Ufunuo 11 – NEN & NIVUK

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Ufunuo 11:1-19

Mashahidi Wawili

111:1 Eze 40:3; Ufu 21:15; 12:3; 11:19; Mwa 37:9Ndipo nikapewa mwanzi uliokuwa kama ufito wa kupimia, nikaambiwa, “Nenda ukapime hekalu la Mungu pamoja na madhabahu, nawe uwahesabu wale waabuduo humo. 211:2 Eze 40:17, 20; Lk 21:24; Ufu 21:2; Dan 12:7; Ufu 13:5Lakini usiupime ua wa nje wa Hekalu, uache, kwa sababu ua huo wamepewa watu wa Mataifa. Hao wataukanyagakanyaga mji mtakatifu kwa muda wa miezi arobaini na miwili. 311:3 Ufu 1:5; 2:13; Neh 9:1; Yon 3:5Nami nitawapa mashahidi wangu wawili uwezo, nao watoe unabii kwa muda wa siku 1,260, wakiwa wamevaa nguo za gunia.” 411:4 Za 52:8; Yer 11:16; Zek 4:14Hawa ndio ile mizeituni miwili na vile vinara viwili vya taa visimamavyo mbele za Bwana Mungu wa dunia yote. 511:5 2Sam 22:9; Ufu 9:17, 18; Hes 16:29, 35Kama mtu yeyote akitaka kuwadhuru, moto hutoka vinywani mwao na kuwateketeza adui zao. Hivi ndivyo impasavyo kufa mtu yeyote atakayetaka kuwadhuru. 611:6 Kut 7:17, 19; Ufu 8:8; Mt 2:13; Ufu 12:5Watu hawa wanao uwezo wa kufunga anga ili mvua isinyeshe wakati wote watakapokuwa wanatoa unabii wao. Nao watakuwa na uwezo wa kuyabadili maji kuwa damu na kuipiga dunia kwa kila aina ya mapigo mara kwa mara kama watakavyo.

711:7 Ufu 13:1-4; 13:7; Dan 7:21; 10:13, 21; 12:1; Yud 9; Mt 25:41Basi watakapokuwa wamemaliza ushuhuda wao, yule mnyama atokaye katika lile Shimo atapigana nao vita, atawashinda na kuwaua. 811:8 Yer 23:14; Eze 16:46; Hes 13:12Maiti zao zitabaki katika barabara ya mji mkubwa,11:8 Mji mkubwa hapa inamaanisha Yerusalemu ambako Bwana wao alisulubiwa. ambao kwa fumbo unaitwa Sodoma na Misri,11:8 Sodoma na Misri hapa inamaanisha Yerusalemu, kwa sababu mataifa watafanya uovu mwingi wa kila aina katika kipindi hicho cha miaka mitatu na nusu. ambapo pia Bwana wao alisulubiwa. 911:9 Za 79:2, 3Kwa muda wa siku tatu na nusu, watu wa kila kabila, jamaa, lugha na taifa wataziangalia hizo maiti zao na hawataruhusu wazikwe. 1011:10 Ufu 3:10; Neh 8:10, 12; Es 9:19, 22Watu waishio duniani watazitazama kwa furaha maiti za hao manabii wawili na kushangilia kwa kupeana zawadi kwa sababu hao manabii waliwatesa watu waishio duniani.

1111:11 Ufu 3:10; Neh 8:10, 12, 14Lakini baada ya zile siku tatu na nusu, pumzi ya uhai kutoka kwa Mungu ikawaingia, nao wakasimama kwa miguu yao na wote waliowaona wakaingiwa na hofu kuu. 1211:12 Ufu 4:1; 2Fal 2:11; Mdo 1:9Kisha wale manabii wawili wakasikia sauti kuu kutoka mbinguni ikiwaambia, “Njooni huku juu!” Nao wakapaa mbinguni katika wingu, wakati adui zao wakiwa wanawatazama.

1311:13 Ufu 6:12; 16:9; 19:7; 16:11; 12:3Saa iyo hiyo, kukatokea tetemeko kubwa la nchi na sehemu ya kumi ya mji ikaanguka. Watu elfu saba wakauawa katika tetemeko hilo, nao walionusurika wakaogopa sana, wakamtukuza Mungu wa mbinguni.

1411:14 Ufu 8:13Ole ya pili imekwisha kupita, tazama ole ya tatu inakuja upesi.

Tarumbeta Ya Saba

1511:15 Mt 24:31; Ufu 10:7; 6:10; 16:17; 19:1; 12:10; Za 145:13; Lk 1:33; Ufu 12:9Yule malaika wa saba akaipiga tarumbeta yake, pakawa na sauti kubwa mbinguni iliyosema:

“Ufalme wa ulimwengu umekuwa ufalme wa Bwana wetu na wa Kristo wake,

naye atatawala milele na milele.”

1611:16 Ufu 4:4Nao wale wazee ishirini na wanne, waliokuwa wameketi mbele za Mungu, kwenye viti vyao vya enzi, wakaanguka kifudifudi, wakamwabudu Mungu, 1711:17 Ufu 1:8; 19:6wakisema:

“Tunakushukuru, Bwana Mungu Mwenyezi,

uliyeko na uliyekuwako,

kwa kuwa umetwaa uweza wako mkuu

na ukaanza kutawala.

1811:18 Za 2:1; Ufu 10:7; 19:5Mataifa walikasirika nao

wakati wa ghadhabu yako umewadia.

Wakati umewadia wa kuwahukumu waliokufa

na kuwapa thawabu watumishi wako manabii

na watakatifu wako pamoja na wale wote

wanaoliheshimu Jina lako,

wakubwa kwa wadogo:

na kuwaangamiza wale wanaoiangamiza dunia.”

1911:19 Ufu 15:5, 8; 16:21Ndipo hekalu la Mungu lililoko mbinguni likafunguliwa, na sanduku la agano lake likaonekana humo ndani. Kukatokea mianga ya umeme wa radi, ngurumo, sauti za radi, tetemeko la nchi na mvua kubwa ya mawe.

New International Version – UK

Revelation 11:1-19

The two witnesses

1I was given a reed like a measuring rod and was told, ‘Go and measure the temple of God and the altar, with its worshippers. 2But exclude the outer court; do not measure it, because it has been given to the Gentiles. They will trample on the holy city for 42 months. 3And I will appoint my two witnesses, and they will prophesy for 1,260 days, clothed in sackcloth.’ 4They are ‘the two olive trees’ and the two lampstands, and ‘they stand before the Lord of the earth.’11:4 See Zech. 4:3,11,14. 5If anyone tries to harm them, fire comes from their mouths and devours their enemies. This is how anyone who wants to harm them must die. 6They have power to shut up the heavens so that it will not rain during the time they are prophesying; and they have power to turn the waters into blood and to strike the earth with every kind of plague as often as they want.

7Now when they have finished their testimony, the beast that comes up from the Abyss will attack them, and overpower and kill them. 8Their bodies will lie in the public square of the great city – which is figuratively called Sodom and Egypt – where also their Lord was crucified. 9For three and a half days some from every people, tribe, language and nation will gaze on their bodies and refuse them burial. 10The inhabitants of the earth will gloat over them and will celebrate by sending each other gifts, because these two prophets had tormented those who live on the earth.

11But after the three and a half days the breath11:11 Or Spirit (see Ezek. 37:5,14) of life from God entered them, and they stood on their feet, and terror struck those who saw them. 12Then they heard a loud voice from heaven saying to them, ‘Come up here.’ And they went up to heaven in a cloud, while their enemies looked on.

13At that very hour there was a severe earthquake and a tenth of the city collapsed. Seven thousand people were killed in the earthquake, and the survivors were terrified and gave glory to the God of heaven.

14The second woe has passed; the third woe is coming soon.

The seventh trumpet

15The seventh angel sounded his trumpet, and there were loud voices in heaven, which said:

‘The kingdom of the world has become

the kingdom of our Lord and of his Messiah,

and he will reign for ever and ever.’

16And the twenty-four elders, who were seated on their thrones before God, fell on their faces and worshipped God, 17saying:

‘We give thanks to you, Lord God Almighty,

the One who is and who was,

because you have taken your great power

and have begun to reign.

18The nations were angry,

and your wrath has come.

The time has come for judging the dead,

and for rewarding your servants the prophets

and your people who revere your name,

both great and small –

and for destroying those who destroy the earth.’

19Then God’s temple in heaven was opened, and within his temple was seen the ark of his covenant. And there came flashes of lightning, rumblings, peals of thunder, an earthquake and a severe hailstorm.