Wafilipi 3 – NEN & NIV

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Wafilipi 3:1-21

Hakuna Tumaini Katika Mwili

13:1 Flp 2:18; 4:4Hatimaye, ndugu zangu, furahini katika Bwana! Mimi kuwaandikia mambo yale yale hakuniudhi, kwa maana ni kinga kwa ajili yenu.

23:2 Za 22:16, 20Jihadharini na mbwa, wale watenda maovu, jihadharini na wale wajikatao miili yao, wasemao ili kuokoka ni lazima kutahiriwa. 33:3 Gal 3:15; Kol 2:11Kwa maana sisi ndio tulio tohara, sisi tumwabuduo Mungu katika Roho, tunaona fahari katika Kristo Yesu, ambao hatuweki tumaini letu katika mwili, 43:4 2Kor 11:21; 11:8, 22ingawa mimi mwenyewe ninazo sababu za kuutumainia mwili.

Kama mtu yeyote akidhani anazo sababu za kuutumainia mwili, mimi zaidi. 53:5 Lk 1:59; 2Kor 11:22; Rum 11:1; Mdo 23:6Nilitahiriwa siku ya nane, mimi ni Mwisraeli wa kabila la Benyamini, Mwebrania wa Waebrania. Kwa habari ya sheria, ni Farisayo, 63:6 Mdo 8:3; Rum 10:5kwa habari ya juhudi, nilikuwa nalitesa kanisa, kuhusu haki ipatikanayo kwa sheria, mimi nilikuwa sina hatia.

73:7 Mt 13:44; Lk 14:33Lakini mambo yale yaliyokuwa faida kwangu, sasa nayahesabu kuwa hasara kwa ajili ya Kristo. 83:8 Yer 9:23, 24; Yn 17:3Zaidi ya hayo, nayahesabu mambo yote kuwa hasara tupu nikiyalinganisha na faida kubwa ipitayo kiasi cha kumjua Kristo Yesu Bwana wangu, ambaye kwa ajili yake nimepata hasara ya mambo yote, nikiyahesabu kuwa kama mavi ili nimpate Kristo. 93:9 Rum 10:5; 9:30Nami nionekane mbele zake bila kuwa na haki yangu mwenyewe ipatikanayo kwa sheria, bali ile ipatikanayo kwa imani katika Kristo, haki ile itokayo kwa Mungu kwa njia ya imani. 103:10 Rum 8:17; 6:3-5Nataka nimjue Kristo na uweza wa kufufuka kwake na ushirika wa mateso yake, ili nifanane naye katika mauti yake, 113:11 Yn 11:24; Rum 6:5; Ufu 20:5, 6ili kwa njia yoyote niweze kufikia ufufuo wa wafu.

Kukaza Mwendo Ili Kufikia Lengo

12Si kwamba nimekwisha kufikia, au kwamba nimekwisha kuwa mkamilifu, la hasha! Bali nakaza mwendo ili nipate kile ambacho kwa ajili yake, nimeshikwa na Kristo Yesu. 133:13 Lk 9:22Ndugu zangu, sijihesabu kuwa nimekwisha kushika. Lakini ninafanya jambo moja: Ninasahau mambo yale yaliyopita, nakaza mwendo kufikia yale yaliyo mbele. 143:14 Ebr 6:1; 1Kor 9:24; Rum 8:28Nakaza mwendo nifikie ile alama ya ushindi iliyowekwa ili nipate tuzo ya mwito mkuu wa Mungu ambao nimeitiwa huko juu mbinguni katika Kristo Yesu.

153:15 1Kor 2:6; Gal 5:10; Efe 1:17; 1The 4:9Hivyo sisi sote tuliokuwa kiroho tuwaze jambo hili, hata mkiwaza mengine katika jambo lolote, Mungu ataliweka wazi hilo nalo. 163:16 Gal 6:16; Rum 12:16; 15:15; Flp 2:2Lakini na tushike sana lile ambalo tumekwisha kulifikia.

173:17 1Kor 4:16; Tit 3:12Ndugu zangu, kwa pamoja fuateni mfano wangu na kuwatazama wale wanaofuata kielelezo tulichowawekea. 183:18 Mdo 20:31; Gal 6:12Kwa maana, kama nilivyokwisha kuwaambia mara nyingi kabla, nami sasa nasema tena hata kwa machozi, watu wengi wanaishi kama adui wa msalaba wa Kristo. 193:19 Za 73:17; Rum 16:18; 5:21; Yud 13; Rum 8:5, 6; Kol 3:2Mwisho wa watu hao ni maangamizi, Mungu wao ni tumbo, na utukufu wao ni aibu, na mawazo yao yamo katika mambo ya dunia. 203:20 Efe 2:19; Kol 3:1; Ebr 12:22; 1Kor 1:7Lakini uenyeji wetu uko mbinguni. Nasi tunamngoja kwa shauku Mwokozi kutoka huko, yaani, Bwana Yesu Kristo, 213:21 Efe 1:19; 1Kor 15:43-53; Rum 8:29; Kol 3:4atakayeubadili mwili wetu wa unyonge, ili upate kufanana na mwili wake wa utukufu, kwa uweza ule ambao kwa huo aweza hata kuvitiisha vitu vyote chini yake.

New International Version

Philippians 3:1-21

No Confidence in the Flesh

1Further, my brothers and sisters, rejoice in the Lord! It is no trouble for me to write the same things to you again, and it is a safeguard for you. 2Watch out for those dogs, those evildoers, those mutilators of the flesh. 3For it is we who are the circumcision, we who serve God by his Spirit, who boast in Christ Jesus, and who put no confidence in the flesh— 4though I myself have reasons for such confidence.

If someone else thinks they have reasons to put confidence in the flesh, I have more: 5circumcised on the eighth day, of the people of Israel, of the tribe of Benjamin, a Hebrew of Hebrews; in regard to the law, a Pharisee; 6as for zeal, persecuting the church; as for righteousness based on the law, faultless.

7But whatever were gains to me I now consider loss for the sake of Christ. 8What is more, I consider everything a loss because of the surpassing worth of knowing Christ Jesus my Lord, for whose sake I have lost all things. I consider them garbage, that I may gain Christ 9and be found in him, not having a righteousness of my own that comes from the law, but that which is through faith in3:9 Or through the faithfulness of Christ—the righteousness that comes from God on the basis of faith. 10I want to know Christ—yes, to know the power of his resurrection and participation in his sufferings, becoming like him in his death, 11and so, somehow, attaining to the resurrection from the dead.

12Not that I have already obtained all this, or have already arrived at my goal, but I press on to take hold of that for which Christ Jesus took hold of me. 13Brothers and sisters, I do not consider myself yet to have taken hold of it. But one thing I do: Forgetting what is behind and straining toward what is ahead, 14I press on toward the goal to win the prize for which God has called me heavenward in Christ Jesus.

Following Paul’s Example

15All of us, then, who are mature should take such a view of things. And if on some point you think differently, that too God will make clear to you. 16Only let us live up to what we have already attained.

17Join together in following my example, brothers and sisters, and just as you have us as a model, keep your eyes on those who live as we do. 18For, as I have often told you before and now tell you again even with tears, many live as enemies of the cross of Christ. 19Their destiny is destruction, their god is their stomach, and their glory is in their shame. Their mind is set on earthly things. 20But our citizenship is in heaven. And we eagerly await a Savior from there, the Lord Jesus Christ, 21who, by the power that enables him to bring everything under his control, will transform our lowly bodies so that they will be like his glorious body.