Ufunuo 21 – Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) NEN

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Ufunuo 21:1-27

Mbingu Mpya Na Nchi Mpya

121:1 Isa 65:17; 2Pet 3:13Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya, kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza vimekwisha kupita, wala hapakuwepo na bahari tena. 221:2 Ebr 11:10; 12:22Nikaona Mji Mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, ukiwa umeandaliwa kama bibi arusi aliyepambwa kwa ajili ya mumewe. 321:3 2Kor 6:16; Zek 2:10; Isa 8:8Nami nikasikia sauti kubwa kutoka kile kiti cha enzi ikisema, “Sasa makao ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atakaa pamoja nao. Yeye atakuwa Mungu wao nao watakuwa watu wake, naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao. 421:4 Ufu 7:17; 1Kor 15:26; Isa 35:10; 65:19Atafuta kila chozi kutoka macho yao. Mauti haitakuwepo tena, wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu, kwa maana mambo ya kwanza yamekwisha kupita.”

521:5 Ufu 4:9; 20:11; 19:9Naye yule aliyeketi juu ya kile kiti cha enzi akasema, “Tazama, nayafanya mambo yote kuwa mapya!” Kisha akasema, “Andika haya, maana maneno haya ni ya kuaminika tena ni kweli.”

621:6 Ufu 16:17; 1:8; 22:13; Yn 4:10Akaniambia, “Imekwisha kuwa. Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Yeye aonaye kiu nitampa kunywa kutoka chemchemi ya maji ya uzima bila gharama yoyote. 721:7 Ufu 2:7; 2Sam 7:14Yeye ashindaye atayarithi haya yote, nami nitakuwa Mungu wake, naye atakuwa mwanangu. 821:8 Za 5:6; Ufu 2:11Lakini waoga, wasioamini, wachafu, wauaji, wazinzi, wachawi, waabudu sanamu, pamoja na waongo wote, mahali pao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.”

921:9 Ufu 15:1, 6, 7; 19:7Mmoja wa wale malaika saba waliokuwa na yale mabakuli saba ya hayo mapigo saba ya mwisho akaja akaniambia, “Njoo, nami nitakuonyesha bibi arusi, yaani, mke wa Mwana-Kondoo.” 1021:10 Ufu 17:3; 1:10; Eze 40:2; Ufu 21:2Naye akanichukua katika Roho hadi kwenye mlima mkubwa na mrefu, akanionyesha ule Mji Mtakatifu, Yerusalemu, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu. 1121:11 Ufu 15:8; 4:6; Isa 60:1, 2; Eze 43:2; Ufu 21:23; 21:18, 19Ulikuwa ukingʼaa kwa utukufu wa Mungu kama kito chenye thamani sana, kama yaspi, safi kama kioo. 1221:12 Eze 48:30-34Ulikuwa na ukuta mkubwa, mrefu wenye malango kumi na mawili, pakiwa na malaika kumi na wawili kwenye hayo malango. Kwenye malango hayo yaliandikwa majina ya yale makabila kumi na mawili ya Israeli. 1321:13 Eze 48:31, 34Kulikuwa na malango matatu upande wa mashariki, matatu upande wa kaskazini, matatu upande wa kusini na matatu upande wa magharibi. 1421:14 Efe 2:20; Ebr 11:10; Mdo 1:2621:14 Ufu 11:1; Eze 40:3; Ufu 21:12Ukuta wa huo mji ulikuwa na misingi kumi na miwili, na juu yake yaliandikwa majina ya wale mitume kumi na wawili wa Mwana-Kondoo.

15Huyo malaika aliyesema nami alikuwa na ufito wa dhahabu wa kupimia huo mji, malango yake na kuta zake. 1621:16 Eze 45:16; 48:16; 17Mji huo ulikuwa mraba, urefu wake ulikuwa sawa na upana wake. Akaupima huo mji kwa huo ufito akakuta una kama kilomita 2,200;21:16 Kilomita 2,200 hapa ni sawa na maili 1,200. urefu wake na upana wake na kwenda juu kwake vilikuwa sawa. 1721:17 Ufu 13:18Akaupima ukuta wake, ulikuwa na unene wa dhiraa 14421:17 Dhiraa 144 ni karibu mita 65. kwa kipimo cha kibinadamu ambacho huyo malaika alikuwa akikitumia. 1821:18 Ufu 21:11, 21Ukuta huo ulijengwa kwa yaspi hali mji wenyewe ulijengwa kwa dhahabu safi, ikingʼaa kama kioo. 1921:19 Kut 28:17-20Misingi ya kuta za mji huo zilipambwa kwa kila aina ya kito cha thamani. Msingi wa kwanza ulikuwa wa yaspi, wa pili yakuti samawi, wa tatu kalkedoni, wa nne zumaridi, 2021:20 Ufu 4:3wa tano sardoniki, wa sita akiki, wa saba krisolitho, wa nane zabarajadi, wa tisa yakuti manjano, wa kumi krisopraso, wa kumi na moja hiakintho, wa kumi na mbili amethisto. 2121:21 Ufu 21:12; Isa 54:12; Ufu 21:18Yale malango kumi na mbili yalikuwa ni lulu kumi na mbili, kila lango lilikuwa limetengenezwa kwa lulu moja. Barabara kuu ya mji huo ilikuwa ya dhahabu safi ingʼaayo kama kioo.

2221:22 Yn 4:21-23; Ufu 1:8; 5:6Sikuona Hekalu ndani ya huo mji kwa sababu Bwana Mungu Mwenyezi na Mwana-Kondoo ndio hekalu lake. 2321:23 Isa 24:23; 22:5Ule mji hauhitaji jua wala mwezi kuuangazia, kwa sababu utukufu wa Mungu ndio nuru yake na Mwana-Kondoo ndiye taa yake. 2421:24 Isa 60:3, 5Mataifa yatatembea yakiangaziwa na nuru yake na wafalme wa duniani wataleta fahari yao ndani yake. 2521:25 Isa 60:11; Zek 14:7; Ufu 22:5Malango yake hayatafungwa kamwe, kwa maana hakutakuwa na usiku humo. 2621:26 Ufu 21:24Utukufu na heshima za mataifa zitaletwa humo. 2721:27 Yoe 3:17; Ufu 22:14, 15Lakini kitu kichafu hakitaingia humo kamwe, wala mtu yeyote atendaye mambo ya aibu au ya udanganyifu. Bali watakaoingia humo ni wale tu ambao majina yao yameandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo.