Ruthu 2 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Ruthu 2:1-23

Ruthu Akutana Na Boazi

12:1 Rut 2:3; 4:21; Mit 7:4; 1Sam 9:1; 1Fal 11:28; 1Nya 2:12; Mt 1:5; Lk 3:32Basi Naomi alikuwa na jamaa wa upande wa mume wake, kutoka ukoo wa Elimeleki, mtu maarufu ambaye aliitwa Boazi.

22:2 Rut 1:22; Law 19:9; 23:22; Mwa 6:8; 18:3; Kum 24:19Ruthu, Mmoabu, akamwambia Naomi, “Nitakwenda mashambani nikaokote mabaki ya nafaka nyuma ya yule nitakayepata kibali machoni pake.”

Naomi akamwambia, “Nenda, binti yangu.” 32:3 2Fal 4:18; Yer 9:22; Amo 9:13Basi akaenda, akaokota mabaki ya nafaka mashambani nyuma ya wavunaji. Ikatokea kwamba alijikuta anafanya kazi kwenye shamba lililokuwa mali ya Boazi, ambaye alitoka kwenye ukoo wa Elimeleki.

42:4 Lk 1:28; Mwa 28:3; 2The 3:16; 2Tim 4:22; Kol 4:6; Hes 6:24; Amu 6:12; Za 129:7-8Papo hapo Boazi akarudi kutoka Bethlehemu, akawasalimu wavunaji, akasema, “Bwana awe nanyi!”

Nao wakamjibu, “Bwana akubariki.”

5Boazi akamuuliza msimamizi wa wavunaji, “Je, yule mwanamwali ni wa nani?”

62:6 Rut 1:22Msimamizi akamjibu, “Ni yule Mmoabu aliyerudi kutoka nchi ya Moabu pamoja na Naomi. 72:7 Mwa 37:7; Law 19:9; 2Sam 4:5Yeye aliomba, ‘Tafadhali niruhusu niokote na kukusanya miongoni mwa miganda nyuma ya wavunaji.’ Naye ameshinda shambani tangu asubuhi pasipo kupumzika, isipokuwa kwa muda mfupi kivulini.”

8Kisha Boazi akamwambia Ruthu, “Binti yangu, nisikilize. Usiende kuokota mabaki ya mavuno katika shamba lingine, na usiondoke hapa. Kaa hapa na hawa watumishi wangu wa kike. 9Angalia shamba wanaume wanamovuna, ufuate nyuma yao. Nimewaamuru wanaume hawa wasikuguse. Wakati wowote ukiona kiu, nenda kwenye mitungi ukanywe maji waliyoyateka wanaume hawa.”

102:10 Mwa 19:1; 31:15; 1Sam 25:23; 20:41; Kum 15:3Kwa ajili ya hili, akasujudu mpaka nchi, akamwambia, “Jinsi gani nimepata kibali machoni pako, hata ukanijali mimi mgeni?”

112:11 Rut 1:5, 14, 16-17; Isa 55:5; Mit 31:31; Rut 1:14; Lk 5:11, 28; 14:33; 18:29, 30Boazi akamjibu, “Nimeambiwa yote uliyomtendea mama mkwe wako tangu mume wako alipofariki, na jinsi ulivyomwacha baba yako na mama yako na nchi yako ulimozaliwa, ukaja kuishi na watu ambao hukuwafahamu awali. 122:12 1Sam 24:19; 26:23-25; Za 17:8; 18:20; 36:7; 57:1; 61:4; 63:7; 91:4; 71:1; Mit 25:22; Yer 31:16; Yos 24:15Bwana na akulipe kwa yale uliyoyatenda. Ubarikiwe kwa wingi na Bwana, Mungu wa Israeli, ambaye umekimbilia mabawani mwake.”

132:13 Mwa 18:3; Flp 2:3; 1Sam 25:41Kisha Ruthu akasema, “Naomba niendelee kupata kibali machoni pako, bwana wangu. Kwa maana umenifariji na umezungumza kwa ukarimu na mjakazi wako, hata ingawa mimi si bora kama mmoja wa watumishi wako wa kike.”

142:14 Mwa 3:19; Law 23:14Wakati wa chakula, Boazi akamwambia Ruthu, “Karibia hapa. Kula mkate na uchovye ndani ya siki.”

Alipoketi pamoja na wavunaji, akampa nafaka zilizookwa. Akala kiasi alichotaka na kusaza. 152:15 Mwa 37:7; Law 19:9Alipoinuka ili kuokota mabaki ya nafaka, Boazi akawaagiza watu wake, “Hata kama atakusanya kati ya miganda, msimzuie. 162:16 Mwa 37:10Badala yake, toeni masuke katika miganda, mwachieni ayaokote, na msimkemee.”

172:17 Amu 6:11; Law 19:36Basi Ruthu akaokota masazo shambani hata jioni. Akatwanga ile shayiri aliyokusanya, ikajaa efa moja.2:17 Efa moja ni sawa na kilo 22. 18Akaibeba na kuelekea mjini, naye mama mkwe wake akaona jinsi alivyoweza kuokota nafaka nyingi. Pia Ruthu akachukua kile alichobakiza baada ya kula na kushiba, akampa.

19Basi mkwewe akamuuliza, “Je, umeokota wapi leo? Umefanya kazi wapi? Abarikiwe mtu yule aliyekujali.”

Ndipo Ruthu akamwambia mama mkwe wake juu ya yule ambaye yeye alikuwa amefanyia kazi katika shamba lake. Akasema, “Yule mtu niliyefanyia kazi kwake leo, anaitwa Boazi.”

202:20 Amu 17:2; 1Sam 23:21; Mwa 11:31; 19:19; 2Sam 2:5; Ay 29:13; 2Tim 1:16; Mit 17:17; Law 25:25; Rut 3:9; 4:1, 14Naye Naomi akamwambia mkwewe, “Bwana ambariki! Hakuacha kuonyesha fadhili zake kwa walio hai na kwa waliokufa.” Pia akamwambia, “Huyo mtu ni mmoja wa jamaa yetu wa karibu anayestahili kutukomboa.”

212:21 Rut 1:22Kisha Ruthu, Mmoabu, akasema, “Hata aliniambia, ‘Kaa pamoja na watumishi wangu mpaka watakapomaliza kuvuna nafaka yangu yote.’ ”

22Kisha Naomi akamwambia Ruthu mkwewe, “Binti yangu, itakuwa vyema wewe ufuatane na wasichana wake, kwa sababu katika shamba la mtu mwingine wanaweza kukudhuru.”

232:23 Kut 9:31; Mwa 30:14; 1Sam 6:13; Kum 16:9Kwa hivyo Ruthu akafuatana na watumishi wa kike wa Boazi, akaokota mpaka mwisho wa mavuno ya shayiri na ya ngano. Naye aliishi na mama mkwe wake.

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

路得记 2:1-23

路得遇见波阿斯

1拿俄米的丈夫以利米勒有个亲戚,名叫波阿斯,是个有名望的财主。 2摩押女子路得拿俄米说:“让我到田里去,跟在那些愿意恩待我的人后面,捡些麦穗回来。”拿俄米说:“去吧,我的女儿!” 3于是,路得便去了。她恰巧来到以利米勒的亲戚波阿斯的田里,跟在收割的人后面捡麦穗。 4当时,波阿斯刚好从伯利恒来到田间,向那些收割的工人问安说:“愿耶和华与你们同在。”他们回答说:“愿耶和华赐福与你。” 5波阿斯问负责收割的工头说:“那是谁家的女子?” 6工头回答说:“她是摩押女子,跟拿俄米刚从摩押回来。 7她求我让她跟在收割的人后面,捡工人扎捆时遗落的麦穗。她一大早就来到这里,一直捡到现在,除了在凉棚里稍微坐了一会儿之外,几乎没有休息。”

8波阿斯路得说:“姑娘2:8 姑娘”希伯来文是“女儿”。,听我说,你不用到别人的田里去拾麦穗了,也不必离开这里,只管留下来跟我的女工在一起。 9你看我的工人在哪一块田里收割,就跟着我的女工去,我已经吩咐工人不可欺负你。要是你渴了,就去水罐那里喝工人打回来的水。” 10路得就俯伏在地叩谢他,说:“我不过是个外族人,你为什么这样恩待我、体恤我?” 11波阿斯说:“自从你丈夫过世之后,你怎样善待婆婆,怎样离开父母和家乡来到素不相识的人当中,我都听说了。 12愿耶和华照你所行的奖赏你!你来投靠在以色列的上帝耶和华的翅膀下,愿祂厚厚地赏赐你。” 13路得说:“我主啊!我真是在你面前蒙恩,虽然我连你的婢女都不如,你还好言安慰我。”

14吃饭的时候,波阿斯路得说:“来,吃一点饼吧,可以蘸着醋吃。”路得便坐在那些收割工人旁边。波阿斯递给她一些烤好的麦穗。她吃饱了,还有剩余的。 15当她起来又要去捡麦穗的时候,波阿斯就吩咐他的工人说:“你们要任由她捡,就算她在割下的麦子中捡麦穗,你们也不要为难她。 16甚至要从麦捆中抽一些出来让她捡,不要责骂她。”

17于是,路得便在田间继续捡麦穗,到了黄昏,她把捡到的麦穗打了,大约有十三公斤大麦。 18她把捡来的麦子带回城里给婆婆拿俄米看,又把剩下来的食物给婆婆。 19婆婆问她:“你今天在哪里拾麦穗?在哪里做工?愿那善待你的人蒙福!”她就告诉婆婆说:“今天我在一个名叫波阿斯的人那里工作。” 20拿俄米说:“愿耶和华赐福给他,他对活着的和过世的都是那么有情有义。”拿俄米又对路得说:“这人是我们本族的人,是我们的一个近亲。” 21摩押女子路得说:“他还对我说,‘你可以跟在我的工人后面捡麦穗,直到他们把我的庄稼都收完为止。’” 22拿俄米对儿媳路得说:“我的女儿啊,你就跟他的女工一起到田里去,免得去别人的田里被欺负。” 23因此,路得便常跟波阿斯的女工在一起捡麦穗,直到大麦小麦都收割完毕。路得就这样陪伴婆婆过日子。