Waebrania 12 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Waebrania 12:1-29

Mungu Huwaadibisha Wanawe

112:1 1Kor 9:24; Ebr 10:36Kwa sababu hii, kwa kuwa tumezungukwa na wingu kubwa namna hii la mashahidi, basi na tuweke kando kila kitu kinachotuzuia na ile dhambi inayotuzinga kwa urahisi, nasi tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa kwa ajili yetu. 212:2 Za 25:15; Ebr 2:10; Flp 2:8, 9; Ebr 13:13; Mk 16:19Basi na tumtazame sana Yesu mwanzilishi na mkamilishaji wa imani yetu, yeye ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake alistahimili msalaba, bila kujali aibu ya huo msalaba, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu. 312:3 Gal 6:9; Ufu 2:3Mtafakarini sana yeye aliyestahimili upinzani mkuu namna hii kutoka kwa watu wenye dhambi, ili kwamba msije mkachoka na kukata tamaa.

412:4 Ebr 10:32-34; 13:13Katika kushindana kwenu dhidi ya dhambi, bado hamjapigana kiasi cha kumwaga damu yenu. 512:5 Ebr 12:3; Mit 3:11, 12Nanyi mmesahau yale maneno ya kuwaonya yanayowataja ninyi kuwa wana, yakisema:

“Mwanangu, usidharau adhabu ya Bwana,

wala usikate tamaa akikukemea,

612:6 Za 94:12; 119:75; Ufu 3:19; Mit 3:11, 12kwa sababu Bwana huwaadibisha wale awapendao,

na humwadhibu kila mmoja

anayemkubali kuwa mwana.”

712:7 Kum 8:5; 2Sam 7:14; Mit 13:24Vumilieni taabu kwa ajili ya kufunzwa adabu. Mungu anawatendea ninyi kama watoto wake, kwa maana ni mtoto yupi asiyeadibishwa na mzazi wake? 812:8 1Pet 5:9Kama hakuna kuadibishwa (ambalo ni fungu la watoto wote), basi ninyi ni watoto wa haramu wala si watoto halali. 912:9 Hes 16:22; 27:16; Ufu 22:6; Isa 38:16Tena, sisi sote tunao baba wa kimwili, waliotuadibisha nasi tukawaheshimu kwa ajili ya hilo. Je, si inatupasa kujinyenyekeza zaidi kwa Baba wa roho zetu ili tuishi? 1012:10 2Pet 1:4Baba zetu walituadibisha kwa kitambo kidogo kama wao wenyewe walivyoona vyema, lakini Mungu hutuadibisha kwa faida yetu ili tupate kushiriki utakatifu wake. 1112:11 Isa 32:17; Yak 3:17, 18Kuadibishwa wakati wowote hakuonekani kuwa kitu cha kufurahisha bali chenye maumivu kinapotekelezwa. Lakini baadaye huzaa matunda ya haki na amani kwa wale waliofunzwa nayo.

1212:12 Isa 35:3Kwa hiyo, itieni nguvu mikono yenu iliyo dhaifu na magoti yenu yaliyolegea. 1312:13 Mit 4:26; Gal 6:1Sawazisheni mapito ya miguu yenu, ili kitu kilicho kiwete kisidhoofishwe bali kiponywe.

Onyo Dhidi Ya Kuikataa Neema Ya Mungu

1412:14 Rum 14:19; 6:22; Mt 5:8Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote na huo utakatifu, ambao bila kuwa nao hakuna mtu atakayemwona Bwana. 1512:15 Gal 5:4; Ebr 3:12; 4:1; Kum 29:18Angalieni sana mtu yeyote asiikose neema ya Mungu na kwamba shina la uchungu lisije likachipuka na kuwasumbua na watu wengi wakatiwa unajisi kwa hilo. 1612:16 1Kor 6:18Angalieni miongoni mwenu asiwepo mwasherati au mtu asiyemcha Mungu kama Esau, ambaye kwa ajili ya mlo mmoja aliuza haki ya uzaliwa wake wa kwanza. 1712:17 Mwa 27:30-40Baadaye kama mnavyofahamu, alipotaka kurithi ile baraka, alikataliwa, maana hakupata nafasi ya kutubu, ingawa aliitafuta kwa machozi.

1812:18 Kut 19:12-22; 20:18; Kum 4:11Hamjaufikia mlima ule uwezao kuguswa na ambao unawaka moto; wala kwenye giza, utusitusi na dhoruba; 1912:19 Kut 20:18; Kum 4:12; Kut 20:19; Kum 5:5, 25; 18:16kwenye mlio wa tarumbeta, au kwenye sauti isemayo maneno ya kutisha kiasi ambacho wale walioisikia waliomba wasiambiwe neno jingine zaidi, 2012:20 Kut 19:12, 13kwa sababu hawangeweza kustahimili neno lile lililoamriwa: “Hata kama mnyama atagusa mlima huu, atapigwa mawe.” 2112:21 Kum 9:19Waliyoyaona yalikuwa ya kutisha kiasi kwamba Mose alisema, “Ninatetemeka kwa hofu.”

2212:22 Isa 24:23; 60:14; Ufu 14:1; Gal 4:26; Ebr 11:10; 13:14; Mit 16:16Lakini ninyi mmekuja Mlima Sayuni, Yerusalemu ya mbinguni, mji wa Mungu aliye hai. Mmekuja penye kusanyiko kubwa la malaika maelfu kwa maelfu wasiohesabika wanaoshangilia, 23kwenye kanisa la wazaliwa wa kwanza wa Mungu, ambao majina yao yameandikwa mbinguni. Mmekuja kwa Mungu, mhukumu wa watu wote, kwenye roho za wenye haki waliokamilishwa, 2412:24 Gal 3:20; Ebr 9:19; 10:22; 1Pet 1:2; Mwa 4:10; Ebr 11:4kwa Yesu mpatanishi wa agano jipya, na kwa damu iliyonyunyizwa, ile inenayo mambo mema kuliko damu ya Abeli.

2512:25 Ebr 3:12; 1:1; 8:5; 11:7; 2:2, 3; 10:29; Kum 18:19Angalieni, msije mkamkataa yeye anenaye. Ikiwa wao hawakuepuka adhabu walipomkataa yeye aliyewaonya hapa duniani, sisi je, tutaokokaje tusipomsikiliza yeye anayetuonya kutoka mbinguni? 2612:26 Kut 19:18; Hag 2:6Wakati ule sauti yake ilitetemesha dunia, lakini sasa ameahidi, “Kwa mara moja tena nitatetemesha si nchi tu bali na mbingu pia.”

2712:27 Isa 34:4; 54:10; 1Kor 7:31; Ebr 1:11; 2Pet 3:10; 1Yn 2:17Maneno haya “kwa mara moja tena” yanaonyesha kuondoshwa kwa vile vitu vinavyoweza kutetemeshwa, yaani vile vitu vilivyoumbwa, kwa kusudi vile tu visivyoweza kutetemeshwa vibaki.

2812:28 Za 15:5; Dan 2:44; Mal 2:5; 4:2; Ebr 13:15Kwa hiyo, kwa kuwa tunapokea ufalme ambao hauwezi kutetemeshwa, basi na tuwe na shukrani, na hivyo tumwabudu Mungu kwa namna inayompendeza, kwa unyenyekevu na uchaji, 2912:29 Kut 24:17; Kum 4:24; 9:3; Za 97:3; Isa 33:14; 1The 1:7kwa kuwa “Mungu wetu ni moto ulao.”

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

希伯來書 12:1-29

仰望耶穌

1既然有這麼多見證人像雲彩一般圍繞著我們,我們就要放下一切重擔,擺脫容易纏累我們的罪,以堅忍的心奔跑我們前面的賽程, 2定睛仰望為我們的信心創始成終的耶穌。祂為了擺在前面的喜樂,就輕看羞辱,忍受了十字架的痛苦,如今已坐在上帝寶座的右邊。 3你們要思想忍受罪人如此頂撞的主,免得疲倦灰心。

愛的管教

4其實你們與罪惡搏鬥,還沒有抵擋到流血的地步。 5你們難道忘了那像勸勉兒子一樣勸勉你們的話嗎?「孩子啊,不可輕視主的管教,被祂責備的時候也不要灰心。 6因為主管教祂所愛的人,責罰12·6 責罰」希臘文是「鞭打」之意。祂收納的兒子。」

7你們要忍受管教,上帝對待你們如同對待自己的兒子。哪有兒子不受父親管教的呢? 8做子女的都會受管教,如果沒人管教你們,那你們就是私生子,不是兒子。 9再者,我們的生身父親管教我們,我們尚且敬重他們,何況是萬靈之父上帝管教我們,我們豈不更要順服祂並得到生命嗎? 10我們的生身父親是按自己以為好的標準暫時管教我們,但上帝是為了我們的益處而管教我們,使我們可以在祂的聖潔上有份。 11被管教的滋味絕不好受,當時都很痛苦,但事後那些受過管教的人會收穫公義和平安的果子。 12所以,你們要舉起下垂的手,挺直發酸的腿, 13修直腳下的路,使瘸腿的人不致扭傷腳,反得痊癒。

切勿違背上帝

14你們要盡力與大家和睦相處,並要追求聖潔的生活,因為不聖潔的人不能見主。 15你們要謹慎,以免有人失去上帝的恩典,長出苦毒的根擾亂你們,玷污眾人。 16要小心,免得有人像以掃那樣淫亂、不敬虔。他為了一時的口腹之慾,賣了自己長子的名分。 17你們知道,他後來想要承受父親對長子的祝福,卻遭到拒絕,雖然聲淚俱下,終無法使父親回心轉意。

18你們並非來到那座摸得到、有火焰、烏雲、黑暗、狂風、 19號角聲和說話聲的西奈山,聽見這些聲音的人都哀求不要再向他們說話了。 20因為他們承擔不了所領受的命令:「即便是動物靠近這山,也要用石頭打死牠!」 21那情景實在可怕,就連摩西也說:「我嚇得發抖。」

22但你們現在來到了錫安山,永活上帝的城邑,天上的耶路撒冷,歡聚著千萬天使的地方。 23這裡有名字記錄在天上的眾長子的教會,有審判眾人的上帝和已達到純全的義人的靈魂, 24還有新約的中保耶穌和祂所流的血。這血比亞伯的血發出更美的信息。

25你們必須謹慎,切勿拒絕對你們說話的上帝。因為以色列人違背了在地上警戒他們的人,尚且逃脫不了懲罰,何況我們違背從天上警戒我們的上帝呢? 26那時上帝的聲音震動了大地,但現在祂應許說:「再一次,我不單要震動地,還要震動天。」 27「再一次」這句話是指上帝要挪去可以被震動的受造之物,使不能被震動的可以長存。 28那麼,既然我們承受的是一個不能被震動的國度,就要感恩,用虔誠和敬畏的心事奉上帝,討祂喜悅。 29因為我們的上帝是烈火。