124:1 Mit 3:31-32; 23:17-18Usiwaonee wivu watu waovu,
usitamani ushirika nao;
224:2 Za 2:1; 10:7; Isa 32:6; 55:7-8; 59:7; 65:2; Hos 4:1kwa maana mioyo yao hupanga mambo ya jeuri,
nayo midomo yao husema juu ya kuleta madhara.
324:3 Mit 14:1Kwa hekima nyumba hujengwa,
nayo kwa njia ya ufahamu huimarishwa
424:4 Mit 8:21kwa njia ya maarifa vyumba vyake hujazwa
vitu vya thamani na vya kupendeza.
524:5 Mit 21:22Mtu mwenye hekima ana uwezo mkubwa,
naye mtu mwenye maarifa huongeza nguvu,
624:6 Mit 11:14; Lk 14:31kwa kufanya vita unahitaji uongozi
na kwa ushindi washauri wengi.
724:7 Za 10:5; Mit 14:6Hekima i juu mno kwa mpumbavu,
katika kusanyiko langoni
hana lolote la kusema.
824:8 Rum 1:30Yeye apangaye mabaya
atajulikana kama mtu wa hila.
924:9 Mwa 6:5; Za 119:113; Mt 9:4; Mdo 8:22; 2Kor 10:524:9 Mwa 6:5; Mdo 8:22; 2Kor 10:5Mipango ya upumbavu ni dhambi,
watu huchukizwa na mwenye dhihaka.
1024:10 Yer 51:46; Ebr 12:3Ukikata tamaa wakati wa taabu,
jinsi gani nguvu zako ni kidogo!
1124:11 Isa 58:6-7; 1Yn 3:16; Za 82:4Okoa wale wanaoongozwa kwenye kifo;
wazuie wote wanaojikokota
kuelekea machinjoni.
1224:12 Za 139:2; Mit 16:24; 21:2; Yer 32:19; Mt 16:24Kama mkisema, “Lakini hatukujua lolote kuhusu hili,”
je, yule apimaye mioyo halitambui hili?
Je, yule awalindaye maisha yenu halijui hili?
Je, hatamlipa kila mtu kulingana na aliyotenda?
1324:13 Wim 5:1Ule asali mwanangu, kwa kuwa ni nzuri;
asali kutoka kwenye sega ni tamu kwa kuonja.
1424:14 Za 119:103; Mit 16:24; 23:18Ujue pia kwamba hekima ni tamu kwa nafsi yako,
kama ukiipata, kuna matumaini kwako ya siku zijazo,
nalo tumaini lako halitakatiliwa mbali.
1524:15 Za 10:9, 10Usivizie kama haramia afanyavyo ili kuyashambulia
makao ya mwenye haki,
wala usiyavamie makazi yake,
1624:16 Ay 5:19; Mik 7:8; Za 34:19Kwa maana ingawa mtu mwenye haki huanguka mara saba, huinuka tena,
lakini waovu huangushwa chini na maafa.
1724:17 Oba 1:12; Ay 31:29Usitazame kwa kufurahia adui yako aangukapo;
wakati ajikwaapo,
usiruhusu moyo wako ushangilie.
1824:18 Ay 31:29Bwana asije akaona na kuchukia
akaiondoa ghadhabu yake mbali naye.
1924:19 Za 37:1Usikasirike kwa sababu ya watu wabaya
wala usiwaonee wivu waovu,
2024:20 Ay 18:5; Mit 13:9; Isa 3:11kwa maana mtu mbaya hana tumaini la siku zijazo,
nayo taa ya waovu itazimwa.
2124:21 Rum 13:1-7; 1Pet 2:17Mwanangu, mche Bwana na mfalme,
wala usijiunge na waasi,
2224:22 Za 73:19kwa maana hao wawili watatuma maangamizi ya ghafula juu yao,
naye ni nani ajuaye maafa wawezayo kuleta?
Misemo Zaidi Ya Wenye Hekima
2324:23 Kut 18:16; Law 19:15; 2Nya 19:7; Za 72:2; Yer 22:16; Yn 7:24Hii pia ni misemo ya wenye hekima:
Kuonyesha upendeleo katika hukumu si vyema:
2424:24 Isa 5:23; Mit 17:15Yeyote amwambiaye mwenye hatia,
“Wewe huna hatia,”
Kabila zitamlaani
na mataifa yatamkana.
25Bali itakuwa vyema kwa wale watakaowatia hatiani wenye hatia,
nazo baraka tele zitawajilia juu yao.
26Jawabu la uaminifu
ni kama busu la midomoni.
2724:27 1Fal 5:17, 18; Lk 14:28Maliza kazi zako za nje,
nawe uweke mashamba yako tayari,
baada ya hayo, jenga nyumba yako.
2824:28 Za 7:4; Efe 4:25Usishuhudie dhidi ya jirani yako bila sababu,
au kutumia midomo yako kudanganya.
2924:29 Mit 20:22; Rum 12:17; Mt 5:39Usiseme, “Nitamtenda kama alivyonitenda mimi;
nitamlipiza mtu yule kwa kile alichonitendea.”
3024:30 Mit 6:6-11; 26:13-16Nilipita karibu na shamba la mvivu,
karibu na shamba la mizabibu la mtu asiye na akili,
3124:31 Yer 4:3; Ebr 6:8miiba ilikuwa imeota kila mahali,
ardhi ilikuwa imefunikwa na magugu, na
ukuta wa mawe ulikuwa umebomoka.
32Nikatafakari moyoni mwangu lile nililoliona,
nami nikajifunza somo kutokana na niliyoyaona:
3324:33 Mit 6:10Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo,
bado kukunja mikono kidogo upate kupumzika:
3424:34 Mit 10:4; Mhu 10:18hivyo umaskini utakuja juu yako kama mnyangʼanyi,
na kupungukiwa kutakujia kama mtu mwenye silaha.
1不要羡慕恶人,
不要向往与他们为友;
2因为他们心里图谋暴行,
口中谈论恶事。
3家靠智慧而建立,
靠悟性而稳固,
4借知识而充满各种珍宝。
5智者充满能力,
哲士力上加力。
6出征打仗,要凭智谋;
谋士众多,胜券在握。
7智慧对愚人高不可及,
他在城门口沉默不语。
8图谋作恶的必被称为阴谋家。
9愚人的计谋是罪恶,
人人都厌恶嘲讽者。
10逆境中丧胆的是弱者。
11被拉去屠杀的,你要抢救;
踉跄受死的,你要拦阻。
12不要推说自己毫不知情,
鉴察人心的主洞悉一切,
保守你生命的上帝知情,
祂必按你的行为报应你。
13孩子啊,你要吃美好的蜂蜜,
蜂房滴下的蜜甘甜可口。
14智慧同样使你的心灵甘甜;
你若找到智慧,前途必光明,
盼望也不会幻灭。
15不要像恶人一样暗算义人,
破坏他的家。
16因为义人跌倒七次也必起来,
恶人却被灾祸击垮。
17仇敌跌倒,不要幸灾乐祸;
仇敌败落,不要心里欢喜。
18否则,耶和华看见会不悦,
不再向仇敌发烈怒。
19不要因恶人而愤愤不平,
也不要羡慕歹徒;
20因为恶人毫无前途,
恶人的灯终必熄灭。
21孩子啊,要敬畏耶和华和君王,
不要跟反复无常之徒为伍。
22因为灾祸必骤然临到他们,
谁知道耶和华和君王如何毁灭他们?
其他智言
23以下也是智者的箴言:
判案时偏袒实为不善。
24判恶人无罪的,
必遭万人咒诅,
为列国痛恨。
25责备恶人的必有欢乐,
美好的福气必临到他。
26诚实的回答如同友好的亲吻。
27要安排好外面的事,
把田间的工作准备妥当,
然后建造房屋。
28别无故作证害邻舍,
也不可撒谎欺骗人。
29不可说:“别人怎样待我,
我就怎样待他;
我要照他所做的报复他。”
30我走过懒惰人的田地和无知者的葡萄园,
31那里荆棘遍地,
刺草丛生,
石墙倒塌。
32我仔细思想所见之事,
领悟到一个教训:
33再睡一会儿,
打个盹儿,
抱着手躺一会儿,
34贫穷必像强盗一样临到你,
缺乏必像武士一样扑向你。