Waamuzi 17 – NEN & JCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Waamuzi 17:1-13

Sanamu Za Mika

117:1 Amu 18:2, 13Palikuwa na mtu aliyeitwa Mika ambaye aliishi katika vilima vya Efraimu. 217:2 Rut 2:20; 3:10; 1Sam 15:13; 23:21; 2Sam 2:5Akamwambia mama yake, “Zile shekeli 1,10017:2 Shekeli 1,100 za fedha ni sawa na kilo 13 za fedha. za fedha zilizochukuliwa kwako, ambazo nilisikia ukizinenea maneno ya laana, hizi hapa; mimi ndiye niliyezichukua, lakini sasa ninakurudishia.”

Ndipo mama yake akamwambia, “Bwana na akubariki, mwanangu.”

317:3 Kut 34:17; Law 19:4; Kut 20:4Alipozirudisha zile shekeli 1,100 za fedha kwa mama yake, mama yake akamwambia, “Mimi nimeiweka fedha hii wakfu kwa Bwana kwa ajili ya mwanangu kutengenezea kinyago cha kuchonga na sanamu ya kusubu. Mimi nitakurudishia wewe.”

417:4 Kut 32:4; Isa 17:8Hivyo akamrudishia mama yake ile fedha, naye mama yake akachukua shekeli mia mbili17:4 Shekeli 200 za fedha ni sawa na kilo 2.3 za fedha. za hiyo fedha na kumpa mfua fedha, ambaye aliifanyiza kinyago na sanamu. Navyo vikawekwa ndani ya nyumba ya Mika.

517:5 Isa 44:13; Eze 8:10; Amu 8:27; Mwa 31:19; Hes 16:10; Kut 29:9; Amu 18:24Basi Mika alikuwa na mahali pa kuabudia miungu, akatengeneza naivera, pamoja na vinyago, na kumweka mmoja wa wanawe kuwa kuhani wake. 617:6 Amu 18:1; 19:1; 21:25; Kum 12:8Katika siku hizo Israeli hawakuwa na mfalme, kila mmoja akafanya kama alivyoona vyema machoni pake mwenyewe.

717:7 Amu 18:3; Mwa 35:19; Mik 5:2; Mt 2:1Basi palikuwa na kijana mmoja wa Bethlehemu ya Yuda. Yeye alikuwa Mlawi aliyeishi miongoni mwa kabila la Yuda. 8Huyu kijana akatoka katika mji huo wa Bethlehemu ya Yuda na kutafuta mahali pengine ambapo angeweza kuishi. Alipokuwa akisafiri, akafika nyumbani kwa Mika katika vilima vya Efraimu.

9Mika akamuuliza, “Wewe umetoka wapi?”

Akamjibu, “Mimi ni Mlawi kutoka Bethlehemu ya Yuda, ninatafuta mahali pa kuishi.”

1017:10 Mwa 45:8; Amu 18:19Ndipo Mika akamwambia, “Ishi pamoja nami, uwe baba yangu na kuhani wangu, nami nitakupa shekeli kumi17:10 Shekeli 10 za fedha ni sawa na gramu 115 za fedha. za fedha, nguo na chakula.” 11Hivyo yule Mlawi akakubali kuishi pamoja naye, naye huyo kijana akawa kwake kama mmoja wa wanawe. 1217:12 Hes 16:10; Amu 18:4Hivyo Mika akamweka wakfu huyo kijana Mlawi, naye huyo akawa kuhani wake na kuishi nyumbani mwake. 1317:13 Hes 18:7Ndipo Mika akasema, “Sasa najua Bwana atanitendea mema, kwa kuwa Mlawi huyu amekuwa kuhani wangu.”

Japanese Contemporary Bible

士師記 17:1-13

17

ミカの偶像

1エフライムの山地に、ミカという名の人が住んでいました。 2ある日、彼は母親に言いました。「盗まれたとお母さんがしきりにのろって言っていた銀千百枚のことだけど、実はあれは私が盗んだのです。」すると母親は、「よく正直に話してくれたね。主が祝福してくださるように」と答えました。 3ミカがその金を母親に返した時、彼女は言いました。「おまえの名誉のためにも、これを主にささげます。これでおまえのために彫像を造り、銀をはってもらいましょう。」 4-5母親は銀二百枚を銀細工人に渡し、彫像を造らせました。彫像は、屋敷内にあるミカの聖堂に安置されました。ミカはたくさんの偶像を集めており、エポデとテラフィム(占いや霊媒に使う偶像)もそろえて、息子の一人を祭司に任命していたほどでした。 6当時イスラエルには王がなく、各人各様、自分の目に正しいと思うことを行っていたのです。

7-8ある日、ユダのベツレヘム出身の若い祭司が、安住の地を求めてエフライム地方にやって来ましたが、道中、ふとミカの家の前で立ち止まりました。 9ミカは、「どちらからお越しですか」と尋ねました。

「ユダのベツレヘムから参った祭司です。どこか住むのによい所はないものかと、旅しております。」

10-11「よろしければ、ここにとどまってください。私どもの祭司になっていただきたいのです。毎年、銀十枚と新しい衣服ひとそろい、それに生活費いっさいを面倒みて差し上げますよ。」

若者は同意し、ミカの家族同様の扱いを受けました。 12ミカはおかかえの祭司を得たのです。 13「私は今、主からほんとうに祝福していただいた。正真正銘の祭司がいるのだから」と、彼は感激して言いました。