Faida Nyingine Za Hekima
13:1 Kum 30:16; Za 44:17; Mit 4:5Mwanangu, usisahau mafundisho yangu,
bali zitunze amri zangu moyoni mwako,
23:2 Mit 9:6; 4:10kwa kuwa zitakuongezea miaka mingi ya maisha yako
na kukuletea mafanikio.
33:3 Kum 6:8; Mit 6:21; 2Kor 3:3Usiache kamwe upendo na uaminifu vitengane nawe;
vifunge shingoni mwako,
viandike katika ubao wa moyo wako.
43:4 1Sam 2:26; Lk 2:52; Mdo 2:47Ndipo utapata kibali na jina zuri
mbele za Mungu na mwanadamu.
53:5 Za 4:5; Yer 9:23Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote
wala usizitegemee akili zako mwenyewe;
63:6 1Nya 28:9; Ay 33:11; Yer 42:3katika njia zako zote mkiri yeye,
naye atayanyoosha mapito yako.
73:7 Isa 5:21; Rum 12:16; Kum 4:6Usiwe mwenye hekima machoni pako mwenyewe;
mche Bwana ukajiepushe na uovu.
83:8 Za 38:3; Mit 4:22; Ay 21:24Hii itakuletea afya mwilini mwako,
na mafuta kwenye mifupa yako.
93:9 Kut 23:19; 26:1-15Mheshimu Bwana kwa mali zako na
kwa malimbuko ya mazao yako yote;
103:10 Kum 28:8; Za 144:13; Ay 22:21; Mal 3:10-12ndipo ghala zako zitakapojaa hadi kufurika,
viriba vyako vitafurika kwa mvinyo mpya.
113:11 Mit 1:8-9; Ay 5:17Mwanangu, usiidharau adhabu ya Bwana
na usichukie kukaripiwa naye,
123:12 Mit 13:24; Ufu 3:19; Ay 3:19; 5:17; Ebr 12:5-6kwa sababu Bwana huwaadibisha wale awapendao,
kama vile baba afanyavyo
kwa mwana apendezwaye naye.
133:13 Mit 8:34, 35Heri mtu yule aonaye hekima,
mtu yule apataye ufahamu,
143:14 Ay 28:15; Mit 16:16kwa maana hekima ana faida kuliko fedha
na mapato yake ni bora kuliko ya dhahabu safi.
153:15 Ay 28:17-19Hekima ana thamani kuliko marijani;
hakuna chochote unachokitamani
kinachoweza kulinganishwa naye.
163:16 1Fal 3:13-14; Mit 8:18Maisha marefu yako katika mkono wake wa kuume;
katika mkono wake wa kushoto
kuna utajiri na heshima.
173:17 Mit 16:7; Mt 11:28-30Njia zake zinapendeza,
mapito yake yote ni amani.
183:18 Mwa 2:9; Ufu 2:7Yeye ni mti wa uzima kwa wale wanaomkumbatia;
wale wamshikao watabarikiwa.
193:19 Ay 28:25-27; Za 104:24; Mit 8:27-29Kwa hekima Bwana aliiweka misingi ya dunia,
kwa ufahamu aliziweka mbingu mahali pake;
203:20 Kum 33:28; Ay 36:28kwa maarifa yake vilindi viligawanywa,
nayo mawingu yanadondosha umande.
213:21 Mit 1:8-9; 6:20; 4:20-22Mwanangu, hifadhi maamuzi mema na busara,
usiache vitoke machoni pako;
223:22 Kum 30:20; Mit 4:20-22ndipo vitakapokuwa uzima nafsini mwako
na pambo la neema shingoni mwako.
23Kisha utaenda katika njia yako salama,
wala mguu wako hautajikwaa;
243:24 Law 26:6; Za 3:5; Ay 11:18; Yer 31:25ulalapo, hautaogopa;
ulalapo usingizi wako utakuwa mtamu.
253:25 Za 91:5; 112:7Usiogope maafa ya ghafula
au maangamizi yanayowapata waovu,
263:26 1Sam 2:9kwa kuwa Bwana atakuwa tumaini lako
na kuepusha mguu wako kunaswa katika mtego.
273:27 Rum 13:7; Gal 6:10Usizuie wema kwa wale wanaostahili
ikiwa katika uwezo wako kutenda.
283:28 Law 19:13; Lk 10:25-37; Kum 24:15Usimwambie jirani yako,
“Njoo baadaye, nitakupa kesho”:
wakati wewe unacho kitu kile karibu nawe.
293:29 Zek 8:17Usifanye hila ya kumdhuru jirani yako,
ambaye anaishi karibu na wewe akikuamini.
303:30 Rum 12:18Usimshtaki mtu bila sababu,
wakati hajakutenda dhara lolote.
313:31 Za 37:1; Mit 24:1-2Usimwonee wivu mtu mwenye jeuri
wala kuchagua njia yake iwayo yote,
323:32 Za 101:4; Ay 29:4kwa kuwa Bwana humchukia mtu mpotovu,
lakini siri yake iko kwa mwenye haki.
333:33 Ay 5:3; Mal 2:2; Zek 5:4Laana ya Bwana i juu ya nyumba ya mwovu,
lakini yeye huibariki nyumba ya mwenye haki.
343:34 Za 18:25-27; Mt 23:12Huwadhihaki wale wanaodhihaki,
lakini huwapa neema wale wanyenyekevu.
35Wenye hekima hurithi heshima,
bali huwaaibisha wapumbavu.
信靠耶和華
1孩子啊,不要忘記我的訓言,
要把我的誡命存在心裡,
2因為這必使你延年益壽,
幸福平安。
3不要讓慈愛和信實離開你,
要把他們繫在你的頸項上,
刻在你的心坎上。
4這樣,你必蒙上帝和世人的喜悅,
享有美譽。
5你要全心信靠耶和華,
不可倚靠自己的悟性。
6凡事都要尋求祂,
祂必指引你走正路。
7不要自以為有智慧,
要敬畏耶和華,遠離惡事。
8這樣可醫治你的身體,
滋潤你的筋骨。
9你要用自己的財富和一切初熟的物產來尊崇耶和華,
10祂必使你五穀滿倉,
榨酒池溢出新釀。
11孩子啊,不可輕視耶和華的管教,
也不可厭煩祂的責備。
12因為耶和華責備祂所愛的人,
就像父親責備他所疼愛的孩子。
13找到智慧、得到悟性的人有福了,
14因為智慧比銀子更有價值,
比金子更有益處,
15比珠寶更珍貴;
你所喜愛的一切都難以相比。
16智慧的右手有長壽,
左手有富貴和尊榮。
17她的路上有福樂,
她的道上有平安。
18對持守智慧的人來說,
智慧是生命樹,
緊握智慧的人必蒙祝福。
19耶和華以智慧奠立大地,
以悟性鋪設諸天;
20祂的知識使深淵裂開,
使天上降下甘霖。
21孩子啊,你要守護智慧和明辨力,
別讓她們離開你的視線。
22她們必給你帶來生命,
作你頸項上華美的裝飾。
23如此,你必步履穩健,不致失足;
24你必安然躺臥,睡得香甜。
25不要怕突來的災禍,
不要怕惡人遭毀滅,
26因為耶和華是你的靠山,
祂使你的腳不陷入網羅。
27倘若有力量行善,
就當幫助有需要的人,不要推託。
28倘若可以幫忙,
就不可對有求於你的鄰人說:
「回去吧,明天再來,我必給你!」
29鄰舍在你附近安分居住,
不可謀害他。
30別人若沒有害你,
不要無故與他相爭。
31不要羡慕殘暴之徒,
也不可步其後塵,
32因為耶和華憎惡邪僻之徒,
喜愛正直的人。
33耶和華咒詛惡人的家,
賜福義人的家。
34耶和華譏笑好譏誚的人,
恩待謙卑的人。
35智者得尊榮,
愚人受羞辱。