Tito 2 – NEN & NIV

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Tito 2:1-15

Fundisha Mafundisho Manyofu

12:1 1Tim 1:10; 6:3; 2Tim 1:13Inakupasa kufundisha itikadi sahihi. 22:2 Tit 1:13; 1Tim 5:1; 3:2; Tit 2:5, 6, 12; 1:8, 13Wafundishe wazee kuwa na kiasi, wastahivu, wenye busara na wanyofu katika imani, upendo na saburi.

32:3 1Tim 3:8; 3:11Vivyo hivyo, wafundishe wanawake wazee kuwa na mwenendo wa utakatifu, wala wasiwe wasingiziaji au walevi, bali wafundishe yale yaliyo mema, 42:4 1Tim 5:2, 14ili waweze kuwafundisha wanawake vijana kuwa na kiasi, wawapende waume zao na kuwapenda watoto wao, 52:5 Efe 5:22; 1Tim 6:1wawe waaminifu, watakatifu, wakitunza vyema nyumba zao, wema, watiifu kwa waume zao, ili mtu yeyote asije akalikufuru neno la Mungu.

62:6 1Tim 5:1Vivyo hivyo, himiza vijana wawe na kiasi. 72:7 1Tim 4:12; Tit 2:14Katika kila jambo uwe kielelezo kwa kutenda mema. Katika mafundisho yako uonyeshe uadilifu, utaratibu, 82:8 1Pet 2:12; 1Tim 6:3; Neh 5:9; 1Tim 5:14; 2The 3:14na usemi sahihi usio na lawama, ili wanaokupinga watahayari, wakose neno lolote baya la kusema juu yetu.

92:9 Efe 6:5; Kol 3:22; 1Tim 6:12; 1Pet 2:18; Efe 5:24Wafundishe watumwa kuwatii mabwana zao katika kila jambo, wakijitahidi kuwapendeza wala wasijibizane nao, 102:10 Mt 5:16; Flp 2:15; Tit 1:3; Lk 1:47wala wasiwaibie, bali waonyeshe kuwa wanaweza kuaminika kabisa, ili kwa kila namna wayafanye mafundisho ya Mungu Mwokozi wetu yawe ya kuvutia.

112:11 1Tim 2:4; Rum 3:24; 2Tim 1:10Kwa maana neema ya Mungu ambayo inawaokoa wanadamu wote imefunuliwa. 122:12 Tit 3:3; 2Tim 3:12Nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia, ili tupate kuishi maisha ya kiasi, ya haki na ya utaua katika ulimwengu huu wa sasa, 132:13 2Pet 1:1; 1Kor 1:7; 1Tim 6:14; Flp 3:20huku tukilitazamia tumaini lenye baraka na ufunuo wa utukufu wa Mungu wetu Mkuu, aliye Mwokozi wetu Yesu Kristo. 142:14 Za 85:4; Mit 16:7Ndiye alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe kutoka uovu wote na kujisafishia watu kuwa mali yake Mwenyewe, yaani, wale walio na juhudi katika kutenda mema.

15Basi wewe fundisha mambo haya. Onya na kukaripia kwa mamlaka yote. Mtu yeyote asikudharau.

New International Version

Titus 2:1-15

Doing Good for the Sake of the Gospel

1You, however, must teach what is appropriate to sound doctrine. 2Teach the older men to be temperate, worthy of respect, self-controlled, and sound in faith, in love and in endurance.

3Likewise, teach the older women to be reverent in the way they live, not to be slanderers or addicted to much wine, but to teach what is good. 4Then they can urge the younger women to love their husbands and children, 5to be self-controlled and pure, to be busy at home, to be kind, and to be subject to their husbands, so that no one will malign the word of God.

6Similarly, encourage the young men to be self-controlled. 7In everything set them an example by doing what is good. In your teaching show integrity, seriousness 8and soundness of speech that cannot be condemned, so that those who oppose you may be ashamed because they have nothing bad to say about us.

9Teach slaves to be subject to their masters in everything, to try to please them, not to talk back to them, 10and not to steal from them, but to show that they can be fully trusted, so that in every way they will make the teaching about God our Savior attractive.

11For the grace of God has appeared that offers salvation to all people. 12It teaches us to say “No” to ungodliness and worldly passions, and to live self-controlled, upright and godly lives in this present age, 13while we wait for the blessed hope—the appearing of the glory of our great God and Savior, Jesus Christ, 14who gave himself for us to redeem us from all wickedness and to purify for himself a people that are his very own, eager to do what is good.

15These, then, are the things you should teach. Encourage and rebuke with all authority. Do not let anyone despise you.