1; Zek 13:9; 2Kor 6:16; Efe 2:21; Ebr 3:6; Eze 11:20Nitatembea katikati yenu niwe Mungu wenu, nanyi mtakuwa watu wangu. 1326:13 Law 11:44; Kut 6:6; 13:3; Isa 10:27; Yer 2:20; 27:2; 28:10; 30:8; Eze 30:18; 34:27; Hos 11:4Mimi ndimi Bwana Mungu wenu, niliyewatoa katika nchi ya Misri ili msiendelee kuwa watumwa wa Wamisri, nikavunja kongwa lenu, na kuwawezesha kutembea mkiwa mmeinua vichwa vyenu juu.

Adhabu Ya Kutokutii

(Kumbukumbu 28:15-68)

1426:14 Kum 28:15-68; Mal 2:2“ ‘Lakini kama hamtanisikiliza na kutimiza maagizo haya yote, 1526:15 Mwa 17:7; 2Fal 17:15nanyi kama mtazikataa amri zangu na kuzichukia sheria zangu, tena mkishindwa kutimiza amri zangu na hivyo mkavunja agano langu, 1626:16 Kum 28:22, 35; Za 78:33; 107:17; 1Sam 2:33; Eze 4:17; 24:23; 33:10; Amu 6:3-6; Ay 31:8ndipo nitakapowafanyia hili: Nitawaletea juu yenu hofu ya ghafula, magonjwa ya kufisha, na homa itakayopofusha macho yenu na kuwaondolea uhai wenu. Mtapanda mbegu bila mafanikio, kwa sababu adui zenu wataila. 1726:17 Law 17:10; Eze 15:7; Kum 28:7, 25, 48; Yos 7:4, 12; Amu 2:15; 1Fal 8:33; 2Nya 6:24; Yer 9:17; 21:7; Za 106:41; 53:5; Mit 28:1; Isa 30:17Nitauelekeza uso wangu dhidi yenu ili mshindwe na adui zenu; wale wanaowachukia watawatawala, nanyi mtakimbia ingawa hakuna mtu anayewafukuza.

1826:18 Za 99:8; Yer 21:14; Amo 3:14“ ‘Kama baada ya haya yote hamtanisikiliza, nitawaadhibu mara saba zaidi kwa ajili ya dhambi zenu. 1926:19 Za 10:4; 73:6; Isa 16:6; 25:11; 28:1-3; Yer 13:9; 48:29; Eze 24:21; Amo 6:8; Sef 3:11; Kum 28:23; Ay 28:28Nitakivunja kiburi chenu cha ukaidi na kuifanya anga iliyo juu yenu iwe kama chuma, na ardhi yenu kama shaba. 2026:20 Kum 11:17; 28:24, 38; Za 127:1; Isa 17:11; 49:4; Yer 12:13; Mik 6:15; Hag 1:6Nguvu zenu zitatumika bila ya mafanikio, kwa sababu ardhi yenu haitawazalia mazao yake, wala miti ya nchi yenu haitazaa matunda yake.

2126:21 Mwa 4:15“ ‘Kama mtaendelea kuwa na uadui nami, na kukataa kunisikiliza, nitawazidishia mateso yenu mara saba zaidi, kama dhambi zenu zinavyostahili. 2226:22 Mwa 37:20; Kum 28:62; Yer 42:2; 5:6; 14:16; 15:3; 16:4; Eze 14:15Nitawatuma wanyama mwitu dhidi yenu, nao watawaibieni watoto wenu, watawaangamiza ngʼombe wenu, na kuifanya idadi yenu kuwa ndogo, hivi kwamba barabara zenu zitakuwa hazina watu.

2326:23 Yer 2:30; 5:3; 7:28; 17:23; 32:33; Sef 3:2“ ‘Ikiwa pamoja na mambo haya hamtakubali maonyo yangu lakini mkaendelea kuweka uadui nami, 2426:24 2Sam 22:27mimi mwenyewe nitaweka uadui nanyi, na kuwatesa kwa ajili ya dhambi zenu mara saba zaidi. 2526:25 Yer 5:17; 15:3; 47:6; 50:28; 51:6, 11; Eze 11:8; 14:17; 21:4; 33:2; Kut 5:3; 9:3; Hes 16:46; 1Fal 8:37; Hab 3:5Nitawaletea upanga juu yenu ili kuwapatiliza kwa kuvunja Agano langu. Mtakapokimbilia mijini mwenu, nitatuma tauni katikati yenu, nanyi mtatiwa mikononi mwa adui zenu. 2626:26 1Fal 8:37; 18:2; 2Fal 4:38; 6:25; 25:3; Za 105:16; Isa 3:1; 9:20; Yer 37:21; 52:6; Eze 4:16-17; 5:16; 14:13; Hos 4:10; Mik 6:14Nitakapowaondolea upatikanaji wa mkate wenu, wanawake kumi wataoka mkate wenu katika tanuru moja, nao wataugawa mkate kidogo kwa kupima. Mtakula, lakini hamtashiba.

27“ ‘Kama hata baada ya haya bado hamtanisikiliza lakini mkaendelea kuweka uadui nami, 2826:28 Kum 32:19; Amu 2:14; Za 78:59; 106:40; Kum 7:10; Ay 34:11; Isa 59:18; 65:5-7; 66:6; Yer 17:10; 25:29; Yoe 3:4ndipo katika hasira yangu nitaweka uadui nanyi, nami mwenyewe nitawaadhibu mara saba kwa ajili ya dhambi zenu. 2926:29 2Fal 6:29; Yer 19:6; Mao 4:10; Eze 5:10; Kum 28:53Mtakula nyama ya wana wenu na nyama ya binti zenu. 3026:30 Kum 12:2; 1Sam 9:12; 10:5; 1Fal 3:2, 4; 12:31; 13:2, 32; 2Fal 17:29; 23:20; 2Nya 34:3, 4; Za 78:58; 106:40; Eze 6:3, 6, 13; 16:16; Amo 6:8; 7:9; Isa 17:8; 27:9; 21:9; Yer 50:2Nitapaharibu mahali penu pa juu pa kuabudia miungu, nibomoe madhabahu zenu za kufukizia uvumba, na kuzilundika maiti zenu juu ya sanamu zenu zisizo na uhai, nami nitawachukia ninyi sana. 3126:31 Neh 1:3; Isa 1:7; 3:8, 26; 6:11; 24:12; 61:4; 63:18; 64:11; Yer 4:7; 9:11; 25:11; 34:22; 44:2-6, 22; Eze 36:33; 24:21; Mik 2:4; 3:12; Sef 2:5; 3:6; 2Fal 22:19; Za 74:3-7; Mao 2:7; Amo 7:9; 5:21; 8:10Nitaifanya miji yenu kuwa magofu, na kuharibu mahali patakatifu penu pa kuabudia, nami sitapendezwa na harufu nzuri ya sadaka zenu. 3226:32 Isa 5:6; 52:14; Yer 9:11; 12:11; 25:11; 26:9; 33:10; 34:22; 44:22; 18:16; 19:8; 48:39; 1Fal 9:8; 2Nya 29:8; Eze 5:14; 26:16; 27:35; 28:19Nitaiharibu nchi, ili adui zenu watakaokuja kuishi humo washangae. 3326:33 Yer 4:11; 7:34; 9:16; 13:24; 31:10; 40:3, 15; 50:17; 42:16; Eze 5:10; 12:15; 17:21; 20:23; 22:15; 34:6; Yoe 3:2; Kum 4:27; 28:64; Neh 1:8; Za 44:11; 106:27; Zek 7:14; Amo 9:4; Isa 49:19; 1Sam 15:22; Ay 36:11Nitawatawanya ninyi miongoni mwa mataifa, na kuufuta upanga wangu na kuwafuatia. Nchi yenu itaharibiwa, nayo miji yenu itakuwa magofu. 3426:34 Isa 1:7; Yer 7:34; 25:11; 44:6; Eze 33:29; 2Nya 36:21Ndipo nchi itafurahia Sabato zake muda wote ule itakapokuwa ukiwa, nanyi mkiwa katika nchi ya adui zenu. Ndipo nchi itapumzika na kufurahia Sabato zake. 3526:35 Law 25:4Wakati wote nchi itakapobaki ukiwa, itapumzika na kufurahia Sabato zake ambazo haikuzipata mlipokuwa mnaishi humo.

3626:36 Ay 13:25; 2Fal 25:5; Za 58:7; Mao 1:3-6; 4:19; Eze 21:7“ ‘Kwa habari ya wenzenu wale watakaobaki, nitaifanya mioyo yao kuwa na hofu kuu katika nchi za adui zao, kiasi kwamba sauti ya jani linalopeperushwa na upepo itawafanya wakimbie. Watakimbia kana kwamba wanakimbia upanga, nao wataanguka, ingawa hakuna anayewafukuza. 3726:37 Yer 6:21; 13:16; 46:16; Eze 3:20; Nah 3:3; Yos 7:12Watajikwaa mmoja juu ya mwingine kama wakimbiao upanga, hata ingawa hakuna anayewafuatia. Hivyo hamtaweza kusimama mbele ya adui zenu. 3826:38 Ay 4:9; 36:12; Isa 1:28; Yer 16:4; 44:27; Kum 4:26Mtaangamia katikati ya mataifa; nchi ya adui zenu itawala. 3926:39 Kut 20:5; Isa 14:21; 24:16; Eze 4:17Wale wenu watakaobaki wataangamia katika nchi za adui zao kwa sababu ya dhambi zao; pia kwa sababu ya dhambi za baba zao wataangamia.

4026:40 Law 5:5; Za 32:5; 38:18; 106:6; Neh 9:2; Yer 3:12-15; 14:20; Hos 5:15; Lk 15:18; 1Yn 1:9“ ‘Lakini kama watatubu dhambi zao na dhambi za baba zao, udanganyifu wao dhidi yangu na uadui wao kwangu, 4126:41 Kum 10:16; 4:31; 30:6; Yer 4:4; 9:25-26; 4:27; 5:10; 30:11; 31:37; 33:26; 51:5; Eze 20:43; 44:7-9; Mdo 7:51; 2Nya 7:14; 12:6; Isa 6:7; 33:24; 40:2; 53:6-11; Amu 2:1ambao ulinifanya niwe na uadui nao hata nikawapeleka katika nchi ya adui zao, wakati mioyo yao isiyotahiriwa itanyenyekea na kutubu dhambi yao, 4226:42 Za 69:25; 106:24; Isa 6:11; 32:14; 62:4; Yer 2:15; 44:2; Eze 20:13; 36:4; Hes 11:20; 14:31; 1Sam 8:7nami nitakumbuka agano langu na Yakobo, na agano langu na Isaki, na agano langu na Abrahamu, nami nitaikumbuka nchi. 43Kwa kuwa wataiacha nchi ukiwa, nayo itafurahia Sabato zake wakati itakuwa ukiwa bila wao. Wataadhibiwa kwa ajili ya dhambi zao, kwa sababu walizikataa sheria zangu na kuzichukia amri zangu. 4426:44 2Fal 17:20; 25:11; 2Nya 6:36; 36:20; Rum 11:2; Kut 6:8; Law 25:38Lakini pamoja na hili, wakati watakuwa katika nchi ya adui zao, sitawakataa wala kuwachukia kiasi cha kuwaharibu kabisa na kuvunja agano langu nao. Mimi ndimi Bwana Mungu wao. 4526:45 Kum 4:31Lakini kwa ajili yao nitalikumbuka agano langu na baba zao, ambao niliwatoa Misri mbele ya mataifa ili niwe Mungu wao. Mimi ndimi Bwana.’ ”

4626:46 Kut 19:11; Law 7:38; 27:34Hizi ndizo amri, sheria na pia masharti ambazo Bwana alifanya kati yake mwenyewe na Waisraeli katika Mlima Sinai kupitia kwa Mose.