Walawi 12 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Walawi 12:1-8

Utakaso Baada Ya Kuzaa Mtoto

1Bwana akamwambia Mose, 212:2 Law 15:19; 18:19; Isa 64:6; Eze 18:6; 22:10; 36:17“Waambie Waisraeli: ‘Mwanamke ambaye atapata mimba na kuzaa mtoto wa kiume atakuwa najisi kwa kawaida ya ibada kwa siku saba, kama anavyokuwa najisi wakati wa siku zake za hedhi. 312:3 Kut 22:30; Mwa 17:10-12; Lk 1:59; 2:21; 2:2; Yn 7:22-23Mvulana atatahiriwa siku ya nane. 4Kisha ni lazima huyo mwanamke asubiri kwa siku thelathini na tatu, ndipo atakaswe kutoka damu kwake. Hataruhusiwa kugusa kitu chochote kilicho kitakatifu au kuingia mahali patakatifu, mpaka siku za kutakaswa kwake zimetimia. 5Kama akimzaa mtoto wa kike, mwanamke huyo atakuwa najisi kwa majuma mawili, kama wakati wake wa hedhi. Kisha atasubiri kwa siku sitini na sita, ndipo atatakaswa kutoka damu kwake.

612:6 Lk 2:22; Kut 29:38; Law 5:7; 23:12; Hes 6:12-14; 7:15; Ufu 5:6-8; 7:14“ ‘Siku zake za utakaso kwa ajili ya mwana au binti zitakapotimia, mwanamke huyo atamletea kuhani kwenye ingilio la Hema la Kukutania mwana-kondoo mwenye umri wa mwaka mmoja kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, na kinda la njiwa au hua kwa ajili ya sadaka ya dhambi. 712:7 Ebr 9:9-28; 10:1-12Atavitoa mbele za Bwana ili kufanya upatanisho kwa ajili yake, na kisha atakuwa safi kwa desturi ya ibada kutokana na kutokwa damu kwake.

“ ‘Haya ndiyo masharti kwa ajili ya mwanamke atakayezaa mtoto wa kiume au wa kike. 812:8 Mwa 15:9; Law 4:26; 14:22; 5:7; Lk 2:22-24; Law 4:26; 2Kor 8:9Kama huyo mwanamke hana uwezo wa kumpata mwana-kondoo, ataleta hua wawili au makinda mawili ya njiwa, moja kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa na mwingine kwa ajili ya sadaka ya dhambi. Kwa njia hii, kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake, naye atakuwa safi.’ ”

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

利未記 12:1-8

產婦潔淨的條例

1耶和華對摩西說: 2「你把以下條例告訴以色列人。

「如果有婦人生了男嬰,她就要不潔淨七天,像在經期內不潔淨一樣。 3第八天,嬰兒要接受割禮。 4婦人因產後流血,要等三十三天才能潔淨。其間,不可接觸任何聖物,也不可進入聖所。 5如果婦人生的是女嬰,她就要不潔淨十四天,像在經期內不潔淨一樣。她因產後流血,要等六十六天才能潔淨。 6不論她生男生女,潔淨期滿後,都要預備一隻一歲的羊羔作燔祭、一隻雛鴿或斑鳩作贖罪祭,帶到會幕門口交給祭司。 7祭司要在耶和華面前獻祭,為她贖罪,她就潔淨了。這是有關產婦的條例。 8她若負擔不起一隻羊羔,可以帶兩隻斑鳩或雛鴿來,一隻作燔祭,一隻作贖罪祭。祭司為她贖罪後,她就潔淨了。」