Wagalatia 3 – NEN & KJV

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Wagalatia 3:1-29

Imani Au Kushika Sheria?

13:1 Gal 5:7; 1Kor 1:23Ninyi Wagalatia wajinga! Ni nani aliyewaroga? Yesu Kristo aliwekwa wazi mbele yenu kwamba amesulubiwa. 23:2 Rum 10:17; Yn 20:22; Gal 3:5, 10; 2:16; Rum 10:17Nataka nijifunze neno moja kutoka kwenu: Je, mlipokea Roho wa Mungu kwa kushika sheria, au kwa kuyaamini yale mliyosikia? 33:3 Gal 4:9; Ebr 7:16; 9:10Je, ninyi ni wajinga kiasi hicho? Baada ya kuanza kwa Roho, je, sasa mwataka kumalizia katika mwili? 43:4 Ebr 10:35, 36; 2Yn 8Je, mlipata mateso kiasi hicho bure? Ni kama kweli yalikuwa bure! 53:5 1Kor 12:10; 2Kor 3:8Je, Mungu huwapa Roho wake na kufanya miujiza katikati yenu kwa sababu mnatii sheria, au kwa sababu mnaamini kile mlichosikia?

63:6 Mwa 15:6; Rum 4:3Kama vile “Abrahamu alimwamini Mungu na ikahesabiwa kwake kuwa haki.” 73:7 Yn 8:39; Rum 4:11, 12, 16Fahamuni basi kwamba wale walio na imani, hao ndio watoto wa Abrahamu. 83:8 Mwa 18:18; Mdo 3:25Maandiko yakitabiri kwamba Mungu angewahesabia haki watu wa Mataifa kwa imani, alitangulia kumtangazia Abrahamu Injili akisema kwamba, “Kwa kupitia kwako mataifa yote yatabarikiwa.” 93:9 Rum 4:16; Gal 3:7; Rum 4:18-22Kwa sababu hii, wale wote wanaoamini wanabarikiwa pamoja na Abrahamu, mtu wa imani.

Sheria Na Laana

103:10 Kum 27:26; Yer 11:3Kwa maana wote wanaotumainia matendo ya sheria wako chini ya laana, kwa kuwa imeandikwa, “Alaaniwe kila mtu asiyeshikilia kutii mambo yote yaliyoandikwa katika Kitabu cha Sheria.” 113:11 Gal 2:16; Hab 2:4; Rum 1:17; Ebr 10:38Basi ni dhahiri kwamba hakuna mtu anayehesabiwa haki mbele za Mungu kwa kushikilia sheria, kwa maana, “Mwenye haki ataishi kwa imani.” 123:12 Rum 4:4, 5; Law 18:5; Neh 9:29; Eze 20:11Lakini sheria haitegemei imani. Kinyume chake, “Mtu atendaye matendo hayo ataishi kwa hayo.” 133:13 Rum 8:3; 2Kor 5:21; 4:5; Kum 21:23Kristo alitukomboa kutoka laana ya sheria kwa kufanyika laana kwa ajili yetu, kwa maana imeandikwa, “Amelaaniwa yeye aangikwaye juu ya mti.” 143:14 Rum 4:9, 16; Isa 32:15; 44:3; Yer 31:33; 32:40; Eze 11:19Alitukomboa ili kwamba baraka aliyopewa Abrahamu ipate kuwafikia watu wa Mataifa kwa njia ya Kristo Yesu, ili kwa imani tupate kupokea ile ahadi ya Roho.

Sheria Na Ahadi

153:15 Ebr 9:17; Rum 7:1Ndugu zangu, nataka nitoe mfano kutoka maisha ya kila siku. Kama vile hakuna mtu awezaye kutangua au kuongeza kitu katika agano la mtu ambalo limekwisha kuthibitishwa, vivyo hivyo kwa hali kama hii. 163:16 Mwa 17:19; Za 132:11; Mik 7:20; Lk 1:55; Rum 4:13, 16Ahadi zilinenwa kwa Abrahamu na kwa mzao wake. Maandiko hayasemi “kwa wazao,” likimaanisha watu wengi, bali “kwa mzao wako,” yaani mtu mmoja, ndiye Kristo. 173:17 Mwa 15:13, 14; Kut 12:40; Mdo 7:6Ninachotaka kusema ni kwamba, sheria, ambayo ilitolewa miaka 430 baadaye, haitangui Agano lililothibitishwa na Mungu ili kuibatilisha ahadi ile. 183:18 Rum 4:14Kwa maana kama urithi hupatikana kwa sheria, basi hautegemei tena ahadi, lakini Mungu kwa neema yake alimpa Abrahamu urithi kwa njia ya ahadi.

Kusudi La Sheria

193:19 Rum 5:20; 3:16; Kum 33:2; Mdo 7:53; Kut 20:19Kwa nini basi iwepo sheria? Sheria iliwekwa kwa sababu ya makosa mpaka atakapokuja yule Mzao wa Abrahamu, ambaye alitajwa katika ile ahadi. Sheria iliamriwa na malaika kwa mkono wa mpatanishi. 203:20 1Tim 2:5; Ebr 8:6; 9:15; 12:24Basi mpatanishi huhusisha zaidi ya upande mmoja, lakini Mungu ni mmoja.

213:21 Gal 2:17; Rum 7:12; Gal 2:21Je basi, sheria inapingana na ahadi za Mungu? La hasha! Kwa maana kama sheria iliyotolewa ingeweza kuwapa watu uzima, basi haki ingepatikana kwa njia ya sheria. 223:22 Rum 3:9-19; 11:32Lakini Maandiko yamefanya vitu vyote vifungwe chini ya nguvu ya dhambi, ili yale yaliyoahidiwa kwa njia ya imani katika Yesu Kristo yapate kupewa wale wanaoamini.

233:23 Rum 11:32; Gal 3:25Kabla imani hii haijaja tulikuwa tumewekwa chini ya sheria, tumefungwa mpaka ile imani ifunuliwe. 243:24 Gal 3:19; Rum 10:4; 4:15; Gal 2:16Hivyo, sheria ilikuwa kiongozi kutufikisha kwa Kristo, ili tupate kuhesabiwa haki kwa imani. 253:25 Rum 7:4; 10:4Lakini sasa kwa kuwa ile imani imekuja, hatusimamiwi tena na sheria.

Watoto Wa Mungu

263:26 Rum 8:14; Yn 1:12; Rum 8:15, 16; Gal 4:5; 1Yn 3:1Kwa maana ninyi nyote mmekuwa watoto wa Mungu katika Kristo Yesu kwa njia ya imani. 273:27 Rum 6:3; 13:14; Mt 28:19Kwa maana wote mliobatizwa ndani ya Kristo, mmemvaa Kristo. 283:28 1Kor 12:13; Kol 3:11; Mwa 1:27; 5:2; Yoe 2:29; Yn 10:16Wala hakuna tena Myahudi au Myunani, mtumwa au mtu huru, mwanaume wala mwanamke, maana nyote mmekuwa wamoja ndani ya Kristo Yesu. 293:29 1Kor 3:22; Gal 3:16; Lk 3:8; Rum 8:17; Gal 3:16Nanyi mkiwa ni mali ya Kristo, basi ninyi ni wa uzao wa Abrahamu na warithi sawasawa na ile ahadi.

King James Version

Galatians 3:1-29

1O foolish Galatians, who hath bewitched you, that ye should not obey the truth, before whose eyes Jesus Christ hath been evidently set forth, crucified among you? 2This only would I learn of you, Received ye the Spirit by the works of the law, or by the hearing of faith? 3Are ye so foolish? having begun in the Spirit, are ye now made perfect by the flesh? 4Have ye suffered so many things in vain? if it be yet in vain. 5He therefore that ministereth to you the Spirit, and worketh miracles among you, doeth he it by the works of the law, or by the hearing of faith? 6Even as Abraham believed God, and it was accounted to him for righteousness.

7Know ye therefore that they which are of faith, the same are the children of Abraham. 8And the scripture, foreseeing that God would justify the heathen through faith, preached before the gospel unto Abraham, saying, In thee shall all nations be blessed. 9So then they which be of faith are blessed with faithful Abraham. 10For as many as are of the works of the law are under the curse: for it is written, Cursed is every one that continueth not in all things which are written in the book of the law to do them. 11But that no man is justified by the law in the sight of God, it is evident: for, The just shall live by faith. 12And the law is not of faith: but, The man that doeth them shall live in them. 13Christ hath redeemed us from the curse of the law, being made a curse for us: for it is written, Cursed is every one that hangeth on a tree: 14That the blessing of Abraham might come on the Gentiles through Jesus Christ; that we might receive the promise of the Spirit through faith. 15Brethren, I speak after the manner of men; Though it be but a man’s covenant, yet if it be confirmed, no man disannulleth, or addeth thereto. 16Now to Abraham and his seed were the promises made. He saith not, And to seeds, as of many; but as of one, And to thy seed, which is Christ. 17And this I say, that the covenant, that was confirmed before of God in Christ, the law, which was four hundred and thirty years after, cannot disannul, that it should make the promise of none effect. 18For if the inheritance be of the law, it is no more of promise: but God gave it to Abraham by promise. 19Wherefore then serveth the law? It was added because of transgressions, till the seed should come to whom the promise was made; and it was ordained by angels in the hand of a mediator. 20Now a mediator is not a mediator of one, but God is one. 21Is the law then against the promises of God? God forbid: for if there had been a law given which could have given life, verily righteousness should have been by the law. 22But the scripture hath concluded all under sin, that the promise by faith of Jesus Christ might be given to them that believe.

23But before faith came, we were kept under the law, shut up unto the faith which should afterwards be revealed. 24Wherefore the law was our schoolmaster to bring us unto Christ, that we might be justified by faith. 25But after that faith is come, we are no longer under a schoolmaster. 26For ye are all the children of God by faith in Christ Jesus. 27For as many of you as have been baptized into Christ have put on Christ. 28There is neither Jew nor Greek, there is neither bond nor free, there is neither male nor female: for ye are all one in Christ Jesus. 29And if ye be Christ’s, then are ye Abraham’s seed, and heirs according to the promise.