Waamuzi 11 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Waamuzi 11:1-40

111:1 Amu 12:1; 1Sam 12:11; Ebr 11:32; Amu 6:12; Hes 26:29; Mwa 38; 15Basi Yefta Mgileadi alikuwa mtu shujaa. Baba yake alikuwa Gileadi, naye mama yake alikuwa kahaba. 2Mke wa Gileadi akamzalia wana wengine, nao watoto hao walipokua, wakamfukuza Yefta na kumwambia, “Wewe huwezi kupata urithi katika jamii yetu, kwa sababu wewe ni mwana wa mwanamke mwingine.” 311:3 2Sam 10:6-8; Amu 9:4Basi Yefta akawakimbia ndugu zake akaenda kuishi katika nchi ya Tobu, mahali ambako watu waasi walijiunga naye na kumfuata.

411:4 Amu 10:9Baada ya muda Waamoni wakafanya vita na Israeli, 5viongozi wa Gileadi wakaenda kumchukua Yefta katika nchi ya Tobu. 6Wakamwambia Yefta, “Uwe jemadari wetu, ili tuweze kupigana na Waamoni.”

711:7 Mwa 26:16, 27Yefta akawaambia, “Je, hamkunichukia mimi na kunifukuza katika nyumba ya baba yangu? Kwa nini mnanijia sasa, wakati mna matatizo.”

811:8 Amu 10:18Viongozi wa Gileadi wakamwambia Yefta, “Lakini sasa tumegeuka kukuelekea wewe, ili uende pamoja nasi kupigana na Waamoni, nawe utakuwa kiongozi wetu juu ya watu wote wa Gileadi.”

9Yefta akawaambia, “Ikiwa mtanirudisha kwetu kupigana na Waamoni, naye Bwana akanisaidia kuwashinda, Je, ni kweli nitakuwa kiongozi wenu?”

1011:10 Mwa 31:50; Isa 1:2; Yer 42:5Viongozi wa Gileadi wakamjibu Yefta, “Bwana ndiye shahidi yetu. Kwa hakika tutafanya kama usemavyo.” 1111:11 1Sam 9:4; 2Sam 3:17; Kut 19:9; 1Sam 8; 21; Yos 11:3Basi Yefta akaenda na viongozi wa Gileadi, nao watu wakamfanya kiongozi na jemadari wao. Naye akarudia maneno yake yote mbele za Bwana huko Mispa.

12Ndipo Yefta akatuma wajumbe kwa mfalme wa Waamoni akisema, “Una nini juu yetu, hata umekuja kushambulia nchi yetu?”

1311:13 Hes 21:13; 21:24; Mwa 32:22Mfalme wa Waamoni akawajibu wajumbe wale wa Yefta, “Wakati Waisraeli walipopanda kutoka Misri, waliichukua nchi yangu kuanzia Arnoni mpaka Yaboki, hadi kufikia Yordani. Sasa rudisha kwa amani.”

14Yefta akarudisha wajumbe kwa mfalme wa Waamoni, 1511:15 Kum 2:9; 1:19kusema:

“Hili ndilo asemalo Yefta, Israeli hawakuchukua nchi ya Moabu wala ya Waamoni. 1611:16 Hes 14:25; Kum 1:40; Mwa 14:7; Hes 20:1Lakini walipopanda kutoka Misri, Israeli walipitia katika jangwa hadi Bahari ya Shamu na wakafika Kadeshi. 1711:17 Mwa 32:3; Hes 20:14-17; Yer 48:1; Yos 24:9Ndipo Israeli wakatuma wajumbe kwa mfalme wa Edomu, wakisema, ‘Tupe ruhusa kupita katika nchi yako,’ Lakini mfalme wa Edomu hakutusikia. Wakapeleka pia wajumbe kwa mfalme wa Moabu, naye akakataa. Kwa hiyo Israeli wakakaa huko Kadeshi.

1811:18 Hes 20:21; Kum 2:8; Hes 21:13; 21:4“Baadaye wakasafiri kupitia jangwa, wakiambaa na nchi za Edomu na Moabu, wakapitia upande wa mashariki wa nchi ya Moabu na kupiga kambi upande mwingine wa Arnoni. Hawakuingia katika nchi ya Moabu, kwa kuwa Arnoni ilikuwa mpaka wake.

1911:19 Hes 21:21-22; Yos 12:2; Kum 2:26-27“Kisha Israeli wakatuma wajumbe kwa Sihoni mfalme wa Waamori, aliyetawala Heshboni, na kumwambia, ‘Tupe ruhusa kupita katika nchi yako ili kufikia mahali petu.’ 2011:20 Hes 21:23; Kum 2:32Hata hivyo, Sihoni hakuwaamini Waisraeli kupita katika nchi yake. Akaandaa jeshi lake lote na kupiga kambi huko Yahasa, nao wakapigana na Israeli.

21“Ndipo Bwana, Mungu wa Israeli, akamtia Sihoni na watu wake wote mikononi mwa Israeli, nao wakawashinda. Israeli wakaitwaa nchi yote ya Waamori, waliokuwa wakiishi katika nchi hiyo, 2211:22 Hes 21:21-22; Kum 2:36wakiiteka nchi yote kuanzia Arnoni mpaka Yaboki, na kutoka jangwani mpaka Yordani.

23“Basi kwa kuwa Bwana, Mungu wa Israeli, amewafukuza Waamori watoke mbele ya watu wake Israeli, wewe unayo haki gani ya kuitamalaki? 2411:24 Hes 21:29; Yos 3:10; Kum 2:3; 1Fal 11:7Je, haikupasi kuchukua kile ambacho mungu wako Kemoshi amekupa? Vivyo hivyo, chochote kile Bwana Mungu wetu alichotupa sisi, tutakimiliki. 2511:25 Hes 22:2; Yos 24:9Je, wewe ni bora kuliko Balaki mwana wa Sipori, mfalme wa Moabu? Je, yeye alishagombana na Israeli au kupigana nao wakati wowote? 2611:26 Hes 21:25; 32:34; Yos 13:9Kwa maana kwa miaka 300 Israeli wameishi Heshboni na vijiji vyake, Aroeri na vijiji vyake, na katika miji yote iliyo kando ya Arnoni. Kwa nini wewe haukuyachukua wakati huo? 2711:27 Mwa 18:25; 16:5; 2Nya 20; 12; Mwa 31:53; 1Sam 24:12-15Mimi sijakukosea jambo lolote, bali wewe ndiye unayenikosea kwa kufanya vita nami. Basi Bwana, aliye Mwamuzi, leo na aamue ugomvi kati ya Waisraeli na Waamoni.”

28Hata hivyo, Mfalme wa Waamoni, hakuyajali maneno ya ujumbe wa Yefta.

2911:29 Amu 3:10; Mwa 31:49; Amu 10:17; Hes 11:25; Isa 11; 2Ndipo Roho wa Bwana akaja juu ya Yefta. Akapita katikati ya Gileadi na Manase, pia akapita katika Mispa ya Gileadi, na kutokea huko akasonga mbele kushambulia Waamoni. 3011:30 Mwa 28:20; Hes 30:10; 1Sam 1:11; Mit 31:2Naye Yefta akaweka nadhiri mbele za Bwana akisema, “Ikiwa utawatia Waamoni mikononi mwangu, 3111:31 Mwa 28:21; 8:20; Law 1:3; Amu 13:16chochote kile kitakachotoka katika mlango wa nyumba yangu cha kwanza ili kunilaki nirudipo kwa amani katika kuwashinda Waamoni, kitakuwa ni cha Bwana na nitakitoa kuwa sadaka ya kuteketezwa.”

32Ndipo Yefta akavuka kupigana na hao Waamoni, naye Bwana akawatia mkononi mwake. 3311:33 Eze 27:17Akawapiga kwa ushindi mkubwa kuanzia Aroeri mpaka karibu na Minithi na kuendelea mpaka Abel-Keramimu, miji yote iliyopigwa ni ishirini. Basi Israeli wakawashinda Waamoni.

3411:34 Kut 15:20; Mwa 31:27; Yer 31:4; Zek 12; 10Yefta aliporudi nyumbani Mispa, tazama, binti yake akatoka ili kumlaki kwa matari na kucheza. Alikuwa ndiye mtoto pekee, hakuwa na mwana wala binti mwingine. 3511:35 Hes 14:6; 30:2; Kum 23:21; Mhu 5:2-5Alipomwona akararua mavazi yake akalia, “Ee! Binti yangu! Umenifanya niwe na huzuni na kunyongʼonyea sana, kwa kuwa nimeweka nadhiri kwa Bwana, ambayo siwezi kuivunja.”

3611:36 Lk 1:38; Hes 31:3; 2Sam 18:19Akajibu, “Baba yangu, umetoa neno lako kwa Bwana. Nitendee mimi kama vile ulivyoahidi, kwa kuwa Bwana amekupa ushindi dhidi ya adui zako Waamoni.” 37Naye akamwambia baba yake, “Naomba nifanyiwe jambo hili. Nipewe miezi miwili ili kuzunguka vilimani nikaulilie ubikira wangu, mimi na wenzangu.”

38Baba yake akamwambia, “Waweza kwenda.” Naye akamwacha aende kwa miezi miwili. Hivyo akaondoka pamoja na wasichana wenzake, naye akaulilia ubikira wake huko vilimani kwa sababu asingeolewa kamwe. 39Baada ya hiyo miezi miwili, alirejea kwa baba yake, naye baba yake akamtendea kama alivyokuwa ametoa nadhiri yake. Naye alikuwa bikira.

Nayo ikawa desturi katika Israeli, 40kwamba kila mwaka binti wa Israeli huenda kwa siku nne ili kumkumbuka huyo binti wa Yefta, Mgileadi.

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

士师记 11:1-40

士师耶弗他

1基列耶弗他是个英勇的战士,他父亲名叫基列,母亲是个妓女。 2基列的妻子还生了几个儿子,他们长大后,便把耶弗他赶出家门,说:“你是别的女人生的,你休想继承我们父亲的任何产业。” 3耶弗他只好逃走,住在陀伯地区。有一群匪徒跟随了他。

4后来,亚扪人攻打以色列5基列的众长老就去陀伯耶弗他6对他说:“请你回来做统帅带领我们对抗亚扪人。” 7耶弗他说:“从前你们不是厌恶我,把我从父亲家赶走的吗?现在你们遭难,为什么来找我?” 8基列的众长老说:“现在我们是来请你跟我们一起回去抵抗亚扪人,你可以做所有基列人的首领。” 9耶弗他说:“如果我跟你们回去与亚扪人作战,耶和华让我打败他们,我就真的可以做你们的首领吗?” 10基列的首领们说:“我们必听从你的吩咐,有耶和华为我们作证。” 11于是,耶弗他便跟他们一起回去。民众拥立他做他们的首领和元帅。耶弗他米斯巴将之前所说的话在耶和华面前重申一遍。

12然后,他派遣使者去问亚扪王:“你与我有什么相干?为什么要攻打我的领土?” 13亚扪王对他的使者说:“因为以色列人从埃及出来的时候占据了我们的土地——从亚嫩河到雅博河,一直到约旦河。现在你们要乖乖地把这些土地还给我们。” 14耶弗他再差遣使者去见亚扪王, 15对他说:“以色列人并没有占据摩押亚扪的土地。 16当年以色列人离开埃及,经旷野渡过红海来到加低斯17然后派遣使者去见以东王,说,‘求你让我们经过你的领土。’以东王却不答应。他们又派遣使者去见摩押王,摩押王也不答应。于是,以色列人就住在加低斯18后来,他们走过旷野,绕过以东摩押,到了摩押的东边,在摩押的边界亚嫩河东岸扎营,并没有进入摩押境内。 19以色列人派遣使者去见希实本亚摩利西宏,对他说,‘求让我们经过你的领土前往我们自己的土地。’ 20西宏不信任以色列人,拒绝了他们的请求,并招聚全军驻扎在雅杂,攻打他们。 21以色列的上帝耶和华帮助以色列人战胜西宏和他的军队,占领了他们所有的土地, 22亚嫩河直到雅博河,从旷野直到约旦河。 23既然是以色列的上帝耶和华为祂的以色列子民赶走了亚摩利人,你凭什么要夺取这块土地? 24你拥有你们的神明基抹给你们的土地,我们也要拥有我们的上帝耶和华赐给我们的土地。 25难道你比摩押西拨的儿子巴勒更强吗?他从未挑战过以色列人,也未和以色列人交过战。 26三百年来,以色列人一直住在希实本及其周围的乡村、亚罗珥及其周围的乡村和亚嫩河沿岸一带的城邑。在这期间,你们为什么不收回这些土地呢? 27我们没有得罪你们,你们却攻打我们。愿审判者耶和华今天在以色列人和亚扪人之间主持公道。” 28可是,亚扪王不理会耶弗他派使者所传的话。

29那时,耶和华的灵降在耶弗他身上,他便经过基列玛拿西,来到基列米斯巴,然后从那里去迎战亚扪人。 30他向耶和华许愿说:“如果你把亚扪人交在我手中, 31让我凯旋而归,第一个从我家门出来迎接我的人必归给你,我必把他献给你作燔祭。” 32于是,耶弗他率军与亚扪人作战,耶和华把敌人交在他手中, 33他大败敌军,摧毁了从亚罗珥米匿、远至亚备勒·基拉明的二十座城。这样,以色列人征服了亚扪人。

34耶弗他返回自己在米斯巴的家,他的独生女儿敲着鼓、跳着舞出来迎接他。 35他一见自己的女儿,便撕裂衣服,说:“唉,我的女儿啊,你真让我伤心欲绝!我向耶和华许了愿,不能收回了!” 36他女儿说:“父亲啊,你既然向耶和华许了愿,就照你许的愿对待我吧!因为耶和华帮你打败了敌军亚扪人,为你报了仇。 37但求你先给我两个月的时间,让我和同伴到山上去为我终身未嫁哀哭。” 38耶弗他答应了,给了她两个月的时间。于是,她便和同伴到山上为自己终身未嫁哀哭。 39两个月后,她回到父亲那里。她父亲履行了自己所许的愿。她终身未嫁。自此以后,在以色列有个习俗: 40每年以色列的女子都去为基列耶弗他的女儿哀哭四天。