Walawi 2 – NEN & TNCV

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Walawi 2:1-16

Sadaka Ya Nafaka

12:1 Kut 29:2, 41; Law 6:14-18; 5:11; 7:12; 24:7; Hes 15:4; 28:5; Neh 13:9; Isa 43:23“ ‘Mtu yeyote aletapo sadaka ya nafaka kwa Bwana, sadaka yake itakuwa ya unga laini. Atamimina mafuta juu yake, aweke uvumba juu yake, 22:2 Law 1:9; 5:11, 12; 6:15; 24:7; Isa 1:13; 53:12; 65:3; 66:3; Hes 5:26; 18:8; Za 16:5; 73:26; Mdo 10:4naye atapeleka kwa makuhani wana wa Aroni. Kuhani atachukua konzi moja iliyojaa unga laini na mafuta pamoja na uvumba wote, na kuuteketeza kama sehemu ya kumbukumbu juu ya madhabahu, sadaka iliyotolewa kwa moto, harufu nzuri ya kumpendeza Bwana. 32:3 Law 6:16; 10:12-13; Kut 30:36; Hes 18:9Sadaka ya nafaka iliyobaki ni ya Aroni na wanawe, ni sehemu ya sadaka iliyo takatifu sana iliyotolewa kwa Bwana kwa moto.

42:4 Law 7:9, 12; 8:26; 26:26; Kut 29:2“ ‘Kama utaleta sadaka ya nafaka iliyookwa jikoni, itakuwa ya unga laini: maandazi yaliyotengenezwa bila kutiwa chachu, yaliyochanganywa na mafuta, au mikate myembamba iliyotengenezwa bila kutiwa chachu, na iliyopakwa mafuta. 52:5 Law 6:21; 7:9; Eze 4:3Iwapo sadaka yako ya nafaka imeandaliwa kwenye kikaango, itakuwa ni ya unga laini uliochanganywa na mafuta, bila chachu. 6Ukande na kumimina mafuta juu yake; hii ni sadaka ya nafaka. 72:7 Law 7:9Kama sadaka yako ya nafaka imepikwa kwenye sufuria, itatengenezwa kwa unga laini na mafuta. 8Ilete hiyo sadaka ya nafaka iliyotengenezwa kwa vitu hivi kwa Bwana; mkabidhi kuhani ambaye ataipeleka madhabahuni. 92:9 Mwa 8:21; Kut 29:18; Rum 12:1Naye atatoa ile sehemu ya kumbukumbu kutoka kwenye hiyo sadaka ya nafaka na kuiteketeza juu ya madhabahu kuwa sadaka iliyotolewa kwa moto, harufu nzuri ya kumpendeza Bwana. 102:10 Ezr 2:63; Kut 29:18, 37Sadaka ya nafaka iliyobaki ni ya Aroni na wanawe; ni sehemu ya sadaka iliyo takatifu sana ya sadaka iliyotolewa kwa Bwana kwa moto.

112:11 Kut 34:25; 23:18; Law 6:16; Mt 16:12; Mk 8:15; 1Kor 5:8; Gal 5:8-9“ ‘Kila sadaka ya nafaka unayoleta kwa Bwana ni lazima ifanywe bila kutiwa chachu, kwa kuwa huna ruhusa kuchoma chachu yoyote au asali katika sadaka itolewayo kwa Bwana kwa moto. 122:12 Kut 34:22; 22:29; Law 23:10-11; Kum 26:10Unaweza kuzileta kwa Bwana kama sadaka ya malimbuko, lakini haziwezi kutolewa juu ya madhabahu kama harufu nzuri ya kupendeza. 132:13 Mk 9:49; Hes 18:19; 2Nya 13:5; Eze 43:24; Kol 4:6Koleza sadaka zako zote za nafaka kwa chumvi. Usiache kuweka chumvi ya Agano la Mungu wako katika sadaka zako za nafaka; weka chumvi kwenye sadaka zako zote.

142:14 Kut 34:22; Hes 15:20; Kum 16:13; 26:2; Rut 3:2; Kut 23:19; Mit 3:9; 2Fal 4:42“ ‘Kama ukileta malimbuko ya sadaka ya nafaka kwa Bwana, utatoa masuke yaliyopondwa ya nafaka mpya iliyookwa kwa moto. 15Weka mafuta na uvumba juu yake; ni sadaka ya nafaka. 162:16 Hes 4:16; Yer 14:12Kuhani atateketeza ile sehemu ya kumbukumbu kutoka kwenye hiyo sadaka ya nafaka iliyopondwa kwa mafuta, pamoja na uvumba wote, kama sadaka iliyotolewa kwa Bwana kwa moto.

Thai New Contemporary Bible

เลวีนิติ 2:1-16

เครื่องธัญบูชา

1“ ‘ผู้ที่จะถวายเครื่องธัญบูชาแด่องค์พระผู้เป็นเจ้าจงนำแป้งละเอียดมา เทน้ำมันลงบนแป้ง และโรยเครื่องหอม 2แล้วนำมามอบแก่บรรดาปุโรหิตบุตรของอาโรน ปุโรหิตจะกอบแป้งละเอียดมากำมือหนึ่งและน้ำมันพร้อมกับเครื่องหอมทั้งสิ้น และเผาเครื่องบูชานี้เป็นส่วนอนุสรณ์บนแท่นบูชา เป็นเครื่องบูชาด้วยไฟ เป็นกลิ่นหอมที่องค์พระผู้เป็นเจ้าพอพระทัย 3ธัญบูชาส่วนที่เหลือยกให้อาโรนกับบุตรชาย เป็นส่วนบริสุทธิ์ที่สุดของเครื่องบูชาด้วยไฟที่ถวายแด่องค์พระผู้เป็นเจ้า

4“ ‘หากจะนำขนมอบมาเป็นธัญบูชาจะต้องทำจากแป้งละเอียดเคล้าน้ำมันไม่ใส่เชื้อ หรือใช้ขนมปังแผ่นบางไม่ใส่เชื้อทาน้ำมัน 5หากจะถวายขนมปังที่ปิ้งบนกระทะ จงทำจากแป้งละเอียดเคล้าน้ำมันไม่ใส่เชื้อ 6บิเป็นชิ้นเล็กๆ รินน้ำมันราดเป็นเครื่องธัญบูชาอย่างหนึ่ง 7หากจะถวายขนมที่ทอดในกระทะก็ทำจากแป้งละเอียดเคล้าน้ำมันเช่นเดียวกัน 8จงนำธัญบูชาที่ทำจากสิ่งเหล่านี้มาถวายแด่องค์พระผู้เป็นเจ้านำมามอบให้ปุโรหิตซึ่งเขาจะนำมาที่แท่นบูชา 9ปุโรหิตจะนำส่วนอนุสรณ์จากธัญบูชานี้มาเผาบนแท่นบูชา เป็นเครื่องบูชาด้วยไฟ เป็นกลิ่นหอมที่องค์พระผู้เป็นเจ้าพอพระทัย 10ธัญบูชาส่วนที่เหลือยกให้อาโรนกับบรรดาบุตรชาย เป็นส่วนบริสุทธิ์ที่สุดของเครื่องบูชาด้วยไฟที่ถวายแด่องค์พระผู้เป็นเจ้า

11“ ‘อย่าใส่เชื้อในเครื่องธัญบูชาที่เจ้านำมาถวายแด่องค์พระผู้เป็นเจ้าเพราะเจ้าจะต้องไม่เผาเชื้อหรือน้ำผึ้งในเครื่องบูชาด้วยไฟที่ถวายแด่องค์พระผู้เป็นเจ้า 12เจ้าอาจจะถวายขนมปังใส่เชื้อและน้ำผึ้งเป็นเครื่องถวายบูชาผลแรกแด่องค์พระผู้เป็นเจ้าแต่ไม่ใช่นำมาเผาถวายบนแท่นบูชาเป็นกลิ่นที่พอพระทัย 13จงใส่เกลือในเครื่องธัญบูชาทุกอย่าง อย่าให้เกลือแห่งพันธสัญญาของพระเจ้าขาดจากธัญบูชา จงใส่เกลือในเครื่องบูชาทุกอย่าง

14“ ‘หากเจ้าถวายธัญบูชาเป็นผลแรก จงเด็ดเมล็ดจากรวงซึ่งเกี่ยวมาใหม่ๆ นำมาบดและย่างไฟถวายแด่องค์พระผู้เป็นเจ้า 15ใส่น้ำมันและเครื่องหอมในนั้น นี่คือเครื่องธัญบูชา 16ปุโรหิตจะเผาส่วนอนุสรณ์ของเมล็ดพืชบดและน้ำมันพร้อมกับเครื่องหอมทั้งหมด เป็นเครื่องบูชาด้วยไฟถวายแด่องค์พระผู้เป็นเจ้า