Mwanzo 41 – NEN & PCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Mwanzo 41:1-57

Ndoto Za Farao

141:1 Kut 2:5Baada ya miaka miwili kamili kupita, Farao aliota ndoto: Tazama alikuwa amesimama kando ya Mto Naili, 241:2 Ay 40:21wakati ngʼombe saba, wazuri na wanono, walitokea mtoni wakajilisha kwenye matete. 3Baada yao ngʼombe wengine saba, wabaya na waliokonda, wakatokea mtoni Naili wakasimama kando ya wale wanono ukingoni mwa mto. 441:4 Mwa 41:7Wale ngʼombe wabaya na waliokonda wakawala wale saba wazuri na wanono. Kisha Farao akaamka.

5Farao akaingia usingizini tena akaota ndoto ya pili: Akaona masuke saba ya nafaka, yenye afya na mazuri, yanakua katika bua moja. 641:6 Za 11:6Baadaye, masuke mengine saba yakachipua, yakiwa membamba yaliyonyaushwa na upepo wa mashariki. 741:7 Mwa 41:4Masuke yale membamba yakameza yale masuke saba yenye afya na yaliyojaa. Basi Farao akaamka kutoka usingizini, kumbe ilikuwa ndoto.

841:8 Kut 7:11, 22; Dan 4:18Asubuhi yake, alifadhaika akilini, hivyo akawaita waaguzi wote pamoja na watu wenye busara wa Misri. Walipokuja, Farao akawaeleza ndoto zake, lakini hakuna hata mmoja aliyeweza kumfasiria.

9Ndipo mnyweshaji mkuu alipomwambia Farao, “Leo nimekumbushwa kuhusu kosa langu. 1041:10 Mwa 40:2Wakati fulani Farao aliwakasirikia watumishi wake, akanifunga mimi na mwokaji mkuu katika nyumba ya mkuu wa ulinzi. 1141:11 Mwa 40:5Kila mmoja wetu aliota ndoto katika usiku mmoja na kila ndoto ilikuwa na maana yake tofauti. 1241:12 Mwa 40:12Basi kijana wa Kiebrania aliyekuwa pamoja nasi huko, alikuwa mtumishi wa mkuu wa kikosi cha ulinzi. Tulimweleza ndoto zetu, naye akatufasiria, akitupa kila mtu tafsiri ya ndoto yake. 1341:13 Mwa 40:22Nayo mambo yakawa sawa kabisa na jinsi alivyotufasiria ndoto zetu: Mimi nilirudishwa kazini mwangu na huyo mtu mwingine akaangikwa.”

1441:14 Za 105:20; Rut 3:3Basi, Farao akatuma Yosefu aitwe, naye akatolewa kifungoni haraka. Baada ya kunyoa na kubadilisha nguo zake akaenda mbele ya Farao.

1541:15 Dan 5:16Farao akamwambia Yosefu, “Nimeota ndoto, wala hakuna mtu hata mmoja anayeweza kuifasiri. Lakini nimesikia ikisemwa kwa habari yako kwamba unapoelezwa ndoto waweza kuifasiri.”

1641:16 Mwa 40:8Yosefu akamjibu Farao, “Siwezi kuifasiri, lakini Mungu atampa Farao jibu analolihitaji.”

17Kisha Farao akamwambia Yosefu, “Katika ndoto yangu nilikuwa nimesimama ukingoni mwa Mto Naili, 18nikawaona ngʼombe saba, wazuri na wanono, wakijitokeza kutoka mtoni wakaja kujilisha kwenye matete. 19Baada ya hao, ngʼombe wengine saba wadhaifu wakatokea, wabaya sana na waliokonda. Kamwe sikuwahi kuona ngʼombe wabaya jinsi hiyo katika nchi yote ya Misri. 20Hao ngʼombe waliokonda na wabaya sana wakawala wale ngʼombe saba walionona waliojitokeza kwanza. 21Lakini hata baada ya kuwala, hakuna mtu ambaye angeweza kusema kwamba wamekula, bado walionekana wabaya kama mwanzoni. Kisha nikaamka kutoka usingizini.

22“Pia katika ndoto zangu niliona masuke saba ya nafaka, yamejaa na mazuri, yanakua katika bua moja. 23Baada ya hayo masuke mengine saba yakachipua, yaliyonyauka, membamba na yamekaushwa na upepo wa mashariki. 24Yale masuke membamba ya nafaka yakayameza yale masuke saba mazuri yaliyojaa nafaka. Nimewaeleza waaguzi, wala hakuna yeyote aliyeweza kunifasiria.”

2541:25 Dan 2:45Ndipo Yosefu akamwambia Farao, “Ndoto za Farao ni ndoto iyo hiyo moja. Mungu amemfunulia Farao jambo analokusudia kufanya karibuni. 26Ngʼombe saba wazuri ni miaka saba, nayo masuke saba mazuri yaliyojaa nafaka ni miaka saba, ni ndoto iyo hiyo moja. 27Ngʼombe saba waliokonda na wabaya wale waliojitokeza baadaye ni miaka saba, vivyo hivyo masuke saba ya ngano yaliyodhoofika na kukaushwa na upepo wa mashariki, ni miaka saba ya njaa.

28“Ni kama vile nilivyomwambia Farao: Mungu amemwonyesha Farao jambo analokusudia kufanya karibuni. 2941:29 Mwa 41:47Miaka saba ya neema inakuja katika nchi yote ya Misri, 3041:30 Mwa 41:54; 47:13lakini itafuata miaka saba ya njaa. Ndipo neema yote ya Misri itasahaulika na njaa itaikumba nchi.

31“Neema iliyokuwa katika nchi haitakumbukwa, kwa sababu njaa itakayofuata itakuwa kali mno. 32Sababu ya ndoto kumjia Farao kwa namna mbili ni kwamba jambo hilo Mungu ameshaamua kwa hakika, naye Mungu atalifanya karibuni.

3341:33 Mwa 41:39“Basi sasa Farao na atafute mtu mwenye akili na hekima ili amweke kuwa msimamizi wa nchi ya Misri. 3441:34 Es 2:3Farao na aweke wenye amri nchini kote wakusanye sehemu ya tano ya mavuno ya Misri katika miaka hii saba ya neema. 3541:35 Mwa 41:48Wakusanye chakula chote katika miaka hii saba ya neema inayokuja na kuhifadhi nafaka chini ya mamlaka ya Farao, iwe akiba ya chakula katika miji. 36Chakula hiki kitakuwa akiba ya tahadhari kwa ajili ya nchi, ili kitumike katika ile miaka saba ya njaa itakayokuja Misri, ili nchi isiharibiwe na njaa.”

37Mpango huu ulionekana mzuri kwa Farao na kwa maafisa wake wote. 3841:38 Hes 27:18; Dan 4:8-9, 18; 5:11, 14Hivyo Farao akawauliza, “Je tunaweza kumpata yeyote kama mtu huyu, ambaye Roho wa Mungu yumo ndani yake?”

39Ndipo Farao akamwambia Yosefu, “Maadamu Mungu amekufunulia yote haya, hakuna mwingine yeyote mwenye akili na hekima kama wewe. 4041:40 Za 105:21-22; Mdo 7:10Wewe utakuwa msimamizi wa jumba langu la kifalme, na watu wangu wote watatii amri zako. Ni kuhusu kiti cha ufalme tu nitakuwa mkuu kuliko wewe.”

Yosefu Msimamizi Wa Misri

4141:41 Mwa 42:6Kwa hiyo Farao akamwambia Yosefu, “Sasa nakuweka uwe msimamizi wa nchi yote ya Misri.” 4241:42 Es 3:10; Dan 5:29Ndipo Farao akaivua pete yake ya muhuri kutoka kidoleni mwake na kuivalisha katika kidole cha Yosefu. Akamvika majoho mazuri ya kitani safi na mkufu wa dhahabu shingoni mwake. 4341:43 Isa 2:7Akampandisha katika gari lake la farasi kama msaidizi wake, watu wakatangulia wakishangilia, wakisema, “Fungueni njia!” Ndivyo Farao alivyomweka Yosefu kuwa msimamizi wa nchi yote ya Misri.

44Kisha Farao akamwambia Yosefu, “Mimi ni Farao, lakini pasipo neno lako, hakuna mtu mwenye ruhusa kuinua mkono au mguu katika nchi yote ya Misri.” 4541:45 Es 2:7Farao akamwita Yosefu Safenath-Panea, pia akampa Asenathi binti Potifera, kuhani wa mji wa Oni,41:45 Yaani Heliopoli (Mji wa Jua). kuwa mke wake. Ndipo Yosefu akaitembelea nchi yote ya Misri.

4641:46 Mit 22:29Yosefu alikuwa na miaka thelathini alipoingia katika utumishi wa Farao mfalme wa Misri. Naye Yosefu akatoka mbele ya Farao akasafiri katika nchi yote ya Misri. 4741:47 Mwa 41:29Katika ile miaka saba ya neema nchi ilizaa mazao kwa wingi sana. 4841:48 Mwa 41:34Yosefu akakusanya chakula chote kilichozalishwa katika ile miaka saba ya neema nchini Misri, akakihifadhi katika ghala za miji. Katika kila mji kulihifadhiwa chakula kilichozalishwa katika mashamba yaliyouzunguka mji huo. 4941:49 Mwa 12:2Yosefu alihifadhi nafaka nyingi, mfano wa mchanga wa bahari, ilikuwa nyingi mno kiasi kwamba walishindwa kuweka kumbukumbu kwa sababu akiba ilizidi sana kupita kipimo.

50Kabla ya miaka ya njaa kuanza, Asenathi binti Potifera, kuhani wa mji wa Oni, alikuwa amemzalia Yosefu wana wawili wa kiume. 5141:51 Hes 1:34Yosefu akamwita mzaliwa wake wa kwanza Manase, akisema, “Ni kwa sababu Mungu amenifanya nisahau taabu zangu zote pamoja na jamaa yote ya nyumba ya baba yangu.” 5241:52 Mwa 17:6Mwana wa pili akamwita Efraimu, akisema, “Ni kwa sababu Mungu amenistawisha katika nchi ya mateso yangu.”

53Ile miaka saba ya neema huko Misri ikaisha, 5441:54 Mdo 7:11nayo miaka ile saba ya njaa ikaanza, sawasawa na alivyosema Yosefu. Kulikuwa na njaa katika nchi nyingine zote, bali katika nchi yote ya Misri kulikuwa na chakula. 55Wakati nchi yote ya Misri ilipopatwa na njaa, watu wakamlilia Farao ili awape chakula. Ndipo Farao alipowaagiza Wamisri wote, akisema, “Nendeni kwa Yosefu, nanyi mfanye anachowaambia.”

56Wakati njaa ilipokuwa imeenea katika nchi yote, Yosefu akafungua ghala za vyakula na kuwauzia Wamisri nafaka, kwa sababu njaa ilikuwa kali mno katika nchi yote ya Misri. 57Pia nchi nyingine zote zilikuja Misri kununua nafaka kutoka kwa Yosefu, kwa sababu njaa ilikuwa kali mno duniani kote.

Persian Contemporary Bible

پيدايش 41:1-57

خوابهای فرعون

1دو سال بعد از اين واقعه، شبی فرعون خواب ديد كه كنار رود نيل ايستاده است. 2ناگاه هفت گاو چاق و فربه از رودخانه بيرون آمده، شروع به چريدن كردند. 3بعد هفت گاو ديگر از رودخانه بيرون آمدند و كنار آن هفت گاو ايستادند، ولی اينها بسيار لاغر و استخوانی بودند. 4سپس گاوهای لاغر، گاوهای چاق را بلعيدند. آنگاه فرعون از خواب پريد.

5او باز خوابش برد و خوابی ديگر ديد. اين بار ديد كه هفت خوشهٔ گندم روی يک ساقه قرار دارند كه همگی پُر از دانه‌های گندم رسيده هستند. 6سپس هفت خوشهٔ نازک ديگر كه باد شرقی آنها را خشكانيده بود، ظاهر شدند. 7خوشه‌های نازک و خشكيده، خوشه‌های پُر و رسيده را بلعيدند. آنگاه فرعون از خواب بيدار شد و فهميد كه همه را در خواب ديده است.

8صبح روز بعد، فرعون كه فكرش مغشوش بود، تمام جادوگران و دانشمندان مصر را احضار نمود و خوابهايش را برای ايشان تعريف كرد، ولی كسی قادر به تعبير خوابهای او نبود.

9آنگاه رئيس ساقيان پيش آمده، به فرعون گفت: «الان يادم آمد كه چه خطای بزرگی مرتكب شده‌ام. 10‏-11مدتی پيش، وقتی كه بر غلامان خود غضب نمودی و مرا با رئيس نانوايان به زندانِ رئيس محافظانِ دربار انداختی، هر دو ما در يک شب خواب ديديم. 12ما خوابهايمان را برای جوانی عبرانی كه غلامِ رئيس محافظان دربار و با ما همزندان بود، تعريف كرديم و او خوابهايمان را برای ما تعبير كرد؛ 13و هر آنچه كه گفته بود اتفاق افتاد. من به خدمت خود برگشتم و رئيس نانوايان به دار آويخته شد.»

14فرعون فوراً فرستاد تا يوسف را بياورند، پس با عجله وی را از زندان بيرون آوردند. او سر و صورتش را اصلاح نمود و لباسهايش را عوض كرد و به حضور فرعون رفت.

15فرعون به او گفت: «من ديشب خوابی ديدم و كسی نمی‌تواند آن را برای من تعبير كند. شنيده‌ام كه تو می‌توانی خوابها را تعبير كنی.»

16يوسف گفت: «من خودم قادر نيستم خوابها را تعبير كنم، اما خدا معنی خوابت را به تو خواهد گفت.»

17پس فرعون خوابش را برای يوسف اينطور تعريف كرد: «در خواب ديدم كنار رود نيل ايستاده‌ام. 18ناگهان هفت گاو چاق و فربه از رودخانه بيرون آمده، مشغول چريدن شدند. 19سپس هفت گاو ديگر را ديدم كه از رودخانه بيرون آمدند، ولی اين هفت گاو بسيار لاغر و استخوانی بودند. هرگز در تمام سرزمين مصر، گاوهايی به اين زشتی نديده بودم. 20اين گاوهای لاغر آن هفت گاو چاقی را كه اول بيرون آمده بودند، بلعيدند. 21پس از بلعيدن، هنوز هم گاوها لاغر و استخوانی بودند. در اين موقع از خواب بيدار شدم. 22كمی بعد باز به خواب فرو رفتم. اين بار در خواب هفت خوشهٔ گندم روی يک ساقه ديدم كه همگی پر از دانه‌های رسيده بودند. 23اندكی بعد، هفت خوشه كه باد شرقی آنها را خشكانيده بود، نمايان شدند. 24ناگهان خوشه‌های نازک خوشه‌های پُر و رسيده را خوردند. همهٔ اينها را برای جادوگران خود تعريف كردم، ولی هيچكدام از آنها نتوانستند تعبير آنها را برای من بگويند.»

25يوسف به فرعون گفت: «معنی هر دو خواب يكی است. خدا تو را از آنچه كه در سرزمين مصر انجام خواهد داد، آگاه ساخته است. 26هفت گاو چاق و فربه و هفت خوشهٔ پُر و رسيده كه اول ظاهر شدند، نشانهٔ هفت سالِ فراوانی است. 27هفت گاو لاغر و استخوانی و هفت خوشهٔ نازک و پژمرده، نشانهٔ هفت سال قحطی شديد است كه به دنبال هفت سال فراوانی خواهد آمد. 28بدين ترتيب، خدا آنچه را كه می‌خواهد بزودی در اين سرزمين انجام دهد، بر تو آشكار ساخته است. 29طی هفت سال آينده در سراسر سرزمين مصر محصول، بسيار فراوان خواهد بود. 30‏-31اما پس از آن، چنان قحطی سختی به مدت هفت سال پديد خواهد آمد كه سالهای فراوانی از خاطره‌ها محو خواهد شد و قحطی، سرزمين را از بين خواهد برد. 32خوابهای دوگانه تو نشانهٔ اين است كه آنچه برايت شرح دادم، بزودی به وقوع خواهد پيوست، زيرا از جانب خدا مقرر شده است. 33من پيشنهاد می‌كنم كه فرعون مردی دانا و حكيم بيابد و او را بر ادارهٔ امور كشاورزی اين سرزمين بگمارد. 34‏-35سپس مأمورانی مقرر كند تا در هفت سال فراوانی، يک پنجم محصولات را در شهرها، در انبارهای سلطنتی ذخيره كنند، 36تا در هفت سال قحطی بعد از آن، با كمبود خوراک مواجه نشويد. در غير اين صورت، سرزمين شما در اثر قحطی از بين خواهد رفت.»

يوسف شخص دوم مملكت می‌شود

37فرعون و همه افرادش پيشنهاد يوسف را پسنديدند. 38سپس فرعون گفت: «چه كسی بهتر از يوسف می‌تواند از عهده اين كار برآيد، مردی كه روح خدا در اوست.»

39سپس فرعون رو به يوسف نموده، گفت: «چون خدا تعبير خوابها را به تو آشكار كرده است، پس داناترين و حكيم‌ترين شخص تو هستی. 40هم اكنون تو را بر اين امر مهم می‌گمارم. تو شخص دوم سرزمين مصر خواهی شد و فرمانت در سراسر كشور اجرا خواهد گرديد.» 41‏-43سپس فرعون انگشتر سلطنتی خود را به انگشت يوسف كرد و لباس فاخری بر او پوشانيده، زنجير طلا به گردنش آويخت، و او را سوار دومين عرابهٔ سلطنتی كرد. او هر جا می‌رفت جلو او جار می‌زدند: «زانو بزنيد!»

بدين ترتيب يوسف بر تمامی امور مصر گماشته شد.

44فرعون به يوسف گفت: «من فرعون، پادشاه مصر، اختيارات سراسر كشور مصر را به تو واگذار می‌كنم.» 45فرعون به يوسف، نام مصری صفنات فعنيح را داد و اسنات دختر فوطی فارع، كاهن اون را به عقد وی درآورد. و يوسف در سراسر كشور مصر مشهور گرديد.

46يوسف سی ساله بود كه فرعون او را به خدمت گماشت. او دربار فرعون را ترک گفت تا به امور سراسر كشور رسيدگی كند.

47طی هفت سالِ فراوانی محصول، غله در همه جا بسيار فراوان بود. 48در اين سالها يوسف محصولات مزارع را در شهرهای اطراف ذخيره نمود. 49به قدری غله در سراسر كشور جمع شد كه ديگر نمی‌شد آنها را حساب كرد.

50قبل از پديد آمدن قحطی، يوسف از همسرش اسنات، دختر فوطی فارع، كاهن اون صاحب دو پسر شد. 51يوسف پسر بزرگ خود را منسی (يعنی «فراموشی») ناميد و گفت: «با تولد اين پسر خدا به من كمک كرد تا تمامی خاطرهٔ تلخ جوانی و دوری از خانهٔ پدر را فراموش كنم.» 52او دومين پسر خود را افرايم (يعنی «پرثمر») ناميد و گفت: «خدا مرا در سرزمينِ سختیهايم، پرثمر گردانيده است.»

53سرانجام هفت سالِ فراوانی به پايان رسيد 54و همانطور كه يوسف گفته بود، هفت سالِ قحطی شروع شد. در كشورهای همسايهٔ مصر قحطی بود، اما در انبارهای مصر غلهٔ فراوان يافت می‌شد. 55گرسنگی بر اثر كمبود غذا آغاز شد و مردمِ مصر برای طلب كمک نزد فرعون رفتند و فرعون نيز آنها را نزد يوسف فرستاده، گفت: «برويد و آنچه يوسف به شما می‌گويد انجام دهيد.»

56‏-57در اين موقع، قحطی سراسر جهان را فرا گرفته بود. يوسف انبارها را گشوده، غلهٔ مورد نياز را به مصريان و به مردمی كه از خارج می‌آمدند می‌فروخت.