Mwanzo 7 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Mwanzo 7:1-24

17:1 Mwa 6:18; 9:6; Mt 24:38; Ebr 11:7; Lk 17:26-27; 1Pet 3:20; 2Pet 2:5; Eze 14:14Ndipo Bwana akamwambia Noa, “Ingia katika safina wewe na jamaa yako yote, kwa sababu katika kizazi hiki nimeona ya kuwa wewe ni mwenye haki. 27:2 Mwa 8:20; Law 10:10; 11:1-47; Kum 14:3-20; Eze 44:23; Hag 2:12; Mdo 10:14-15Uchukue wanyama saba walio safi wa kila aina, wa kiume na wa kike, na wanyama wawili wawili wa kila aina walio najisi wa kiume na wa kike. 37:3 Mwa 6:20Pia uchukue ndege saba walio safi wa kila aina, wa kiume na wa kike, ili kuhifadhi aina zao mbalimbali katika dunia yote. 47:4 Mwa 2:8; 6:7, 13; 1Fal 13:34; Yer 28:16; Hes 13:25; 1Sam 17:16; 1Fal 19:8; Kut 24:18; 32:1; 34:28; Kum 9:9, 11, 18, 25; 10:10; Ay 37:6; Mt 4:2Siku saba kuanzia sasa nitaleta mvua juu ya nchi kwa siku arobaini usiku na mchana, nami nitafutilia mbali kutoka uso wa nchi kila kiumbe hai nilichokiumba.”

57:5 Mwa 6:22Noa akafanya yote kama Bwana alivyomwamuru.

67:6 Mwa 5:32Noa alikuwa na miaka 600 gharika ilipokuja juu ya dunia. 77:7 Mwa 6:18Noa na mkewe na wanawe na wake zao wakaingia katika safina ili waepuke ile gharika. 8Jozi ya wanyama walio safi na walio najisi, ndege na viumbe vitambaavyo, 97:9 Mwa 6:22wa kiume na wa kike, walikuja kwa Noa wakaingia katika safina kama Mungu alivyomwamuru Noa. 10Baada ya siku saba, maji ya gharika yakaja juu ya dunia.

117:11 Mwa 5:32; 8:2, 4, 14; Ay 28:11; Za 36:6; 42:7; 78:23; Mit 8:24; Isa 24:18; 51:10; Eze 26:19; 2; 2Fal 7:2; Mal 3:10Katika siku ya kumi na saba ya mwezi wa pili mwaka wa 600 wa kuishi kwake Noa, siku hiyo ndipo chemchemi zote hata zilizo chini sana ya ardhi zilibubujika kwa nguvu, na malango ya mafuriko ya mbinguni yakafunguliwa. 127:12 1Sam 12:17; Ay 28:26Mvua ikanyesha juu ya nchi siku arobaini usiku na mchana.

137:13 Mwa 8:16; 6:18; 1Pet 3:20; 2Pet 2:5Siku hiyo Noa, na mkewe, na wanawe Shemu, Hamu na Yafethi pamoja na wake zao wakaingia katika ile safina. 147:14 Mwa 1:11Nao walikuwa pamoja na kila mnyama wa mwituni kufuatana na aina yake, wanyama wote wafugwao kufuatana na aina zao, kila kiumbe kitambaacho juu ya ardhi kwa aina yake, na kila ndege kufuatana na aina yake, naam kila kiumbe chenye mabawa. 157:15 Mwa 6:19Viumbe vyote vyenye pumzi ya uhai ndani yake vikaja kwa Noa viwili viwili, vikaingia katika safina. 167:16 Mwa 6:22Wanyama walioingia katika safina walikuwa wa kiume na wa kike, wa kila kiumbe chenye uhai kama Mungu alivyomwamuru Noa, ndipo Bwana akamfungia ndani.

17Kwa siku arobaini mafuriko yaliendelea kujaa duniani na maji yalivyozidi kuongezeka, yaliinua safina juu sana kutoka kwenye uso wa nchi. 18Maji yakajaa na kuongezeka sana juu ya nchi, na safina ikaelea juu ya uso wa maji. 197:19 Za 104:6Maji yakazidi kujaa juu ya nchi, yakaifunika milima yote mirefu chini ya mbingu yote. 207:20 Mwa 8:4-5; 2Pet 3:6Maji yakaendelea kujaa yakaifunika milima kwa kina cha zaidi ya dhiraa kumi na tano.7:20 Dhiraa 15 ni sawa na mita 7. 217:21 Mwa 6:7, 13; 2Pet 3:6Kila kiumbe hai kitambaacho juu ya nchi kikaangamia: Ndege, wanyama wa kufugwa, wanyama pori, viumbe vyote juu ya nchi na wanadamu wote. 227:22 Mwa 1:30Kila kiumbe juu ya nchi kavu chenye pumzi ya uhai kikafa. 237:23 Ay 14:19; 21:18; 22:11, 16; Lk 17:27; Za 90:5; Isa 28:2; Mt 24:39; Ebr 11:7; 1Pet 3:20; 2Pet 2:5Kila kitu chenye uhai juu ya uso wa nchi kilifutiliwa mbali, watu, wanyama, viumbe vitambaavyo na ndege warukao angani wakafutiliwa mbali toka duniani. Waliobaki ni Noa peke yake na wale waliokuwa pamoja naye ndani ya safina.

247:24 Mwa 8:3; Ay 12:15Maji yakaifunika dunia kwa siku 150.

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

創世記 7:1-24

洪水氾濫

1耶和華對挪亞說:「你和你一家都進入方舟,因為這個世代只有你在我眼中是義人。 2潔淨的動物,你要每樣帶七公七母,不潔淨的動物每樣帶一公一母, 3飛鳥每樣帶七公七母,叫牠們以後可以在地上繁衍後代。 4因為七天之後,我要在地上降雨四十晝夜,毀滅我所造的一切生靈。」 5凡耶和華所吩咐的,挪亞都照辦了。

6洪水氾濫的那一年,挪亞正好六百歲。 7挪亞與妻子、兒子們和兒媳們都進了方舟,躲避洪水。 8潔淨的動物、不潔淨的動物、飛禽和地上的一切爬蟲, 9都一公一母成對地到挪亞那裡,進了方舟,正如上帝對挪亞的吩咐。 10那七天過後,洪水在地上氾濫起來。

11挪亞六百歲那年的二月7·11 二月」按猶太曆計算,本卷書所用月份都是按猶太曆計算。十七日,所有深淵的泉源都裂開了,天上的水閘也打開了, 12地上傾盆大雨降了四十晝夜。 13那天,挪亞與他的兒子雅弗,還有挪亞的妻子和三個兒媳婦都進了方舟。 14所有的野獸、牲畜、地上的爬蟲和飛鳥都按種類進入方舟。 15-16這些動物都一公一母成對地到挪亞那裡,進入方舟,正如上帝對挪亞的吩咐。耶和華關上了方舟的門。

17洪水在地上氾濫了四十天,水不斷地往上漲,把方舟漂了起來。 18洪水來勢洶洶,淹沒大地,方舟漂浮在水面上。 19水勢越來越大,把天下各處的高山都淹沒了。 20水淹沒了群山,水面高出群山七米。 21世上所有的飛禽、走獸、牲畜、爬蟲和人類都死了。 22在陸地上所有用鼻孔呼吸的生靈都死了。 23地上的人類、飛禽走獸和爬蟲等一切生靈都被毀滅了,只剩下挪亞和跟他同在方舟裡的生靈。 24洪水淹沒大地一百五十天。