Waebrania 5 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Waebrania 5:1-14

15:1 Ebr 2:17; 8:3; 9:9-27Kwa maana kila kuhani mkuu anayechaguliwa miongoni mwa wanadamu anawekwa kuwawakilisha kwa mambo yanayomhusu Mungu, ili apate kutoa matoleo na dhabihu kwa ajili ya dhambi. 25:2 Ebr 2:18; 4:15; 7:28Kwa kuwa yeye mwenyewe ni dhaifu, aweza kuwachukulia kwa upole wale wasiojua na kupotoka. 35:3 Law 4:3; 9:7; 16:6; 15:16, 17; Ebr 7:27; 9:7Hii ndiyo sababu inampasa kutoa dhabihu kwa ajili ya dhambi zake mwenyewe na vivyo hivyo kwa ajili ya dhambi za watu. 45:4 Kut 28:1; Hes 14:40; 18:7; 2Nya 26:18; 1Nya 23:13; Yn 3:27Hakuna anayejitwalia heshima hii mwenyewe; ni lazima aitwe na Mungu, kama vile Aroni alivyoitwa. 55:5 Yn 8:54; Ebr 2:17; 1:5; 1:1; Za 2:7; Mdo 13:33Pia Kristo hakujitwalia utukufu yeye mwenyewe wa kuwa Kuhani Mkuu, bali Mungu alimwambia,

“Wewe ni Mwanangu;

leo mimi nimekuzaa.”

65:6 Ebr 5:10; 6:20; 7:2-22; 7:17, 21; Mwa 14:18; Za 110:4Pia mahali pengine asema,

“Wewe ni kuhani milele,

kwa mfano wa Melkizedeki.”

75:7 Lk 22:41-44; 23:46; Mt 27:46; Za 22:24; Mk 14:36Katika siku za maisha ya Yesu hapa duniani, alimtolea maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, yeye awezaye kumwokoa na mauti, naye Mungu akamsikia kwa sababu ya kutii kwake kwa unyenyekevu. 85:8 Ebr 1:2; 3:6; Flp 2:8Ingawa alikuwa Mwana, alijifunza utiifu kutokana na mateso aliyoyapata, 95:9 Ebr 2:10; 11:40; Isa 45:17; Yn 17:1, 5na akiisha kukamilishwa, akawa chanzo cha wokovu wa milele kwa wote wanaomtii. 105:10 Ebr 5:6; 6:20; 2:17Naye amewekwa na Mungu kuwa Kuhani Mkuu kwa mfano wa Melkizedeki.

Wito Wa Kukua Kiroho

115:11 Yn 16:12; 2Pet 3:16; Mt 13:15Tunayo mengi ya kusema kuhusu habari ya ukuhani huu, lakini ni vigumu kuyaeleza, kwa sababu ninyi ni wazito wa kuelewa. 125:12 Ebr 6:1; 1Kor 3:2; 1Pet 2:2Kwa hakika, ingawa mpaka wakati huu ingewapasa kuwa walimu, bado mnahitaji mtu wa kuwafundisha tena hatua za awali za kweli ya Neno la Mungu. Mnahitaji maziwa, wala si chakula kigumu! 135:13 1Kor 13:11; 14:20; Efe 4:14; 1Pet 2:2Kwa maana yeyote aishiye kwa kunywa maziwa bado yeye ni mtoto mchanga, hana ujuzi katika mafundisho kuhusu neno la haki. 145:14 1Kor 2:6; Isa 7:15; 1Kor 2:14, 15Lakini chakula kigumu ni kwa ajili ya watu wazima, ambao kwa kujizoeza wamejifunza kupambanua kati ya mema na mabaya.

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

希伯來書 5:1-14

1從人間選出來的大祭司,都是受委任代表人辦理與上帝有關的事,為人的罪向上帝獻上禮物和贖罪祭。 2他能體諒那些無知和迷失的人,因為他自己也有人性的軟弱。 3所以,他不但要為眾人的罪獻祭,也要為自己的罪獻祭。 4沒有人能自取這大祭司的尊榮,只有像亞倫一樣蒙上帝呼召的人才可以做大祭司。

5同樣,基督也沒有自取榮耀做大祭司,是上帝對祂說:

「你是我的兒子,

我今日成為你父親。」

6在聖經的另一處,上帝又說:

「你照麥基洗德的模式永遠做祭司。」

7基督在世為人的時候,曾經聲淚俱下地祈求能救祂脫離死亡的上帝。祂因為敬虔而蒙了應允。 8基督雖然是上帝的兒子,仍然從所受的苦難中學習了順服。 9祂既然達到了純全的地步,就成了永恆救恩的源頭,使所有順服祂的人都得到拯救。 10上帝照著麥基洗德的模式立祂做大祭司。

信徒要長進

11關於這方面的事,我們還有很多話要說,但因為你們已經聽不進去,很難向你們解釋。 12按你們學習的時間來算,你們本該做別人的老師了,可惜你們還需要別人向你們傳授上帝話語的基本道理,成了不能吃乾糧、只能吃奶的人。 13因為只能吃奶的人還是嬰孩,不熟習仁義的道理。 14乾糧是給成年人吃的,他們的心思歷經鍛煉,能夠分辨善惡。