Ufunuo 10 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Ufunuo 10:1-11

Malaika Mwenye Kitabu Kidogo

110:1 Ufu 5:2; Mt 17:2; Ufu 1:16; 1:15Kisha nikamwona malaika mwingine mwenye nguvu akishuka kutoka mbinguni. Alikuwa amevikwa wingu na upinde wa mvua juu ya kichwa chake. Uso wake ulingʼaa kama jua na miguu yake ilikuwa kama nguzo za moto. 210:2 Ufu 10:8-10; 5:1; 10:5, 8Mkononi mwake alikuwa ameshika kijitabu kilichokuwa kimefunguliwa. Akauweka mguu wake wa kuume juu ya bahari na mguu wake wa kushoto akauweka juu ya nchi kavu. 310:3 Ufu 4:5; Hos 11:10; Yer 25:30; Amo 1:2Naye akapiga kelele kwa sauti kuu kama simba anayenguruma. Alipopiga kelele, zile radi saba zikatoa ngurumo zake. 410:4 Dan 8:26; Ufu 22:10Nazo zile radi saba zilipotoa ngurumo, nilitaka kuanza kuandika, lakini nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, “Yatie muhuri hayo yaliyosemwa na hizo radi saba na usiyaandike.”

510:5 Dan 12:7Kisha yule malaika niliyekuwa nimemwona akiwa amesimama juu ya bahari na juu ya nchi akainua mkono wake wa kuume kuelekea mbinguni. 610:6 Ufu 4:11; 16:17Naye akaapa kwa Yule aishiye milele na milele, aliyeumba mbingu na vyote vilivyomo, dunia na vyote viijazavyo, pamoja na bahari na vyote vilivyomo ndani yake, akasema, “Hakuna kungoja tena! 710:7 Rum 16:25Lakini katika siku zile ambazo huyo malaika wa saba atakapokaribia kuipiga hiyo tarumbeta yake, siri ya Mungu itatimizwa, kama vile alivyowatangazia watumishi wake manabii.”

8Ndipo ile sauti niliyokuwa nimeisikia kutoka mbinguni ikasema nami tena ikaniambia, “Nenda, chukua kile kitabu kilichofunguliwa kilichoko mkononi mwa yule malaika aliyesimama juu ya bahari na juu ya nchi kavu.”

910:9 Yer 15:16; Eze 2:8; 3:3Basi nikamwendea nikamwomba yule malaika anipe kile kitabu kidogo. Akaniambia, “Chukua na ukile. Kitakuwa kichungu tumboni mwako, lakini kinywani mwako kitakuwa kitamu kama asali.” 1010:10 Ufu 10:9; Eze 3:3; 2:10Hivyo nikakichukua kile kitabu kidogo kutoka mkononi mwa yule malaika nikakila. Kilikuwa kitamu kama asali kinywani mwangu, lakini baada ya kukila, tumbo langu likatiwa uchungu. 1110:11 Eze 40:3; Ufu 21:15; 12:3; 11:19; Mwa 37:9Kisha nikaambiwa, “Imekupasa kutoa unabii tena kuhusu makabila mengi, mataifa, lugha na wafalme.”

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

启示录 10:1-11

天使与小书卷

1我看见另一位大力天使从天而降。他身披云霞,头顶彩虹,脸如太阳,双腿如火柱, 2手中拿着一卷打开了的小书卷,右脚踏在海中,左脚踏在地上。 3他大喊的时候,声如狮吼,之后有七声雷鸣。 4我正要将雷鸣的意思记录下来,就听见天上有声音说:“你要封住七声雷鸣所说的事,别写下来。”

5我刚才所见的那位脚踏海洋和陆地的天使向天举起右手, 6凭着活到永永远远、创造天地海洋和其中一切的上帝起誓说:“必不再耽延了。 7等第七位天使吹响号角时,上帝奥秘的计划就实现了,正如上帝向祂的奴仆——众先知所宣告的。”

8先前从天上对我说话的声音又吩咐我:“你去,从那位脚踏海洋陆地的天使手中把展开的小书卷拿来。”

9于是,我走到那天使面前,请他将小书卷给我。他对我说:“拿去,把它吃了。你的腹中会感到苦涩,可是你口中会觉得甘甜如蜜。” 10我就从天使手中接过小书卷,将它吃了,我口中果然甘甜如蜜,之后腹中觉得苦涩。 11那天使又对我说:“你必要再对许多民族、国家、语言族群、君王说预言。”