Wakolosai 1 – NEN & KJV

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Wakolosai 1:1-29

Salamu

11:1 1Kor 1:1; 2Kor 1:1; Mdo 16:1Paulo, mtume wa Kristo Yesu, kwa mapenzi ya Mungu, na Timotheo ndugu yetu:

21:2 Kol 4:18; Rum 1:7Kwa ndugu watakatifu na waaminifu katika Kristo, waishio Kolosai:

Neema na amani zitokazo kwa Mungu Baba yetu ziwe nanyi.

Shukrani Na Maombi

31:3 Rum 1:8Siku zote tunamshukuru Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, tunapowaombea ninyi, 41:4 Gal 5:6; Mdo 9:13; Efe 1:15; Flm 5kwa sababu tumesikia kuhusu imani yenu katika Kristo Yesu, na upendo wenu mlio nao kwa watakatifu wote: 51:5 Kol 1:23; 1The 5:8; Tit 1:2; 1Pet 1:4; 2Tim 2:15imani na upendo ule utokao katika tumaini mlilowekewa akiba mbinguni, na ambalo mmesikia habari zake katika neno la kweli, yaani, ile Injili 61:6 Kol 1:23; Rum 10:18; Yn 15:16iliyowafikia ninyi. Duniani kote Injili hii inazaa matunda na kuenea kama ilivyokuwa kwenu tangu siku ile mlipoisikia na kuielewa neema ya Mungu katika kweli yote. 71:7 Kol 4:12; Flm 23; Kol 4:7Mlijifunza habari zake kutoka kwa Epafra, mtumishi mwenzetu mpendwa, yeye aliye mhudumu mwaminifu wa Kristo kwa ajili yenu, 81:8 Rum 15:30ambaye pia ametuambia kuhusu upendo wenu katika Roho.

91:9 Kol 1:4; Efe 1:15; Rum 1:10; Efe 5:17Kwa sababu hii, tangu siku ile tuliposikia habari zenu, hatujakoma kuomba kwa ajili yenu na kumsihi Mungu awajaze ninyi maarifa ya mapenzi yake katika hekima yote ya kiroho na ufahamu. 101:10 Efe 4:1; 2Kor 5:9; Kol 1:6Nasi tunaomba haya ili mpate kuishi maisha yanayostahili mbele za Bwana, na mpate kumpendeza kwa kila namna: mkizaa matunda kwa kila kazi njema, mkikua katika kumjua Mungu, 111:11 Flp 4:13; Efe 4:2mkiwa mmetiwa nguvu kwa uwezo wote kwa kadiri ya nguvu yake yenye utukufu, ili mpate kuwa na wingi wa saburi na uvumilivu. Nanyi kwa furaha 121:12 Efe 5:20; Mdo 20:32; 26:18mkimshukuru Baba, ambaye amewastahilisha kushiriki katika urithi wa watakatifu katika ufalme wa nuru. 131:13 Mdo 26:13; 2Pet 1:11; Mt 3:17Kwa maana ametuokoa kutoka ufalme wa giza na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wake mpendwa, 141:14 Rum 3:24; Efe 1:7ambaye katika yeye tunao ukombozi, yaani msamaha wa dhambi.

Ukuu Wa Kristo

151:15 Yn 14:9; 1:18; 1Tim 1:17; Ebr 11:27; Kol 1:18Yeye ni mfano wa Mungu asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote. 161:16 Yn 1:3; Efe 1:20, 21; Rum 11:36Kwake yeye vitu vyote vilivyoko mbinguni na juu ya nchi viliumbwa: vitu vinavyoonekana na visivyoonekana, viwe ni viti vya enzi au falme, au wenye mamlaka au watawala; vitu vyote viliumbwa na yeye na kwa ajili yake. 171:17 Yn 1:2Yeye alikuwepo kabla ya vitu vyote, na katika yeye vitu vyote vinashikamana pamoja. 181:18 Efe 1:22; Kol 1:24; 1Kor 12:27; Za 89:27; Rum 8:29Yeye ndiye kichwa cha mwili, yaani kanisa, naye ndiye mwanzo na mzaliwa wa kwanza kutoka kwa wafu, ili yeye awe mkuu katika vitu vyote. 191:19 Efe 1:15; Yn 1:16Kwa kuwa ilimpendeza Mungu kwamba utimilifu wake wote ukae ndani yake, 201:20 Rum 5:10; Efe 1:10; Lk 2:14; Efe 2:13na kwa njia yake aweze kuvipatanisha vitu vyote na yeye mwenyewe, viwe ni vitu vilivyo duniani au vilivyo mbinguni, kwa kufanya amani kwa damu yake, iliyomwagika msalabani.

211:21 Rum 5:10; Efe 2:3Hapo kwanza mlikuwa mmetengana na Mungu, na mlikuwa adui zake katika nia zenu kwa sababu ya mienendo yenu mibaya. 221:22 Kol 1:20; Rum 5:10; 7:4; 2Kor 4:14; Efe 1:4; 5:27Lakini sasa Mungu amewapatanisha ninyi kwa njia ya mwili wa Kristo kupitia mauti, ili awalete mbele zake mkiwa watakatifu, bila dosari wala lawama, 23ikiwa mnaendelea katika imani yenu mkiwa imara na thabiti, pasipo kuliacha tumaini lililoahidiwa katika Injili. Hii ndiyo ile Injili mliyoisikia, ambayo imehubiriwa kwa kila kiumbe chini ya mbingu, na ambayo mimi Paulo nimekuwa mtumwa wake.

Taabu Ya Paulo Kwa Ajili Ya Kanisa

241:24 2Kor 6:10; 1:5; 1Kor 12:27Sasa nafurahia kule kuteseka kwangu kwa ajili yenu, na katika mwili wangu ninatimiliza yale yaliyopungua katika mateso ya Kristo kwa ajili ya mwili wake, ambao ni kanisa. 251:25 Kol 1:23; 1Kor 3:5; Efe 3:2; Ebr 4:12Mimi nimekuwa mtumishi wa kanisa kwa wajibu alionipa Mungu ili kuwaletea ninyi Neno la Mungu kwa ukamilifu: 261:26 Rum 16:25Hii ni siri iliyokuwa imefichika tangu zamani na kwa vizazi vingi, lakini sasa imefunuliwa kwa watakatifu. 271:27 Mt 13:11; Rum 2:11, 24; 8:10Kwao, Mungu amechagua kujulisha miongoni mwa watu wa Mataifa utukufu wa utajiri wa siri hii, ambayo ni Kristo ndani yenu, tumaini la utukufu.

281:28 Kol 3:16; 1Kor 2:6, 7; Mt 5:48; Efe 5:27Yeye ndiye tunayemtangaza, tukimwonya kila mtu na kumfundisha kila mtu kwa hekima yote ili tuweze kumleta kila mmoja akiwa amekamilika katika Kristo. 291:29 1Kor 15:10; 2Kor 11:23; Kol 2:1; Efe 1:19; 3:7Kwa ajili ya jambo hili, ninajitaabisha, nikijitahidi kwa kadiri ya nguvu zake ambazo hutenda kazi ndani yangu kwa uweza mwingi.

King James Version

Colossians 1:1-29

1Paul, an apostle of Jesus Christ by the will of God, and Timotheus our brother, 2To the saints and faithful brethren in Christ which are at Colosse: Grace be unto you, and peace, from God our Father and the Lord Jesus Christ. 3We give thanks to God and the Father of our Lord Jesus Christ, praying always for you, 4Since we heard of your faith in Christ Jesus, and of the love which ye have to all the saints, 5For the hope which is laid up for you in heaven, whereof ye heard before in the word of the truth of the gospel; 6Which is come unto you, as it is in all the world; and bringeth forth fruit, as it doth also in you, since the day ye heard of it, and knew the grace of God in truth: 7As ye also learned of Epaphras our dear fellowservant, who is for you a faithful minister of Christ; 8Who also declared unto us your love in the Spirit. 9For this cause we also, since the day we heard it, do not cease to pray for you, and to desire that ye might be filled with the knowledge of his will in all wisdom and spiritual understanding; 10That ye might walk worthy of the Lord unto all pleasing, being fruitful in every good work, and increasing in the knowledge of God; 11Strengthened with all might, according to his glorious power, unto all patience and longsuffering with joyfulness; 12Giving thanks unto the Father, which hath made us meet to be partakers of the inheritance of the saints in light: 13Who hath delivered us from the power of darkness, and hath translated us into the kingdom of his dear Son: 14In whom we have redemption through his blood, even the forgiveness of sins: 15Who is the image of the invisible God, the firstborn of every creature: 16For by him were all things created, that are in heaven, and that are in earth, visible and invisible, whether they be thrones, or dominions, or principalities, or powers: all things were created by him, and for him: 17And he is before all things, and by him all things consist. 18And he is the head of the body, the church: who is the beginning, the firstborn from the dead; that in all things he might have the preeminence. 19For it pleased the Father that in him should all fulness dwell; 20And, having made peace through the blood of his cross, by him to reconcile all things unto himself; by him, I say, whether they be things in earth, or things in heaven. 21And you, that were sometime alienated and enemies in your mind by wicked works, yet now hath he reconciled 22In the body of his flesh through death, to present you holy and unblameable and unreproveable in his sight: 23If ye continue in the faith grounded and settled, and be not moved away from the hope of the gospel, which ye have heard, and which was preached to every creature which is under heaven; whereof I Paul am made a minister; 24Who now rejoice in my sufferings for you, and fill up that which is behind of the afflictions of Christ in my flesh for his body’s sake, which is the church: 25Whereof I am made a minister, according to the dispensation of God which is given to me for you, to fulfil the word of God; 26Even the mystery which hath been hid from ages and from generations, but now is made manifest to his saints: 27To whom God would make known what is the riches of the glory of this mystery among the Gentiles; which is Christ in you, the hope of glory: 28Whom we preach, warning every man, and teaching every man in all wisdom; that we may present every man perfect in Christ Jesus: 29Whereunto I also labour, striving according to his working, which worketh in me mightily.