Mithali 4 – Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) NEN

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Mithali 4:1-27

Hekima Ni Bora Kupita Vitu Vyote

14:1 Mit 1:8; 19:20; Ay 8:10Sikilizeni wanangu, mafundisho ya baba yenu;

sikilizeni kwa makini na mpate ufahamu.

2Ninawapa mafundisho ya maana,

kwa hiyo msiyaache mafundisho yangu.

34:3 1Nya 29:1; 2Sam 12:24Nilipokuwa mvulana mdogo katika nyumba ya baba yangu,

ningali mchanga na mtoto pekee kwa mama yangu,

44:4 Mit 7:2; 1Nya 28:9baba alinifundisha akisema,

“Yashike maneno yangu yote kwa moyo wako wote;

yashike maagizo yangu na wewe utaishi.

54:5 Mit 3:13-18; 16:16Pata hekima, pata ufahamu;

usiyasahau maneno yangu wala usiyaache.

64:6 2The 2:10; Mit 2:11Usimwache hekima naye atakuweka salama;

mpende, naye atakulinda.

74:7 Mt 13:44-46; Mit 23:23Hekima ni bora kuliko vitu vyote; kwa hiyo jipe hekima.

Hata ikikugharimu vyote ulivyo navyo, pata ufahamu.

84:8 1Sam 2:30; Mit 3:18Mstahi, naye atakukweza;

mkumbatie, naye atakuheshimu.

94:9 Mit 1:8-9Atakuvika shada la neema kichwani mwako

na kukupa taji ya utukufu.”

104:10 Kum 11:21; Mit 3:2Sikiliza mwanangu, kubali ninachokuambia,

nayo miaka ya maisha yako itakuwa mingi.

114:11 1Sam 12:23; 2Sam 22:37; Za 5:8Ninakuongoza katika njia ya hekima

na kukuongoza katika mapito yaliyonyooka.

124:12 Ay 18:7; Yer 13:16; Za 18:36Utembeapo, hatua zako hazitazuiliwa;

ukimbiapo, hutajikwaa.

134:13 Mit 3:22Mkamate sana elimu, usimwache aende zake;

mshike, maana yeye ni uzima wako.

144:14 Za 1:1; Mit 1:15Usiuweke mguu wako katika njia ya waovu

wala usitembee katika njia ya watu wabaya.

15Epukana nayo, usisafiri katika njia hiyo;

achana nayo, na uelekee njia yako.

164:16 Za 36:4; Mik 7:3Kwa kuwa hawawezi kulala mpaka watende uovu;

wanashindwa hata kusinzia mpaka wamwangushe mtu.

174:17 Mwa 49:5; Za 73:6; Mit 1:10-19; Isa 59:6; Yer 22:3; Hab 1:2; Mal 2:16Wanakula mkate wa uovu,

na kunywa mvinyo wa jeuri.

184:18 Mt 5:14; Ay 17:9; Isa 26:7; Dan 12:3; Yn 8:12Njia ya wenye haki ni kama nuru ya kwanza ya mapambazuko,

ambayo hungʼaa zaidi na zaidi mpaka mchana mkamilifu.

194:19 Ay 18:5; Yn 12:35Lakini njia ya waovu ni kama giza nene;

hawajui kinachowafanya wajikwae.

204:20 Za 34:11-16; Mit 1:8-9; 5:1Mwanangu, yasikilize kwa makini yale ninayokuambia;

sikiliza kwa makini maneno yangu.

214:21 Mit 3:21Usiruhusu yaondoke machoni pako,

yahifadhi ndani ya moyo wako;

224:22 Mit 3:8kwa sababu ni uzima kwa wale wanaoyapata

na afya kwa mwili wote wa mwanadamu.

234:23 Mit 10:11; Mt 12:34Zaidi ya yote, linda moyo wako, kuliko yote uyalindayo,

maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.

24Epusha kinywa chako na ukaidi;

weka mazungumzo machafu mbali na midomo yako.

254:25 Ay 31:1Macho yako na yatazame mbele,

kaza macho yako moja kwa moja mbele yako.

264:26 Ebr 12:13Sawazisha mapito ya miguu yako

na njia zako zote ziwe zimethibitika.

274:27 Law 10:11; Kum 28:14Usigeuke kulia wala kushoto;

epusha mguu wako na ubaya.