Mika 1 – Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) NEN

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Mika 1:1-16

11:1 Yer 26:18; 2Pet 1:21; 1Nya 3:12-13; Hos 1:1; Isa 1:1Neno la Bwana lilimjia Mika, Mmoreshethi, wakati wa utawala wa Yothamu, Ahazi na Hezekia, wafalme wa Yuda; ufunuo aliouona kuhusu Samaria na Yerusalemu.

21:2 Kum 4:26; 32:1; Yer 6:19; Mwa 31:50; Za 11:4; Isa 1:2Sikieni, enyi mataifa, enyi nyote,

sikilizeni, ee dunia na wote mliomo ndani yake,

ili Bwana Mwenyezi ashuhudie dhidi yenu,

Bwana kutoka Hekalu lake takatifu.

Hukumu Dhidi Ya Samaria Na Yerusalemu

31:3 Isa 18:4; 64:1; 26:21; Eze 3:12; Ebr 12:18, 19; Amo 4:13Tazama! Bwana anakuja kutoka mahali pake;

anashuka na kukanyaga

mahali palipoinuka juu pa dunia.

41:4 Za 46:2-6; Hes 16:31; Nah 1:5Milima inayeyuka chini yake

na mabonde yanagawanyika

kama nta mbele ya moto,

kama maji yatiririkayo kasi

kwenye mteremko.

51:5 Amo 8:14; Hos 5:5; Yer 2:18-19Yote haya ni kwa sababu ya kosa la Yakobo,

ni kwa sababu ya dhambi za nyumba ya Israeli.

Kosa la Yakobo ni lipi?

Je, sio Samaria?

Je, mahali pa juu pa Yuda pa kuabudia miungu ni nini?

Je, sio Yerusalemu?

61:6 Kum 20:6; Amo 5:11“Kwa hiyo nitaufanya Samaria kuwa lundo la kokoto,

mahali pa kuotesha mizabibu.

Nitayamwaga mawe yake katika bonde

na kuacha wazi misingi yake.

71:7 Eze 6:6; Kut 32:20; Kum 9:21; 23:17-18Sanamu zake zote

zitavunjwa vipande vipande;

zawadi zake zote za Hekalu

zitachomwa kwa moto;

nitaharibu vinyago vyake vyote.

Kwa kuwa alikusanya zawadi zake

kutokana na ujira wa kahaba,

nazo zitatumika tena

kulipa mishahara ya kahaba.”

Kulia Na Kuomboleza

81:8 Isa 15:3; 20:2Kwa ajili ya hili nitalia na kuomboleza;

nitatembea bila viatu na tena uchi.

Nitabweka kama mbweha

na kuomboleza kama bundi.

91:9 Yer 46:11; 10:19; 2Fal 18:13; Isa 3:26Kwa sababu jeraha lake halitibiki;

limekuja Yuda.

Limefika hasa kwenye lango la watu wangu,

hata Yerusalemu kwenyewe.

10Usiliseme hili huko Gathi;

usilie hata kidogo.

Huko Beth-le-Afra

gaagaa mavumbini.

111:11 Eze 23:29Piteni mkiwa uchi na wenye aibu,

ninyi mkaao Shafiri.

Wale waishio Saanani

hawatatoka nje.

Beth-Eseli iko katika maombolezo;

kinga yake imeondolewa kwako.

121:12 Yer 14:19; 40:2Wale waishio Marothi wanagaagaa kwa maumivu

wakingoja msaada,

kwa sababu maangamizi yamekuja

kutoka kwa Bwana,

hata katika lango la Yerusalemu.

131:13 Yos 10:3; Za 9:14Enyi mkaao Lakishi,

fungeni farasi kwenye magari ya vita.

Mlikuwa chanzo cha dhambi

kwa Binti Sayuni,

kwa kuwa makosa ya Israeli

yalikutwa kwako.

141:14 2Fal 16:8; Yos 15:44; Yer 15:18Kwa hiyo utaipa Moresheth-Gathi

zawadi za kuagana.

Mji wa Akzibu utaonyesha wazi udanganyifu

kwa wafalme wa Israeli.

151:15 Yos 15:44; 12:15Nitawaleteeni atakayewashinda

ninyi mnaoishi Maresha.

Yeye aliye utukufu wa Israeli

atakuja Adulamu.

161:16 Law 13:40; Ay 1:20; 2Fal 18:13; Amo 5:27; Kum 4:27Nyoeni nywele zenu katika kuomboleza

kwa ajili ya watoto wenu mnaowafurahia;

jifanyieni upara kama tai,

kwa kuwa watawaacha

na kwenda uhamishoni.