Mika 4 – Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) NEN

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Mika 4:1-13

Mlima Wa Bwana

(Isaya 2:2-4)

14:1 Za 48:1; 86:9; Zek 8:3; Isa 2:2; Dan 2:35; 2:44; Eze 17:22; Yer 3:17; 31:12Katika siku za mwisho

mlima wa Hekalu la Bwana utaimarishwa

kama mlima mkuu miongoni mwa milima yote;

utainuliwa juu ya vilima,

na watu wa mataifa watamiminika humo.

24:2 Yer 31:6; Yn 6:45; Eze 20:40; Zek 2:11; 14:16; Isa 54:13; Za 25:8-9; 119:171Mataifa mengi yatakuja na kusema,

“Njooni, twendeni mlimani mwa Bwana,

kwenye nyumba ya Mungu wa Yakobo.

Atatufundisha njia zake,

ili tuweze kuenenda katika mapito yake.”

Sheria itatoka Sayuni,

neno la Bwana litatoka Yerusalemu.

34:3 Isa 2:4; 11:4; Yoe 3:10; Hos 2:18; Za 72:7; Zek 8:20-22; 9:10; Za 46:9Atahukumu kati ya mataifa mengi,

na ataamua migogoro ya mataifa

yenye nguvu na yaliyo mbali.

Watafua panga zao ziwe majembe,

na mikuki yao kuwa miundu ya kukata matawi.

Taifa halitainua upanga dhidi ya taifa jingine,

wala hawatajifunza vita tena.

44:4 1Fal 4:25; Law 26:6; Eze 39:26; Isa 1:20; 36:16; Yer 31:10; Zek 3:10Kila mtu ataketi chini ya mzabibu wake

na chini ya mtini wake,

wala hakuna mtu atakayewaogopesha,

kwa kuwa Bwana Mwenye Nguvu Zote amesema.

54:5 2Fal 17:29; Mdo 14:16; Yos 24:14-15; Isa 26:8; Yer 2:11; Zek 10:12Mataifa yote yanaweza kutembea

katika jina la miungu yao;

sisi tutatembea katika jina la Bwana

Mungu wetu milele na milele.

Mpango Wa Bwana

64:6 Yer 31:8; Isa 56:8; Za 147:2; 106:47; Eze 34:13, 16; 37:21; Sef 3:19“Katika siku hiyo,” asema Bwana,

“nitawakusanya walemavu;

nitawakusanya walio uhamishoni

na wale niliowahuzunisha.

74:7 Yoe 2:32; Mik 2:12; Isa 9:6; Mwa 12:2; Dan 2:44; 7:14; Ufu 11:15; Lk 1:33Nitawafanya walemavu kuwa mabaki,

wale waliofukuzwa kuwa taifa lenye nguvu.

Bwana atatawala juu yao katika Mlima Sayuni

kuanzia siku hiyo na hata milele.

84:8 Isa 1:26; Zek 9:9Lakini kuhusu wewe, ee mnara wa ulinzi wa kundi,

ee ngome ya Binti Sayuni,

milki ya awali itarudishwa kwako,

ufalme utakuja kwa Binti Yerusalemu.”

94:9 Yer 8:19; 30:6; 48:41; Mwa 3:16Kwa nini sasa unalia kwa nguvu:

kwani huna mfalme?

Je, mshauri wako amekufa, hata maumivu yakukamate

kama ya mwanamke

aliye na utungu wa kuzaa?

104:10 Kum 21:10; 2Fal 20:18; Isa 43:14; 48:20Gaagaa kwa utungu, ee Binti Sayuni,

kama mwanamke mwenye utungu wa kuzaa,

kwa kuwa sasa ni lazima uuache mji

ukapige kambi uwanjani.

Utakwenda Babeli;

huko utaokolewa.

Huko Bwana atakukomboa

kutoka mikononi mwa adui zako.

114:11 Mao 2:16; Oba 1:12; Mik 7:8Lakini sasa mataifa mengi

yamekusanyika dhidi yako.

Wanasema, “Mwache anajisiwe,

macho yetu na yatazame Sayuni kwa furaha!”

124:12 Mwa 50:20; Isa 55:8; Rum 11:33-34Lakini hawayajui

mawazo ya Bwana;

hawauelewi mpango wake,

yeye awakusanyaye kama miganda

kwenye sakafu ya kupuria.

134:13 Isa 21:10; 23:18; 45:1; Ufu 21:24; Dan 2:44“Inuka upure, ee Binti Sayuni,

kwa kuwa nitakupa pembe za chuma;

nitakupa kwato za shaba

na utavunja vipande vipande mataifa mengi.”

Utatoa mapato yao waliopata kwa udanganyifu kwa Bwana,

utajiri wao kwa Bwana wa dunia yote.